Elections 2010 Kikwete apendekezwa na CCM kugombea urais 2010

KwaniMbasha anaimba nyimbo hizi za kidunia, ama ndio yale ya Kikwete chaguo la Mungu, asante Invisible, endelea kutujuza hayo yanayoendelea kwenye mkutano huo wa mabaka uchumi.

Mkuu ujasiriamali na ubepari uchwara si ajabu mtu mzima kutoa shikamoo kwa mtoto au kuchojoa hadharani alailimradi mkono uende kinywani.
 
Imefika wakati wa kuwaandama viongozi wa upinzani ambao ni mapandikizi tu, si wa kuonea aibu tena!

Na nadhani imefika wakati ambao baadhi ya wana CCM wanatakiwa waache kufurahia nyimbo tu na kukatiwa viuno walifikirie taifa zaidi.

Ukitaka kujua hali ni mbaya na tunahitaji kujiepusha na ushabiki usokuwa na maana basi angalia hapa: JamiiForums|TMF Blogs hasa kwenye hoja hii kutoka kwenye vijiji vyetu ambapo watanzania wapo hali mbaya sana:

Pres. Kikwete’s “Maisha bora kwa kila Mtanzania”

Hii ndiyo hali halisi ya maisha ya watanzania asilimia kubwa... Hii kuburudishwa na nyimbo
 
Wanafunzi wa vyuo vikuu wanaimba "CCM kiboko yao, na wapinzani wanajua". Wanasisitiza CUF wanajua...! Hahaha na TLP wanajua! Aibu kwa Mrema na Lipumba....

Hapana mkuu, kwa Prof Lipumba tu maana Mrema ameshamaliza kazi.
 
Daaaaaaah nchi inaangamizwa na hili kundi la wavaa nguo za kijani, mawazo yangu yananituma kufanya jambo baya sana, ili kuwafanya wale jamaa na mawazo yao waishie mle.
 
Utenzi kutoka Zanzibar umeisha - Wajumbe wengi walienda Kutuza!

"Komandoo" Dr. Salim ndiye mjumbe pekee katika "high-Table" ambaye hajaweza kutabasamu mpaka wakati huu - he seems so depressed!

Chiligati ametambulisha "so and so": Mama Maria Nyerere na Mama Karume e.t.c na anaendelea kutambulisha wageni "so and so" kutoka Vyama vya siasa vya nje ya nchi : Angola (imebidi arudie kutambulisha kwa Kiingereza - maana hawa wajumbe walibaki wameduwaa), Mozambique (FRELIMO) wanafuata (bla blah zinafuata), then Botswana...
 
Cpt Chiligati anaendelea kuwataja wawakilishi wa vyama mbalimbali:

Cuba wamewakilisha na RPF (!!!) pia wapo, DRC wamewakilisha, Uganda (NRM) wakiogozwa na na Dr Lukunda, Zimbabwe (ZANU-PF) wakiongozwa na Ma-Komredi, China (CP) wakiongowa na Komredi Lee, Korea (Workers Party) - TUCTA mpo?, .... And Vietnam!
 
Utenzi kutoka Zanzibar umeisha - Wajumbe wengi walienda Kutuza!

"Komandoo" Dr. Salim ndiye mjumbe pekee katika "high-Table" ambaye hajaweza kutabasamu mpaka wakati huu - he seems so depressed!

Chiligati ametambulisha "so and so": Mama Maria Nyerere na Mama Karume e.t.c na anaendelea kutambulisha wageni "so and so" kutoka Vyama vya siasa vya nje ya nchi : Angola (imebidi arudie kutambulisha kwa Kiingereza - maana hawa wajumbe walibaki wameduwaa), Mozambique (FRELIMO) wanafuata (bla blah zinafuata), then Botswana...

anajionea karaha tu, watu wanaacha kujadili issue sensitive kwa maendeleo ya taifa wamekalia viuna viuno, eti wasomi wazima wa elimu ya juu, wanakalia kuimba nyimbo za ujinga ujinga. halafu mnasema nchi hii itakombolewa na kizazi cha wasomi, hawa wenye simple mind, wanapata wapi muda wakutunga na kujifunza nyimbo, hakuna Test, hakuna assignmenty ama ? kweli nashangaa. wanapata wapi muda kushiriki mazoezi ya kwaya ?
 
Masikini weeee... Mrema anapita mbele kusalimiana na JK na wanamcheka huku wakidai alihama CCM kwenda kuimarisha demokrasia ya upinzani (inahitaji akili ndogo kuelewa maanake)...

Lipumba nae anaenda kusalimiana na JK huku akitabasamu kwa nguuuvu!
 
NCCR-Mageuzi wamemtuma Makamu mwenyekiti pia. UMDP wapo pia. AFP wapo pia, hiki ni chama kipya?
 
Invisible,

Huyu mwakilishi wa Wa-CCM wa nje ya nchi ingefaa arudi achukue nafasi ya Cpt Chiligati (maoni yangu)

Amepewa nafasi kutoa hotuba fupi ameonge for more than 20 minutes!
 
Masikini weeee... Mrema anapita mbele kusalimiana na JK na wanamcheka huku wakidai alihama CCM kwenda kuimarisha demokrasia ya upinzani (inahitaji akili ndogo kuelewa maanake)...

Lipumba nae anaenda kusalimiana na JK huku akitabasamu kwa nguuuvu!

Mrema sasa hivi ana kamtindio kidogo, hawezi kuelewa hata jambo moja, yeye kwake ni kuganga njaa, kweli Mrema leo wa kuhongwa na hawa kina Makamba..... kwisha habari yake, bahati mbaya na maradhi yanamwandama sana sasa.
 
haya matawi ya nje ya nji yapo kila siku au ni mwaka huu wa uchaguzi tu jamani? ikifika wakati wa kupiga kura wataru home au?
 
Back
Top Bottom