Kikwete anaweza kuongoza mabadiliko tunayoyataka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anaweza kuongoza mabadiliko tunayoyataka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 7, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Ili Kikwete aweze kuliongoza taifa kuielekea mabadiliko tunayoyataka ni lazima kwanza kabisa atambue kuwa ipo haja ya mabadiliko. Ninapozungumzia mabadiliko nazungumzia mfumo mzima wa utawala ambao nimeuita ni "MFUMO WA UTAWALA WA KIFISADI". Matatizo yetu mengi kama taifa yanatokana na mfumo huu ambao umejikita katika taratibu za sheria, fikra, na taratibu mbalimbali.

  Mabadiliko haya ni lazima yaanzie kwenye kuelewa haja ya kuandika upya Katiba. Jambo hili Kikwete halioni au hataki kuliona kwani kufanya hivyo ni kukiri kuna mapungufu makubwa ya Kikatiba. Mabadiliko haya ni lazima yaingie katika mfumo wa kuwajibishana na kusimamiana kitu ambacho Kikwete na chama chake bado hawajaona ulazima wa kushughulikia na matokeo yake kwa kutumia mfumo ule ule ulioshindwa kwa miaka 50 wanafikiria wataweza kujenga taifa la karne ya ishirini na moja.

  Lakini jambo la pili ni lazima kutambua kuwa aina ya viongozi wanaoingia madarakani huamua kabisa jinsi gani taifa linatawaliwa. Kwa muda mrefu nimekuwa nikisema na sitojuta kurudia tena kuwa tatizo kubwa la Tanzania na uongozi wake siyo elimu, fedha, mipango, au tafiti za kuelezea matatizo yetu. Tatizo letu kubwa ni aina ya viongozi tunaowaingiza madarakani. Mojawapo ya hofu zangu kubwa ni kwamba mwaka huu tunaweza tukajikuta tunaingiza kundi la ajabu sana kutuongoza na tutakuwa watu wa kwanza kulalamika "viongozi wetu vipi?".

  Kuanzia utendaji kazi wa Bunge lililopita, kura za maoni na sasa kampeni za uchaguzi naweza kuona ndani ya CCM aina ya viongozi ambao hawana tofauti na watawala wetu walioshndwa wa miaka mitano au kumi iliyopita. Matokeo yake ni kuwa mabadiliko tunayoyataka hayawezi kutokea kwa sababu viongozi wenyewe wanaoingizwa hasa kutoka upande wa CCM wao wenyewe nao hawatambui au hawako tayari kukiri kuwa kuna haja ya mabadiliko. Wao kama ilivyo Kikwete wanafurahia hali iliyopo sasa (status quo).

  Ndio maana basi utaona kuwa katika kampeni za Rais Kikwete na wagombea wa CCM dhima hii ya Mabadiliko haipo. Kutaka kupigia kelele mabadiliko ni kujaribu kusema kuwa kilichopo hakiko sawasawa na hivyo kukiri udhaifu. CCM na Kikwete hawako tayari kukubali kuwa kuna mapungufu yanayohitaji mabadiliko makubwa isipoikuwa yale ya kimapambo (cosmetic change). Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa ya kimuundo na kimfumo ambayo yataliweka taifa katika nafasi ya kuwa taifa la kisasa kwani ilivyo sasa, njia tuliyoichagua ni njia ya Nigeria; upande mmoja kuna mafanikio ya namna mbalimbali, na upande mwingine kuna ufisadi ambao umeuwa ni utamaduni. Kwa kuendelea kuchagua watu wale wale tunazidi kurasimisha ufisadi na kuufanya kuwa ni sehemu ya maisha yetu hasa unaposikia viongozi wa CCM wakituambia kuwa "hakuna aliye msafi" na hivyo kujaribu kuhalalisha uchafu wao.

  Swali kubwa kumbe kwa wapiga kura wetu linazunguka katika suala hili la mabadiliko. Je umeridhika na hali iliyopo? Je unaridhika na mfumo uliopo wa utendaji kazi wa serikali na watumishi wake? Je unaridhika na uongozi unaotolewa kwa taifa letu. Ukijibu "Ndiyo" kwa maswali yote hayo maana yake ni kuwa na wewe huoni haja ya mabadiliko na hivyo una uwezekano mkubwa wa kuchagua wagombea wote wa CCM ambao mtazamo wao unashirikiana nao.

  Kwa sasa, naweza kusema kwa uhakika mkubwa tu kwamba bado Rais Kikwete na uongozi wa juu wa CCM hawajashawishi kuonesha kuwa wanatambua kuwa muda wa mabadiliko umefika. Itakuwaje lakini kama ni kweli bado hatujafikia huko kwani hadi tutapojikuta tumesukumizwa katika kona ya dhulma, ufisadi, na uonevu ndipo tutakapoamua kusema "imetosha"? Labda ni kweli muda wa mabadiliko bado haujafika na hilo CCM wanalitumia kwa manufaa yao.


  Lakini, hata leo hii bado kizazi cha Watanzania kinaitwa kuamua kama kinataka mabadiliko na kama mabadiliko hayo yanaweza kuletwa na watu wale wale, wenye fikra zile zile, kutoka chama kile kile chenye sera zile zile. Ukijibu "hapana", basi ni lazima uongozwe na dhamira yako kupiga kura kuchagua mabadiliko kwa kupigia wagombea wenye kuwakilisha mabadiliko.  Itakuwaje hata hivyo kama sisi na wao tumeshindwa kutambua uwepo wa muda huo sasa?
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Sep 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  You sound more like Ronaldus Magnus to me......

  YouTube - Ronald Reagan Endorses Obama
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu kudos! Mie nasema na nasema kwa msisitizo CCM hawana dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko yeyote Tanzania. Na tusije kujilaumu nchi ikienda kombo kwani hakuna atakayebaki salama si mwanaCCM wala Chadema. Natolea mfano hai mmoja rushwa kama CCM hawanadhamira ya dhati kuwakamata mafisadi papa unadhani litatokea nini watu watazidi kula rushwa na hiyo Takakukuru itakuwa kama mchezo wa kuigiza kwani watu wataiba mchana mchana na watahakikisha wanaiba katika misingi ambayo Takukuru wanaona safi kabisa. Kila la kheri
   
 4. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dhamira ya chama cha mafisadi ni kuiangamiza nchi na upo ushahidi wa kutosha tu katika maamuzi yao mbali mbali ambayo yanaiangamiza nchi, lakini tatizo ni wapiga kura ambao ama uwezo wao wa kuchanganua mambo ni finyu sana au hawana kabisa uwezo huo au ni mataahira hawaoni jinsi nchi inavyoangamizwa.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unafikiri JK anatambua haja ya mabadiliko na anaweza kutuongoza kuelekea mabadiliko hayo?
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Sep 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hapana hawezi kwani angekuwa anaweza angelikuwa keshafanya au keshaonyesha nia ya kufanya hivyo. Miaka 5 ijayo kama wakishinda itakuwa more of the same. Mbaya zaidi huenda hata kutambua hatambui. Ni heri walau kulitambua tatizo halafu ukashindwa kulitatua. Unaweza kuomba msaada wa wengine. Ila usipolitambua inakuwa kasheshe zaidi maana hatua muhimu unakuwa hata hujaifikia.

  Na nilijua hayo tokea 2005. CCM wanajua lip service tu.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama anatambua kuna haja ya mabadiliko. Nitakupa mfano anasema anajenga uwanja mpya wa ndege mbeya wakati hana hata ndege moja ya kurusha bendera ya Tanzania. Unadhani huyo anafahamu tatizo la watanzania au la? Uwanja wa ndege utawasaidia nini watanzania kama shirika la ndege ni mgonjwa mahtuti? Au tutajenga uwanja uwe eneo la makumbusho. Angelikuwa kweli anataka mabadiliko angelisema Tanzania nataka tuwe na ndege tatu baada ya miaka mitatu. Sasa unaona kiongozi wetu hana nia ya mabadiliko kwa kweli zaidi ya mabadiliko yenye nyanja za kifisadi.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  lakini inakuwaje kuna watu wanaruka ruka na vibwebwe na nyimbo za shangwe wakionesha kuridhika na hali iliyopo? Yawezekana sisi ndio tumekosea kwa kushindwa kuona wanachokiona wao?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  tena hapa umesema jambo jingine muhimu, kutoka Mbeya wanajenga uwanja mwingine Mpanda na ameahidi kujenga uwanja mwingine wa kimataifa huko Kigoma, wakati upo uwanja wa Dar wanaongeza na wa Bagamoyo.. labda wenzetu kuna kitu wanakiona ambacho hatukioni..
   
 10. M

  Mutu JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mimi nadhani CCM ana take advantage ya wananchi wanashindwa kuhoji ,wananchi ambao wanaona hali ni sawa tu kama wengi wana mawazo kuwa kama Mungu alikupangia kupata utapata so hawa hawatambui kuwa Mungu anahitaji ufanye jitihada kwanza.
  Kwa misingi hiyo hawaoni kuwa maendeleo yao yanarudishwa nyuma na CCM ,ingekuwa wanaona vinginevyo wasingekuwa wana ruka na kushangilia watu wanaokufanya ukose huduma za msingi kama maji ,umeme,barabara.
   
 11. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  This election u r very sober my friend but I support what u wrote 100%. There is nothing worse than a person who does not know and does not know that he doesn't know and he thinks that he knows... :smile-big: And our current Prez is a typical case study of the above...
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Sep 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wanachokiona wao mzee mwanakijiji ni mianja ya ufisadi wanajua wakijenga viwanja vitatu washapata pesa za kuendesha Chama cha Mafisadi (CCM).
   
 13. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  CCM wanachowaza sio mabadiliko wala maendeleo ya Taifa letu, bali mawazo yao ni kutawala watanzania. Na hiyo wamesisitiza viongozi wao kwa kusema tutatawala hata miaka 100 ijayo.

  CCM wakileta mabadiliko ya kimuundo hawataweza tena kutawala watanzania. Hivyo usiote ndote ya ccm kuleta Mabadiliko Tz.

  Mabadiliko ya kweli ya Tanzania yataletwa na watanzania ambao wameonewa kiasi cha kutosha, wamenyanyaswa kiasi cha kutosha, wamedhulumiwa na kudharauliwa kiasi cha kutosha, wamenyonywa kiasi cha kutosha, wamekandamizwa kiasi cha kutosha. Hawana cha kupoteza bali minyororo yao.

  Mabadiliko ya kweli yatafanywa na Watanzani katika sanduku la kura kwa kuwakataa watawala ambao wamewakandamiza na kuwadharau bila kusikiliza maoni yao tangu uhuru. Watawala ambao wanafikiri wao ndio wanajua kila kitu
   
 14. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kiongozi mkuu wa nchi (sio mtawala mind you) anaweza kuwa chanzo na chachu ya mabadiliko chanja (even hasi) akiamua kwa dhati kufanya hivyo.
  Kwa kweli mimi silioni hilo, wala dalili ya hilo kwa kikwete, chama chake na serikali wanayoiongoza.
  Tumechelewa sana na tunazidi kuburuza miguu kufanya maamuzi ya kueleke kwenye maendeleo ya watu.
  We need changes NOW!!
   
 15. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Muonapo chukizo la uharibifu limesimama......(changanya na za kwako..)
  Nadhani watanzania wataanza kuamini CHADEMA wanachokisema pale ambapo Chama Cha Mafisadi wataanza kutafuta Visa za kwenda kushi ng'ambo maana muda huo nchi itakuwa imenyonywa mpaka imebaki mifupi karibu na kulipuka. Na kipindi hicho si mbali ni katika awamu ijayo endapo watanzania watathubutu kuirudisha CCM madarakani...!

  Lisemwalo lipo, nalo laja...!
   
 16. F

  Froida JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  JK hana utashi wa Kisiasa na hata utashi wa dhamila,mapinduzi ya kweli huwa hayahitaji watu wawili katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa nchi yenye utajiri mkubwa kama huu,kwa kipimi changu ameshindwa katika vigezo vyote muhimu vya kufanikisha kuongeza pato la taifa ambalo lingepunguza matatizo mengi kwa mwananchi na kuboresha maisha yake,Anastahili kupumzika inatosha aende zake salama
   
 17. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #17
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mabidiliko popote Duniani hayaletwi na Watala. Mabadiliko chanya huletwa na wannchi. Tucta wamejaribu. Mabadiliko hayawezi kuletwa na Kikwete. Yeye angependa aweraisi, mke wake wazriri mkuu, Mto makamu wa rais nk.
   
 18. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #18
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,465
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ndiyo maana mada inasema "kuongoza".. siyo "kuleta"...
   
 20. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  CCM imeshakufa siku nyingi, cha kushangaza ni kuona wasomi wanaitetea kwa nguvu zote kwani wasomi wakibadilika vijijini wanawafuata.
   
Loading...