Kikwete anaweza kama Kabila?

GAMBLER

JF-Expert Member
Nov 22, 2009
303
11
1262764475_kabila.jpg

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila
Kinshasa:
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amewafukuza kazi watumishi zaidi wa umma nchini humokatika juhudi zake za kupambana na rushwa, usimamizi mbaya wa matumizi ya fedha katika idara mbalimba nchini humo ikiweno forodha na idara ya utozaji kodi.

Rais Kabila amewafukuza kazi wafanyakazi 119 huku wengine zaidi ya 2,500 kulazimishwa kustaafu.
Mwaka uliopita Rais Kabila aliwafukuza kazi ama kuwastaafisha watumishi wa umma wapatao 1,300 na majaji wapatao 100.
Rais huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amekuwa akipambana kuinua uchumi wa nchi hiyo na kupunguza madeni ya nje.
Rais Kabila anahitaji mapato zaidi kutoka katika miradi ya madini ambayo ndiyo uti wa mgongo wa taifa
 
Thumbs up for the young man!

Huyu kijana kakulia Tanzania, kasoma Tanzania amerithi fikra za uongozi thabiti alizowahi kuziona Tanzania kwa hiyo anaelewa wajibu wake kama Rais wa nchi na wajibu wake kwa wananchi wa nchi anayoiongoza. Hana inda wala ikidi katika kuiga na kufuata nyayo za viongozi thabiti aliowahi kuwaona!
 
Ni somo zuri sana kwa JK. Kijana aliyekulia na kusoma Tanzania anadiriki kufanya maamuzi magumu. JK akiambiwa kuwa anashindwa kufanya maamuzi magumu watu wanapiga kelele. Njii hii bila kuwatimua kazi na kuwafunga baadhi ya watumishi na watendaji serikalini huu ujinga ujinga utaendela. Big Up Kabila..
 
Nasikia hata Kagame pale Rwanda anafanya kazi nzuri ya kufanya maamuzi magumu! Hakuna kesi inayodumu miezi pale Rwanda. Mzembe yeyote ndani ya Serikali hutimuliwa haraka mradi taarifa zimfikie mkuu wa nchi na zithibitishwe kwa kasi ile ile kama ni za kweli ama uongo. Watu hawaachiwi wakapewa muda wa kuvurga ushahidi!
 
Big up Kabila! tunataka na rais wetu aige mfano wako, anadai yeye hana mamlaka ya kuwabana mafisadi...usanii mtupu
 
Big up Kabila! tunataka na rais wetu aige mfano wako, anadai yeye hana mamlaka ya kuwabana mafisadi...usanii mtupu
.. Na yeye ni mkora tu that's why anashindwa kuwabana na hao wakora wengine anajua watatoa siri....
 
Anaweza kwa wafanya kazi wa chini kama hao wa TRA na walimu !!! Ila sidhani kwa wala Rushwa na mafisadi kama anaweza !!

Hali ya uchumi Tanzania imekuwa mbaya mbaya sana.. Jana nilikuwa najaribu kuzungumza na jamaa zangu kuhusu mambo ya kawaida yanayo tuzunguka..

Kwa sasa imeonekana hata biashara ya ukahaba kwa vibinti vidogo vya miaka 16 na 17 imeongezeka sana kutokana na hali ya kipato kuwa ndogo kwa wananchi.!!

Hii ni dalili tosha kabisa kwamba tunaelekea mahala kubaya sana ...No point of return hata iwe je kwa sasa !!!
 
Anaweza kwa wafanya kazi wa chini kama hao wa TRA na walimu !!! Ila sidhani kwa wala Rushwa na mafisadi kama anaweza !!

Hali ya uchumi Tanzania imekuwa mbaya mbaya sana.. Jana nilikuwa najaribu kuzungumza na jamaa zangu kuhusu mambo ya kawaida yanayo tuzunguka..

Kwa sasa imeonekana hata biashara ya ukahaba kwa vibinti vidogo vya miaka 16 na 17 imeongezeka sana kutokana na hali ya kipato kuwa ndogo kwa wananchi.!!

Hii ni dalili tosha kabisa kwamba tunaelekea mahala kubaya sana There is no point of return hata iwe je kwa sasa !!!

Na chama kinachotuongoza ndiyo hicho. Mungu apishe mbali.
 
Rais wetu hawezi full stop

FirstLady1, Kikwete anaweza kuwafukuza watumishi wa umma (na hata wanasiasa kutegemea na madaraka husika)...

Ila tatizo ni kuwa anaweza tu kuwafukuza wale ambao si wanamtandao, na ambao si marafiki au wapambe wa Lowassa au Rostam.
Wapambe & marafiki wa watuhumiwa wa Ufisadi Lowassa na Rostam hawawezi kuguswa na Kikwete.

Hata siku ukisikia cabinet reshuffle kabla ya Uchaguzi, lengo halitakuwa kuboresha utendaji, bali itakuwa ni mafisadi kujipanga kung'ang'ania madaraka zaidi na zaidi.
Ingekuwa anaangalia utendaji, watu kama Shukuru Kawambwa, Sofia Simba, Masha, Ngeleja, Hawa Ghasia, Hussein Mwinyi, Nchimbi wasingekuwa mawaziri. Makamba (Katibu Mkuu CCM) naye siyo.

The most important qualification ya kuteuliwa na JK ni USHKAJI...

Baya zaidi ni katika uchaguzi wa Chipukizi wa CCM. Watoto wadogo miaka 10 hadi 13 wanafundishwa kuhonga na kuhongwa (na viongozi wa UVCCM walikuwa wakisimamia uchaguzi huo, huku wakiwa na maelekezo ya kuwachagua watoto wa vigogo).

Kama kufukuza wasiofaa, JK labda aanze kujifukuza mwenyewe (asigombee)...
 
JK anaouwezo wa kumfukuza yeyote anaetaka kumfukuza. Ila anachokosa ni nia tu.

Mamlaka aliyonayo yanampa uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Inawezekana anahofia kufanya maamuzi magumu halafu akakosea.
 
Hivi kwa miaka minnne hii hamjamchoka tu kumsema JK! hata kuuliza kuwa anaweza? jamani ebu tuangalie upande mwingine.

unafahamu robot wewe??
 
Dakika za majeruhi na awamu ya mwisho atakuwa mbogo sana.....stay tuned....lazima awaadabishe,awabadilikie na mahakamani pia!!!!
 
Dakika za majeruhi na awamu ya mwisho atakuwa mbogo sana.....stay tuned....lazima awaadabishe,awabadilikie na mahakamani pia!!!!

Huu ni utani wa mwaka !

  • Eti tu stay tuned kwani atakuwa mbogo sana - toka lini ukapanda sukuma wiki ukavuna dengu ?
  • Believe this and you can believe anything - remember kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya ?
  • Sikutegemea kuwa hata JF inaweza kuathirika kiasi hiki - hiyo asilimia 70% itatufikisha pabaya.
Watu wengine Bwana !
 
Hivi kwa miaka minnne hii hamjamchoka tu kumsema JK! hata kuuliza kuwa anaweza? jamani ebu tuangalie upande mwingine.

unafahamu robot wewe??
Haa Haaa umenifurahisha sana mkuu.Naifahamu. Juzi nikiwa Ubungo ilipoa ishara ya gari kuanza kuondoka nusura niingonge ya mbele yangu maana kumbe trafik alikuwa yuko pale aaongoza jinsi ilivyokuwa inampendeza.
Kuna mwalimu wangu mwingine alijaribu kunifundisha nadharia ya kuandika program za Robot maana hakuwa hata na moja ya kutuonyesha mfano. Alipoona kazi imekuwa mbaya akarudi Holland alikofanya Phd. Sijamuona tena
 
Back
Top Bottom