Kikwete anatayarisha kuanguka kwa CCM mwaka 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anatayarisha kuanguka kwa CCM mwaka 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngekewa, Oct 27, 2010.

 1. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ama kweli CCM ni chama kinachotegemea"Zidumu fikra za Mwenyekiti". Hivyo CCM wameshapima madhara ya baadae yatakayosababishwa na "ahadi zisizotekelezeka" zinazotolewa na Mwenyekiti wao katika jitihada zake za kuendelea madarakani?

  Ahadi anazotowa JK zinataka kutekelezwa na Serikali na uzoefu umetuonyesha kuwa Serikali yetu haina uwezo na viongozi wenye utashi wa kutekeleza yale yatakayowanufaisha walio wengi. Naamini Kikwete angependa atekeleze yale alioyaahidi mwaka 2005 lakini factors mbili za juu zinamgomba. Angekuwa na uwezo wa kutekeleza ahadi zake asingerejea kutowa ahadi kwa mambo yale yale. Kila anapopita anatowa ahadi ya barabara, maji, elimu, afya na mengine ambayo yeye alishindwa kuyatafutia ufumbuzi na CCM ilishindwa kwa kipindi cha karibu miaka 50 iliyopita.

  Inapaswa kujiuliza huu mwaka wa 2010 baada ya kupita miaka yote hiyo ndiyo umepatikana muarubaini wa kutatuwa matatizo yote hayo? Na kwanini kipindi chote hicho hawakuwa tayari kututatulia matatizo yanayotukabili isipokuwa sasa? JK amekuwa akitembea na kile kinachoitwa"kipete wa kipete" yaani anatembea na utatuzi wa kila shida hivi sasa.Amekuwa na jibu kwa kila tatizo, amekuwa msikivu na kukubali kila ombi la mgombea wa CCM, amekuwa na fedha lukuki katika Coffers za Serikali. WHY ONLY NOW? Mbona tungekwishapiga hatuwa ya maendeleo na watoto wasingekosa elimu , watu tungekuwa na maji safi, afya bora na miundombinu bora kama hiki kipete wa kipete cha JK kingefanyakazi mapema.

  NI kweli kuwa Watanzania ni rahisi kudanganyika lakini tabu za maisha zinawafanya taratibu kujiuliza iwapo wanaowadanganya wanawaona wajinga au vipi? Ninahakika hakuna kitu kitachomzuia JK kurudi madarakani lakini nawatahadharisha CCM kuwa kwanza hawatapata msanii mwengine kama walienae sasa,pili harakati za upinzani mwaka2015 zitapata silaha ya kuimaliza CCM kwa kushindwa kutimiza ahadi zinazoahidiwa sasa kwani nina hakika kwa uongozi wa CCM (ule ule) serikali haiwezi kabisa kupata uwezo wa kutekeleza ahadi lukuki zinazoahidiwa sasa. Wapinzani watawaambia wapiga kura kiwapi mlichoahidiwa? Na tatu wapiga kura watakasirika kuchukuliwa kama watoto na ahadi bila utekelezaji.

  Ole wake CCM na tabia ya zidumu fikra za mwenyekiti. Sijui harakati hizi za ahadi zina organization au ni fikra binafsi. Hongera CCM kwa ushindi wa 2010 utakaoleta kuporomoka mwa 2015!
   
 2. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pumba!!!!!
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  sCRAP!!!
  unapaswa kuliwa ban wewe.
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hata akiwa ndani ya chupa ata....!
   
 5. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  kuna ambao hawajui na hawajui kuwa hawajui basi hao ni wajinga na wapumbavu achana nao nadhani wewe ni kati ya wale ambao hawajui na hawajui kuwa hawajui hivi kuna nini utakachojivunia kuhusu CCM au na wewe ni wale mnao kemea rushwa machoni lakini mioyoni ni wala rushwa au ni kati ya wale wenye vitambi vya 10%
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,076
  Trophy Points: 280
  Mwenyezi Mungu atakinusuru CCM kwa kuhakikisha kinashindwa vibaya chaguzi huu ili kiende kujipanga upya kwa kuifuta kazi kamati kuu ikijumuisha JK, Makamba na Lowassa wote wakitupiwa virago vyao.

  Miaka kumi na tano ijayo ndiyo watarudi madarakani wakiwa wameshika adabu na kutambua nini maana ya imani yao ya sita ya CCM.........."Cheo ni dhamana sitakitumikia cheo changu kwa manufaa yangu binafsi." ..........kama mafisadi ndani ya chama hicho wanavyofanya hivi sasa........
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Hayo mashuzi peleka CCM Forum.
   
 8. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  JamiiForums Message

  mang'ang'a, you do not have permission to access this page. This could be due to one of several reasons:

  1. Your user account may not have sufficient privileges to access this page. Are you trying to edit someone else's post, access administrative features or some other privileged system?
  2. If you are trying to post, the administrator may have disabled your account, or it may be awaiting activation.
  NISAIDIENI, NI KWANINI NINAPATA MSG HII NIKIJARIBU KUFUNGUA BAADHI YA THREADS??


   
Loading...