Kikwete anaposema wanachama wenzake wanamkubali ndo maana hawajajitokeza ni kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anaposema wanachama wenzake wanamkubali ndo maana hawajajitokeza ni kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kichenchele, Jul 2, 2010.

 1. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Habari yenu wadau a.k.a great thinkers wa JF, naomba tujadili kauli za kikwete alizozitoa jana wakati anarudisha form zake za kuomba awamu nyingine tena ya miaka 5. nilisikiliza kwa umakini mkubwa sana japo nilishikwa na hasira pale alipofunguwa kinywa chake na kusema, wanachama wenzake wa CCM wanamkubali ndiyo maana hawajajitokeza kuchukuwa form za kuwania kuteuliwa kuwania Urais, nafikiri aliongea hivi ili kuwatukana wale ambao walikuwa na nia ya kutaka kuonyesha ushindani mojawapo akiwepo Mh. John Shibuda, alijuwa hata kama wangejitokeza wangenyongewa baharini maana utaratibu wao ni kuhakikisha rais anakaa miaka 10 madarakani sasa ni nani mwenye moyo wa chuma aweze kupinga utaratibu huu wa kisultani? mtu hata akiboronga ni lazima amalize miaka yake 10? hiki ni kichekesho, taifa changa kama hili linahitaji watu makini. Anaendelea kusema; apewe miaka mingine 5 ili aweze kuendeleza mazuri aliyoyafanya, ikiwa ni pamoja na kuondoa umasikini, hivi anatumia takwimu za mwaka gani ambazo hazina kipengele kisemacho umasikini nchini Tanzania umeongezeka kuliko awamu nyingine zilizo mtangulia? Hivi hajui watanzania katika uongozi wake wamekuwa fukara kupindukia? Anatueleza nini wakati tofauti ya wenye nacho na wasio nacho inazidi kuwa kubwa kiasi cha kutisha,katika Kiongozi makini na mwenye uchungu ,mzalendo na mtenda haki ni yule atowaye maamuzi mazito kwenye mambo mazito.
   
Loading...