Kikwete anaongoza nchi kinafki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anaongoza nchi kinafki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anyisile Obheli, May 4, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Ni ukweli usiyopingika kwamba raisi wetu, analiongoza taifa kimajungu,
  Unafki, na uzandiki, tangu nimeanza kumfuatilia na staili ya utendaji,
  Na utatuzi wa majukumu yanayolikabili taifa letu, siyo uongo nikisema kuwa
  Mengi yameonekana kumzidi umri wa fikra na busara juu ya nini akifanye,
  Ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.

  Hivi majuzi ametoa mpya ambayo mimi kwa upeo wangu huu nilionao,
  Naona kama ni kuchanganyikiwa, kwa bwana raisi, kama si kuishiwa hoja,
  Kwa kitendo chake cha kujifanya anaitisha mkutano wa kuongea na wazee wa
  Jiji la Dar es Salaama, cha ajabu ni kwamba, nilitegemea kuwa angetumia
  Muda huo zaidi kuzungumza nao jinsi ya nini amepanga kukifanya kwa
  Wazee wetu ambao wamekuwa wakiidai serikali ya CCM kuwalipa mafao
  Yao ya iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Lakini amekwenda kuweka chunvi kwenye chai badala ya sukari, kwanini
  Badala ya kuzungumzia maswala yanayo wahusu hao wazee, akatumia muda huo
  Kufoka na kuwapiga mkwara wafanyakazi wanaojiandaa kufanya mgomo, na kudai
  Kuwa hiyo haimbabaishi, hata kama wanafanya hivyo kushinikiza ili
  Atatue matatizo yao kabla ya uchaguzi kufanyika na kudai, kwa jinsi hiyo hata
  Kura zao hazitaki. Hebu tupime hapa ni kweli kiongozi wa jamii ya watu, anweza kutoa maneno mabovu kama haya? Mbona hakwenda kuwavaa na kuwahutubia wahusika?

  Hiyo siyo jeuri bali ni kuchanganyikiwa na majukumu, ningelimuona mwenye
  Ujasiri kama maneno hayo angekwenda kuwahutubia wafanyakazi kwenye uwanja wa
  Uhuru wakati wa kusherehekea sikukuu ya Mei Mosi ambayo inawahusu wafanya
  Kazi duniani kote. Huu ni uzandiki na ujuha wa bwana raisi wetu.

  Imeonesha kuwa kabineti nzima ya Ikulu, raisi, na washauri wote ni wapungufu wa hekima, busara na uelewa wa kusoma alama za nyakati.
  Nimemsikia mara nyingi bwana raisi kutokana na kushindwa kuwa mwenye maarifa
  Miongo mwa wanajamii, akiropoka mambo ambayo, baadaye humuabisha, kama
  Pale kipindi fulani alipostuliwa juu ya mawaziri wake mafisadi, akadai ‘kelele za mlango haziwezi kumzuia mwenye nyumba kuingia ndani’ lakini ni nini kilifuata baadaye? Kama si aibu kwake? Leo tena anafanya jambo ambalo hata mtu asiyekuwa na elimu kichwani basi asingelifanya.

  Kwa mtazamo wangu naona kama ni raisi wa kwanza duniani katika maraisi ninawaowajua, kuweza kuongoe mbovu kiasi hiki, hapo si maswala ya kula wala nini, kikubwa ni kutatua majukumu yanamkabiri yeye kama kiongozi wa nchi na si vinginevyo.
  Hata ukiondoka madarakani uwe umetimiza japo punje ya ulezi ya majukumu yako.
  Mi naona hata baadhi ya wazee wenye hekima na busara zao walikkuwa wakikushangaa kijana wao jinsi unavyo bwabwaja, na kituko chako cha kwenda kufungua bucha ya
  Nyama ya nguruwe karibu na msikiti,
   
 2. G

  Godwine JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kama akiwashukia mafisadi kwa mkwara kama wa jana basi tutafurahi
  lakini kwa wafanyakazi sioni sababu ya kugombana nao
   
 3. G

  Godwine JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kama akiwashukia mafisadi kwa mkwara kama wa jana basi tutafurahi
  lakini kwa wafanyakazi sioni sababu ya kugombana nao
   
 4. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wengi wa watanzania wamejaa chuki binafsi na wivu wa madaraka including mwandishi wa habari hii,nilitarajia ungemsifu JK kwa ujasiri wa kuwakumbusha watz majukumu yao sasa unakuja na ngonjera oo Jk kafanya hivi katenda vile!Acha chuki ili moyo wako ufunguke na kuweza kufikia kilele cha maendeleo,bwana Yesu anawachukia sana wenye chuki kama wewe,jirekebishe tunataka maendeleo na si mapambano!
   
 5. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sawa mkuu lakini muono wako si lazima uwe wa mwingine, tambua kuwa
  yupo mtu aneona kuwa siku zote ni sawa, na mwingine anaona tofauti
  baina ya siku na siku, sasa wewe ndiyo umeona kuwa kuwa jamaa ni jasiri
  na kuona mimi nimekuja na ngonjera sawa, yawezekana uonavyo sivyo nionavyo
  Kikwete siyo new product kwa wenye kumfuatilia

  siyo siri ameaprove failure kwa kipindi chake chote cha uongozi maana hajafikia hata
  punje ya sera na ahadi za chama chake, sasa si rahisi mtu unayeishi jikoni kwake kama
  wewe ukayaona hayo
  sitakushangaa mtu kumsifu yeye kwa ujasiri wa kiini macho auoneshao,
  aliwaambia maisha bora kwa kila mtanzania, bila ya kueleza yata kujaje
  wajinga walimpigia makofi, lakini waelevu walitamani hata nafasi ya kumwuliza
  yatakuja kwa njia gani? ndipo wampigie makofi,,, siwezi jua wewe uko katika upande gani hapo,,,,

  narudia tena Kikwete anaongoza nchi kinafki
   
 6. F

  FM JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya bwana, na wewe unaendeleza vitisho?? Ukweli utabaki kuwa kuweli daima
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Deep Green, Kagoda, Maremeta, Vingunguti Gold Refinery(Mwanachi Gold) Chenge Rada, RA&EL Richmond, KR TICTS nk
   
 8. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kiongozi wala usipate taabu ya kuumiza kichwa juu ya hawa watu wengine hapa ni watoto wa JK, wengine ni marafiki zake, wengine ni ndigu zake, wengine ni marafiki wa watoto wake basi ilimradi tu wanalink naye wewe unategemea nini? Hawawezi kuuona udhaifu wake. Jamaa ni bonge moja la actor na anajua sana kushika watu masikio. Mi nashangaa kwenda kuongea na wazee kila siku kwanini siku moja asichague hotuba kama hizi akazipige pale UDSM? Hizi sio zama za Nyerere ambapo wazee wanajua kila kitu hizi ni zama mpya za uelewa wa mambo sio desturi ya mambo.
   
Loading...