Kikwete anajua Pinda hajui kilichopo uamiaji… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anajua Pinda hajui kilichopo uamiaji…

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KUN, Oct 11, 2012.

 1. KUN

  KUN JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wachina wanazidikushika kasi hapa nchini, wengine wakiwa na sifa za kufanya kazi hapa nchiniwengine hawana kabisa, ninavosema hawana ni hawana uwezo sababu nimefanya naokazi.
  Sio wachinatu hata wageni wengine wanazidi kuingia nchini na kuteka soko la ajira na sisivijana tunakosa hizo fursa wakati uwezo wa kufanya kazi tunao.
  Kikwete:
  Kikweteakiwa kwenye sherehe za sikukuu ya mei mosi kule songea mwaka juzi alinukuliwaakisema kuwa sisi watanzania tunakosa kazi kwenye taasisi binafsi kwa sababu ya“UAMIAJI” akilenga kuwa uamiaji wanatoa vibari vya kuishi na kufanya kazi kwawageni hata ambao hawana sifa za kufanya kazi na hata ambao wanazo hizo sifaunakuta hapa nyumbani hao wataalamu tunao wa kuweza kuziba hizo nafasi. (Kikwetealikuwa sahihi)

  Liwalo na Liwe:
  Akiwaa bungeni(sikumbuki ni kiako gani na ni nani alimuuliza swali lakini ilikuwa 2011,kilikuwa kipindi cha maswali ya papo hapo) nachokumbuka aliulizwa swali na mmojawa wabunge wa upinzani, Mbunge huyu alitaka kujua serikali inampango gani wakuwahahakikishia vijana wa kitanzania ajira kwenye taasisi binafsi ambazozinaonekana wamejaa wageni….??
  Majibu yaPinda: anasema tatizo lipo kwetu sisi watanzania, tukiajiriwa kwenye hizitaasisi tunakuwa na visingizio vingi hasa pale tunapokuwa na matatizo madogomadogo ndo mana hatuajiriwi. Utaskia mtu ansema mara ooh mjomba anumwa naombaruhusa, mara mtoto wa shangazi anaolewa naomba ruhusa, mara ooh bibi yangukijijini kafariki naomba ruhusa nikamzike. Pinda akakonkludi hivi, ili mwajirikukwepa huo usumbusu wa watanzania kuomba ruhusa mara kwa mara kwa mwajiri ndomaana wanaamua kuja na watu wao kutoka huko kwao kama wafanyavyo wachina. akawa ameshauri watanzania tubadilike..
  Hapa Pinda alichemka na alipotosha ukweli kuhusu hili jambo..

  KwaniniKikwete alikuwa Sahihi japo ameshindwa kutatua hili tatizo? Najua ameshindwakwa sababu ya “UDHAIFU”
  Nimeona kibaricha mgeni mmoja amabaye yupo hapa nchini tangu 2010 akifanya kazi za ujenzi wamajengo na barabara ambaye hana sifa hata kidogo. Kibari kilitolewa na UAMIAJItarehe 30 SEP 2010, hiki kibari kimesainiwa na Director of Immigration servicesna kina namba NO. 095093 DN. 617395 & EP 2107/10.
  Kwanini nasema hana sifa?
  Kwenye hiihati kipengere (b) Nanukuu..The holder shall not engage in any employment,trade, business or profession other than PLASTERMANAGER.
  Swali kwaKikwete, Pinda na Uamiaji, Hivi kweli sisi watanzania hatuwezi kusimamia plaster? (wanaiita Lipu kwa Kiswahili).

  Ukombozi unakaribia.......2015...................

   
 2. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bado unamtegemea JK. Mfuate Canada utamkuta akikotwa na wazungu. Ukimkosa huko nenda sijui wapi kule kwenye vibebembea. Ukimkosa huko nenda Beigin, New York, Washngton DC na kwingineko. Wewe tafuta tu hadi umfikie atakupa majibu. Mbona hao wachina wasiende Kenya, Rwanda, Uganda, na kwingineko? Kama shamba ni la bibi kwa nini wasije wakajivunia kile kilichobaki?
   
 3. B

  Bijou JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Watanzania Kiswahili bado sana ni Uhamiaji na SI ulivyoandika
   
 4. KUN

  KUN JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana kwa kuliona hilo! Lakini Lengo langu lilikuwa kufikisha ujumbe nilio nao, na nahisi umenielewa, pili kutojua kishwahili si tatizo langu ni serikali yako na mifumo yake mibovu ndo imesababisha haya yoye kwa sababu 2.

  1. nimezaliwa kijijini, kule nilikuwa natumia lugha ya kabila langu mpaka naenda shule, bado nilivofika shule ya msingi niliendelea kutumia lugha hiyo ya kabila langu japo lugha ya kufundishia ilikuwa kishwahili kwa masomo yote tisa isipokuwa English, kuanzia Hisabati, kiswahili, jiografia, siasa/uraia, sayansi, sayansi kimu, elimu dhidi ya ukimwi/EDU, sayansi kilimo na Dini hapa nilikuwa na nafasi ya kukijua vizuri kiswahili kwa sababu masomo mengi nilijifunza kupitia kiswahili, tatizo la serikali yako ni hawa walimu nilioletewa kunifundisha shule ya msingi.....walikuwa ni wa hapahapa kijijini kwetu, tukiwa shuleni ama mtaani Lugha yetu ni ile ile kibantu hata wanafunzi wenzangu na hawa hawa wa mtaani kwetu na ndicho kinachokuja kutokea kwenye hizi shule za kata.....lakini ningeletewa mwalimu kutoka nyanda za juu kusini nahisi habari ingekuwa nyingne mda wote tungeongea kiswahili na ningeweza kuimudu hii lugha kuanzia kuandika mpaka kuongea....

  2. Nilibahatika kuendelea na shule ya sekondari, na kwa kuwa nilijua kiswahili ndo lugha ya taifa na me binfasi najivunia kiswahili japo sikijui vizuri mambo yalikuwa kinyume na hapo juu...sekondari somo moja tu ndo kishwahili mengne ni lugha ya kigeni....hivi kweli Bijou ntajua kiswahili kweli katika mazingira haya? Serikali ingepitisha uamzi wa kabadilisha mitaala yote ya sekondari na vyuo kuwa Kiswahili naamini ningekuwa mtaalamu wa hii Lugha...

  kwa kumalizia, hata haya niliyoyaandika hapa ni kwa kiswahili lakini bado naamini nimekosea kwa sababu kiswahili sikijui vizuri.   
Loading...