Elections 2010 Kikwete ana washabiki wengi sijui ni kwanini

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
mbali na wananchi wa tz kuwa katika shida kubwa katika kipindi cha kwanza cha kikwete lakini ni umati mkubwa ulijitokeza jana kumuunga mkono mjini morogoro , sijui ni kwanini watu wamefurahisha na yeye anavyoonekana bila ya sera au nini wanachokiona ambacho ni kikubwa toka kwake.
 
Ndio ujue kwanini TZ hatuendelei? Ushabiki wa kijinga. Wengi wanamwita JK kiboko, kwa lipi? Matokeo ya kutawaliwa na CCM kwa muda mrefu, watu wanabadilika kuwa kondoo wa kupelekwa pelekwa. Mimi simo. Sijawahi kumshabikia JK katika maisha yangu kwani ukimpima unajua wazi hawezi uongozi hivyo sikko tayari kumunga mkono asiyeweza kuongoza hata darasa.
 
Its all about being sentimental and emotional. Ngoma ya leo inakufanya usahau kuwa wahitaji kula kesho!
 
mbali na wananchi wa tz kuwa katika shida kubwa katika kipindi cha kwanza cha kikwete lakini ni umati mkubwa ulijitokeza jana kumuunga mkono mjini morogoro , sijui ni kwanini watu wamefurahisha na yeye anavyoonekana bila ya sera au nini wanachokiona ambacho ni kikubwa toka kwake.

Mbona alishasema wanafuata upepo siku nyingi sana mkuu, upepo na shekhe Yahya anasaidia pia ndo mkuu wa nchi
 
Usishangae ndugu hao jamaa wanaompokea, hiyo ni hula tu ya watz kuona kwenda kuwatazama viongozi ni jambo la maana. Lakini pia lazima ujue kuwa duniani werevu ni wachache kuliko mbumbumbu!!!!!
 
wapumbavu ni mtaji wa mafisadi,
na wengine wamelewa mvinyo aina ya CCM,
mvinyo huu ukinywa wala hujisikii maumivu hata ukiburuzwa kwenye michongoma,
 
Watanzania hawajafahamu kwamba hawa watawala wanahakikisha kwamba hakuna hatua ya maendeleo inayofikiwa ili kutumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa siasa.
mwenye akili na afahamu.
 
daima nimeamini kwamba hakuna ukombozi wa kweli bila jamii kusumbuka nadhani ni zamu ya watanzania kusumbuka ili baadae watafute ukombozi wao
 
mbali na wananchi wa tz kuwa katika shida kubwa katika kipindi cha kwanza cha kikwete lakini ni umati mkubwa ulijitokeza jana kumuunga mkono mjini morogoro , sijui ni kwanini watu wamefurahisha na yeye anavyoonekana bila ya sera au nini wanachokiona ambacho ni kikubwa toka kwake.

Watu wengi kujitokeza haimaanishi wote wanakukubali ndiyo maana hata kibaka akishikwa mtaani na kupewa kichapo umati wa watu hukusanyika kumuona alivyopata kichapo au alivyochomwa moto. Tusiangalie wingi wa watu na kukubalika kwani hata CCM waliisha wahi sema kuwa wananchi wengi wanahudhuria mikutano ya CHADEMA kuona helikopta pia wakasahau kuwa na wao hutumbuiza kwa muziki wa Komba huvyo watu hawana budi kujivinjari. Leo hii likitokea JOKA kubwa likawa katikati ya jiji kila mtu atataka kuliona japo anajua kuwa joka hilo ni adui kwani huuma na hata kuua.
 
Nadhani kipindi cha uongozi wa JK, wanachi wamekuwa huru zaidi kwenye kutoa maoni yao, kuliko vipindi kilichopita cha mheshimiwa sana che Mkapa.
 
Nadhani kipindi cha uongozi wa JK, wanachi wamekuwa huru zaidi kwenye kutoa maoni yao, kuliko vipindi kilichopita cha mheshimiwa sana che Mkapa.

Mkuu hii ni bigest credit ambayo hata mimi ninamkubali JK kwa hili. Na kuruhusu watu ku-vent ni kitu muhimu sana kwa usalama wa Taifa na kukua kwa demokrasia, mara nyingi anaye umia ndani kwa ndani huwa na reaction mbaya sana pindi apatapo chance.
 
Wakuu ina maana bongo uhuru wa mwananchi kutoa maoni yake unatolewa na Rais?
 
Wakuu ina maana bongo uhuru wa mwananchi kutoa maoni yake unatolewa na Rais?

Mkuu nafikiri labda huenda huijui bongo au siku nyingi hujawa bongo. Uhuru wa kutoa mawazo hautolewi na rais kwani ni haki ya kila raia kikatiba, ila ukiangalia watawala waliotangulia kabla ya JK walikuwa wanauminya uhuru huo kwa makusudi, ama kwa kutisha watu kutumia TISS au hata kuwatoesha kabisa. Nakumbuka wakati wa Nyerere mimi binafsi wazazi wangu walikuwa wananitahadharisha kuongea mambo ya kuisema serikali kwani mashushushu walikuwa everywhere kwa lengo moja tu kunyamazisha watu.

Ninakuhakikishia kuwa madudu mengi ya kuiibia serikali hayakuanza leo ila kulikuwa hakuna uwazi wa kuweka mambo hadharani na kwa CCM, utakumbuka yaliyompata Horace Kolimba baada ya kutamka hadharani kuwa "CCM Imepoteza muelekeo" leo hii ni wana-CCM wangapi ukiacha wananchi walioikosoa CCM wazi wazi na wanadunda?. Hili ninasema kuwa JK amekuwa mvumilivu sana kwa wakosoaji wa serikali. katika Tanzania ya kidikteta anaweza kufanya lolote, mfano mzuri ni TUCTA.
 
JK ana mvutoo kwenyee jamii ya kitanzaniaa....

Mchonga alishawaambia wabongo msimuangalie mtu anavyocheka, kama mnampenda mtu kwa sababu ya anavyocheka mualikeni mkanywe naye chai, sio kumpa urais, wabongo wagumu kuelewa somo.

Halafu wengi wetu tuko overly passive, tunaona kama hatuna control na situation, na mtu kama Kikwete akishapitishwa na CCM mwananchi wa kawaida kumpinga anaona ni kama kujitafutia ugonjwa wa moyo tu, after all Marijani Rajab, jabali wetu wa muziki, alishatuambia "Kula ugali wako ukalale" katika "Sikia Mambo" kwa hiyo hata wale wachache wenye mwanga kidogo wanaanza ku justify, wanatafuta kitu kimoja hapa na pale na kusema "lakini amefanya hiki na kile" huku overall trend ya nchi ni mbaya ajabu.

Wewe nchi illiteracy rate inafukuza 30% saa hizi (tulikuwa na literacy rates in the 90% under Nyerere, one of the leading African countries, mpaka vibabu na vibibi vilipelekwa elimu ya watu wazima).Nchi haina civil society ya kusema, kila mtu anaganga njaa, hamna press ya kusema, hamna trade unions za kusema hiyo opposition ndiyo kabisaa usinivunje mbavu.

Unategemea ni kwa nini JK asiwe popular? JK hata akijikojolea kwenye podium wakati anatoa speech, anaendelea na kuchukua urais vizuri tu.
 
Ndio ujue kwanini TZ hatuendelei? Ushabiki wa kijinga. Wengi wanamwita JK kiboko, kwa lipi? Matokeo ya kutawaliwa na CCM kwa muda mrefu, watu wanabadilika kuwa kondoo wa kupelekwa pelekwa. Mimi simo. Sijawahi kumshabikia JK katika maisha yangu kwani ukimpima unajua wazi hawezi uongozi hivyo sikko tayari kumunga mkono asiyeweza kuongoza hata darasa.

Hata hapa kaangalie alivyopigiwa debe katika thread ya Marilyn Mashiba sijui kwa kikubwa kipi alichokifanya. Mitanzania ndivyo ilivyo!
 
lakini wachangiaji wengine wanatumia pointi ya kuwa wananchi wetu hawana elimu lakini cha kushangaza wanachuo wa UDOM nao walikuwa kwenye mkumbo wa kujianika juani kumshangilia kikwete mbaya zaidi wanachuo hawa ambao wanalalamikia bodi ya mikopo kutowapa pesa ya kutosha na wanajiita watoto wa wakulima walimchangia kikwete mamilioni ya kuchukua fomu na kufanya kampeni hapa wajumbe suala hili mnalionaje?
 
Back
Top Bottom