Kikwete amwapisha Gen. Ndomba; Awapandisha wengine karibu 40! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amwapisha Gen. Ndomba; Awapandisha wengine karibu 40!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by figganigga, Sep 26, 2012.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,613
  Trophy Points: 280
  Rais wa Tanzania dr. Jakaya Kikwete amemuapisha ruteni generali Samwel Albert Ndomba kuchukua nafasi ya aliyekuwa mnadhimu mkuu wa jeshi A.A.Shimbo aliye fikisha umri wa kusitafu wa miaka 60. Mwingine aliye apishwa ni Rafael Muhuga Mgoya atakaye kuwa mkuu wa utawala wa mafunzo wa JKT.
  Ni hayo tu. mia
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,836
  Trophy Points: 280
  Kila la kheri!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu @figgganigga hii habari tulishaisoma kitambo ebu peruzi peruzi utakutana nayo.
   
 4. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,366
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  Ngongo kilichoandikwa humu siku zilizopita ni kuwa hao wanajeshi waliteuliwa na alichoandika figganigga hapa leo ndio wanaapishwa rasmi ikulu. Kwa hiyo nadhani ungepaswa kutofautisha kati ya kuteuliwa na kuapishwa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Mkuu umerekebisha tabia ya watu humu kukurupuka kama huyu Ngongo asante Arushaone
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  JUMATANO, SEPTEMBA 26, 2012 10:56 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

  RAIS Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, amewapandisha vyeo maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kuanzia juzi. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana, ilisema vyeo vipya ni pamoja na cheo kimoja cha Luteni Jenerali, Meja Jenerali 15 na Brigedia Jenerali 33.

  Akizungumza makao makuu ya Jeshi muda mfupi kabla ya kuwavisha vyeo vipya maafisa hao, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange alisema, “Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete, alimpandisha cheo Meja Jenerali Samuel Ndomba kuwa Luteni Jenerali kuanzia juzi.

  Wakati huo huo, Rais amemteua Luteni Jenerali Samuel Ndomba, kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kushika nafasi iliyoachwa wazi, baada ya Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo kustaafu utumishi kwa mujibu wa sheria.

  Kwa mujibu wa Kanuni na Sheria za Majeshi katika Juzuu la Kwanza (Utawala), Jenerali Mwamunyange alimvisha cheo cha Luteni Jenerali, Meja Jenerali Ndomba kwa niaba ya Rais.

  Kabla ya uteuzi huo mpya, Luteni Jenerali Ndomba alikuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

  Katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Jeshi, Jenerali Mwamunyange alisema, Rais Kikwete alimpandisha cheo Brigedia Jenerali Rafael Muhuga, kuwa Meja Jenerali kuanzia Septemba 21, mwaka huu na kumteua kuwa mkuu mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

  Kabla ya madaraka mapya hayo, Meja Jenerali Rafael Muhuga, alikuwa Mkuu wa Utawala wa Jeshi hilo.

  Jenerali Mwamunyange alimvisha cheo hicho kipya kwa niaba ya amiri jeshi mkuu.

  Wakati huo huo, makamanda wengine waliopandishwa vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali, miongoni mwao wamo maafisa wakuu wa kike, Meja Jenerali Grace Mwakipunda, ambaye kwa sasa ni Kaimu Mkuu wa Utumishi jeshini na Meja Jenerali Lilian Philimon Kingazi, ambaye ni Mkurugenzi wa Utumishi jeshini, Meja Jenenali Farah Mohamed, Meja Jenerali Kevin George Msemwa, Meja Jenerali Patrick Peter Mlowezi, Meja Jenerali Charles Mayunga Jitenga, Meja Jenerali Charles Nobat Mzanila na Meja Jenerali Daniel Chacha Igoti.

  Makamanda wengine, ni Meja Jenerali Vicent Kilihongo Mritaba, Meja Jenerali Ipanda Hussein Ipanda, Meja Jenerali Adam Simon Mwabulanga, Meja Jenerali Ezekiel Elias Kyunga, Meja Jenerali Projest Anatory Rwegasira na Meja Jenerali Juma Furaha Kapwani.

  Pia aliwavalisha vyeo vipya makamanda 33, waliokuwa na cheo cha Kanali kuwa Brigedia Jenerali, makamanda hao wa ngazi za juu ni pamoja na Brigedia Jenerali Pellegrin Jacob Mrope.

  wengine ni Brigedia Jenerali Ryakitimbo Magige Ryakitimbo, Brigedia Jenerali Mimy Mrisho Abdallah, Brigedia Jenerali John Mwita Chacha, Brigedia Jenerali Ezira Wilson Ndimbwambo, Brigedia Jenerali Augostino Simule Gailanga, Brigedia Jenerali Gadence Salim Milanzi, Brigedia Jenerali Masumbuko Mashembele Mndeme, Brigedia Jenerali Daniel Laswai, Brigedia Jenerali Sarah Thomas Rwambali, Brigedia Jenerali Mathew Mayela Sukambi, Brigedia Jenerali Narcis Chande Lubamba, Brigedia Jenerali Mwapipo Kyalaliko, Brigedia Jenerali OS Mateka, Brigedia Jenerali Jairo Mwaipopo Mwaseba, Brigedia Jenerali Abdullah Athuman Mwenjudi, Brigedia Jenerali Cosmas Frances Kayombo, Brigedia Jenerali Honoratus Pascal Lyamba, Brigedia Jenerali Ramadhani Abdi Kimweri, Brigedia Jenerali Nicodem Elias Mwangela, Brigedia Jenerali Abbas Hussein Mnyani, Brigedia Jenerali RA Rukya, Brigedia Jenerali Elias Nicano Athanas.

  Wengine ni Brigedia Jenerali Fabiani Edward Mangore, Brigedia Jenerali George Ndika Mashamba, Brigedia Jenerali Zoma Matiku Kongo, Brigeia Jenerali Harison Joseph Masebo, Brigedia Jenerali Paul Peter Masao, Brigedia Jenerali Clemence kahama, Brigedia Jenerali Jacob Hassan Mohamed, Brigedia Jenerali Mbazi Abdul Msuya, Brigedia Jenerali Alfred Fabian kapinga na Brigedia Jenerali George Wiliam Ingrim.

  Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya makamanda wenzake wa ngazi za juu waliopandishwa vyeo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, alimweleza Mkuu wa Majeshi kwa pamoja, wanatambua majukumu yaliyo mbele yao na aliahidi watayatekeleza majukumu mapya kikamilifu.

  Alisema, “tutaendelea kumwomba Mwenyezi Mungu, atupe busara na hekimu ya hali ya juu katika kutekeleza majukumu yetu mapya,” alisema Luteni Jenerali Ndomba, kwa niaba ya wenzake alimwomba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi kufikisha shukurani na salamu zao za dhati kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu kwa imani aliyokuwa nayo kwao na hatimaye kuwapandisha vyeo na kuwapa madaraka mapya.

  Jenerali Mwamunyange aliwahakikishia makamanda hao kuwa, atamfikishia Rais na Amiri Jeshi Mkuu salamu za dhati kama walivyomtuma kwake.

  Akiwaasa baada ya kuwavisha vyeo vipya, Jenerali Mwamunyange alisema, tukio la kupandishwa vyeo lilikuwa ni tukio muhimu kwa Taifa, kwa ajili ya kuendeleza ulinzi wa nchi na uhai wa Taifa la Tanzania.

  Alisema, “Ninyi sasa nyote ni sehemu kamili ya uongozi wa jeshi letu, mnatakiwa kuelewa uongozi wa jeshi hauishii makao makuu ya jeshi, bali ni kwa ngazi mbalimbali kama mnazoshika sasa,” alisema.

  Jenerali Mwamunyange, alisema uongozi imara na ufanisi jeshini unachangia na baadhi ya mambo, ikiwa ni pamoja na maafisa kufanya kozi, mafunzo na mazoezi ya mara kwa mara ili kuwajengea uwezo na uzoefu viongozi watendaji.

   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nilisoma humu ndani ya Jamii Forums - Mmoja wetu akisema kuna Wanajeshi Wanaandamana wanataka POSHO Na Mishahara kuongezwa...

  RAIS KUFANYA HIMA na kuongeza VYEO ni Sababu ya kuzuia hiyo Karaha ???
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  anajikosha maana anateua JKT kuongoza JWTZ siwahi ona jeshi kama la Tanzania tangu lini wahitimu wa Jk wakaongoza JW? ni tanzania pekee yenye maajabu kama haya tusubiri ndio maana uasi kwa nchi yetu unaweza fanyika haraka sana na kwa muda mfupi kama mnavyo ona kwa sasa information nyingi za siri zinapatiakana mitaani kama hakuna usalaama wa taifa kutokana na uteuzi usiozingatia masirahi ya taifa.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Wanajiandaa kwa vita, pia Kikwete anawapoza machungu ya uongozi mbaya wasije kumgeuka.
   
 10. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza"
  Kuna afisa usalama aliwahi kuniambia kuwa,Kuongoza JKT kunahitaji mtu mwadilifu sana, kwani JKT ina vikosi vingi hata kuliko JWTZ, kwahiyo JKT ikihasi inaweza leta matatizo mingi.

  Kutokana na uteuzi huu kuna mjeshi ameniambia hata wao wameshtushwa na uteuzi huu,kwani hao jamaa wa juu mf;ma major General wanatakiwa kuwa makao makuu, hivyo serikali inaingia gharama za bure hawafanyi kazi yoyote.Na alisema inaelekea kama vile mh. amewatunuku wale wa kizazi chake ili wamalizie ustahafu wao vizuri.

  Kwa mujibu wa mjeshi huyo makao makuu ikibaki na hao ma major gen wanne, wanatosha wengine wabaki huku chini wafanye kazi.

  Tatizo hakuna Tundu lissu wa jeshi.Hizi teuzi zimekaa kirafiki zaidi.
   
 11. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Fanya utafiti, JKT ni tawi la JWTZ......miaka yote vingozi wa JKT wanatoka jeshini

   
 12. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
 13. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Umeanza vizuri, ukapotea njiani.......JKT ni tawi la JWTZ, wakufunzi wote wa JKT JWTZ, hata Mwanyange alitokea JKT, kwa sasa nadhani ndio mfumo walioamua kuufuata, maana ukitoka JKT, unakwenda Unahimu, kisha ndio CDF

   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  I think it was about time
   
 15. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mabadiliko ni lazima, kwenye jeshi hupandishwi jeo kama huna kazi nacho, ndio maana wapandishwa vyeo na kuteuliwa, ukiona watu wanapandishwa vyeo ujue kuna vacancy nyingi, watakuwa wamestafuu, n.k
   
 16. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sasa sijui kama kule kwetu Namanyere tumeambulia nini maana naona majina ya Pwani pwani, Tarime, Mbeya na Kagera kwingine sijaona.Samahani kwa kuwa mtu wa kikanda ingawa najua haitakiwi
   
 17. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tuviheshimu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kama JWTZ na JKT lakini tuwadharau polisi kwa sababu polisi wanatumiwa na CCM kama leso ya kujifutia jasho ikichafuka inatupwa!
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Sep 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu, jitahidi kusoma historia ya nchi yetu itakusaidia sana kuyajua mambo vizuri.
   
 19. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #19
  Sep 26, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Haisaidii kwasababu hao wachini ndio wengi halafu wanataabika, atajuta kugombea Urais
   
 20. p

  pilau JF-Expert Member

  #20
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 16, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  ............. Ni matumaini yangu kuwa wakuu hawa wote ni safi na kwamba hakuna aliyechakachua vyeti, maana kulikuwa na sakata la VYETI na Kwamba hawa wote wamepitia katika michakato mbalimbali ambayo ni halali kabla ya uteuzi ... pia ninaamini sitasikia mambo kama ya MAJAJI kuwa wengine hawana sifa za kuwa majaji
   
Loading...