Kikwete amwalika Rais Malawi kuzuru Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amwalika Rais Malawi kuzuru Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 19, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 18 August 2012 11:59

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Mwandishi Wetu

  KATIKA kile kinachoonekana kudumisha uhusiano baina ya nchi zao, Rais Jakaya Kikwete amemwalika Rais wa Malawi, Joyce Banda kufanya ziara ya kiserikali nchini.Hayo yalielezwa juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Malawi, Ephraim Chiume katika mahojiano na Shirika la Habari la Malawi (Mana), huko Maputo, Msumbiji.


  Mwaliko huo umekuja wiki chache tangu kusambaa kwa taarifa kuhusu uwezekano wa nchi hizo mbili kuingia vitani kutokana na mzozo wa mpaka kwenye Ziwa Nyasa.Mzozo huo unatokana na msimamo wa Tanzania kuwa mpaka baina ya nchi hizo upo katikati ya ziwa hilo wakati Malawi inadai kuwa eneo lote la maji ni halali ya nchi hiyo.

  Mvutano huo ulianza miezi michache iliyopita baada ya Malawi kuanza kufanya utafiti juu ya uwezekano wa kuchimba mafuta eneo ambalo Tanzania inadai lipo ndani ya mipaka yake na kuamuru kazi hiyo isimamishwe mara moja.


  Chiume alisema ziara ya Rais Banda nchini inatarajia kufanyika hivi karibuni akisisitiza kuwa hayo ni matunda ya uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo ambazo wananchi wake wamekuwa wakilitumia ziwa hilo pasipo kuwekeana vikwazo na wamekuwa wakitegemeana kimaisha.


  Licha ya ziara hiyo, Chiume alisema marais hao wawili pia walitarajiwa kuteta faragha kabla ya mkutano wa wakuu wa Nchi za Jumuia ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ilioanza Maputo jana.


  Chiume alitoa maelezo hayo muda mfupi baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe huko Maputo juzi kuzungumzia juu ya mzozo huo wa mpaka.Katika mahojiano na vyombo vya habari nchini Msumbiji, Membe alisema mzozo huo utatatuliwa kwa njia ya amani na kwamba suala la kuingia kwenye vita halipo.


  “Suala hili litatafutiwa ufumbuzi kwa mazungumzo ya kidiplomasia baina ya nchi hizi. Hakutakuwa na suluhu nje ya mkakati wa kidiplomasia. Tutaendelea kufanya mazungumzo,” alisema Membe na kusisitiza kuwa mkakati wa mazungumzo ndiyo suluhu pekee la mgogoro huo.


  Aliwahakikishia wananchi wa nchi hizo kwamba wataendelea kuishi kwa amani na ushirikiano na kwamba hakutakuwapo na mpango wowote wa kuingia kwenye vita.


  Aliwataka wananchi kutosikiliza maneno ya uchochezi akisema kwamba wenye mamlaka ya kutoa kauli za kuaminika juu ya misimamo ya nchi hizo ni Marais na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa mataifa hayo mawili.

  Katika kutatua mzozo huo, Membe alisema imeundwa Kamati Maalumu ya Usuluhishi ambayo wapo wataalamu kutoka pande zote na wanatarajia kukutana katika Mji wa Mzuzu, uliopo Kaskazini mwa Malawi.

  Upinzani wambana Banda
  Katika hatua nyingine vyama vya upinzani Malawi, vimemshauri Rais Banda kuhakikisha kwamba anatumia mbinu zote ili kuhakikisha mzozo huo unatatuliwa kwa amani na siyo vita.


  Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limenukuu baadhi ya vyombo via habari Malawi vikitaja vyama hivyo kuwa ni Malawi National Assembly (MNA), Malawi Congress Party (MCP), Democratic Progressive Party (DPP), United Democratic Front (UDF) na Peoples Progressive Party (PPM).

  Hata hivyo, vyama hivyo vimemtaka Rais Banda kuhakikisha hakuna ardhi ya Malawi itakayochukuliwa na Tanzania.

  Rais Banda aliingia kwenye madaraka ya kuiongoza Malawi Aprili, mwaka huu kwa nguvu ya katiba ya nchi hiyo, baada ya kifo cha Rais Bingu wa Mutharika ambaye ndiye aliyesaini vibali vya kuruhusu utafiti wa mafuta kwenye eneo hilo lililozua mzozo.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Sasa Kwanini tunaanza kuishia kulalalia kujipendekeza kwa MALAWI; Rais Kikwete ataishia kuachia hili suala ovyo ovyo tu kama anavyo itawala Tanganyika

  Inasemekana anaitawala Zanzibar Vizuri anapata Pongezi kwa Wazanzibari kuliko Maraisi wote waliotoka Bara waliotawala...

  Ingekuwa ahueni angeachiwa atawale wakati ule wa MKAPA angesha ondoka sasa hivi na MADINI, ARDHI na UGOMVI kati ya WAKRISTO na WAISLAMU

  Usingekuwa MBAYA hivi Nchini kwetu kama Sasa Hivi...
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ivi mbona kama wanainyenyekea malawi..wangekunja ndita sikunde kumi mbele ya mama banda si ndo uanaume..simkubali lowasa ila kwa hili alistahili akaimu uamiri jeshi mkuu kwa muda.
   
 4. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Huku ni kuwanyenyekea, hata mkutano tunaenda kufanya nchini kwao kana kwamba tunawaomba.hii ni aibu. Nyerere yuko wapi jamaniiiiiiiiiii
   
Loading...