Kikwete amwagiza Subash Patel akarabati nyumba ya watawa

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
45
Rais Jakaya Kikwete ( mwenye miwani) ,kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Morogoro Mhashamu Telesphory Mkude. Kushoto kwa Rais ni Sista Mkuu Parokia ya Lugoba akifuatiwa na Mfanyabiashara Bw.Subhash Patel wakati wa ufunguzi wa nyumba ya watawa. Nyumba hiyo imefanyiwa ukarabati mkubwa. Ufunguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Lugoba, Pwani. (Picha na Freddy MARO)

Kutoka: www.majira.co.tz

Heh, jamani-awe anampeleka na kwenye misikiti na madrassa basi.
 
...
Heh, jamani-awe anampeleka na kwenye misikiti na madrassa basi.
Mimi nadhani amefanya vizuri kwani afanyavyo ni mfano bora wa kuondoa udini na manung'uniko madogomadogo ya udini...Je angeomba huyo mfanyabiashara ajenge msikiti au madrasa si watu wangepiga mayowe?

Binafsi sijapenda alivyomwomba huyo mfanyabiashara kwani kama kiongozi wa nchi huko ni kujishusha na kushusha hadhi ya taifa, hususan kwa hawa wafanyabishara wadogowadogo.
 
Mimi nadhani amefanya vizuri kwani afanyavyo ni mfano bora wa kuondoa udini na manung'uniko madogomadogo ya udini...Je angeomba huyo mfanyabiashara ajenge msikiti au madrasa si watu wangepiga mayowe?

Amefanya vizuri sana kupeleka fedha za mafisadi kwa wagalatia, niliuliza mbona hamleti kwenye misikiti na madrassa? Nadhani akija huko ataumbuliwa

"Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu. Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme’ iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: “Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)

Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: “Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila. Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa. Nimrod Mkono alikuwa Mkurugenzi Mkazi wa Kampuni ya Oxford Services Ltd. na pia anamiliki Kampuni ya Marcus Ltd., makampuni ambayo kwa pamoja yamefaidika kwa kuupata jumla ya Shs. 4,477,870,279.61 chini ya utaratibu wa DCP.”
 
Rais Jakaya Kikwete ( mwenye miwani) ,kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Morogoro Mhashamu Telesphory Mkude. Kushoto kwa Rais ni Sista Mkuu Parokia ya Lugoba akifuatiwa na Mfanyabiashara Bw.Subhash Patel wakati wa ufunguzi wa nyumba ya watawa. Nyumba hiyo imefanyiwa ukarabati mkubwa. Ufunguzi huo ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Lugoba, Pwani. (Picha na Freddy MARO)

Kutoka: MAJIRA - GAZETI HURU LA KILA SIKU:

Heh, jamani-awe anampeleka na kwenye misikiti na madrassa basi.

Subash Patel...... Ok...... Swahiba yake baba Riz
 
Back
Top Bottom