Kikwete amuandalia Dr. Husein Mwinyi urais 2015

Wana JF.

Hivi Hizi nchi zetu za Kiafrika tumerogwa nini?? Mbona mifano na matukio mengi tuu yanaashiria wananchi hawataki kuburuzwa eg Gbagbo mumeona jana alichofanyiwa kutoka urais mpaka mahali alipo sasa, Ndio yale ya Gaddafi ajilaumu yeye mwenyewe maana hakuwa na misimamo kwani angeliwashughulisha wananchi wake katikla serikali Sidhani kama USA na nchi za Ulaya zinge mgusa kwani wananchi wangesimama nae kupinga uvamizi wa mataifa ya nje sasa ni aibu tu kwa viongozi wetu wa africa maana wengi wana interest zao na hayo mataifa ya nje kuwa watumwa tuu maana Africa still ina resource za hali ya juu sana na hazijaisha na stil hayo mataifa ya nje yanataka kuja kuzichuma

Sasa sielewi nini viongozi wa CCM hawakioni utawala wa kisultani mwiko jamani kuweni waelewa
hawa wanaoandaliwa kama successors tayari wana mtaji kipesa (nasikia Rz1, mwinyi mwenyewe, nk) na wanadhani umaskini wa WaTZ watautumia vizuri, pia wanataka kuwa partners na haya mataifa ya nje kuwadominate wananchi. Ukweli watakuwa wanapoteza muda ...Ghadafi ana pesa nyingi sana lakini hazionekani kumsaidia wakati huu!
 
kwa yale yaliotokea juzi na jana mjini Dodoma, ni dhairi ya kwamba kikwete anamuandalia mtoto wa mzee mwinyi kuwa raisi wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania. Vigezo ni vingi, ebu angalia halimashauri mpya ya chama? angalia pia kamati kuu. nafiki mpango umeanza na utatimia. Nawasilisha

NANI?? NINI?? come oooonn.. kwanza hii siyo nchi ya kifalme hadi tuteuliwe viongozi watoto wa vigogo. Tunao watoto wa wakulima halisi wenye uwezo kuongoza nchi. Nashangaa katika kamati, wizara nyeti lazima watawaweka vitoto vyao tu kwani wengine hawataki hizo nafasi?? ona hata CC ya ccm, J. Makamba, Mwinyi, Nnauye etc ni watoto wao wenyewe. kwani hakuna wengine wa kuteuliwa hizo nafasi? ndiyo maana tunageukia People's Power... long live!!
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Wakuu upo uwezekano wa Dr Kikwete kumuandaa Dr H Mwinyi baada ya awamu yake kumalizika mwaka 2015 nia ikiwa nikulipa fadhila za mzee Mwinyi.Yapo maslahii baina ya hizi familia mbili hasa ukizingatia Kikwete alishapotezwa kama si Mzee Ruksa Mwinyi kumuibua from nowhere,lakini pia haiatakuwa kazi rahisi sana ndani ya CCM yenyewe atakumbana na vizuizi vya nguvu kutoka makundi mengine ambayo wanadhani tangu kuzaliwa kwa JMT kanda zao hazijawahi kushika wadhifa wa Urais.Kuna kanda za Kaskazini na Nyanda za juu na nyingine wanaweza kuunganisha nguvu na kumshinda kirahisi sana Dr H Mwinyi.

Hali ya muungano si nzuri sana Wazanzibar hawataki muungano kabisa wanataka nchi yao wanaamini wanagandamizwa/wananyanyaswa.serekali ya umoja wa kitaifa haitamuunga mkono Dr Mwinyi kwa gharama ya kukubali Zanzibar iendelee kuwemo ndani ya JMT.Wadhani pwani ya Zanzibar ina mafuta iwapo watachimba mafuta uchumi wa Zanzibar utapaa hawana sababu za kugawana umaskini na ndugu zao wa Tanzania Bara.Dr H Mwinyi atakumbana na upinza mkali toka bara ambao bado hawajasahau jinsi Mzee Mwinyi alivyowabeba wazanzibar kipindi cha utawala wake.Wapo watanganyika wasiopenda/wasiotaka upuuzi wa kuwabeba wazanzibar,sehemu ndogo ya JMT yenye watu wasiofika milioni mbili wanauwakilishi mkubwa ndani ya Bunge,wanauhakika wa kutoa nafasi moja ya juu ya uongozi kwa katiba ya sasa,je hiyo haitoshi hadui wape urais ?.

Zanzibar ilikuwa na nafasi pekee ya kutwa urais mwaka 2005 kupitia kwa Salim A Salimu lakini wazanzibar wenyewe walihakikisha wanamwangusha na kumwangamiza mtu wao sioni nafasinyingine tena ikijitokeza.Dr H Mwinyi kaishindwa wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa mazingira ya sasa hayatoi nafasi kwa wazembe na magoigoi.

CCM haitakuwa chama pekee kinachoweza kutwaa nafasi ya urais,hivyo basi lazima watachukua tahadhari zote kumweka mwanachama makini,mchapakazi na anayekubalika ndani ya ya jamii kubwa.Enzi za siasa za kuburuzana zimekwisha CCM wakijaribu kulazimisha Dr H Mwinyi siasa za kikanda zitachukua nafasi yake,maswali ya usultani yatachukua nafasi yake na nk.Zipo kanda amabazo zimeshaanza kujipanga haiatakuwa kazi rahisi kuzizuia hata kidogo.Dr H Mwinyi hawezi kupenya hata kama Kikwete atalazimisha atajikuta akianguka kama ilivyotokea Kenya enzi za utawala wa Rais Moi alijaribu kumpachika Uhuru kenyata akajikuta akiangukia pua historia ni mwalimu mzuri Kikwete asithubutu kuwachagulia CCM bali aache demokrasia ichukue mkondo wake.

Mchakato wa katiba mpya Tanzania unaweza kuwaweka pembeni kabisa wazanzibar.Kwakuwa bado haujaanza tusubiri lakini nahisi utengano mkubwa.
 
Huu muungano tuumalize, mie binafsi sitaki kusikia neno muungano. Tuumalize kwanini sisi hatuwezi kushika nafasi ktk serikali ya zanzibar? muungano gani huo.
Mkuu.
Tupo wengi tusiouelewa Muungano huu.
Tupo wengi sana tuna-confuse serikali ya Muungano na serikali ya Tanganyika.

Muundo huu wa muungano ni mbovu.
Kwa ulivyo, mtanganyika aka mtanzania bara hana haki ya kushika nafasi katika serikali ya Zanzibar.

Pia kutokana na kutokuwa na umakini au mipaka ya ugawaji madaraka, Rais wa Muungano anaweza kumchagua Mzanzibari kushika wadhifa katika wizara za mambo ya Tanganyika...kitu ambacho ilipasa kuwekwa wazi kuwa Mzanzibari anaweza kupewa wadhifa katika wizara za mambo ya Muungano tu.

Kutoka kwenye "upuuzi" huu ni kwa kuwepo kwa serikali ya Tanganyika au kama tunakubali kuiita serikali ya Tanzania bara sawa pia. Itakuwa kama ile ya Zanzibar.Itakuwa inashughulikia mambo ya Tanganyika tu na hapo Mzanzibari hatakuwa na haki ya kushika nafasi au wadhifa.

Na serikali ya muungano ni ya wote, watanganyika na wazanzibari. Wala hakutakuwa na umuhimu wa kuwa na serikali kubwa. Mambo ya Muungano sio mengi, pia hatutahitaji bunge kubwa, Bunge la Muungano linaweza kuwa na wabunge 20 tu.

Kama ulielewa Serikali anayoiongoza Kikwete ni serikali ya Tanganyika aka Tanzania bara hukuwa sahihi katika premise yako ya kwa nini wazanzibari wanashika nafasi humo.Serikali ya kikwete ni ya Muungano.

Kwa mfumo mbovu wa Muungano, serikali ya Kikwete pia inafanya kazi za serikali ya Tanganyika kwa mambo ambayo si ya Muungano. Na mzanzibari akipewa wadhifa katika wizara ambazo si za mambo ya muungano basi ni abusive of power.
 
Hivi marais wa Afrika huwa hatatosheki na pensheni ya ustaafu na marupurupu mpaka wachakachue? watu wafe? katiba ifanyiwe mizengwe n.k

Mfano Gbagbo pamoja na kuwa Profesa wa History lakini alishindwa kukumbuka historia za marais waliongolewa kwa aibu duniani na bado marais wengine wanafikiri hayatawakuta ya Gbagbo!

Viongozi waafrika bana - haya ndiyo wanayotaka! Heshima kiasi gani angepata huyu bwana kama angekubali matokeo ya uchaguzi.
LAURENT.jpg
 
Mkuu.
Tupo wengi tusiouelewa Muungano huu.
Tupo wengi sana tuna-confuse serikali ya Muungano na serikali ya Tanganyika.

Muundo huu wa muungano ni mbovu.
Kwa ulivyo, mtanganyika aka mtanzania bara hana haki ya kushika nafasi katika serikali ya Zanzibar.

Pia kutokana na kutokuwa na umakini au mipaka ya ugawaji madaraka, Rais wa Muungano anaweza kumchagua Mzanzibari kushika wadhifa katika wizara za mambo ya Tanganyika...kitu ambacho ilipasa kuwekwa wazi kuwa Mzanzibari anaweza kupewa wadhifa katika wizara za mambo ya Muungano tu.

Kutoka kwenye "upuuzi" huu ni kwa kuwepo kwa serikali ya Tanganyika au kama tunakubali kuiita serikali ya Tanzania bara sawa pia. Itakuwa kama ile ya Zanzibar.Itakuwa inashughulikia mambo ya Tanganyika tu na hapo Mzanzibari hatakuwa na haki ya kushika nafasi au wadhifa.

Na serikali ya muungano ni ya wote, watanganyika na wazanzibari. Wala hakutakuwa na umuhimu wa kuwa na serikali kubwa. Mambo ya Muungano sio mengi, pia hatutahitaji bunge kubwa, Bunge la Muungano linaweza kuwa na wabunge 20 tu.

Kama ulielewa Serikali anayoiongoza Kikwete ni serikali ya Tanganyika aka Tanzania bara hukuwa sahihi katika premise yako ya kwa nini wazanzibari wanashika nafasi humo.Serikali ya kikwete ni ya Muungano.

Kwa mfumo mbovu wa Muungano, serikali ya Kikwete pia inafanya kazi za serikali ya Tanganyika kwa mambo ambayo si ya Muungano. Na mzanzibari akipewa wadhifa katika wizara ambazo si za mambo ya muungano basi ni abusive of power.

Hakuna haja yakuuunda serikali tatu, kwa hali iliopo sasa tuuvunje muungano.Muungano gani huu, baadae tutaungana ktk shirikisho la EAF. Huu upuuzi wa muungano tuseme sasa basi kama tulivyosema basii kwa azimio la arusha.
 
kwa yale yaliotokea juzi na jana mjini Dodoma, ni dhairi ya kwamba kikwete anamuandalia mtoto wa mzee mwinyi kuwa raisi wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania. Vigezo ni vingi, ebu angalia halimashauri mpya ya chama? angalia pia kamati kuu. nafiki mpango umeanza na utatimia. Nawasilisha
Unajuaje kama raisi atatoka ccm? Naona watu wamezoea kusema fulani kutoka ccm atakuwa raisi n.k. Tunasahau kuwa nchi hii ni ya vyama vingi, na huko tuendako, mawazo na fikra a wananchi zitabadilika, na pengine hata tabia yao ya upigaji kura na mapenzi ya vyama yanaweza kubadilika vilevile. Tumo katika mfumo wa vingi, tuondokane na mawazo ya mfumo mmoja, hasa hayo ya kufikiria kuwa raisi atatoka ccm kila wakati.
 
Jamani wananchi acheni hasira.. Hatuwezi kuwa marais wote, wengine tutawawakilisha..>LMAO
 
Kwa nini alikataliwa kugombea Zanzibar. Kule hafai huku anafaa sivyo?!!Hatutaki kwa maneno ,hatutaki kwa vitendo.Atapambanishwa na Mtanganyika,je ataona ndani?
Ndoto za mchana mwema. Vipi mswada wa katiba Zanzibar?
 
kwa yale yaliotokea juzi na jana mjini Dodoma, ni dhairi ya kwamba kikwete anamuandalia mtoto wa mzee mwinyi kuwa raisi wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania. Vigezo ni vingi, ebu angalia halimashauri mpya ya chama? angalia pia kamati kuu. nafiki mpango umeanza na utatimia. Nawasilisha

Kwa watanzania wa leo sijui kama ataupata akiingia kilingeni.
 
Ni kile nilichosikia kwamba Kikwete aliapa haachi nchi kwa MAKAFIRI!

Haya ngoja tuone ingawa huyu kilaza hajawahi hata siku moja kusema la maana kwa miaka yote ya uwaziri wake wa zawadi.
 
Mlio karibu naye mwambieni akaandae mazingira ya kuishi zanzibar.. Na hiyo ni kama atafanikiwa kufika 2015.
 
Back
Top Bottom