Kikwete amuandalia Dr. Husein Mwinyi urais 2015

markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
12
kwa yale yaliotokea juzi na jana mjini Dodoma, ni dhairi ya kwamba kikwete anamuandalia mtoto wa mzee mwinyi kuwa raisi wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania. Vigezo ni vingi, ebu angalia halimashauri mpya ya chama? angalia pia kamati kuu. nafiki mpango umeanza na utatimia. Nawasilisha
 
kama hawezi kuwa rais wa visiwani ataweza bara (muungano)!? Watanganyika/Waunguja wa leo sio wa mwaka 47, wengine wanaandamana, wengine wanachana katiba hadharani, wengine wako fb na JF! Huyo aliyeshindwa report ya mabomu atawaweza!? ngoja tuone
 
Inawezekana kabisa kwa jinsi mambo yalivyo ndani ya chama..
 
Ni kweli huu ndio mpango wa siri wa JK; na si JK peke yyake bali ccm kwa ujumla hasa ngazi za juu. Wanatuletea yale yale ya zanzibar; kutoka karume hadi karume, akitoka anaingia wa abdulwakil, akitoka anaingia wa Mwinyi, then wa Jumbe, then back to Karume nk. Kwa Tanzania wanajipanga ili akitoka Kikwete aje Mwinyi, then Nnauye, then Riziwani, then January nk
Ndiyo maana Lipumba aliwaambia hivi -suala la urais liongelewe kwenye mabadiriko kwani inawezekana wengine wanataka usultani yaani akitoka sultani Kikwete anamuachia mwanae sultani Riziwani! nk.
Tusome alama za nyakati lakini nao wazisome pia. Mubaraka alimwandaa mwanae, Ben Ali alimwandaa mwanae, Gadafi alimwandaa mwanae nk, yanayowakuta tunayaona!
 
Not is my country. Tumechoka mfumo huo wa kitumwa kutumia wananchi kama ngazi za kujipatia ulaji binafsi. Mfumo huo umeishashtukiwa Kwa Ghadafi na nchi nyingi za kiarabu ambako uliota mizizi. Wajaribu waaibike.
 
kwa yale yaliotokea juzi na jana mjini Dodoma, ni dhairi ya kwamba kikwete anamuandalia mtoto wa mzee mwinyi kuwa raisi wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania. Vigezo ni vingi, ebu angalia halimashauri mpya ya chama? angalia pia kamati kuu. nafiki mpango umeanza na utatimia. Nawasilisha

Kaka CCM baaaaado ndio kwanza inaanza. Kumbuka mwaka kesho kuna uchaguzi ndani ya Chama!! Hii CC ni kama care taker tu!! Minyukano bado inaendelea!! Unaweza kushituka ukakuta waliopigwa ngumi ya pua mwaka kesho wanapiga ngumi ya jicho!! Manake uchaguzi wa mwakani unahusisha mkutano mkuu kuchagua halmashauri na kisha halmashauri kuchagua CC, kaka bado patamu.
 
shhhhhh.............tena naomba tuuchune msimshitue JK kwa huu upuuzi
 
LAURENT.jpg
 
Maoni yako yanaweza kuwa sahihi. Kwa kuangalia wingi wa mawaziri toka Zanzibar ktk serikali ya Muungano unapata picha kwamba mpango wake wa 2015 atafanya kampeini kwamba ni zamu ya Zanzibar kutoa mgombea urais kupitia chama chake. Hata haya madai ya Waislamu kwamba wanaonewa ni mwendelezo wa kampeini za 2015. Jambo ambalo pengine CCM hawajui ni kwamba uchaguzi ujao hawana uwezo kushinda kirahisi. Siyo ajabu hata wagombea wazuri wa ubunge toka CCM watapigiwa kura za chuki. Watu wamechoka kusikia majina na sura zilezile!
 
Wana JF.

Hivi Hizi nchi zetu za Kiafrika tumerogwa nini?? Mbona mifano na matukio mengi tuu yanaashiria wananchi hawataki kuburuzwa eg Gbagbo mumeona jana alichofanyiwa kutoka urais mpaka mahali alipo sasa, Ndio yale ya Gaddafi ajilaumu yeye mwenyewe maana hakuwa na misimamo kwani angeliwashughulisha wananchi wake katikla serikali Sidhani kama USA na nchi za Ulaya zinge mgusa kwani wananchi wangesimama nae kupinga uvamizi wa mataifa ya nje sasa ni aibu tu kwa viongozi wetu wa africa maana wengi wana interest zao na hayo mataifa ya nje kuwa watumwa tuu maana Africa still ina resource za hali ya juu sana na hazijaisha na stil hayo mataifa ya nje yanataka kuja kuzichuma

Sasa sielewi nini viongozi wa CCM hawakioni utawala wa kisultani mwiko jamani kuweni waelewa
 
Muungano tunauuvunja kabla ya 2013. Tumechoka Tanganyika kukosa ajira, na mimi nautaka uwaziri.
 
kwa yale yaliotokea juzi na jana mjini Dodoma, ni dhairi ya kwamba kikwete anamuandalia mtoto wa mzee mwinyi kuwa raisi wa Jamuhuri ya mungano wa Tanzania. Vigezo ni vingi, ebu angalia halimashauri mpya ya chama? angalia pia kamati kuu. nafiki mpango umeanza na utatimia. Nawasilisha


Nani Hussein Mwinyi kuwa rais? haiwezekani sema Kikwete na CCM yake wanamwandaa kuwania urais kupitia CCM. Mimi nionavyo 2015 rais wa jamhuri ya muungano Tanzania au Tanganyika kama Wazanzibar watajichomoa kwenye muungano atatoka upinzani.
 
Zanzibar kwa sasa hawana haja ya urais wa JMT. Mradi wao mkubwa kwa sasa ni NCHI YAO ZANZIBAR. JK anaweza kumsaidi Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar endapo Dr Shein kama inavyotarajiwa atakuwa "one term President" kama alivyokuwa Dr Idris AbdulWakil.
 
Huu muungano tuumalize, mie binafsi sitaki kusikia neno muungano. Tuumalize kwanini sisi hatuwezi kushika nafasi ktk serikali ya zanzibar? muungano gani huo.
 
Back
Top Bottom