Kikwete amteua wakili wa Lulu kuwa Jaji

kuwa mwanasheria wa Lulu kuna usihana nini na kuteuliwa be reasonable for Pete's sake

We unasoma tu habari hii hapa bila kuunganisha ukanda wa video tangu kifo cha Kanumba, yaliyosababisha kifo cha Kanumba, aliokuwa anaongea kwa simu Lulu wakati wanazozana na Kanumba kabla ya kifo chake, na mengineyo utajua mahesabu ya kalikulas na jibu pengine si la moja kwa moja sababu fomula yake ni kubwa kupata jibu.
 
Hivi hakuna limit ambayo ya majaji wa kuteua kwa Rais? sababu hata jana kuna kiongozi nadhani naibu waziri wa sheria kama sikosei kasema Kikwete ndio Rais anayeongeza kwa kuchagua majaji wengi mpaka sasa toka nchi yetu ipate uhuru.

Au ndio anajiwekea shield mapema?

Tena wanawake. Moto ukiwaka hakuna shield hapo.
 
224960_126471244096505_100002008907798_183410_2770049_n.jpg
images


Rais amteua wakili wa Lulu kuwa Jaji

RAIS Jakaya Kikwete amemwapisha kuwa Jaji wakili wa kujitegemea, Joaquine De-Mello ambaye alikuwa akimtetea msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Wakili huyo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya Martin Luther King ya mwaka 2012 na ambaye alikuwa pia alikuwa mmoja wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG) ni miongoni mwa majaji 10 walioapishwa jana na Rais Kikwete, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
De-Mello ni miongoni mwa mawakili wanne waliojitokeza Aprili mwaka huu kumtetea Lulu katika kesi hiyo ya mauaji inayomtuhumu kumuua usiku wa kuamkia Aprili 7, mwaka huu.

Mawakili wengine wanaomtetea Lulu ambaye umri wake umekuwa na utata ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Massawe.

Akizungumza kwenye viwanja vya Ikulu, De-Mello alisema baada ya kuteuliwa kuwa Jaji, sasa atafanya kazi hiyo na moja ya mikakati yake ni kukabiliana na changamoto za wingi wa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Huyo Jaji Joquina mwenyewe mwingi wa habari!!

Human rights.jpg Human rights 2.jpg

Source: bang! Dec 11/ Jan 12, Issue no. 40
 
There must be something seriously wrong with Kikwete.This is complete lack of judgement.For Gods,sake why Lulu's wakili,why now under this heavy cloud of Kanumba's death,why this *****!I am lost.
Tuhabarishe habari za huyo jani aliyekuwa mtetezi wa Lulu
 
Labda tuangalie je huko siku za nyuma hakuna wakili wa kujitegemea aliteuliwa kuwa jaji huku akiwa ana mteja mahakama kuu?
 
Labda tuangalie je huko siku za nyuma hakuna wakili wa kujitegemea aliteuliwa kuwa jaji huku akiwa ana mteja mahakama kuu?
attachment.php



Wakili wa Lulu aliyeteuliwa kuwa Jaji

Kifo cha Stephen Kanumba kuna baadhi ya watu wanafunikwa funikwa, na mmoja ambaye anafunikwa ambaye alitajwa katika kipindi cha kifo cha Kanumba ni Ridhiwan Kikwete ambaye anasemekana alikuwa na mawasiliano na Lulu kabla, wakati na baada ya kifo cha Kanumba. Mheshimiwa Baba Ridhiwani kutoa ubani wa millioni 10 kwa familia ya wafiwa wa Kanumba na hali kadhalika uteuaji wa wakili wa Lulu kuwa Jaji wakati nyuma ya pazia kuna kitu kinachofunikwafunikwa yawezekana jitihada zote hizo ni kujaribu kusawazisha mazito ambayo yanaweza kuibuka na kuhusisha familia au watoto wa vizito katika kifo cha Kanumba.

Lulu anayo siri nzito moyoni mwake, na pengine jitihada pekee zinahitajika kujaribu kumpunguzia machungu ya gerezai/mahabusu kwa hoja ya kuwa umri wake ni mdogo kwani litampunguzia uchungu wa yampatayo ili asije legea nguvu na kupasua bomu lenye kuonyesha vimelea vilivyotengeneza mzimu wa kifo cha Kanumba.

Wakili wa Lulu kupata offer ya kuteuliwa kuwa miongoni mwa majaji nchini huku akiwa ni mmoja mtetezi mkubwa wa Lulu mwenye kukabiliwa na tuhuma za mauaji ya Kanumba ingawa hatujajua bado
first or second degree murder Lulu ametuhumiwa, lakini jaji huyo anaweza kuwa ni changamoto kubwa katika utekelezaji wa mwenendo wa kesi hii kwa kujaribu kupunguza uzito wa kesi hii kwa kumtengenezea Lulu mazingira ya kutoka first degree muder to second degree murder kwa hoja ya kuwa wakati wa tukio alikuwa bado mtoto. Hatujui nini kinaendelea kutokana na kile kinachofichwafichwa juu ya mazungumzo ya Lulu na mtu mwingine kwa simu wakatu Lulu yuko na hali ya kusigana na Kanumba pale chumbani na hata baada ya kifo cha Kanumba bado imekuwa ni siri katika kutoa siri ya nani alikuwa anaongea na Lulu.

Hatuna maana kuteuliwa mama huyu kuwa jaji kunahusiana na kesi hii, lakini lo lote lawezekana kutokana na usanii mwingi uliozoeleka katika haki za mnyonge kunyongewa kwani wenye uwezo wamejichukulia haki za kuruka na kupindisha sheria na wanaotetea sheria wako kwa ajili ya kulinda masilahi ya wenye nafasi na kumkosesha mlala hoi.

attachment.php


attachment.php


 
Hongera lulu na hongera jk
Hivi hakuna limit ambayo ya majaji wa kuteua kwa Rais? sababu hata jana kuna kiongozi nadhani naibu waziri wa sheria kama sikosei kasema Kikwete ndio Rais anayeongeza kwa kuchagua majaji wengi mpaka sasa toka nchi yetu ipate uhuru.

Au ndio anajiwekea shield mapema?
 
Nlisoma judgment yake moja inachekesha,kumbe ndo huyu.?yupo mahakama kuu mwanza..!
 
Back
Top Bottom