Kikwete amtema rasmi Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amtema rasmi Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 26, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kikwete amtema rasmi Lowassa

  Na Mwandishi wetu, Mwanahalisi

  * Amwandaa Karume kumrithi 2015
  * Dk. Shein ‘kupewa’ urais Zanzibar
  * Lengo ni kumaliza makundi, fitina


  RAIS Jakaya Kikwete na Rais Amani Abeid Karume watakabidhiana urais wa Jamhuri ya Muungano mwaka 2015, taarifa zimeeleza.

  Taarifa zilizoenea Dar es Salaam na mjini Zanzibar zinasema mwaka huu, Rais Karume ndiye atateuliwa kuwa mgombea mwenza wa Kikwete ili kuhakikisha rais wa Muungano ajaye anatoka Zanzibar.

  Kwa hatua hiyo, ndoto za Edward Lowassa, waziri mkuu aliyelazimshwa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, za kujisafisha na kuwa rais baada ya Kikwete, zitakuwa zimezimwa.

  Aidha, ndoto za Dk. Mohammed Gharib Billali kuwa rais wa Zanzibar baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu, zitakuwa zimeyeyuka pia, kwani anayeandaliwa kwa nafasi hiyo ni makamu wa rais wa sasa wa Muungano, Dk. Ali Mohammed Shein.

  Taarifa zinasema kwa mpangilio huo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitakuwa kimeondokana na ushindani wa “niue-nikuue” na makundi ambayo yanakaribia kukisambaratisha.

  “Kuna hili la Shein kupitishwa na hilo likimalizika, tunataka Rais Kikwete amteue Karume kuwa mgombea mwenza. Hapa kila kitu kitakuwa kimefikia tamati na umoja na mshikamano ndani ya chama utakuwa umeimarika,” ameeleza mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika serikali na CCM.

  “Mkakati wa kumpitisha Dk. Shein umelenga pia kumuinua Karume. Huyu ndiye tunayetaka awe mgombea mwenza wa Kikwete, lengo likiwa kumjenga kwa ajili ya 2015,” kimeeleza chanzo cha taarifa.

  Kwa mujibu wa mtoa taarifa, mkakati umewekwa kuhakikisha jina la Dk. Shein ndilo pekee linalofikishwa katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kwa ajili ya kupigiwa kura.

  Kiongozi mmoja wa serikali aliye karibu na mpango wa kutaka Shein kuwa mgombea pekee, ameliambia MwanaHALISI kwamba tayari mikakati yote imekamilika.

  “Mambo yote yanakwenda kama yalivyopangwa. Tunataka Dk. Shein ndiye pekee aingie katika kinyang’anyiro cha urais Zanzibar. Hili litasaidia kuondoa makundi na kumaliza fitina za kisiasa visiwani,” amesema akimnukuu kiongozi mmoja wa serikali na CCM.

  Alisema kwamba ili kuhakikisha mpango huo unafanikiwa, “Mkakati unasukwa wa kuhakikisha jina la Dk. Shein ndilo linakuwa jina pekee linalofikishwa NEC kwa ajili ya kupigiwa kura.”

  “Hili la Shein likimalizika, tunataka Rais Kikwete amteue Karume kuwa mgombea mwenza. Hapa kila kitu kitakuwa kimefikia tamati na umoja na mshikamano ndani ya chama utakuwa umeimarika,” alisema.

  Habari zinasema lengo la kumuibua Karume kutoka Zanzibar na kumleta Bara ni kutaka kumrithisha urais wa Muungano, baada ya Kikwete kumaliza kipindi chake cha urais.

  Habari zinasema mchakati huo utaepusha kile kinachoitwa, “misuguano ya urais 2015” kutoka kwa wanasiasa wa Bara.

  Wanasiasa kadhaa, akiwamo Lowassa, waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye na waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, wanatajwa kutaka kumrithi Kikwete.

  Mwingine anayetajwa na ambaye amekuwa akitajwa sana kuwa mwiba kwa kambi ya Lowassa na swahiba wake mkuu, Rostam Aziz, ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe.

  Urais wa 2015 ndio unaotajwa kuwa kiini cha msuguano ndani ya bunge na katika chama ambapo Lowassa na mshirika wake, Rostam wanatajwa kujenga ngome ya kuwatetea kwa gharama yoyete ile.

  Katika mchakato huu, mwanasiasa mmoja mwanammke ambaye ametangaza kugombea ubunge katika jimbo moja la Kanda ya Ziwa Victoria, ndiye anatajwa kuandaliwa nafasi ya waziri wa mambo ya nje na uhusiano wa kimataifa.

  Hata hivyo, wachambuzi wa mambo ya siasa wanasema mkakati wa kumfanya Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar, utakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa wapambe wa Dk. Billali.

  Taarifa zinaeleza, miongoni mwa sababu zitakazotumika kumwengua Dk. Billali ni pamoja na uamuzi wake wa kugombea urais Zanzibar mwaka 2005 kupingana na rais aliyepo madarakani.

  “Unajua yule bwana alikosa subira. Chama chetu kimeweka utaratibu wa rais aliyepo kuachiwa kumaliza vipindi vyake viwili kwa mujibu wa katiba. Lakini yeye katikati ya shughuli alikuja kuanua majanvi na kumwaga ubwabwa,” kimeeleza chanzo cha taarifa.

  Amesema, mbali na tuhuma za kuchukua fomu kumpinga Karume, Dk. Billali anakabiliwa na tuhuma nyingine ya “kuhujumu chama” siku chache kabla ya uchaguzi kutokana na hatua yake ya kumtuhumu Karume kuendesha nchi kifamilia.

  Vilevile Dk. Billali anadaiwa kubeba watu waliowahi kuonywa na Kamati Kuu (CC) kuvuruga chama; kuleta mpasuko katika chama na kumdhalilisha rais wa Jamhuri.

  Wanaotajwa kubebwa na Dk. Billali na ambao waliwahi kuonywa na CC, ni pamoja na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), Zahoro Mohammed na mwanachama wa Zanzibar, Mohammed Hija.

  Tayari Rais Kikwete amechukua fomu za kugombea urais wa Muungano na mjini Zanzibar, juzi Jumatatu, Dk. Shein alichukua fomu za kugombea urais ikiwa ni hatua moja katika kufanikisha mchakato unaoripotiwa.

  Hadi Jumatatu ni Jakaya Kikwete pekee aliyekuwa amechukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM kwa upande wa Tanzania Bara.

  Mbali na Dk. Shein, waliochukua fomu kugombea urais Zanzibar ni pamoja na Billali, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna, Naibu Waziri Afrika Mashariki Mohamed Abood, mdogo wake rais wa Zanzibar, Balozi Ali Karume na Kamishna wa wizara ya elimu na utamnadiuni, Hamza Bakari Mshindo.

  Mohammed Seif Khatib, waziri katika ofisi ya waziri mkuu (Muungano), jana alitarajiwa kutoa msimamo wake iwapo atagombea urais Zanzibar.

  Hata hivyo, mchakato huu wa kuandaa viongozi una dalili za kukumbana na upinzani mkali ndani ya vikao vya CCM kutokana na kuwepo mikakati ya awali kuwania uongozi miongoni mwa viongozi mbalimbali.

  Kwa mchakato huu, wawaniaji urais waliokuwa wakitajwa, akina Lowassa, Sumaye, Mwandosya na Membe hawana upenyo labda kwa njia ya upinzani.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I have never read such nonsense as this one! Yaani yule ambaye hajatenda lolote la maana kwa watu wake katika miaka 10 iliyopita, yule 'Rais' ambaye huteremshwa kutoka kwenye majukwaa na wapambe kutokana na kuunyaka kisawasawa, yule kiongozi ambaye aka 'Chai Jaba' -- ndiye awe Rais wa Muungano? NO WAY!!!

  Hivi hii nchi sasa imekuwa ni ya holela? Yaani any impostor can be President? MY GOD!!

  Ni vyema JK, baada naye kuivurunda nchi hii kwa miaka 10 iliyopita, aondoke kwa usalama na kutuuachia nchi yetu bila kutuchagulia mtu, tutamchagua wenyewe na asiwe na hofu iwapo swahiba wake EL atapata upenyo wa kuingia Ikulu. NEVER!!!!!
   
 3. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  So much more are yet to be heard and seen!! Mikakati, mipango, maazimio, blah blah blah. Hicho ndio Chama Chawala!
   
 4. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Karume!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Fedheha!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Alaaa,ndo mambo yamepangwa namna hiyoo!!!
   
 6. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  huu mchezo wa kupokeza pokezana huu ndio unafanya nchi isiendelee.kama kungekuwa na uchaguzi wa haki tungeseme CCM watajijua wenyewe na mchezo wao lakini kwa vile hakuna uchaguzi wa haki sisi wananchi tunaendelea kupangiwa viongozi na ccm hata kama kiongozi aliowekwa tunajua sifa zake.

  sasa shida tunazo lia sasa hivi huku tukiomba Kikwete amalize mda wake hili tupate mwenye uwezo ndio kwaaanza tunaenda kutangaziwa Karume.

  Wananchi tunahitaji kuamka hili kuokoa nchi yetu,huu ukoo wa kifalme wa CCM unatuchimbia kabuli.
   
 7. T

  Tajiri Mtoto Senior Member

  #7
  Jun 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 131
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Nina wasi wasi kuna siku tutachaguliwa "mbuzi" atuongoze as long as ndio matakwa ya watu fulani...:mmph:
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bwe he he he..hii mijitu bana aarrrghh..ngoja nimalizie kucheka kwanza..
   
 9. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kama JK-licha ya madudu yake yooote- sio tu amekuwa Rais wetu kwa takriban 5 yrs sasa bali pia anaelekea kuendelea kushikilia wadhifa huo for the next 5 yrs,basi hata mtu aliyetoroka wodi ya vichaa Mirembe anaweza kabisa kukabidhiwa urais wa bongo.Walalahoi wanaofisadiwa kila kukicha.ndio haohao wanaojazana na kugombea kumdhamini JK!
   
 10. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kumbe ndo maana Dr. Shein kachukua fomu ya kugombea urais wa zanzibar.
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Unajua tatizo ni la wananchi wenyewe wanaiamini sana ccm hata kama wanamweka mtu yeyote ili mradi ni wa ccm basi anapewa kura kibao na ndio maana ccm ina jeuri ya kurithishana tu uongozi kadri wanavyotaka.
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nchi hii imekuwa ya holela kwelikweli. Wakuja wanachukuwa kutwaa ardhi, na biashara. Kwa mfano Wachina wanafanya 'umachinga' hapa as if wako kwao na sidhani iwapo wazalendo hapa watakubaliwakufanya biashara za kimachinga kwao. Serikali iko kimyaaaa. Halafu sasa urais wa holela -- wa kuachiana tu utafikiri usultani. Mwee jamani!!!!!
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Dhambi aliyofanya Mkapa na wana CCM wenzake ya kuikabidhi nchi kwa wana mtandao ambao walitumia fedha kuwahonga wajumbe wa mkutano mkuu na waandishi wa habari itaendelea kuitafuna Tanzania kwa muda mrefu. Na bado... wengi waliokuwa kwenye ule mtandao ndio watakaokuwa waathirika wakuu...
   
 14. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dr Hapa Pangu anakuja kuwa rais Bongo tumeisha maana Zanzibar ameshatafuna yote sasa anapewa dar. Hii sitoshangaa kama si dili ya kuficha maovu ya JK.
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sina matatizo na Shein kuwa rais wa Z'bar, lakini Karume kuwa makamu wa rais na hatimaye Rais wa Tanzania baada ya 2015 ni kichekesho. Hivi ni kwa sifa gani aliyonayo hasa? Halafu JK mwenyewe baada ya kuboronga kwa miaka hii mitano na kusababisha nchi kuyumba, hastahili kabisa kuendelea kuwa rais kwa miaka mingne mitano! Ni ujinga wetu tu ndio utasababisha arejee tena Ikulu. Huwa najiuliza, hivi Watanzania tumerogwa au?
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sio tumelogwa ni ulimbukeni wa watanzania kudhania CCM wanajua wanalolifanya na ubabe unaotawala CCM kwamba viongozi hawataki kukosolewa madudu wanayoyafanya. Mfano kuna watu wanapiga kelele kujitenga zanzibar mara sasa wamekuja na serikali ya umoja. Behind the scene nasikia kuna makampuni kutoka Canada, Norway na nchi zenginezo yanamezea mate mikataba ya mwanzo ya kuchimba mafuta sasa ikiteuliwa serikali ya umoja itanullify mikataba ya zamani na ndio hapo vigogo wataingiza kampuni zao za kuchimba mafuta Zanzibar!!! In short CCM ndani kuna wanaCCM mafisadi na WanaCCM wakawaida (wasio mafisadi). Wasiokuwa mafisadi wanafata mkumbo tu baadhi yao kwa njaa na kuogopa kuvunja protocol ya chama ndio matokeo yake ni haya CCM mafisadi wanarithishana , atafuatia Karume, 2015-2025 tutasikia kapewa Lowassa, 2025 kama bado ana nguvu hivyo hivyo!!!
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Huu ni uongo na ni kauli ya ujanja ujanja kuzuia demokrasia ndani ya chama. Hili la kudai aliyechaguliwa mwaka juzi aachiwe aendelee kupegta ndiko kulikokifanya CCM iendelee na utamaduni wa kijima wa watu kusema mwachieni mzee, mwachieni kwa heshima huku mtu aliyepo madarakani awe ni mbunge au rais ni mbangaizaji na anayeboroonga.

  Ama utamaduni huu ndio unaolea na kukuza makundi na magenge ambayo leo hii wanadai wanataka kuyavunja.

  Kama CCM kingekuwa na demokrasia ya kweli ndani ya Chama na mfumo wake, pasingekuwa na ulazima wa Halmashauri Kuu, Kamati Kuu au Vikao vya siri kuamua ni nani awe mgombea wa Ubunge wa jimbo hata Uraisi. Kura za wanachama katika ngazi ndiyo zilizopaswa kuchagua mgombea wa wilaya na hata uraisi.

  Ni kuua Demokrasia kunakofanyika ndani ya CCM ambako kunalea uzembe, ufisadi na uozo ambao unaenea katika Taifa ukizingatia kuwa kipengele cha kwanza cha Katiba ya CCM kuhusu madhumini yake ni kushinda uchaguzi.

  Ni ajabu sana leo hii ambapo Dunia inasonga mbele katika kila nyanja, lakini CCM na hata Vyama vya Upinzani Tanzania vina mawazo mgando kama hayo niliyoyanukuu hapo juu. Mtu anakataliwa na kufanywa ADUI kisa anapingana na Utaratibu wa Kidikteta na kuzima haki ya kila mwanachama kugombea nafasi. Ndiyo maana Tanzania na mfumo wa kiuongozi na utendaji havipigi hatua za kwenda mbele bali kurudi nyuma kutokana na ukandamizaji wa haki za mtu kama unavyoonyeshwa hapa na si la ajabu kuona yanayofanyika CCM kuingia katika mfumo wa Serikali, iwe ni Serikali Kuu, Bunge na hata Mahakama.

   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Reverend,
  Kwa kuongezea tu inakinzana na kanuni ya uchaguzi wa baada ya miaka 5. Kama huyu aliyechaguliwa tumwache aendelee basi tungechagua rais wa kipindi cha miaka kumi.
   
 19. R

  Ramos JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  No, la Shein is just a guess, la Karume ......is more of Kubenea vs Lowassa...
   
 20. k

  kiuno Member

  #20
  Jun 27, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo ni hili, watu wote mnao oongea hapa ni kama 2% ya wapiga kura na wala hampo bongo, 98% ndio wale waliojazwa ujinga ambao hawaoni maovu yoyote ya ccm,kwahiyo ni kupiga kelele tu, cha maana tupigane mpaka ccm ing'oke bila ya hivyo 2025 ridhwani kikwete atakuwa raisi wa muungano na kule visiwe mtoto wa karume atakuwa raisi.
   
Loading...