Kikwete amsikia Shyrose Banji kuhusu ushindi wa Londa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amsikia Shyrose Banji kuhusu ushindi wa Londa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Nov 11, 2008.

  1. H

    Habarindiyohiyo JF-Expert Member

    #1
    Nov 11, 2008
    Joined: Aug 11, 2008
    Messages: 263
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    na Mwandishi Wetu    MGOMBEA wa nafasi ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) NEC, Shyrose Bhanji, jana aliwatoa machozi wajumbe wa NEC, alipotoa maneno ya shukrani baada ya kushindwa kwenye kiti hicho.

    Shyrose alipewa nafsi ya kutoa maneno ya shukrani na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ili kuwaeleza wajumbe wa NEC alivyopokea matokeo ya kushindwa kwake katika nafasi hiyo iliyochukuliwa na Meya wa Kinondoni, Salum Londa.

    Shyrose alisema kushindwa kwake kwa tofauti ya kura moja kunaonyesha ni jinsi gani NEC inavyozidi kumsogeza karibu kushika uongozi.

    “Nimefurahi sana na nimepokea kwa mikono miwili matokeo haya ya tofauti ya kura moja, kwani nikilinganisha na chaguzi za nyuma nilizoshiriki nilikuwa naachwa mbali na wagombea walionishinda.

    “….lakini safari hii nimefurahi kwa sababu nimezidi kusogezwa karibu na uongozi,” alisema Shyrose na kusababisha baadhi ya wajumbe waliompigania kwenye kinyang’anyiro hicho kutokwa na machozi.

    Wakati baadhi ya wajumbe wakifuta machozi, Rais Kkiwete alikuwa akitikisa kichwa na baadaye alikiri kuwa Shyrose alitoa maneno mazito.

    “Shyrose maneno yako ni mazito sana…. tumeyasikia, tumekuelewa, hayo mengine tuachie tutayafanyia kazi,”alisema Rais Kikwete.

    Kwa upande wake, Londa aliwashukru wajumbe waliomchagua kwamba wameonyesha imani kubwa kwake na kwamba hatawaangusha.

    Nafasi hiyo iliachwa wazi na Jack Mwambi, aliyeomba kujiuzulu baada ya Rais Kikwete kumteua kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.

    Londa alimshinda Shyrose Banji katika raundi ya pili ya kinyanganyiro hicho kwa tofauti ya kura moja ambapo Londa alipata kura 80 na Shyrose 79.

    Katika duru la kwanza, wagombea wa kiti hicho walikuwa watatu ambapo Londa alipata kura 62, Shyrose kura 60 na Peter Selukamba kura 42, ndipo ilipoamuliwa Londa na Shyrose waingie katika duru la pili na wapigiwe kura upya, hatimaye Londa kuibuka kidedea.

    Katika kinyang’anyiro hicho jumla ya waombaji 20 walijitokeza kuwania kiti hicho kilichokuwa na ushindani mkubwa hasa katika kampeni zilizofanyika juzi mjini hapa.
     
  2. Mchaga

    Mchaga JF-Expert Member

    #2
    Nov 11, 2008
    Joined: Apr 11, 2008
    Messages: 1,372
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 135
    Kaza buti dada yangu Shyrose Banji uongozi unahitaji dhamira ya dhati wala usikate tamaa...
     
  3. Dark City

    Dark City JF-Expert Member

    #3
    Nov 11, 2008
    Joined: Oct 18, 2008
    Messages: 16,279
    Likes Received: 205
    Trophy Points: 160
    Sijui hawa watu wanalia nini wakati nchi inaangamia?

    Kuna nini la maana kung'ang'ania NEC NEC NEC wakati wakati kila kona ya nchi watu wanateseka? Huyu mwanamke ningemwona wa maana kama angekuwa anawatoa watu machozi kwa kuhudumia watu wenye shida na kuwaamsha masikini wadai haki zao. Lakini kwa kuhangaikia NEC anatafuta misifa kama mafisadi wengine wa CCM.
     
  4. Selous

    Selous JF-Expert Member

    #4
    Nov 11, 2008
    Joined: Jan 13, 2008
    Messages: 1,319
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 135
    May be huyu ni kama FEMS ila hamuwezi jua. tumpe muda but........ i like this mana nchi inaelekea kunoga
     
  5. Bongolander

    Bongolander JF-Expert Member

    #5
    Nov 11, 2008
    Joined: Jul 10, 2007
    Messages: 4,882
    Likes Received: 32
    Trophy Points: 135
    Uheshimiwe mkuu
    Naona kama uko anti-shyrose, which is fine. Lakini inawezekana kuwa sio kutafuta sifa bali ni kutafuta nafasi ya kuwa part ya decision making. Ukisema uwasaidie masikini watatu pale vingunguti au huku manzese ni vizuri, lakini ukiwa mjumbe wa NEC uamuzi wako ukasaidia mamilioni naona ni jambo la maana zaidi. Lakini cha kushukuru mungu ni kuwa mtetea mafisadi Serukamba amepigwa chini, that is really encouraging. Lakini nashangaa hujasema hao wagombea wengine wanatafuta misifa.
     
  6. Mchaga

    Mchaga JF-Expert Member

    #6
    Nov 11, 2008
    Joined: Apr 11, 2008
    Messages: 1,372
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 135
    Hii habari ya kubpigwa chini Serukamba ni njema maana jamaa ni shabiki sana wa mafisadi....
     
  7. Fidel80

    Fidel80 JF-Expert Member

    #7
    Nov 11, 2008
    Joined: May 3, 2008
    Messages: 21,982
    Likes Received: 77
    Trophy Points: 145
    Huyu mama mbona analia lia anafikiri kuna upendeleo?
    Sasa wajumbe wanalilia nini kaongea maneno gani mazito kusema anakaribia kwenye uongozi ndo kuongea maneno mazito?
     
  8. M

    Masatu JF-Expert Member

    #8
    Nov 11, 2008
    Joined: Jan 29, 2007
    Messages: 3,287
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 135
    Shy-Rose ni mpiganaji wa kweli ipo siku zamu yake itafika anahitaji kuungwa mkono
     
  9. Dark City

    Dark City JF-Expert Member

    #9
    Nov 11, 2008
    Joined: Oct 18, 2008
    Messages: 16,279
    Likes Received: 205
    Trophy Points: 160
    Samahani sana mimi siko anti-Shyrose au mtu yeyote. Nachukia watu wanaotafuta nafasi kuendeleza yale yale ya jana, leo na milele.

    Kama Shyrose angekuwa kweli anatafuta nafasi ya kusaidia kufanya maamuzi, basi huko anakokimbilia siko kwenyewe. Kule maamuzi yalishafanywa. Akajiunge na wapambanaji wengine na siyo lazima kwenye vyama hata kwenye mikusanyiko ya kijamii. Maamuzi yapi ya maana unayategema au tuyategemee toka CCM baada ya kudumaza nchi kwa nusu karne?? That's not the plate to go! Unless she was crying for something else!
     
  10. Kevo

    Kevo JF-Expert Member

    #10
    Nov 11, 2008
    Joined: Jun 12, 2008
    Messages: 1,332
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 0
    What is this supposed to mean?The Bolded Part!
     
  11. FDR.Jr

    FDR.Jr JF-Expert Member

    #11
    Nov 11, 2008
    Joined: Jun 17, 2008
    Messages: 1,302
    Likes Received: 42
    Trophy Points: 145
    tusaidie kichwa ngumu, mkuu wa medani anafananiaje na shy rose bhanji?

    Tupatie ufafanuzi maana naona sasa unaanza kuwazungumza watu baadala ya issues.

    Ni vema unapomjadiri mtu ukawa wazi ili kuepuka diversion ya hoja mama.
     
  12. Baba_Enock

    Baba_Enock JF-Expert Member

    #12
    Nov 11, 2008
    Joined: Aug 21, 2008
    Messages: 6,759
    Likes Received: 97
    Trophy Points: 145
    """""""Shyrose maneno yako ni mazito sana…. tumeyasikia, tumekuelewa, hayo mengine tuachie tutayafanyia kazi,"alisema Rais Kikwete.""""

    It means next round "You will have my VOTE and trust me You will WIN"

    teh teh teh teh...
     
  13. k

    kingabdiel Member

    #13
    Nov 11, 2008
    Joined: Mar 7, 2008
    Messages: 28
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 13
    Sikubaliani nawengi wape kwani kura moja tu haitoshi kumpa mtu uongozi . We need majoority rrule but protection of minority. HAO waliompigia shyrose haki yao imepotea thus CCM wanatafuta njia nzuri ya kupata viongozi .
     
  14. Kaa la Moto

    Kaa la Moto JF-Expert Member

    #14
    Nov 11, 2008
    Joined: Apr 24, 2008
    Messages: 7,589
    Likes Received: 119
    Trophy Points: 160
    Jamani tuwe wakweli huyu Shyrose ni opportunist tu na anatafuta madaraka basi, wala hakuna cha kutaka kusaidia lolote maana niseme ukweli hakuna anayekwenda sisiemu ili asaidie kitu. Wote wanakuja kwa lugha hiyo lakini nyuma ya yote wanajua kuwa wanatafuta tu kupata madaraka na misifa basi. Kesho umuone anatembea kwenye shangingi lakini hakuna mabadiliko.

    Hapo usishangae kesho kusikia anachaguliwa kuwa mkuu wa wilaya mojawapo katika nchi hii iliyojaa uoza wa kila namna.

    BTW hawa sisiemu kila siku nasikia wanapigia kelele wapinzani kwamba huwa hata wakishindwa chaguzi hawaweki mtu mwingine ila wanarudisha majina yale tena kila ukija uchaguzi mwingine. Sasa mbona lugha hii hawamwambii huyo Shyrose wao ambaye kila kakiti ka uongozi ndani ya chama chao inapotokea huwa hakosi kujiingiza kugombea bila mafanikio? Ngoja kije kiti kingine lazima utasikia ameweka jina:)

    Huwezi kujiingiza katikautumishi wa chama cha sisi mafisadi na kutuambia unakwenda huko ukiwa na nia safi ya kuwatumikia wananchi. Wote wanaokimbilia huko ni kutafuta kuganga njaa zao kwa tiketi za kuwatumikia wananchi wa Tanzania. Ama kweli wajinga ndio waliwao.
     
  15. Dark City

    Dark City JF-Expert Member

    #15
    Nov 11, 2008
    Joined: Oct 18, 2008
    Messages: 16,279
    Likes Received: 205
    Trophy Points: 160
    Brilliant!

    She was just on and has been on a display. But finally she has been asured that customers have spotted her. Who knows, she might be brought within reach now, .. in case she was not reachable!!!
     
  16. K

    Koba JF-Expert Member

    #16
    Nov 11, 2008
    Joined: Jul 3, 2007
    Messages: 6,124
    Likes Received: 463
    Trophy Points: 180
    ...kwa hiyo fisadi Serukamba Peter alishindwa....thats good news!
     
  17. K

    Katibu Tarafa JF-Expert Member

    #17
    Nov 11, 2008
    Joined: Feb 16, 2007
    Messages: 981
    Likes Received: 29
    Trophy Points: 145
    Hata huyo londa na yeye si fisada tu,ccm hakuna mzima pale wote wamaathirika na ufisadi.
     
  18. Calnde

    Calnde JF-Expert Member

    #18
    Nov 11, 2008
    Joined: Oct 7, 2008
    Messages: 1,373
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 0
    Hapo upo sawa.I think its what he meant!
     
  19. Mzuzu

    Mzuzu JF-Expert Member

    #19
    Nov 11, 2008
    Joined: Jul 11, 2007
    Messages: 478
    Likes Received: 26
    Trophy Points: 45
    Anaandaliwa sehemu safi akapumzike! Kamgusa mkuu na kamsikia yupo eager kuwa karibu nao kwa nguvu zote ila tu kura hazikutosha awamu zote sasa ana karibia. So muungwana anamuahidi kufanyia kazi kumsogeza kwa nguvu zingine................ Lets wait and see wapi soon
     
  20. S

    S. S. Phares JF-Expert Member

    #20
    Nov 11, 2008
    Joined: Nov 27, 2006
    Messages: 2,141
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 0
    Ni habari njema sana kusikia watu wanagombea uongozi wa kisiasa wakiwa na pumzi za siasa.

    Wale wengine waliofilisika kisiasa wanalia faulo ya ukabila..!!
     
Loading...