Kikwete ampokea Ikulu kijana aliyesafiri kutoka Geita kwa baiskeli kwenda kumpongeza!

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
Wandugu,

Mmeisikia hiyo???? Kuna kijana amesafiri kwa baiskeli kutoka wilayani Geita hadi Ikulu Dar es Salaam kumpongeza mhe. jk kwa kushinda kwa mara nyingine kiti cha urais. ITV wamemwonyesha kijana akiwa anamkabidhi mhe. jk bahasha ya kaki ya A4 sijui ilikuwa na nini ndani yake!!! Vipi wakuu, inaingia akilini hiyo????

Chanzo cha Habari: Taarifa ya Habari ya Saa 2 Usiku.
10884537_10205987437871341_160921660_n.jpg
 
The boy has got problem between his two ears; Badala angetumia huo muda na hizo nguvu constructive kupanda mahindi (Since mvua karibia zinaanza) kuliko ku - waste his energy, kama alitaka sana kumpokea angetuma sms..... Wastage of energy
 
Ningemwona wa maana angetumia baiskeli kuhamasisha watu kupiga kura.
 
Hivi punde nilikuwa nikiangalia taarifa ya habari toka Star Tv, kijana mmoja aliejitambulisha kwa jina la MUSA mkazi wa mkoani Geita, amesafiri umbali wote huo mpaka Ikulu kumshika mkono Jakaya kikwete kama ishara ya kutoa pongezi kwa rais kwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Taarifa inasema amefanya safari hiyo kutimiza nadhiri aloiweka mwaka 2008 baada ya kuota ndoto kuwa jakaya atashinda urais mwaka 2010.

Na katika risala yake fupi kwa rais anadai katumia siku 7 njiani mpaka kufika dar akitokea Mkoani geita. Jamani watu wana roho ngumu aisee.
 
Discusting....but may be he gave the president his priorities au amempatia ukweli wake. can we get what was in the envelop?
 
Pumbafu huyo kijana inawezekana Lowassa au Ridh1 amempa kitu cha ufisadi ili ijulikane kuwa Kikwete bado anapendwa na watanzania kumbe hapendwi kabisa kw auongo na ufisdi wake wa kuimaliza nchi yetu na kuwapa wawekezaji kuiba resource zetu
 
kila mtu ana maamuzi yake binafsi nyie inawauma nini ? kama anafanya mazoezi je ? fateni mambo yenu.
 
basi usikute ni muuza mayai katoka kitunda eti wanajifanya Geita..unafanya mchezo nini kutoka geita kwa baiskeli..Hivi JK utaacha uchekibobu na uongo lini???
 
kila mtu ana maamuzi yake binafsi nyie inawauma nini ? kama anafanya mazoezi je ? fateni mambo yenu.
True.. Lakini The question is... Je maamuzi hayo ni ya Busara.... Kaacha Geita mvua zinanyesha badala ya kupanda mahindi....... kapanda Baiskeli kwenda dar
 
Hua wanaishia kujinyonga baada ya kuona alichokua akikiamini sicho ( frustration)
 
Discusting....?

Ndiyo nini hii? Huo wote ni wivu mbona wale wa enzi ya Nyerere walikuwa wanatembea kutoka Butiama mpaka Mwanza kuunga mkono azimio la Arusha?

Mwacheni kijana a enjoy ujana wake angalau atapata la kuhadithia akiwa mzee.

By the way, kuna yo yote mwenye mzee wake alijiunga na yale matembezi atuletee stori?
 
Ndiyo nini hii? Huo wote ni wivu mbona wale wa enzi ya Nyerere walikuwa wanatembea kutoka Butiama mpaka Mwanza kuunga mkono azimio la Arusha?

Mwacheni kijana a enjoy ujana wake angalau atapata la kuhadithia akiwa mzee.

By the way, kuna yo yote mwenye mzee wake alijiunga na yale matembezi atuletee stori?

Angetumia hizo nguvu akalima hekari ya mpunga ningemsifu zaidi
 
Let's be realistic and balanced. Kuendesha baiskeli kutoka Geita kunawezekana. Pia watu kumpenda bado Kikwete hadi kusafiri safari ndefu vile kunawezekana pia na ni sehemu ya uhuru na demokrasia. Mtu ana uhuru kufanya anachoona kinamfaa mradi asivunje sheria, kama mimi na wewe tulivyoacha shughuli nyingine na kutembelea jamvi.
 
Jamani comment nyingine, haya mie naongeza kidogo tu kuwa basi angevaa japo fulana mpya mpya, yaani ile aliyovaa ni ya uchaguzi wa 2005!!! Ya kasi mpya......
 
Back
Top Bottom