Kikwete ampigia debe Mramba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ampigia debe Mramba!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PayGod, Sep 15, 2010.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ijapokuwa MRAMBA, ana kashifa kubwa ya matumizi mabaya ya uongozi, jk amempigia debe B MRAMBA, achaguliwe tena kuwa mbunge wa ROMBO, JK alikuwa anampigia debe MRAMBA, leo katika mkutano wa siasa uliofanyika katika kiwanja cha shule ya msingi mbomai kati, TARAKEA, ROMBO.
  Ambapo asilimia 50 ya waliohudhuria , walikuwa wanafunzi wa shule mbalimbali hapa tarakea, kama mboma sec, nduweni sec, motamburu sec, mbomai primary, tarakea primary, na nyingine nyingi
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kweli huyu mtu ana uchu wa kuendelea kukaa mjengoni! Kwani ilikuwa lazima aende kule kumpigia kampeni mtu mwenye ksei kubwa ya ufisadi? Kweli yuko serious kupiga vita ufisadi?

  Jamani hata nyie mliomo CCM, hili ni sahihi kwa mkuu wa nchi kufanya? Mramba aliiba hela nyingi sana na angeweza kujikampenia mwenyewe. nadhani kuna uswahiba mkubwa kati ya wawili hawa, na hivyo hiyo kesi ni changa la machoni tu!
   
 3. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Nimepata habari kutoka Rombo Kuwa JK amesema kuwa Mramba ana kesi ndogo na atashinda hivyo wananchi wamchague !!!

  Jamaa wa huko kasema kuwa Mramba hajafanya lolote kwa sekta ya afya, maji, uchumi na elimu kwa miaka 15.

  Nyanda za chini wilaya ya Rombo maji ni shida sana.

  Maji yaliyopo nyanda za juu Rombo yaliletwa na Mbunge wa miaka ya 80 - Ngalai.

  Watu wanasema bila maji, afya, elimu, hiyo barabara ya lami ni ya nini? Kwa ajili ya matajiri.

  Wanasema kuwa Mramba anakaa meza moja na matajiri wa Rombo, hana habari na walalahoi
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  Ha ha ha ha!!!!!

  Haihitaji kwenda shule kujua kuwa Serikali ya CCM inawaona wanachi mafala malimbukeni wasiojua lolote
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  wote ni wezi
   
 6. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  CCM sasa ni ya matajiri, maskini wakafie mbele!


  • Wengi wakimbilia Ubunge, Udiwani kuficha maovu yao
  • Agizo la kutenganisha biashara na siasa lawekwa kapuni

  Na Daniel Mbega

  “CHEO ni dhamana, nitatumia cheo changu kwa faida ya wote.” Hii ni mojawapo ya Ahadi 10 za Mwana-TANU ambazo zilirithiwa na Chama cha Mapinduzi inayosisitiza kwamba mtu yeyote anayepewa uongozi hapaswi kuutumia kwa maslahi yake binafsi bali kwa maslahi ya wote.

  Ahadi hii na nyinginezo zilikuwa zikiimbwa kila mahali kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuo vikuu ambako somo la Siasa lilianzishwa na serikali ya TANU na kuendelezwa na CCM kabla ya kufutwa mwanzoni mwa miaka ya 1990 kufuatia kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.

  Vijitabu vingi vya TANU na Azimio la Arusha vilikuwa vimesambazwa ambapo kila mjumbe wa nyumba kumi kumi alikuwa navyo vya kutosha kuwagawia wananchi wake ili waweze kuelewa wajibu wao na siasa kwa ujumla na kuhamasisha Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambayo sasa imezikwa na wajanja wachache walioamua kuukumbatia ubepari kwa kisingizio cha Soko Huria.

  TANU (na baadaye CCM) iliamini binadamu wote ni sawa na kusisitiza raia wote kwa pamoja wamiliki utajiri wa asili wa nchi hii ukiwa kama dhamana kwa vizazi vyao; na Kwamba ni wajibu wa Serikali, ambayo ni watu wenyewe, kuingilia kati kwa vitendo maisha ya uchumi ya Taifa ili kuhakikisha usitawi wa raia wote na kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine au kikundi kimoja kunyonya kikundi kingine na kuzuia limbikizo la utajiri kufikia kiasi ambacho hakipatani na siasa ya watu wote kuwa sawa.

  Tunaelezwa bayana kwamba TANU (sasa CCM) ni chama cha wakulima na wafanyakazi na ikasisitiza katika katiba yake kwamba, Serikali lazima itumie mali yote ya nchi yetu kwa kuondoshea umaskini;ujinga na maradhi;

  Kuona kwamba Serikali inaondoa kila namna ya dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa na upotofu; na Kuona kwamba Serikali ya nchi yetu inasimamia barabara njia kuu za kuzalisha mali na inafuata siasa ambayo itarahisisha njia ya kumiliki kwa jumla mali za nchi yetu.

  Njia kuu za uchumi ambazo zinapaswa kuwa chini ya wakulima na wafanyakazi ni pamoja na ardhi, misitu, madini, maji, mafuta na nguvu za umeme;njia za habari, njia za usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari, simenti, mboleo; nguo, na kiwanda chochote kikubwa ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine; mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima katika viwanda vikubwa.

  Suala la mgawanyo wa mali za umma limekuwa kitendawili kigumu kuteguliwa hasa baada ya kushuhudia namna viongozi wa chama na serikali wanavyojilimbikizia mali nyingi za umma, wakijali zaidi matumbo yao kuliko ya Watanzania licha ya kuwepo kwa maadili ya uongozi ambayo nayo yameendelea kubaki kwenye makaratasi na kufungiwa kabatini huku agizo la kutenganisha biashara na siasa likiwa limesahauliwa kitambo!

  Viongozi hawa ambao wanaagizwa na chama kwamba ‘Cheo ni dhamana’, pamoja na kubadili mfumo wa siasa kutoka Ujamaa kuja kwenye Ubepari, bado wanashindwa kufuata maadili sahihi ya uongozi, yakiwemo kutojilimbikizia mali kwa kutumia vyeo vyao, kutaja mali zao kabla ya kuingia madarakani na baada ya kutoka, badala yake wanaendelea kuchota mali za umma kadiri wapendavyo huku wananchi wakiendelea kuogelea kwenye umaskini.

  Kila kiongozi anayeingia madarakani kwa sasa huangalia kwanza tumbo lake, na kadiri siku zinavyosonga hupata tamaa ya kuchota zaidi na zaidi na mwishowe huona kwamba ni haki yake kuwa tajiri huku wengine wakiendelea kupiga miayo bila kuwa na uhakika hata wa kipande cha mhogo kushibisha tumbo kwa mlo mmoja.

  Viongozi wa chama hiki ambacho tulitegemea kingeleta na kuendeleza mapinduzi ya kweli kwa kila Mtanzania, leo hii si chama cha wakulima na wafanyakazi kama tulivyoelezwa enzi zile za Mwalimu.

  Tangu tulipopata uhuru wetu Desemba 9, 1961 Serikali ya Awamu ya Kwanza ilihimiza lazima kusiwe na tabaka mbili:tabaka ya chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, natabaka ya juu ya watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi.

  Yale yaliyokatazwa, hasa ya kuweka matabaka baina ya matajiri na maskini, leo hii siyo jambo geni ndani ya CCM ambayo imefuta kabisa dhana ya mkulima na mfanyakazi kuwa muhimili wa chama.

  CCM kimekuwa chama cha mabwanyenye ambao kila siku ama wanafikiria namna ya kuingia madarakani au jinsi ya kuendelea kuchota na kukalia madaraka hata kwa kuzivunja zile ahadi za chama, ikiwemo kutumia rushwa ingawa midomoni mwao wanaimba kuwa ‘rushwa ni adui wa haki’, tena wengine wanaongeza kwamba ‘ni dhambi’!

  Ukitazama mchakato wa kura za maoni kwa mwaka 2010 ndani ya chama hicho utaamini kwamba CCM ni Chama cha Matajiri, si Chama cha Mapinduzi kama ambavyo tunaimba midomoni. Wengi ni wanafiki wakubwa na wameanza kuitumbua nchi mara tu baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kufariki dunia mwaka 1999.

  Ukiwachungulia baadhi ya walioshinda kura za maoni lazima utakutana na majina ya watu ambao wanasifika ndani ya jamii yetu kwa mambo maovu, yakiwemo ya ukwepaji wa kodi kwenye biashara zao nyingi zikiwa hazifahamiki sawasawa.

  Kwa ujumla utakutana na wafanyabiashara wengi ambao wanatajwa kwamba wamepata nafasi hiyo kutokana na ‘mchango wao kwa chama’, hasa fedha, bila kujali misingi iliyounda chama hicho kikongwe zaidi barani Afrika, na pekee ambacho kinaendelea kusimama imara ingawa kwa sasa kinaelekea kuyumba.

  Nakumbukwa wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais kupitia CCM mwaka 1995 walijitokeza wanachama wengi ambao wengi wao nilihudhuria hata mikutano yao ya kutangaza azma za kuwania nafasi hiyo.


  Lakini kuibuka kwa wagombea wengi kiasi hicho kulimpagawisha sana Mwalimu Nyerere, ambaye aliamini kwamba hiyo haikuwa demokrasia tena bali chama kilikuwa kimevamiwa na kwamba kilikuwa na viongozi ‘wabaya’, ambao dhahiri aliwaona walikuwa na nguvu na wangeweza kupitishwa na chama kushika madaraka ya nchi.


  Nyerere aliona kwamba chama kilikuwa kimevamiwa na watu wenye fedha, ambao walikuwa tayari kumsimika ‘mtu wao’ kwa kutumia fedha hizo ambazo Mwalimu Nyerere aliziita ‘fedha za bhangi’, akimaanisha kwamba zilikuwa fedha chafu ambazo hata upatikanaji wake ulikuwa wa njia zisizo halali ndiyo maana walikuwa tayari kuzitumiza watakavyo ili kulinda ‘maslahi’ yao.


  Akawaponda wagombea wengine waliokuwa kwenye mchakato huo akisema; “Mnakimbilia Ikulu, Ikulu kuna biashara gani pale? Mnataka kwenda kufanya nini Ikulu? Ikulu ni mahali patakatifu, si mahali pa mchezo mchezo pale. Ni mahali pa kuheshimika!”


  Hata hivyo, miaka michache baadaye wale aliodhani wangefuata falsafa yake wakawa wamekengeuka na kuamua kuitia najisi Ikulu, sehemu takatifu ambayo Nyerere alipigania kuhakikisha hakiingii kilicho ‘kichafu’.


  Kusema ukweli, CCM ya sasa imebaki na katiba tu, ndani yake hakuna wanachama wenye katiba ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, kwa sababu misingi aliyoiacha imebomolewa na kuigeuza rushwa kuwa ni sehemu ya maamuzi ndani ya Chama hicho.


  Watu wenye fedha haijalishi kama ni za halali au za ‘bhangi’ kama mwalimu Nyerere alivyopata kusema ndio wenye sauti kwenye chama na wanaweza kushinikiza jambo lolote kwa wananchi kwa kutumia pochi zao.


  Kukosekana kwa kanuni madhubuti za kukiendesha ndiko kumefanya wakulima na wafanyakazi wasipate nafasi na badala yake kimevamiwa na wafanyabiashara na walanguzi wakubwa. Wafanyabiashara hawa ndio wenye sauti ndani ya chama, wanaweza kuamua lolote kwa nguvu ya fedha.


  Kwa sasa mkulima, ambaye ni maskini wa mwisho ndani ya nchi hii kutokana na kutowezeshwa, anaonekana dhahiri hawezi kupata nafasi ya kuongoza ndani ya Chama hicho, zaidi ya kuwa shabiki wa vitendo viovu kama vile rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.


  Wapo wanachama wengi wa CCM ambao wameelekea upinzani baada tu ya kura za maoni. Ingawa ni kawaida kwa mambo haya kutokea kila ifikapo kipindi cha uchaguzi, lakini kuondoka kwa makada wengi kunaonyesha dhahiri mambo si shwari.


  Ni ukweli ulio wazi kuwa mchakato wa kura za maoni uligubikwa na vitendo vya hila, chuki na rushwa za waziwazi miongoni mwa wanachama na viongozi wa juu hawakukemea vitendo hivyo, licha ya kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilijitahidi kudhibiti.


  Yawezekana kuna ukweli ndani yake, lakini CCM inapaswa isiwakemee wale wanaoikosoa, badala yake ijichunguze kama imesimama sawasawa katika misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili.


  Leo hii mtu akipata ujasiri wa kuhoji ni wapi matajiri hawa ‘wanaoisaidia CCM’ ataonekana katumwa ama anatumiwa. Kwa bahati nzuri, sisi tunapenda kuona Tanzania inaendelea na wananchi wananufaika na matunda ya rasilimali zao, hivyo hatuna budi kukikosoa chama ili kijirekebishe.


  Inakuwaje watu ambao wanasifika kwa tabia za utapeli, ufisadi na ukwepaji wa kodi leo hii ndio wawe na nafasi kubwa ndani ya chama? CCM huwa hailioni jambo hili mapema ama huleweshwa na fedha wanazozitoa kukisaidia?


  Tukiwachunguza hata hawa waliopitishwa kwenye ubunge na udiwani mwaka huu ndani ya CCM, hakika tutawakuta ‘waovu’ ambao wamejificha kwenye siasa kulinda maslahi yao. Kwamba wakiwa ndani ya ‘chama’ hakuna atakayewanyooshea kidole, hasa ikizingatiwa kwamba bado wanaendelea ‘kukisaidia’ chama.


  Vijana wenzangu tuna wajibu wa kuwahoji watu hawa wamepata mali hizo kwa njia zipi hata kama watakuwa ni ndugu zetu wa karibu ama wazazi wetu. Jambo hili linawezekana tukipata ujasiri wa kuhoji wakati tunapoona rasilimali za nchi zinahodhiwa na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.


  SOURCE: DIRA YA MTANZANIA, AGOSTI 30, 2010
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  I think this has gone beyond help...
   
 8. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haya jamani, Kikwete amegeuka kuwa hakimu, anajua kuwa kesi ya mramba ni ndogo na atashinda tu
  Loooh, this is a type of president we have now, ila ngoja tarehe 31, viziwi watasikia bandugu au mnasemaje?
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Kwa mtazamaji wa picha hii naona unafiki umezidi sasa!!
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Heading yako ilipaswa kuwa hivi: Wezi wakubwa wa nchi hii wapigiana debe
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Kichwa chaumaaaaaaaaaaaaa
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama kweli JK alitamka maneno hayo, basi ninasubiri kauli ya Jaji Mkuu. Maana alimjia juu Marando kwamba anaongelea kesi ambazo ziko mahakamani. Kikwete hajaongelea kesi iliyo mahakamani tu, bali ameenda mbali zaidi kwa kutoa hukumu na yeye bado ni Rais, so kwa kofia yake ya urais, kauli kama hiyo inaweza ku-influence hukumu.

  Kikwete siyo mwana sheria, amejuaje kwamba kesi ni ndogo na kwamba Mramba atashinda? Anajua ushahidi uliokusanywa na PCCB na DPP? Tukisema kwamba kesi ya Mramba ilipelekwa kisanii mahakamani ili kuonyesha kwamba JK anapiga vita ufisadi, atasemaje?

  Hiyo statement ni mtaji tosha kwa wapinzani ili kuiumbua serikali ambayo haina nia ya kupiga vita ufisadi na pia kuingilia uhuru wa mahakama.

  Ni JK huyu huyu alikuwa anasema anataka ofisi ya DPP na PCCB wapeleke kesi mahakamani ambazo wana ushahidi wa kutosha na siyo kupeleka kesi ambazo wanaishia kushindwa na kupata aibu. Huyu jamaa kila siku ni kuji-contradict yeye mwenyewe.
   
 13. Chacha wa Mwita

  Chacha wa Mwita Senior Member

  #13
  Sep 15, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 166
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kweli rais wetu amechiz, nasubiria kwa hamu kubwa kuona atamnadi vipi rostam aziz siku akiwa igunga!
   
 14. M

  Masauni JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna watu wanamshangilia kikwete nadhani inabidi inabidi wachunguzwe akili.
   
 15. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  WanaCCM wanamshangilia Kikwete lakini wananchi watamchagua Dr. Slaa
   
 16. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ikiwa hadi kesho kama Jaji Mkuu hajatoa statement ya kumkemea Kikwete, basi waandishi wa habari waende kumuuliza kwa nini.
   
 17. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  anajua wazi kuwa kesi iliyoko mahakamni ni usanii mtupu hakuna ushahidi wowote wa maan uliowasilishwa mahakani ili kumtia hatiani ndio maana wamempitisha agombee na anampigia debe. Usanii mtupu. Akili kichwani mwetu. mahakama ya kisutu imezungushiwa uzio wa bati sijui ndiio inabomolewa?
   
 18. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2010
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Kuna mwenye RATIBA YA KUBADILISHA DAMU? Labda muda umefika au unaelekea kufika.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Sep 15, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Swala la CCM kumsimamisha Mgombea ambaye ana kesi mahakamani ni makosa makubwa sana ya kisiasa. Na kila atakalosema Kiktwete lazima litakuwa na walakini kwani haiwezekani kumtetea mtu wa aiana hii kwa njia yeyote. Ilitakiwa kesi ya hawa watu imekwisha kabla hajajiandikisha kugombea na maadam CCM imempitisha, basi pengine wao wanajua zaidi ya hata mahakama.
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Sep 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kauli hii inanihuzunisha sana! Ama kweli Rais tunaye!
   
Loading...