Kikwete amka, fanya maamuzi na tafuta wasaidizi au unakwenda na maji.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amka, fanya maamuzi na tafuta wasaidizi au unakwenda na maji....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Dec 7, 2009.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kikwete amka au unakwenda na maji

  TATIZO la rais wetu mpendwa ni kujisahau na kuwaachia maofisa wa Ikulu kuendesha nchi.

  Inaeleweka tena sana kuwa ni aina ya watu gani tuliokuwa nao pale Ikulu. Sio watu wanaona mbali wala wenye kuaminika kwa maana baadhi yao walikwishawauza wenzao katika biashara walizokuwa wakifanya pamoja.

  Maamuzi ndio uongozi
  Inavyoelekea sasa ni kwamba kuna 'paralysis' ya serikali katika masuala mbalimbali ambayo wananchi wamesubiri mpaka wamechoka kuona kama kuna maamuzi ya maana yatafanyika. Lakini hadi wa leo hayajafanyika.

  Wakati Evo Morales katika kipindi cha chini ya miaka mitatu amefanya maajabu makubwa huko Bolivia bila kugwaya mahakama au nchi kubwa sivyo alivyo kiongozi wetu. Anaota matende hadi pale ambapo kila kitu kiko wazi kwamba lazima yeye abaki au sheria fulani iende.

  Tukio la hivi karibuni la silaha kuuzwa kwa waasi Kongo ni kielelezo tosha kuwa katika serikali kuna serikali nyingine ambayo Kikwete haijui na hana mamlaka nayo kabisa. Na haya ni matokeo ya kuwashirikisha maswahiba wa Muairishi Nolan na wale Maburushi waliokubuhu kwa uroho wa fedha na maisha ya anasa kwa kutumia wajinga waliomo serikalini mwetu. Ninasema wajinga kwa makusudi kwa kuwa ni ukweli usiofichika kwamba Wanasiasa hawajui kabisa kutengeneza fedha ila wanajua kuzitumia. Na pale wanapoishiwa kabisa watu kama hao hapo juu huwatumia jinsi wapendavyo. Maaana wanasiasa wetu au viongozi wetu huweza kuwapa dili la bilioni moja wao wakatengneza bilioni 10 na bado wakakiachia chama hako kabilioni tu. Bilioni 9 wanaziswaga wao wenyewe.

  Mfumo huu wa kutumia NJIA ZA PANYA katika kupata fedha kwa ajili ya chama na uchaguzi ndio uliotufikisha hapa. Tukitaka tutoke huko lazima kila kitu kifanyike juu ya meza.

  Jamaa wa Ikulu na watumishi kadhaa katika wizara wameamua kujichukulia mamlaka wao wenyewe ama kwa kuamua au kutoamua juu ya chochote.

  Inavyoelekea kuna mtu hapo Ikulu keshatangaza vita dhidi ya mtu yeyote anayeamua na kutekeleza jambo bila idhini yao na sio ya rais. Na rais inavyoelekea hajui kinachoendelea.

  Kwa maneno mengine rais hana udhibiti wowote wa wale walio chini yake achilia mbali serikali yake katika mikoa 26 ya Tanzania.

  Nchi inajiendesha yenyewe au inaendeshwa na wajanja wachache. Na hili linatutia wasiwasi kwamba njama za wasiomtaka Kikwete zinaweza kufanikiwa. Njama hizo ni zile za kuhonga wajumbe wote wa mkutano mkuu Tanzania nzima kumpigia kura mtu mwingine zaidi ya Kikwete. Na hivi sasa makundi ndani ya Vijana, Wazazi, wajumbe wa mkutano mkuu na wazee wa chama yameanza kujiuza kwa wenye bahasha kubwa tayari kuifanya kazi hiyo ambayo hatima yake ni ile ya jina la Kikwete kutorudi kati ya wagombea tano watarajiwa kwa tiketi ya CCM hapo mwakani.

  Huyu Katibu Mkuu anayeropoka ovyo naye ni tatizo kwa chama. Hivi kweli kuna kiongozi anayeweza kusema kuwa kuna mtu fulani ni mkubwa zaidi kuliko chama au serikali ? Akili zake huyu ni sawa. Labda kwa kiongozi ambaye hataugua wala hatakufa. Lakini sio kwa viumbe hawa tunaowajua.

  Makamba ni Liability kwa CCM. Na jinsi wanavyochelewa kumtosa ndivyo atakavyosababisha hasara kubwa zaidi kwa chama.

  Rais anahitaji kuvuta hatua moja nyuma na kutafuta watu wasio karibu naye lakini wanaojua kinachoendelea katika nchi hii na wenye uchungu wa hasara uongozi mbovu unaosababishia nchi na mapenzi ya kuwaona Watanzania hawaendelei kubeba misalaba isiyo ya lazima ili kunufaisha mafisadi na viongozi walioiuza nchi huko nyuma.

  Kubwa zaidi ni kwamba rais muoga wa mwamuzi, kilio kitamuumbua. Rais kuonekana kweli rais budi afanye maamuzi ambayo kila mtu anategemea yafanyike. Huu si wakati wa kujificha nyuma ya utawala wa sheria au ushahidi uliokamilika -maana kama ndivyo basi hiyo itakuwa kama sheria ya Kiislamu ambapo watu zaidi ya wawili wanahitajika kuona kabisa tendo la kuzini likifanyika ili mkeo au mmeo asemekane ana kosa la kuzini nje ya ndoa. Sahau kabisa hilo kutokea.

  Aidha, staili ya uongozi wa Kikwete ni mbaya, mbaya kabisa. Huwezi kufanya kazi zote. Pengine hii inachangia kushikwa kisunzi na kuzirai majukwaani. Gawa madaraka mzee. Na hakikisha unaowagawia madaraka wanawajibika ipasavyo. Si wanakula kodi ya wananchi. Anayeshindwa atakuwa kashindwa na kujifukuzisha kazi mwenyewe. Sasa mzee masuala ya barabara na miundo mbinu ikiwe ni wewe, michezo ikiwa ni wewe, shule ikiwa ni wewe, albino ikiwa ni wewe, trafiki na ubabaishaji barabarani ikiwa ni wewe, nje ikiwa ni wewe, mikoani ikiwa ni wewe basi kweli kuna kitu kitafanyiaka hapo au ni kurashiarashia tu?

  Kuna wizara au sio. Miundo mbinu tupate habari za barabara na tujue kinachoendelea. Afya nako tupate taarifa na tuone kazi inayofanyika. Tumsikie Waziri anayehusika na michezo na programu yake ya kuhakikisha kila kata ina stadium Tanzania au hilo ananyimwa kufanya. Tusikie Madini na nIshati wanavyowawezesha wachimba migodi wazawa kuwekeza katika uchimbaji madini na kadhalika.

  Katika miaka hii ya TEKNOHAMA ni rahisi kabisa kujua kila kinachoendelea katika kila mkoa na wilaya, kila wizara na idara na kila ubalozi na wakala wa Kimataifa Mtanzania alioko. Na kwa utawala wa Management by Exception wawakilishi husika watakupa kile unachohitaji tu na sio cha kukusumbua kichwa. Waoneni wataalamu muwatumie, lakini sio kwa tamaa yenu ya fedha za wananchi na ukubwa wa ofisi ya ikulu na mawizara kula na kunywa tu halafu kutuharibia maisha yetu Watanzania ndio iwe asante yenu.

  Haya nalo hilo Kongamano la Nyerere -limefanyiak kwa ajili ya kumsuta na kumuaibisha Kikwete au kumshauri na kumsaidia ili ajue kile kinachotakikakana kufanyika. Pengine masikini aliutaka urais kwa mteremko lakini kakuta sasa ni kupanda jilima hasa jilima zaidi ya Eversts niini Kilimanjaro!! Pole mjomba ushauri wangu ni huu. Lazima udhibiti serikali yako. Huwezi kuwa na usalama wa Taifa wanaowapelekea taarifa marais na mawaziri wakuu wa zamani na wewe ukasema kweli uko kwenye kiti cha udereva wa nchi hii.
   
 2. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ningekuwa Kikwete naitisha mkutano wa halamshauri kuu ya taifa na kuwambia wale wote wanaojifanya wapiganaji wa ufisadi na wale wanaotuhumiwa kwa ufisadi wote wajiuzulu nyadhifa zao na wale ambao ana uwezo wa kuwatimua awatimulie mbali!Aanza na safu mpya ya watu wataye kisaidia chama na serikali yake!
  Makundi yote ayatimue !Au la sivyo atakuwa ana yumbishwa na kuonekana Rais asiye kuwa na maamuzi!
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuwalundikia lawama maafisa wa Ikulu kwa mtazamo wangu naona si sahihi. Rais hahitaji kushauriwa maana yeye kama hao washauri anaona na anajua kinachoendelea ni nini. Yeye kama Rais anayo madaraka yake tena makubwa kabisa ya kuweza kuamua kutenda jambo analoona linafaa kwa manufaa ya Taifa bila kutafuta ushauri kutoka kwa mtu yeyote.

  Juzi niliwasikiliza wale Wazee na Wanasheria kwenye Kongamano lile wakitoa ushauri kwamba Rais anahitajika kufanya MAAMUZI MAGUMU ili kuinusuru nchi kutokana na hatari inayoonekana mbele yetu. Kwa maana hiyo basi uwezo wa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya taifa anao lakini kama hataki kuchukua uamuzi hakuna yeyote aliyekaribu naye ama wananchi kwa ujumla wanaoweza kumlazimisha kuchukua uamuzi. Kwa maana nyingine mustakabali wetu kama taifa uko mikononi mwake yeye na si washauri wake!
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wapambanaji dhidi ya ufisadi wanafanya hivyo baada ya Kikwete kushindwa kukemea na sio wanajifanya. Kwani wewe huamini au hujui kuwa mnaotuhumiwa ni kweli mna vitendo vya kifisadi?
   
 5. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Rais wetu hana nguvu juu ya hawa mafisadi.
  Nadhan chakufanya nikuondoa serikali yao ya CCM tuanze na wengine. tumechoka. hawana jipya. hawarekebishiki
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
   
 7. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Tatizo Muungwana ni Mvivu...Si mtu wa kujisomea hata magazeti...anapenda kufanyiwa kila kitu...Hawa watu wa karibu yake wanamshauri vibaya...Hakuna lolote la maana alilofanya katika uongozi wake wa miaka 4......anachojua ni kusafiri..kupigiwa makofi,kula vizuri,wanawake na kuvaa vizuri!...(Typical mswahili).Serikali inaendeshwa kama Danguro kila mtu ana lwake!...Hata junior ministers wanamuona Chief wao kama mtu mzembe,Mbabaishaji na mjinga....Nahisi kabisa Kikwete ataomba kwa hiari yake kuachia Uongozi ili Mwanachama mwingine wa CCM amalizie Nngwe iliyobaki ya miaka Mitano.
   
 8. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Home of great Thinkers

  sasa akishakwenda na maji nani anachukua? Please dont tell me ni Freeman Mbowe au CHADEMA
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Home of great Thinkers

  sasa akishakwenda na maji nani anachukua? Please dont tell me ni Freeman Mbowe au CHADEMA
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Januari Kamba
   
 11. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Sasa kama washauri wako ni aina ya akina Makamba snr na Makamba Jnr,Sophia Simba na akina Salva kwa mbali na akina Mamvi na rosttamu utegemee nini kama si uiozo?
   
 12. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki tanzania
   
Loading...