Kikwete amewadhulumu WaZanzibari

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,608
1,743
seif.JPG

Katibu Mkuu wa chama upinzani (CUF), Seif Shariff Hamad, ambaye ameondoka nchini kwenda nchi za Ulaya ambako inadaiwa atakishtaki chama tawala (CM) kwa kuzorotesha muafaka wa kisiasa Zanzibar.


Maalim Seif wa CUF aenda Ulaya kuishitaki CCM
*Kueleza uamuzi wa Butiama Jumuiya ya Madola
*Kukutana na mawaziri wanaoshughulikia Afrika
*Balozi wa Marekani kukutana na wabunge Pemba

KUKWAMA kwa utiaji saini makubaliano ya mwafaka wa kisiasa visiwani Zanzibar yaliyofikiwa kati ya Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumezidi kuibua mambo, baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho cha upinzani, Seif Shariff Hamad kuondoka jana kwenda nchi za Uholanzi na Uingereza kuishitaki CCM.
Katika ziara hiyo, ambayo hata hivyo haijulikani atatumia siku ngapi, atakutana na watu mashuhuri nchini Uholanzi na Uingereza ambako pia atakutana na uongozi wa Jumuiya ya Madola kueleza jinsi CCM ilivyokiuka makubaliano ambayo vyama vyote vilikuwa vimefikia katika majadiliano.Akizungumza na Mwananchi, Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye pia ni mbunge wa CUF, Hamad Rashid alisema kwamba kutokana na uamuzi wa CCM kurudisha nyuma hatua iliyokuwa imefikiwa katika mwafaka, kiongozi huyo ameamua kutumia nafasi hiyo kueleza ukweli jumuiya za kimataifa na nchi wafadhili ili wainusuru Zanzibar kabla janga kubwa halijatokea.
Wakati akizungumza na waandishi wa habari juzi, Maalim Seif aliitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia suala hilo kwa lengo la kunusuru mgogoro ambao unaweza kuibuka katika Visiwa hivyo baada ya kile alichokiita CCM kurudisha nyuma mwafaka.
Baadhi ya wanasiasa na wasomi wamepinga hatua ya CCM kurudisha suala la mwafaka kwa wananchi kwa maelezo kwamba itachochea hali ya uhasama kuliko kuleta amani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoifikia Mwananchi, akiwa nchini Uholanzi, Maalim Seif atajumuika na viongozi 40 mashuhuri duniani katika mkutano ambao unazungumzia masuala ya utatuzi wa migogoro.
Maalim Seif katika mkutano huo, anatarajia kuwaeleza wajumbe hao jinsi ambavyo mwafaka wa chama chake na CCM ulivyokwama. Mjumbe mwingine kutoka Tanzania anayeshiriki kakika mkutano huo, ni Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Afrika (AU), Salim Hamed Salim.
"Katika mkutano huo, Maalim Seif awali alipanga kuelezea mafanikio ya mwafaka, lakini sasa ataeleza jinsi CCM ilivyowahadaa wapenda amani katika suala hilo," alisema Ismail Jussa ambaye ni Msaidizi wa Katibu Mkuu CUF.
Jussa alisema kwamba pia Maalim Seif atakutana na maofisa wa mambo ya nje ya nchi ya Uholanzi na kuwaeleza kwa kina jinsi CCM walivyotumia usanii kuwahadaa katika kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar.
Wakati Katibu huyo akiwa nchi za nje, tayari maafisa wa Chama hicho wameanza kukutana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania. Jana walikutana na Balozi wa Norway nchini na kueleza kilio chao kwa jinsi CCM ilirudisha nyuma mwafaka.
"Tuna mpango wa kutembelea balozi zote nchini ili kuonyesha jinsi CCM wasivyoitakia amani Zanzibar, pia tumeandika barua pamoja na tamko la chama kwa balozi zote nchini," alisema Jussa.
Alisema kabla ya Maalim Seif kuondoka juzi kuelekea Uholanzi, alimwandikia Rais Kikwete barua kuelezea masikitiko yake kuhusiana na suala zima la kile alichokiita unafiki wa CCM.
Pia chama cha CUF kinatarajia kufanya mkutano na wanahabari wakati wowote kuanzia sasa na kugawa makubaliano ambayo walikuwa wamefikia na CUF ili waweze kuwaonyesha wananchi.
Katika hatua nyingine, Balozi wa Marekani nchini, Mark Green, ameomba kukutana na wabunge na wawakilishi wanaotoka Kisiwani Pemba kuzungumzia mambo mbalimbali, likiwamo suala hilo.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam jana, zinaeleza kuwa Balozi Green anatarajiwa kukutana na wabunge na wawakilishi hao kisiwani humo keshokutwa.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa Upinzani Bungeni Hamad Rashid, Balozi Green amefikia uamuzi huo ikiwa ni siku moja baada ya CUF kuwaomba marafiki wa Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua madhubuti na za haraka kuingilia kati mgogoro huo.
Hamad ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa, alisema wamepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani inayofahamisha kwamba, Balozi huyo atakutana na wabunge na wawakilishi wanaotoka Pemba.
"Ni kweli tumepata taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani nchini ukielezea uamuzi wake wa kukutana na wabunge na wawakilishi wanaotoka Pemba siku ya Jumamosi," alisema Hamad.
Hata hivyo, Hamad ambaye pia ni Waziri Mkuu Kivuli, hakueleza eneo ambalo Balozi Green atakutana na wabunge na wawakilishi hao kisiwani humo.
Lakini alisema, mazungumzo kati ya Balozi Green na wabunge na wawakilishi hao ambao karibu wote wanatoka CUF, yatahusu hali ya siasa, maendeleo na mwafaka wa kisiasa visiwani humo.
Serikali ya Marekani kupitia Balozi huyo, imekuwa ikihimiza haja na umuhimu wa kupatikana haraka kwa mwafaka wa kisiasa Zanzibar ili kuleta utengamano, maelewano na maendeleo miongoni mwa wananchi visiwani humo.
Suala la mwafaka lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kuamuliwa na NEC baada ya kudumu kwa takriban miaka miwili chini ya makatibu wakuu wa vyama hivyo, Yusuf Makamba (CCM) na Maalim Seif Shariff Hamad (CUF).
Akisoma tamko la kikao cha NEC kwa wajumbe wake na waandishi wa habari baada ya kumalizika Machi 30, mwaka huu, kijijini Butiama, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, alisema halmashauri hiyo, iliyakubali mapendekezo yaliyomo katika taarifa ya mazungumzo ya mwafaka kati ya CUF na CCM, lakini imetaka suala hilo likaamuliwe na wananchi wa Zanzibar kwa kura ya maoni.
Hata hivyo, CUF kinapinga hoja ya CCM ya kutaka ifanyike kura ya maoni Zanzibar na kukitaka chama hicho kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Mazungumzo ya Vyama hivyo, ikiwa ni pamoja na kutia saini makubaliano hayo na kuyatekeleza mara moja.
Katika mazungumzo yao yaliyochukua takriban miezi 14, pamoja na mambo mengine, CUF ilidai kuwa walikubaliana na wenzao wa CCM kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, maarufu kama "serikali ya mseto" itakayoshirikisha pande mbili za vyama hivyo.
Maalim Seif alisema kinyume na hayo, CUF inatoa wito kwa marafiki wa Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kchukua hatua madhubuti za uhakika na za haraka kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisa makubaliano yaliyofikiwa yanatiwa saini.
 
Hakuna hata mtu mmoja ambae ametoa sapoti kwa Mh.Kikwete ,mambo ambayo yamechukua miezi kumi na nne,na yeye kuchukua ahadi kwa kila mtu kwamba atamaliza mgogoro ,bila ya shaka alijiaminisha kuwa yeye ni Raisi na Mwenyekiti ,je watu wa Mataifa ya nje watamwamini tena ,huo Uwenye kiti wa AU umeshaingia doa kubwa itabidi ajiuzulu na mapema kabla hajatolewa nishai ,naamini Wakenya watatupita na wazimbabwe nao hao wanaelekea kwenye mseto nao watatuacha mbali.kila nikipima naona jinamizi la mapambano ya ndani linaitembelea Tanzania.Kama nilivyosema nyoka alikuwa mbali na sasa ameshapita Kenya sijui kama ataruka na kurukia Zimbabwe kabla hajakatiza Tanzania.
 
Hakuna hata mtu mmoja ambae ametoa sapoti kwa Mh.Kikwete ,mambo ambayo yamechukua miezi kumi na nne,na yeye kuchukua ahadi kwa kila mtu kwamba atamaliza mgogoro ,bila ya shaka alijiaminisha kuwa yeye ni Raisi na Mwenyekiti ,je watu wa Mataifa ya nje watamwamini tena ,huo Uwenye kiti wa AU umeshaingia doa kubwa itabidi ajiuzulu na mapema kabla hajatolewa nishai ,naamini Wakenya watatupita na wazimbabwe nao hao wanaelekea kwenye mseto nao watatuacha mbali.kila nikipima naona jinamizi la mapambano ya ndani linaitembelea Tanzania.Kama nilivyosema nyoka alikuwa mbali na sasa ameshapita Kenya sijui kama ataruka na kurukia Zimbabwe kabla hajakatiza Tanzania.

\

JK ameshindwa hili sasa ndiyo mjue kwamba lile la Kenya hakuliweza kalikuta na akamaliza nalo maana uwezo wa kumaliza hana na kipimo chake ni Zanzibar mnasemaje ?
 
Whatever happenned to the charismatic alleged statesman-diplomat who brokered a deal that Annan,Mkapa and Machel could not in Nairobi?
 
Whatever happenned to the charismatic alleged statesman-diplomat who brokered a deal that Annan,Mkapa and Machel could not in Nairobi?

Alipoenda Mererani aliambiwa kuwa mashine kubwa za kutoa maji zimefika na in 2 days zitaweza kutoa maji yote hivyo miili itaweza kutolewa yote.

Alipofika jukwaani akasema, natoa siku tatu uokoaji miili ukamilike. ahahahahhaha

Michezo ya kuigiza mingi tu tanzania. Wenzako wanashindana na ze comedy.
 
Waungwana,
Nafikiri hapa hatumdei haki JK, yeye ameonyesha dhamira kubwa kulishuburikia swala la Zanzibar lakini ili amani ya kudumu ipatikane ni lazima wazanzibar wenyewe waikubali.
Sasa rejea makala ya gazeti la Raia Mwema lilolonukulu yaliyokuwa yakisemwa na wajumbe wa NEC Zanzibar na hotuba ya JK leo.
Utaona kuwa wazanzibar wenyewe hawajawa tayari kumaliza tofauti zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom