Kikwete ameufanya Urais uonekane ni mrahisi; Kila mtu anataka kuwa RAIS! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ameufanya Urais uonekane ni mrahisi; Kila mtu anataka kuwa RAIS!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Oct 4, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania JK ameufanya uraisi wa TZ kuonekana ni kazi inayoweza kufanywa na mtu yeyote bila uwezo, utashi, fikra na sababu za kusaidia watanzania ila uchu tu wa kuishi ikulu na kusafiri kwa ndege.

  Leo hii kila aliyekaribu ya JK anataka kuwa raisi kwani anaamini ni kazi rahisi na kusafiri tu huku nakule. Tunashuhudia vijana kwa wazee wameacha kufanya kazi za kuwaletea watanzania maendeleo na kushadadia uraisi eti tu wanauwezo.

  Tukianzia hanang na munduli kule kuna mafisadi eti wanataka kuuwana ili tu waende ikulu. Ukiangalia uwezo wao wa kuongoza nchi unapata mashaka makubwa sana, kama ulikuwa waziri mkuu kwa miaka kumi huna kitu cha kutueleza ulifanya zaidi ya kufurahia msafara usio na foleni ni nini. Mwingine aliondoka kwa kashfa ambayo hajawahi kuilezea inatutesa mpaka leo tunalipa madeni ya fedha zilizokwenda mifukoni mwao.

  Vijana wameacha kufanya kazi wanalilia uraisi, tukienda kigoma kaskazini rafiki yangu amesema yeye hawezi kugombea tena ubunge kwani hawezi kuwaletea tena wananchi wake maendeleo zaidi ya aliyoyafanya, ila anataka uraisi. Hapo nimejiuliza sana kama kajimbo kamoja umefikia mwisho wa uwezo kuwahudumia je kweli utayaweza majimbo zaidi ya 189. Nimetafakari sana, je raisi wa TZ anachaguliwa kwa vigezo vya kushindwa kuwa mbunifu, mwenye fikra sahihi za kuwaletea watu maendeleo endelevu?? Ni kweli jimbo la kigoma kaskazini limefikia ukomo wa maendeleo??

  Kijana wetu wa Bumbuli yeye ameamua kujikita kwenye kampeni bubu za kuusaka uraisi kisa tu aliwahi kushika mabegi ya JK. CV yake ni kutembea nchi nyingi na JK kuishi ikulu na kupita bumbuli kwa mgongo wa katibu mkuu wa magamba na kumwangusha shelukindo na kukosa mpinzania, mwenyekiti wa tume ya kudumu ya madini aliyoiacha na kashfa iliyosababisha kusambaratishwa. Je kawafanyia nini wana bumbuli ili tuweze kumpima au na yeye amemaliza mbinu??

  Membe anausaka uraisi kwa uwezo wa kuzunguka na JK. tumuulize watu wa mtama wana hali gani? kweli wako bora leo kuliko 2005. Ni kipi chema anaweza kutueleza kwamba amewafanyia watu wa mtama atawafanyia watanzania? JK aliingia madaraka bila record yeyote ya uwajibikaji na anatoka akiwa anatabasamu kwani aliingia na tabasamu tu.

  Mzee wa tabora Sita yeye anaamini bila yeye haliwezekani. Undumila kuwili na uchu wa madaraka yuko radhi afanye lolote kwani anaamini JK ni mtupu kuliko yeye. Ila na yeye kawa mbunge jabla wengi hatujazaliwa. Twendeni jimboni mwake tuulize wananchi wake kipi cha kutufanya tumuone atatufaa kuwa Raisi wetu zaidi ya uchu wa kupakia ndege first class??

  JK ameufanya uraisi mrahisi sana kiasi cha watu kuacha kufanya kazi na kuwa wabunifu na wote kupigana mieleka ya kusubiria kuingia ikulu mika mitatu kutoka leo. Makundi yote haya yanasigishana ndani ya vyama vyao vya siasa na kutengeneza ufa mkubwa wa uwajibikaji na kuacha wananchi wakikosa huduma za kiuongozi kwani wanawagawa wananchi na kushindwa kuwajibika. Mijizi imejificha kwenye kivuli hiki cha eti wivu au vita vya makundi ya kuingia ikulu 2015. Kwa sasa Tanzania imesimama kwani kila mtu anataka kwenda ikulu hata ikibidi kwa kuwafanya watanzania masikini.

  Ndugu zangu kwa sasa kila anayetaka kwenda ikulu tumuulize je amewafanyia nini watanzania?? Je Jimbo lake kweli amelihudumia kwa nguvu zake zote akili zake na weledi usio na mawaa, je amewahi kutuhumiwa au kuhisiwa kuibia jamhuri ya muungano na watu wake kwa madaraka yake au kuihujumu??

  Tuangalia rekodi za utendaji wao bila kujali itaikadi zao kwanza kwani mwisho wa siku tunampata Raisi wa Tanzania sio chama cha siasa tena.
  KILA MWENYE UCHU WA MADARAKA LAZIMA ANAKITU BINAFSI ANAKIHITAJI SIO KUTUHUDUMIA.

  Ni maneno ya
  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Naipenda nchi yangu na watu wake - umasikini wa mtanzania ni wa kutengenezwa
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hata mimi nautaka
   
 3. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Asante kaka sio urais hata ubunge kina lusinde wameufanya kuea mrahisi
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Hapana hajaufanya URAIS RAHISI; Ameufanya URAIS LEGELEGE... Kila MTU anaona kosa... hata MTOTO MDOGO anaona KOSA na anataka kulirekebisha an ili kulirekebisha kwa UCHOYO WAKE BADALA ya kusema jinsi
  ya kurekebisha MAKOSA ya RAIS WETU huyo MTOTO anataka kwa UDI na UVUMBA kuwa RAIS...

  Wakati wa MWL. NYERERE tulikuwa na SHIDA zaidi ya Sasa lakini alikuwa anaongea kwa kutupiga MSASA
  kila mtu alikuwa anajiona kama KICHUGUU, anaona WAHAH siutaki URAIS nitanung'unika chinichini tuuu basi alikuwa anatupa phrases; vocabularies, text alafu anatuacha tufikirie kwa butwaa... hatuoni matatizo yetu na tunakuwa UGALI WA YANGA...

  Angalia Sasa hivi tuna hadi pesa USWISI, tuna Ma-RANGE ROVER na Majumba ya Kifahari na bado tunaona

  Kasoro za Rais wetu kila mtu anataka cheo chake; Hauni ni MUFLISI wa KISIASA ??? na SIO URAHISI wa URAIS >>>
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,354
  Trophy Points: 280
  Unajua title imenishtua...nikadhani umempa Jk sifa za kuwa na extraordinary skills kiasi cha kufanya mambo kwa njia rahisi na yenye ufanisi sana.Nilidhani ningekuta JK`s Theories and Laws kibao....teh teh...Kumbe ni kama kusikia mtu mwenye hela Sumbawanga akiitwa prof.Kama ana umri mdogo unaweza ulizia kuna project gani kule?Ama kuna univeristy gani?ama kwanini kajiuzulu mapema..kabla hujashtuliwa kuwa ni manga maarufu, kama ilivyo kwa prof Long/deep water.
   
 6. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu, wabunge wengi wanakula mshahara wa bure. Hawana sifa hawafai hawana historia ya utendaje popote pale. Tuache kuokoteza watu barabarani imefika wakati tukubali midahalo kwa lazima ili kuweza kuchambua pumba na mchele.
   
 7. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yes if lusinde and mwigulu can why cant i?
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hapo wengi watakimbia, unakumbuka katika kuelekea uchaguzi uliopita namna wale wagombea wa CCM walivyokuwa wanakiaibisha chama kupitia midahalo??
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mimi naamini namzidi kwa mbali sana, ila sio lazima wote tuwe Maraisi, ila huyu hata. Mimi sikumpa kura kabisaa.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,320
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Na mimi naomba kuwa Rais basi kama urais umefanywa rahisi....well kwa mtazamo wangu watu wanataka madaraka ili wajineemeshe kuliko kuwa kazi rahisi
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa wengi wameacha professions zao na kukimbilia huko. Najiuliza hivi ni mwanasiasa gani ambaye ni Political Scientist?
   
 12. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  mwenye kichwa cha nazi!
   
 13. Mwamba Usemao Kweli

  Mwamba Usemao Kweli JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Mkwawa, nimefurahi kufahamu kuwa kuna watanzania wengi tunaoshuhudia uliyoyasema na ni kweli kabisa na ninaomba M4C waendelee kuwaelimisha watanzania wawatambue watu hawa C.C.M na wengineo wanafikiria kwamba uraisi ni kazi rahisi sana kama alivyo JK dhaifu.

  JK ametufedhehesha sana watanzania na naamini mara baada ya muhula wake kukamilika yeye na mafisadi wenzake akina Beny watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashitaka na tuhuma mbalimbali za matumizi mabovu ya rasilimali za umma.
   
 14. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Hapo Mkwawa umenena, maana mambo ya msingi na magumu tumeyafanya mambo rahisi na ya mazoea. Ni kama kwamba hakuna tena miiko na taratibu za kuwa kiongozi, tena wa nchi!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Nasikia mining'ono ya sumaye kutaka kuhamia CDM. Kati ya makosa CDM watayafanya ni kuendeleza utamaduni wa kuwachukua waliogombana au kushindwa CCM ili kuja kugombea CDM.

  Sumaye hafai kuwa hata mbunge wa CDM. Alishindwa kabisa kwenye uwaziri wake mkuu. Hana rekodi ya uwajibikaji wala kuwawajibisha walio chini yake.

  Ikumbukwe tu wakati deepgreen, kagoda, EPA, minara pacha, nk wanakwapua yeye alikuwa waziri mkuu na alikaa kimya kama hajui kitu. No Sumayi hata akichukua kadi awe mwanachama tu kwani ni haki yake kikatiba.
   
 16. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sumaye ni fundi nchundo.
   
 17. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Kama lusinde,nchembas,na lakaro ni wabunge mimi nitashidwa je? Kama jk kila kukicha yuko kwenye dege shibuba ,zzk,saba,membe watashidwaje?kila mtu anaweza kuwa rais na mbunge!

  TANZANIA YENYEWE NI MAAJABU 7 YA ULIMWENGU!
   
 18. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mkwawa mimi nina swali moja tu. we binafsi unamwona nani anafaa kua rais 2015?
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,707
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu, ikiwa huyu bingwa wa kukenua kenua ameweza kuwa rais tangu 2005 mpaka leo hii 2012 basi kila mtu anaweza kuwa rais ili mradi tu unamajeshi ya kuweza kutii amri dhalimu basi umemaliza, unaweza hata kuwa rais wa milele.
   
 20. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Aisee! Kweli Tanzania tuna safari ndefu. Nimsaidie kukujibu. Ni wewe ndiye unayefaa

  hii inaonesha hata hukumuelewa kabisa alichomaanisha kwenye makala yake.
   
Loading...