Kikwete ameteleza kushinikiza gas kupelekwa Dar es Salaam

----- huu kama la Songas linatosha mbona tuna mgao wa umeme?

Mgao wa umeme unatokana na sababu nyingi sana, sio uhaba wa gesi tu. Kunaweza kuwa na uzalishaji wa kutosha (kama ilivyo sasa)lakini miundombinu ya isafirishaji na ugavi wa umeme isiwe ya uhakika. Ndio sababu kubwa ya mgao unaoendelea sana. Gridi imezidiwa, uzalishaji umeongezeka lakini gridi haiwezi kuhimili ongezeko hilo. Ukilazimisha kuigniza umeme zaidi basi gridi nzima inazimia.

huwezi kulazimisha viwanda viwe wapi zaidi ya soko kuamua...
Sijalazimisha, nimeshauri. Kuna nadharia nyingi sana za kichumi, kisayansi na kijamii za kuamua kiwanda kiwe wapi. Nadhani tunahitaji thread ya kujitegemea kujadili hilo!
 
Kimsingi kuna mambo ambayo hayako sawa ambayo nadhani ndio yanaweza kutuletea matatizo(kama tahadjari na umakini hautazingatiwa)

-Wananchi wa kusini hawako 'well informed' juu ya nafasi yao katika kunufaika na rasilimali husika,kinachotokea ni kwa viongozi na wataalamu kutoa kauli zao tena wengine kwa kashfa jambo mbalo linaongeza 'frusturation' kwa wananchi kila uchao na kupoteza imani,maelezo ya kina juu ya namna watakavyonufaika hayaepukiki.

-Suala la gesi lingeweza kueleweka na wananchi kuwa watulivu tu na kukubali matokeo kama ambavyo baadhi ya sehemu zenye rasilimali zingine wananchi wamejikalia kimya na kuiacha serikali ifanye itakavyo-though it is a time bomb!

-Kinachotokea ni ule ule mwendelezo wa 'top down' na mwenye nguvu mpishe! Wanasiasa wanajaribu kupanga karata zao,hivi mchakato mzima wa bomba unaanza mpaka kuzinduliwa ujenzi wananchi hawakuwepo? kwani seriki haikujua kuwa kuna maswali ambayo hayajapata majibu? what if wananchi wasinge andamana ..that means ndo ingekua mbele kwa mbele na ku assume kua kila kitu kiko shwari..of which si sahihi.Frankly speaking mifumo inayotumika katika kufanya maamuzi juu ya rasilimali za uma imekua na usanii mkubwa!

-ni kweli kuwa kusafirisha umeme to dar ni gharama kuliko gesi,ila hii pekee inatosha kuwa justification kwa wananchi wa kusini? wananchi waambiwe waelewe ili nao wawe sehemu ya mchakato.Tuache tabia za ku-suppress mawazo mbadala,tuyafanyie kazi.tatizo la sasa kila mtu anapretend kuwa expert! wanasiasa wanajiona wao ni think tanks na manabii wadogo-kila kitu wanajua wao!kwani nchi haina mipango ya muda mrefu na mifupi ya nishati? na inasemaje?
 
Thanks, unaonekana kuyajua vizuri mambo yaliyoko huko jikoni, wapishi wanavyo tupia kando viungo vuzuri vilivyoandaliwa na wao kuwaka makorokoro yao wasiyotaka walaji.
Asiposikilizwa mwananchi aliyewaweka madarakani watamsikiliza nani?
Mwamko wa wananchi wa leo natia khofu usalama wa miundombinu hiyo, sina maana ya kutisha kama alivyosema mdau mmoja, lakini ukweli historia ni mwalimu mzuri kama ulivyosema yaliyotokea Mara.
Ikifika hapa ndipo ninapopatwa na uchungu sana. huwa ninajuta kwa hii mifumo ya kulishwa na wazungu yaani demokrasia. Kila kitu waulizwe wananchi?? kuna vitu vya kuwauliza lakini si hivi vya kitaalamu. Hivi kama 95% ya watanzania ni mabogasi wa mambo ya umeme na gesi bado tuwaulize tuu?? Kwani gesi ikija dar hawatafaidika?? kwani Dar hatupo watu wa Mtwara?? Vipi kama the big 4 nao wakasema hawasafirishi mahindi tena ila kama unataka ukajenge mashineza kusaga nafaka kulekule?? Hizo mbegu za ukanda mnazozipanda bila kujali matokeo yake zitawatokea puani. Mmeanza kulewa sifa hata kabla ya sherehe?? Msitumie ujinga wao kutaka kuvuruga mipango ya maendeleo ili neno litimie. tutapoteza imani kwenu
 
wewe mpungufu wa mawazo unashindanda mpaka na financial magerzine mbalimbali duniani zinakomet kama wrong project hiyo cake inataka kuliwa na wachahe tu
 
Mtwara Nadhani imelaaniwa toka kitambo!!! Nipo Mtwara kwa shughuli zangu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa but yanayoendelea ni aibu kuyasema, Kabla ya Hili la GAS Nilitaka wananchi wa Mtwara waungane na Kumng'oa KANJI BAI ambae ndo mbunge wao, hana msaada zaidi ya kutumia fulsa ya yeye kuwa mbunge kuilinda Diplomatic Passport yake, pia Kama vila la Mbunge halitoshi wakachagua KANJI BAI mwingine kuwa Mwenyekiti wa Mkoa CCM, najua nitaibua hisia za watu wasioipenda CCM hapa lakini kama unafuatilia mambo mengi ya kisiasa hapa nchi basi maamuzi mengi ya Serikali yetu hufanywa na SISIEMU kwenye vikao vyao vya NEC na Kutekelezwa na SERIKALI yake, hivyo kuwa na watu wawili ambao nathubutu kusema kuwa sio watanzania potelea mbali nikiitwa MBAGUZI lakini sio watu amabao wanaweza kuwatetea WANAMTWARA kwenye shida zao. HIVYO UKOMBOZI WA MTWARA UANZIA HAPO KWANZA NA WAKIWA NA WAWAKILISHI MAKINI BASI NAFASI YA MADAI YA MSINGI HASA HILI LA GAS BASI LIOTAWEZEKANA. INATOSHA SASA KUTAWALIWA NA WAGENI
Tuhakikishie wewe huitaki hiyo nafasi ya Kanji Bai kwanza...maana gas ni zaidi ya siasa za hapa na pale tukiangalia kwa makini.
 
Tupo pamoja na watu wa mtwara hakitoki kitu hapo.kama rais unazungumzia usawa .mbona mikoa ya kusini ipo nyuma???????.acha kuimba tarabu.kila mwanamchi amwelimishe kak,shangazi baba,mabibi kuwa gesi ni muhimu kwa maendeleo pale pale mtwara sio kupeleka huko mbali.vijana wanataka kazi pale mtwara na sio kukimbilia kuomba ajira mbali.stop stop stop stop .tuma msg kwa kila mtu ongea ana kwa ana na mwenzako hapo mtwara .wana mtwara haturudi nyuma tena
 
Hao ma-KHANJ BAI unaowasema mkuu ni watu wadogo sana, Mtwara na Lindi ina mawaziri katika serikali hii ambao kama wangekuwa na uwezo wa kujenga hoja kwa maana ya kuwa na uchungu wa kimaendeleo ya kusini, sidhani kama hata hilo wazo la kusafirisha gesi kwenda Dar kama lingekuwepo. Tatizo wabunge-mawazi wetu ni mazuzu. Nafikiri sasa hivi muda umefika kwa watu wa kusini kuangalia upande wa pili wa shilingi. CCM tumekuwa nayo kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote, hata kuanza kwa miradi ya gesi na mafuta ni juhudi binafsi za ex-president Ben. Mkapa. Otherwise nawashauri wenzangu wa Mtwara tujaribu kubadilisha, wabunge wa CCM hawana faida na sisi.

hahahah! utawaambia nini hao wabunge wa CCM, wanajli matumbo yao tu na kuna waziri mmoja kila siku anaota u-rais, anafanya jitihada kubwa kuandaa sherehe za wajumbe wa NEC wilayani kutengeneza mtandao, amkeni wana Kusini, huyo hafai kuwa rais,
 
Kashfa,dharau,matusi au lugha ya ukali sio dawa ya kukwepa hoja.
Kiwango cha elimu sio kigezo cha mtu kutoa hoja yenye mashiko.wapo watu wana elimu lakini hawaja elimika.hapa watu wanaakili zao timaaam.hoja na hoja ndio ziwe zenye nafasi.
 
hii nchi inaongozwa na watu wenye akili ndogo sana, kwakuangalia mambo aliyotamka jk mwisho wa mwaka unagundua kabisa huenda pale ikulu amejaza waganga wakienyeji na wapika majungu ambao hawaezi kumpa msaada wowote katika kuendesha nchi, siamini kama rais ambae yuko vizuri kichwani na kuwa na washauri ambao ni credible anaweza kusema watanzania tuko wengi tuache kuzaana, analeta gesi dsm kwa sababu wanalipa kodi kuliko mikoa mingine hili ni wazo la kijinga, hiyo kodi dsm inatokana na nini? hao wafanabiashara bidhaa wanauza wapi? kwa kuwa azam iko dsm kodi wanayolipa inatokana na mauzo ya dsm pekee? au kwa kuwa benki zote makao makuu yako dsm kwa hiyo kodi wanazolipa zinatokana na faida inayotokana na matawi dsm pekee? raw rubbish, kama umempa riziwan tenda ya kutandika maboma ya gesi toka mtwara hadi dsm safari hii mwambie atafute deal ingine, huyo professa muongo anasema gesi ya mtwara ni kidogo nyingi iko kwenye kina kirefu basi mkaivute huko kwenye kina kirefu mpitishe bomba baharini hadi bagamoyo kwani lazima lipitie mtwara? hii nchi tatizo ni kukubali akili ndogo itawle akili kubwa.
 
Ikifika hapa ndipo ninapopatwa na uchungu sana. huwa ninajuta kwa hii mifumo ya kulishwa na wazungu yaani demokrasia. Kila kitu waulizwe wananchi?? kuna vitu vya kuwauliza lakini si hivi vya kitaalamu. Hivi kama 95% ya watanzania ni mabogasi wa mambo ya umeme na gesi bado tuwaulize tuu?? Kwani gesi ikija dar hawatafaidika?? kwani Dar hatupo watu wa Mtwara?? Vipi kama the big 4 nao wakasema hawasafirishi mahindi tena ila kama unataka ukajenge mashineza kusaga nafaka kulekule?? Hizo mbegu za ukanda mnazozipanda bila kujali matokeo yake zitawatokea puani. Mmeanza kulewa sifa hata kabla ya sherehe?? Msitumie ujinga wao kutaka kuvuruga mipango ya maendeleo ili neno litimie. tutapoteza imani kwenu

Utaalamu wa umeme na gas nini? Hakuna binadamu asiyekuwa na ufahamu wa mambo muhimu anayohitaji katika maisha yake. Unaowaita wataalamu ni mfumo tu wa kizungu wa kuandika kwenye makaratasi kwa mpangilio fulani. Mababu zetu walikuwa na elimu nzuri na kuweza kufanya mengi ya ajabu na wazungu hao wasingeharibu maendeleo hayo sina shaka mengi wangeshayavumbua. Sio wazungu waliovumbua nyengo za kufyekea, majembe, mapanga, shoka, visu. Waliweza kugundua baadhi ya mawe yenye madini ya chuma wakichomwa moto huyehuka, na kuganda yakipoa, ndipo walipogundua kuyachoma moto yakeshapata moto mkali kuyapondaponda kwa kuyaunda majembe, nyengo, mapanga, visu, nk. Hayo walifunzwa na wasomi gani miaka hiyo kama si akili zao mababu zetu?

Nikuambie: Je, wajua elimu ya PHD nini?
Kwa taarifa yako kama huna PHD nikufahamishe hakuna tofauti na wazee wetu vijijini wanapokaa kwenye vikao vyao na kushinda kwa hoja ni hicho ndicho wanachofanya huko kusomea PHD. Haitofautiani na mambo ya kushindana kwa hoja vijiweni, ila kule kuna hoja inayotolewa na kujadiliwa iwe oral or written kwa kuhakikiwa na mwingine au jopo la watu wengine.

Historia ya falsafa ni wagiriki (wayunani) hasa wazee wale waliokuwa wanashindana falsafa kwenye kile kilima cha Aleopago walipokuwa wazee wa kiyunani wakishindana hoja, na vijana akina Sokrates, Plato na Aristotle kwa nyakati tofauti wakawa wanawasikiliza wazee wale. Hawa vijana wameanza kujulikana kama mabingwa wa falsafa ni kwa sababu tu waliweza kunakili hoja za wazee wale pale kilima cha Aleopago katika maandishi tofauti na wazee wale ambao waliwafundisha hayo hawakuyaweka kwenye kumbukumbu kimaandishi. Leo hao wanaonekana ndio wasomi waliobobea kwa falsafa.

Huo utaalamu unaotueleza ndio unaotuharibia nchi kila leo na hao unaowasifia ndio wanaouza rasilimali za nchi yetu kwa wazungu na kuwaacha wajichumie utajiri wa nchi yetu hata kodi yenyewe wanasamehewa, huo ndio utaalamu unaouona wewe hawa wanao?

Jaribu kuingiza pua nchi za wazungu uone kama unaweza kufanya kama unaowaita wasomi wanavyowahemekea wazungu huku wakichota utajiri wetu na kuhamishia kwao.


 
Tuhakikishie wewe huitaki hiyo nafasi ya Kanji Bai kwanza...maana gas ni zaidi ya siasa za hapa na pale tukiangalia kwa makini.

Nafasi ya KANJIBAI ni ngumu na sio kila mtu anaweza kuwatimizia wananchi dhidi ya matatizo yao so kuhusu nafasi yake kwangu haina nafasi maana kafanya kazi na safi iliyopo ya walaji na mimi naweza ishia kuwasahau wenye shida plus watu wa Hapa wako ladhi KANJIBAI awawakilishe kuliko mtu toka pande nyingine ya nchi hii mwenye uwezo wa kuwasaidia awe representative wao.
 
hii nchi inaongozwa na watu wenye akili ndogo sana, kwakuangalia mambo aliyotamka jk mwisho wa mwaka unagundua kabisa huenda pale ikulu amejaza waganga wakienyeji na wapika majungu ambao hawaezi kumpa msaada wowote katika kuendesha nchi, siamini kama rais ambae yuko vizuri kichwani na kuwa na washauri ambao ni credible anaweza kusema watanzania tuko wengi tuache kuzaana, analeta gesi dsm kwa sababu wanalipa kodi kuliko mikoa mingine hili ni wazo la kijinga, hiyo kodi dsm inatokana na nini? hao wafanabiashara bidhaa wanauza wapi? kwa kuwa azam iko dsm kodi wanayolipa inatokana na mauzo ya dsm pekee? au kwa kuwa benki zote makao makuu yako dsm kwa hiyo kodi wanazolipa zinatokana na faida inayotokana na matawi dsm pekee? raw rubbish, kama umempa riziwan tenda ya kutandika maboma ya gesi toka mtwara hadi dsm safari hii mwambie atafute deal ingine, huyo professa muongo anasema gesi ya mtwara ni kidogo nyingi iko kwenye kina kirefu basi mkaivute huko kwenye kina kirefu mpitishe bomba baharini hadi bagamoyo kwani lazima lipitie mtwara? hii nchi tatizo ni kukubali akili ndogo itawle akili kubwa.

Umemfunua mno, maana hapa hakuna kumung'unya maneno wala dalili za kigugumuzi, ni kupasua jipu kabisa maaumivu yatapoa yenyewe wakati jipu limeshakamuliwa.
 
Kashfa,dharau,matusi au lugha ya ukali sio dawa ya kukwepa hoja.
Kiwango cha elimu sio kigezo cha mtu kutoa hoja yenye mashiko.wapo watu wana elimu lakini hawaja elimika.hapa watu wanaakili zao timaaam.hoja na hoja ndio ziwe zenye nafasi.

Nilipoleta mada hii wiki chache zilizopita kutahadharisha msimamo wa wananchi wa Mtwara kuhusu usafirishaji wa gas ulinipopoa kwa mawe, leo nini kinaendelea kwa kudharau matakwa ya wananchi wa Mtwara?
 
President-Jakaya-Kikwete.jpg

Rais kikwete kutoguswa na shinikizo la maandamano ya wananchi wa Mtwara kuhusu usafirishaji wa bomba la Gas kwenda Dar es Slaam ni kutokuangalia kwa makini mambo ya msingi kwa mtazamo wa kiuchumi, usalama wa mradi na uwiano wa maendeleo kitaifa.

Usalama:

  • Ulimwengu wa leo wakati unakabiliwa na hatari ya maadui wenye kuharibu miundo mbinu sina hakika usalama wa bomba hilo la gas usalama wake toka Mtwara hadi Dar, kwani pamoja na umuhimu wake, kunaweza kutokea hujuma kubwa katika bomba hili kutokana na umbali huo, wakati vinu vya kufua umeme vingewezekana kujengwa eneo ambalo maliasili inapatikana.

  • Hatari kubwa Electric power plant kuwa sehemu moja, hujuma ikifanyika, au itokeapo vita shabaha moja italitia taifa zima gizani. Muhimu Electric power plants zikawa sehemu mbalimbali na grid network power iunganishwe. Ukikatwa umeme Dar es salaam basi nchi nzima gizani.
  • Ndege moja tu inatosha kudondosha bomu moja Ubungo na lingine Kinyerezi kisha taifa zima likawa gizani mara moja, no alternative, tutaonekana si watu wa kuona mbali. Ukaribu uliopo Ubungo na Kinyerezi vigumu kupata muda wa papo kwa papo emergency respond.

Kiuchumi:
Ujenzi wa vinu vya kufua umeme karibu na eneo inakopatikana rasilimali ni bora na inapunguza gharama nyingi. Litakapotokea tatizo la gas kutofika kwa kiwango kinachotakiwa toka Mtwara kuna ziada ya kuhangaika kutafuta uvujaji uliko kwa umbali mkubwa toka Dar hadi Mtwara, jambo ambalo linaweza kusababisha uhaba wa umeme kwa muda mrefu.

Ukuzaji wa bandari ya Mwara kwa uanzishwaji wa viwanda huko papo kuunganisha ukanda wa kusini na ukanda wa kusini nyanda za juu kunakopatikana makaa ya mawe na chuma kutaongeza msisimko wa maendeleo zaidi wakati Wachina wanampango wa kujenga reli toka Mkoa mpya wa Njombe hadi Mtwara. Uanzishwaji viwanda mikoa ya Ruvuma, Njombe, Lindi na Mtwara ni muhimu kutokana rasilimali nyingi kupatikana eneo hili.

Wanaosoma jiografia, mtakumbuka eneo la Essen nchini ujerumani lilivyo na viwanda vizito tokana na upatikanaji wa maliasili huko, Wajerumani hawakujenga miundo mbinu ya kuhamishia maliasili iende Berlin na kwengineko kwani kufanya hivyo kungekuwa na athari zaidi kiutendaji, kiuchumi na kiusalama pia, hali kadhalika kusahaulika wananchi wanaoishi maeneo inakopatikana maliasili.

Uwiano wa maendeleo
Uwiano wa maendeleo kitaifa ni jambo linalotakiwa kutiliwa maanani, kwani kushinikiza gasi ipelekwe Dar es Salaam kwa mahitaji ya nchini nzima si vema kwani ni kuongeza zaidi msongamano wa viwanda jijini Dar es Salaam hatari ya uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa na papo kuzidi kuongeza mmiminiko wa watu kutafuta ajira huko badala ya kuanzishwa viwanda eneo la maliasili ili kuvutia watu wabaki huko kwa vile ajira ipo eneo lao.

Pamoja na kwamba uwiano wa maendeleo si rahisi kuwa sawa, lakini kuna sababu za msingi kutumia vyanzo vya rasilimali za mahali zinakopatikana kusaidia kuleta maendeleo kwa kuanzisha kwa makusudi miradi ya maendeleo kama uanzishwaji wa viwanda. Hatuhitaji machinga kuendelea kumiminika Dar es Salaam kwani wanachofuata ni hali njema ya maisha na ajira. Lakini ukishaweka mtego wa ajira na vivutio vingine kama hali nzuri ya umeme, viwanda nk hawatakuwa na sababu ya kuja Dar kwa vile wanachofuata dar kinapatikana kwao.

Tutakuwa tumekuwa na mtazamo finyu kama tutakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwamba kwa sababu Dar es Salaam wanaota mapato makubwa ya kodi kwa kulisha nchini nzima basi iwe hoja ya kupeleka rasilimali pale. Nakumbuka Hayati Nyerere aliamua kiwanda cha SPM Mgolole, Mufindi karibu na Makambako kijengwe huko badala ya kusafirisha magogo kwa TAZARA kuja kutengeneza karatasi Dar es Salaam. Gharama nyingi ziliepukika na pia ajira ilipatikana sehemu hilo badala ya watu wa huko kulazimika kuja Dar kupata ajira.

Tungetazamia wabunge wangeanzisha mjadala wa jambo hili kuishinikiza serikali kusitisha mpango huu kwani hoja ya kuwauzia mitungi ya gas wananchi wa Mtwara si ufumbuzi wa ajira na mendeleo, bali ujenzi wa viwanda vitakavyoendeshwa au kuzalisha gas na pia ujenzi wa vinu vya kufua umeme huko kutawanufaisha zaidi wananchi, taifa, na pia kuondolea taifa msongo wa ukuaji jiji la Dar es Salaam.

Good analysis jamaa sidhani kama anajua hili ila najua atakuwa anasoma jf.Hili ni zaidi ya darasa
 
Wakati mwingine nashawishika kwamba, washauri/hutuba zake zinaandaliwa na TOT chini ya Hadija Kopa! Maana hotuba zake zimejaa mipasho na vina vya mashairi kama ya Taarabu ati!!!!

Hivi kwanini huwa hachukui muda wa kutosha kufanyia utafiti jambo analo kashauriwa (kama ni kweli ana washauri)? Maana, mambo mengi anayo yatolea uamuzi hayaendani na hali halisi kama kiongozi mkuu!!!


Yale yale aliyosema waziri wa Nishati siku moja kabla ya hotuba ya Mkuu, ndio yalayale aliyo sema mkulu. Maana yake ni kwamba, hakuwa hata na muda wa kujiuliza yeye binafsi kuhusu nini misingi ya maandamano ya wananchi wa Mtwara/ Lindi!!!!

Hitimisho langu ni kwamba; watu walisha tia ndani pesa za watu, hivyo kuwageuka itakuwa ni kizaa zaa na ndiyo maana wanakazania gesi lazima iende Bagamoyo.

Mtwara/ Lindi komaeni. Haki/ Usawa haviji kwa kupigia watawala magoti. Lazima kuipigania kwa nguvu zote. Heri mkoloni mweupe maana alikuwa anajua siku moja lazima atarudi kwao, kuliko mkoloni mweusi ambaye anajuwa kwake ni hapahapa na akizembea mwisho wake ni kuishia gerezani.



Offcourse yes..... Hapa umenena mkuu....... Yawezekana kweli kimeundwa kwa Nazi. Hapa ndugu yangu umelonga haswaaa
 
Back
Top Bottom