Kikwete ameteleza kushinikiza gas kupelekwa Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete ameteleza kushinikiza gas kupelekwa Dar es Salaam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 1, 2013.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Rais kikwete kutoguswa na shinikizo la maandamano ya wananchi wa Mtwara kuhusu usafirishaji wa bomba la Gas kwenda Dar es Slaam ni kutokuangalia kwa makini mambo ya msingi kwa mtazamo wa kiuchumi, usalama wa mradi na uwiano wa maendeleo kitaifa.

  Usalama:

  • Ulimwengu wa leo wakati unakabiliwa na hatari ya maadui wenye kuharibu miundo mbinu sina hakika usalama wa bomba hilo la gas usalama wake toka Mtwara hadi Dar, kwani pamoja na umuhimu wake, kunaweza kutokea hujuma kubwa katika bomba hili kutokana na umbali huo, wakati vinu vya kufua umeme vingewezekana kujengwa eneo ambalo maliasili inapatikana.

  • Hatari kubwa Electric power plant kuwa sehemu moja, hujuma ikifanyika, au itokeapo vita shabaha moja italitia taifa zima gizani. Muhimu Electric power plants zikawa sehemu mbalimbali na grid network power iunganishwe. Ukikatwa umeme Dar es salaam basi nchi nzima gizani.
  • Ndege moja tu inatosha kudondosha bomu moja Ubungo na lingine Kinyerezi kisha taifa zima likawa gizani mara moja, no alternative, tutaonekana si watu wa kuona mbali. Ukaribu uliopo Ubungo na Kinyerezi vigumu kupata muda wa papo kwa papo emergency respond.

  Kiuchumi:
  Ujenzi wa vinu vya kufua umeme karibu na eneo inakopatikana rasilimali ni bora na inapunguza gharama nyingi. Litakapotokea tatizo la gas kutofika kwa kiwango kinachotakiwa toka Mtwara kuna ziada ya kuhangaika kutafuta uvujaji uliko kwa umbali mkubwa toka Dar hadi Mtwara, jambo ambalo linaweza kusababisha uhaba wa umeme kwa muda mrefu.

  Ukuzaji wa bandari ya Mwara kwa uanzishwaji wa viwanda huko papo kuunganisha ukanda wa kusini na ukanda wa kusini nyanda za juu kunakopatikana makaa ya mawe na chuma kutaongeza msisimko wa maendeleo zaidi wakati Wachina wanampango wa kujenga reli toka Mkoa mpya wa Njombe hadi Mtwara. Uanzishwaji viwanda mikoa ya Ruvuma, Njombe, Lindi na Mtwara ni muhimu kutokana rasilimali nyingi kupatikana eneo hili.

  Wanaosoma jiografia, mtakumbuka eneo la Essen nchini ujerumani lilivyo na viwanda vizito tokana na upatikanaji wa maliasili huko, Wajerumani hawakujenga miundo mbinu ya kuhamishia maliasili iende Berlin na kwengineko kwani kufanya hivyo kungekuwa na athari zaidi kiutendaji, kiuchumi na kiusalama pia, hali kadhalika kusahaulika wananchi wanaoishi maeneo inakopatikana maliasili.

  Uwiano wa maendeleo
  Uwiano wa maendeleo kitaifa ni jambo linalotakiwa kutiliwa maanani, kwani kushinikiza gasi ipelekwe Dar es Salaam kwa mahitaji ya nchini nzima si vema kwani ni kuongeza zaidi msongamano wa viwanda jijini Dar es Salaam hatari ya uchafuzi wa mazingira na hali ya hewa na papo kuzidi kuongeza mmiminiko wa watu kutafuta ajira huko badala ya kuanzishwa viwanda eneo la maliasili ili kuvutia watu wabaki huko kwa vile ajira ipo eneo lao.

  Pamoja na kwamba uwiano wa maendeleo si rahisi kuwa sawa, lakini kuna sababu za msingi kutumia vyanzo vya rasilimali za mahali zinakopatikana kusaidia kuleta maendeleo kwa kuanzisha kwa makusudi miradi ya maendeleo kama uanzishwaji wa viwanda. Hatuhitaji machinga kuendelea kumiminika Dar es Salaam kwani wanachofuata ni hali njema ya maisha na ajira. Lakini ukishaweka mtego wa ajira na vivutio vingine kama hali nzuri ya umeme, viwanda nk hawatakuwa na sababu ya kuja Dar kwa vile wanachofuata dar kinapatikana kwao.

  Tutakuwa tumekuwa na mtazamo finyu kama tutakubaliana na kauli ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwamba kwa sababu Dar es Salaam wanaota mapato makubwa ya kodi kwa kulisha nchini nzima basi iwe hoja ya kupeleka rasilimali pale. Nakumbuka Hayati Nyerere aliamua kiwanda cha SPM Mgolole, Mufindi karibu na Makambako kijengwe huko badala ya kusafirisha magogo kwa TAZARA kuja kutengeneza karatasi Dar es Salaam. Gharama nyingi ziliepukika na pia ajira ilipatikana sehemu hilo badala ya watu wa huko kulazimika kuja Dar kupata ajira.

  Tungetazamia wabunge wangeanzisha mjadala wa jambo hili kuishinikiza serikali kusitisha mpango huu kwani hoja ya kuwauzia mitungi ya gas wananchi wa Mtwara si ufumbuzi wa ajira na mendeleo, bali ujenzi wa viwanda vitakavyoendeshwa au kuzalisha gas na pia ujenzi wa vinu vya kufua umeme huko kutawanufaisha zaidi wananchi, taifa, na pia kuondolea taifa msongo wa ukuaji jiji la Dar es Salaam.
   
 2. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati mwingine nashawishika kwamba, washauri/hutuba zake zinaandaliwa na TOT chini ya Hadija Kopa! Maana hotuba zake zimejaa mipasho na vina vya mashairi kama ya Taarabu ati!!!!

  Hivi kwanini huwa hachukui muda wa kutosha kufanyia utafiti jambo analo kashauriwa (kama ni kweli ana washauri)? Maana, mambo mengi anayo yatolea uamuzi hayaendani na hali halisi kama kiongozi mkuu!!!

  Yale yale aliyosema waziri wa Nishati siku moja kabla ya hotuba ya Mkuu, ndio yalayale aliyo sema mkulu. Maana yake ni kwamba, hakuwa hata na muda wa kujiuliza yeye binafsi kuhusu nini misingi ya maandamano ya wananchi wa Mtwara/ Lindi!!!!

  Hitimisho langu ni kwamba; watu walisha tia ndani pesa za watu, hivyo kuwageuka itakuwa ni kizaa zaa na ndiyo maana wanakazania gesi lazima iende Bagamoyo.

  Mtwara/ Lindi komaeni. Haki/ Usawa haviji kwa kupigia watawala magoti. Lazima kuipigania kwa nguvu zote. Heri mkoloni mweupe maana alikuwa anajua siku moja lazima atarudi kwao, kuliko mkoloni mweusi ambaye anajuwa kwake ni hapahapa na akizembea mwisho wake ni kuishia gerezani.
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2013
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CCM imejichimbia kaburi yenyewe mikoa ya Lindi na Mtwara, kwani vyama vikuu vya upinzania nchini Chadema na CUF vimeungana kutetea matakwa ya Wanamtwara na Wanalindi.

  Sijaona sababu ya kung'ang'ania gas lazima iende Bagamoyo, kwani watu wa Mtwara hawahitaji viwanda na mwamko wa maendeleo? Hapa naona patachimbika.
   
 4. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #4
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KIla kitu Bagamoyo! Si mnakumbuka mshikemshike wa kuhamisha makao makuu ya Hifadhi ya Saadan ilivyo leta tibwilitibwili na wazee wa Pangani kipindi kile? Kwamba yahamie wilaya ya Bagamoyo!!!!??? Na wazee wa Pangani wakatia mpira kwapani.

  Kusini komaeni. Msimuangalie shemeji usoni, bhaa!!!!!
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2013
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Misitu ya kusini hatuijui zaidi ya wamakonde, wamakua na wamwera linakopia bomba hili. Wasiposikilizwa hao walishatamka siku ya maandamano kiakachoendelea kuhujumu mradi huo.
   
 6. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2013
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,820
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Wana Mtwara hakikisheni gas haisafiri kwenda Dar hata wakijenga hilo bomba, Yeye J.K si anajifanya anataka kushindana na nguvu ya umma? Muonesheni kuwa hakuna serikali duniani iliyowahi kushindana na wananchi wake halafu ikashinda.
   
 7. G

  Gongerfasil Member

  #7
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 25
  Umeandika vizuri sana maana hata mtu akitaka kujenga kiwanda raw material availability is one of the deciding factor lakini hawa ccm sijui wanaongozwa na nini kufanya maamuzi
   
 8. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 632
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Waambie watu wa Mtwara. Mradi huo haubadilishwi ng'o!Ni mradi uliokoa kichwa cha mwana mfalme kukatwa huko uchina.
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Jan 1, 2013
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,979
  Trophy Points: 280
  acha kutudanganya viwanda vingi Ujerumani vipo Baden Wurtemberg na si Essen! Na jaribu kutueleza ukweli hicho kiwanda cha Mgololo kipo wapi sasa? Hizi akili za kuharibu miundo mbinu ni za watu wenye utovu wa mawazo gesei itaenda Dar na manufaa yake yatakuwa makubwa zaidi hatuwezi kusema tuhamishe viwanda huko wakati gesi inaweza kufika viwanda vilipo.
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,849
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Laiti kama Serikali yetu ingelikuwa sikivu, tungeokoa Gharama na pia kuinua wana-Mtwara kiuchumi. Kwa hili Kikwete atajitetea vipi kama akishutumiwa kwa Ubaguzi na Kujali alipotoka tu?
   
 11. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #11
  Jan 1, 2013
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,914
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  mikoa hiyo yote mwaka 2015 itaenda upinzani, yangu macho
   
 12. K

  Kanundu JF-Expert Member

  #12
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 891
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Alaaa...!!!!!!! Kumbeee!!!!!!!!!!!!! Ndiyo maana watu mishipa inawatokaaaaa kiasi hichoeeeee!!!!!!!!!!!!!
   
 13. k

  kapongoliso JF-Expert Member

  #13
  Jan 1, 2013
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,133
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Una maana mradi huu ni barter trade na misokoto inayouzwa Uchina na prince wa Tz?
   
 14. s

  sabas matata Member

  #14
  Jan 1, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni kweli gas inayopatikana Mtwara ni malia ya watanzania wote lakini busara na hekima kutoka kwa viongozi wa ngazi husika zinahitajika kuhusu suala hill.tuache politiki.Tumie akili /brain kuliko kutumia mdomo sana.
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jan 1, 2013
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 13,377
  Likes Received: 1,114
  Trophy Points: 280
  Laiti kama tungeelewa maana halisi ya mabadiliko ya muda, pengine tungelikuwa tofauti. Kuna ukweli fulani juu ya maandamano yale ingawa sio kamili kabisa.
  We need pipelines to distribute gas from Mtwara to other places. Urusi inauza gas karibu ulaya yote through pipelines. Ingawa kwenye suala la kuzalisha umeme, pengine strategically Lindi ingelifaa zaidi maana ilivyo sasa Mtwara imeelemewa mno na shughuli nzima zinazoenda na utafutaji wa gas.
   
 16. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Please elewa mada, viwanda vilivyoko Esseni ni vile vinavyotokana na machimbo ya madini yaliyokuwa yanapatikana huko, haina maana eneo jingine la Ujerumani halina viwanda. Madini kama chuma na makaa ya mawe yaliyokuwa yanapatikana hapo yalichochea uanzishwaji wa viwanda hivyo.

  Kumbuka viwanda katika nchi za magharibi havifanyi kila kitu kwa sababu ya mfumo wa industrialization, process za awali hufanyika zinakopatikana raw material na kisha products husafirishwa kulisha viwanda vingine. Essen ilikuwa ni viwanda vya ku-process raw material na products zake zilipelekwa kwenye viwanda vingine. Hawakusafirisha mabongo ya madini ya chuma yaliyochimbuliwa ardhini kupelekwa huko unakosema ila processed products.

   
 17. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #17
  Jan 1, 2013
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,905
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kiufupi hatuwa na uwezo wa kujilinda dhidi ya wahujumu uchumi! Mfano: Ni mara ngapi watu wanashindwa kuzalisha sababu za kipuuzi na bado shirika husika la umeme linatembea kifua mbele bila kuwajibika? Lets wait for serious disaster when most of our people will suffer from long effects or poor services without any hope. This is Mtwara Oil and Gas Exploration Plant, Kazi inaendelea!!

  [​IMG]
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Jan 1, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama shinikizo la Wanamtwara ni kugomea gas isiende Dar es Salaam, bali kwanza juhudi za wadi zionekane kuwanufaisha wananchi hawa ikiwemo miradi inayokusudia kujengwa Dar es salaam ijengwe Mtwara au Lindi.
   
 19. MkoPoKa

  MkoPoKa JF-Expert Member

  #19
  Jan 1, 2013
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 354
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 45
  Mtwara Nadhani imelaaniwa toka kitambo!!! Nipo Mtwara kwa shughuli zangu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa but yanayoendelea ni aibu kuyasema, Kabla ya Hili la GAS Nilitaka wananchi wa Mtwara waungane na Kumng'oa KANJI BAI ambae ndo mbunge wao, hana msaada zaidi ya kutumia fulsa ya yeye kuwa mbunge kuilinda Diplomatic Passport yake, pia Kama vila la Mbunge halitoshi wakachagua KANJI BAI mwingine kuwa Mwenyekiti wa Mkoa CCM, najua nitaibua hisia za watu wasioipenda CCM hapa lakini kama unafuatilia mambo mengi ya kisiasa hapa nchi basi maamuzi mengi ya Serikali yetu hufanywa na SISIEMU kwenye vikao vyao vya NEC na Kutekelezwa na SERIKALI yake, hivyo kuwa na watu wawili ambao nathubutu kusema kuwa sio watanzania potelea mbali nikiitwa MBAGUZI lakini sio watu amabao wanaweza kuwatetea WANAMTWARA kwenye shida zao. HIVYO UKOMBOZI WA MTWARA UANZIA HAPO KWANZA NA WAKIWA NA WAWAKILISHI MAKINI BASI NAFASI YA MADAI YA MSINGI HASA HILI LA GAS BASI LIOTAWEZEKANA. INATOSHA SASA KUTAWALIWA NA WAGENI
   
 20. Mawaiba

  Mawaiba JF-Expert Member

  #20
  Jan 1, 2013
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 420
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao ma-KHANJ BAI unaowasema mkuu ni watu wadogo sana, Mtwara na Lindi ina mawaziri katika serikali hii ambao kama wangekuwa na uwezo wa kujenga hoja kwa maana ya kuwa na uchungu wa kimaendeleo ya kusini, sidhani kama hata hilo wazo la kusafirisha gesi kwenda Dar kama lingekuwepo. Tatizo wabunge-mawazi wetu ni mazuzu. Nafikiri sasa hivi muda umefika kwa watu wa kusini kuangalia upande wa pili wa shilingi. CCM tumekuwa nayo kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote, hata kuanza kwa miradi ya gesi na mafuta ni juhudi binafsi za ex-president Ben. Mkapa. Otherwise nawashauri wenzangu wa Mtwara tujaribu kubadilisha, wabunge wa CCM hawana faida na sisi.
   
Loading...