Kikwete amefanikisha lipi tangu aingie madarakani!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete amefanikisha lipi tangu aingie madarakani!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jun 1, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,237
  Likes Received: 5,621
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni nimeona sasa nianze kuangalia hii miaka mitano inaishia sioni allicchokifanya rais wetu ukiacha safari za nje za kila siku..labda tusaidiane kwa hili...nimejaribu kuangalia hata miradi ya mikoani kama mmoja wa juzi mradi wa maji...alieenda kufungua lakini umeanzishwa na fisadi BWM.
  Chuo kikuu cha DODOMA kakuta BWM akamalizia...kila sehemu yeye anamalizia nini anachoakianzisha yeye mwenyewe awe ameweka pale kwa ajili ya safari na PER DIEM....../
   
 2. k

  kizimkazi Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  kubadlisha picha yake kuweka aliyopendeza zaidi,kubadilisha tai kuvaa nyekundu.kuwasamehe marafiki zake na mkono wa sheria,kumpa ndege mkewe aeendee unyagoni swazland,kutengeneza bakulikubwa la kuombea,na kupiga picha na steven seagal,na ku make sure akijikuna nywele zisitimke,na kupima ngoma.
   
 3. r

  rahamajo Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 25
  Kwa kweli mzee wa kaya ananichefua kutochukua hatua kali kwa mafisadi, eti ni washikaji
   
 4. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Amefungua chuo kikuu Dodoma (UDOM) ... atakumbukwa kwa hilo, na mramba kuka bench kisutu hatutasahau ...
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  lakini ni wazo alilokuta limezaliwa,na limewekewa mikakati sawiya na bomba la Kahama,tukubaliane na swali la mwenzetu miaka mitano inaishia kafanya nini jamani hebu atuambia
   
 6. B

  Bobby JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Kwa kuongezea, kujenga ikulu kijijini kwao msoga/msata. Waliomtangulia wote, mwalimu, ruksa na anbem hawakuthubutu kufanya hivyo huyu peke yake ndio ameliweza. I think he should be remembered for that. Nchi chovu na ya kimaskini kama hii rahisi (sio rais) kujenga 14 presidential houses kijijini kwake si kitu kidogo ati. Hivi kwa wanaojuwa zinazinduliwa lini rasmi? I would wish to attend.
   
 7. B

  Bobby JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Watu lazima uwe mpenzi sana wa sinema maana hata hizi movies za kisutu cinema naona unazishabikia sana. Anyway endelea kuenjoy, ukiishiwa pop cons na coke just let us know tukuongeze mkuu.
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ameagiza wahusika wa KAGODA wasipelekwe mahakamani.
  Amekutana na FISADI Rostam South africa
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,051
  Trophy Points: 280
  hakika ndugu yangu uko juu...
  Kujenga ajenge mkapa..
  Sifa ziende kwa mfunguzi!!
  Kwani wewe ungeambiwa ufungue ungeshindwa nini?/
   
 10. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pdidy,
  Yaani huwezi kuamini umeniwahi, hili wazo limekuwa nalo tangu jana na nilitaka kuanzisha thread ya kuwalingalisha fisadi BWM na msanii wa Kikwere JK.

  Ukimwangalia fisadi BWM pamoja na ufisadi wake jamaa kafanya mambo ya kuonekana kwa mfano:
  1. Ujenzi wa barabara za lami kwa pesa za serikali
  2. Ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa kabisa
  3. Ujenzi wa ukumbi wa Bunge bomba kabisa hata ule wa Uingereza haufui dafu
  4. Mradi wa maji kutoka Mwanza hadi Shinyanga
  5. Ujenzi wa daraja la mto Rifiji
  6. Chuo Kikuu cha Dodoma
  7. Kuanzishwa kwa TRA na kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa karibu mara kumi ya yale ya serikali ya Mwinyi
  n.k.
  Na kuna tetesi kuwa fisadi BWM wakati anaondoka madarakani aliacha pesa nyingi sana ambazo inasemekana JK katafuna zote.

  Mwenye kujua JK kafanya nini atufahamishe
   
 11. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,275
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  JK katoka ndani ya CCM, anatimiza ilani, kuna vitu vya kuendelezwa na kuanzishwa. ili kuwa fair ungekuja na data ili kuona commitment ya serikali hii ni kiasi gani? mawazo ya vitu vingi yalishakuwepo toka siku nyingi. mf barabara, mashule/vyuo nk pamoja na kuajiri wataalam, lakini tungekuwa na data tungesema BWM alikuwa na wazo hili na alifanikisha kiasi gani na huyu mawazo haya na ameyafanikisha kiasi gani then tunaendelea.
  ukisema hajafanya lolote hayo ni maneno ya vijiweni
   
 12. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  BWM kuna hili la maboresho ya sekta ya umma (PSRP 1 &11) iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuwa na sura za watumishi hao tulionao mtaani na ofisi za viwangoo hivyoo..kama unapenda kusoma hebu isome hiyo reform programme in detail kwenye site ya wizara..

  upanuaji wa uhuru wa vyombo vya habari (natumai idadi iliongezekaa sanaaa)

  kuna haya mataasisi yanaitwa regulatory bodies (ile mifumo ya kuianzisha achilia mbali kuanza kama tunayaonavyo leo..TCRA, EWURA,SUMATRA,TIC,FCC, nk..)

  kuna mahakama ya biashara natumai ilikuwa ndo moja ya focus ya jamaa ili kuvutia uwekezaji na kuspeed up economic growth..(BEST programme hiyooooooooo)

  Elimu wala sijui nianzie wapi (MMEM, MMES, MEMKWA, MMEJ...HESLB)

  JK ana yake...nayeeeee......si amepokea kijiti na ni chama kimoja chenye malengo hayoo hayoo, viongozi wale wale, nk....wanatofautiana mtazamo tuu ambao ni purely individually based na ambao ni muhimu sanaaa..

  twaweza anza kazi pamoja, mshahara sawa, BACKGROUND SAWA, ila baada ya muda maendeleo tofautii nikimaanisha hakuna kipato cha zaidi ila KUPANGA NI KUCHAGUA....
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Makala kutoka Kwanzajamii:

  Safari za JK Nje ya Nchi:
  2 June 2009 17 views No Comment
  Profesa Joseph L. Mbele
  Leo nimeamua kuongelea safari za Rais Kikwete, maarufu kama JK, katika nchi za nje. Suala hili linazungumzwa sana na waTanzania. Wako wanaodai kuwa JK anatumia muda mwingi mno nje ya nchi badala ya kubaki nchini na kushughulikia masuala ya nchi. Wako wanaodai kuwa JK anaenda kuomba omba misaada. Wengine wanasema kazi ya kuzunguka nje ni ya waziri wa mambo ya nchi za nje, na kwamba kwa vile JK alizoea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje, bado hajabadilika, hata baada ya kuwa rais. Basi, kila mtu anasema yake, nami nimeona nichangie.
  Naanza kwa kukiri kuwa nchi ya nje ninayoifahamu kuliko zote ni Marekani. Nimeishi na waMarekani katika nchi yao kwa miaka mingi, nikiwafundisha na kujumuika nao kwa namna mbali mbali. Naweza kusema nawafahamu, na suala la safari za JK katika nchi za nje, naweza kuliongelea kwa kutumia mfano wa Marekani.
  Rais Kikwete ameshatembelea Marekani mara kadhaa, tangu awe rais. Binafsi, naona safari zake ni za manufaa. Kwanza, waMarekani kwa ujumla hawazijui nchi za Afrika kwa majina. Sana sana wanajua tu Afrika. Kuja kwa JK daima imekuwa ni fursa nzuri ya waMarekani kuijua na kuikumbuka nchi inayoitwa Tanzania. Kwa vile JK ni mtu mkubwa, ujio wake unatangazwa vilivyo, na hivi wahudhuriaji wanakuwa wengi. Fursa ya kuitangaza Tanzania inakuwa kubwa zaidi kuliko kama angekuja mbunge au waziri kama wanavyotaka baadhi ya Watanzania. Sio rahisi mbunge au waziri aje Marekani aweze kuwavuta watu kama anavyowavuta JK.
  Watanzania wanaoishi Marekani wanayo fursa ya kuitangaza Tanzania, na wako wanaofanya hivyo, kwa kadiri ya uwezo wao. Lakini mtu kama Rais Kikwete anapokuja, suala hili linakuwa na mafanikio mara dufu. Kinachosaidia zaidi ni kuwa JK ana mvuto wa pekee kwa watu. Wamarekani walishangaa kuona alivyokuwa na uhusiano wa karibu na Rais Mstaafu Bush. Na hilo niliwahi kuelezwa pia na mzee mmoja Mmarekani, ambaye ni balozi mstaafu na mtu mashuhuri. Tayari, dalili zinaonekana kuwa JK na Rais Obama wataelewana vizuri. Kwa mtazamo wangu, ziara za JK zinatuweka waTanzania kwenye chati inayohitajika vichwani mwa watu wa huku nje.
  Suala la uwezo wa JK kuitangaza Tanzania nililishuhudia alipofika katika jimbo la Minnesota, Septemba 26, 2006. JK alitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas, mjini Minneapolis. Baada ya Chuo kutoa wasifu wa JK na msingi wa kumpa tuzo hiyo, JK alitoa hotuba ambamo aliwaelimisha watu wa Minnesota kuhusu hali halisi, uwezo, malengo na mahitaji ya Tanzania na Afrika. Alielezea utajiri na fursa zilizomo katika nchi yetu na bara letu. Katika kuiongelea Tanzania, alitaja rasilimali tulizo nazo, kama vile madini, ardhi ya kilimo, vivutio vya utalii, na taratibu muafaka za kuwezesha uwekezaji. Aliongelea pia hali ya kijamii na kisiasa, kuwa ni nchi ya amani, ukifananisha na nchi zingine. Alisisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji na ubia ni mazuri katika Tanzania na kuwa yanazidi kuboreshwa.
  Hakuishia hapo, bali aliezea pia matatizo na mahitaji. Alisema kuwa pamoja na rasilimali zake, Tanzania haina uwezo wa kuziendeleza ipasavyo bila ushiriki wa wengine. Alisema kuwa Tanzania inahitaji mitaji na wawekezaji. Alisisitiza kuwa Tanzania si maskini anayehitaji kuhurumiwa na kutupiwa misaada. Inachohitaji ni washiriki katika kuufanyia kazi huu utajiri na kuleta faida kwa pande zote.
  Kwa namna hii, JK alituweka Watanzania na Waafrika katika akili za WaMarekani, kwa namna tofauti na walivyozoea. Wao wamezoea kuisikia Afrika, na wengi wanadhani Afrika ni nchi ndogo, ambayo ni hoe hae kwa dhiki, njaa, maradhi na vita. JK alijenga picha tofauti miongoni mwa wali0hudhuria. Kwa yeyote anayewafahamu waMarekani, huu ni mchango mkubwa wa fikra, hasa tukizingatia kuwa vyombo vya habari viliripoti vizuri ujio wake.
  Rais Kikwete alikuja na ujumbe mkubwa kutoka Tanzania, hasa wafanyabiashara. Kuja kwake na ujumbe wa wafanyabishara kulimaanisha kuwa Tanzania inataka kufanya biashara, si kuomba misaada. Ilifanyika semina kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji Tanzania. WaTanzania wengi wanaoishi huku Minnesota walihudhuria, na walikiri kuwa semina hii ilikuwa muhimu sana. Kwa maoni yangu, JK alitekeleza vizuri jukumu lake.
  Kilichobaki ni upande wetu waTanzania. Ingekuwea bora kama waTanzania waliohudhuria wangefanya utaratibu wa kuwaelezea wenzao ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria, ili kuyatafakari na kuyafanyia kazi yale ambayo yalitokana na ujio wa JK. Ulihitajika utaratibu wa sisi waTanzania kuendeleza mawasiliano na waMarekani, baada ya JK kuwahamasisha. Sisi tungepaswa tuikuze ile mbegu ambayo JK alikuwa ameipanda.
  Lakini waTanzania hatukujizatiti kufanya hayo. Inawezekana wako wanaoendeleza masuala aliyoanzisha Rais Kikwete, lakini sio kama jumuia. Labda wako ambao wanafuatilia, lakini hakuna taarifa. Hatuna vikao ambapo tunaelimishana na kuhamasishana. Tunakutana tu kwenye misiba au sherehe. Kama vile ilivyo Tanzania, kwenye sherehe waTanzania tunajitokeza kwa wingi. Lakini kwenye masuala ya kushirikiana katika maendeleo, ni wazi tunahitaji kujirekebisha.
  Ziara ya JK ilileta msisimko miongoni mwa watu wa Minnesota, na iliripotiwa vizuri katika vyombo vya habari. Ilikuwa ni juu yetu waTanzania kutumia fursa hii iliyotengenezwa na JK ili kuendelea kuwa karibu na watu wa Minnesota, na kuwa nao bega kwa bega, kupanga mipango na mikakati ya uwekezaji, ubia, biashara, na kadhalika.
  Kwa maoni yangu, wale wanaosema JK anazunguka nchi za nje kuomba omba misaada hawasemi ukweli. Kuhusu hoja kuwa kazi ya kuzunguka nje JK awaachie wengine, sina hakika kama tutapata mafanikio kama anayoyapata yeye. Ikiwa tutamleta mbunge au waziri, sina hakika ni waMarekani wangapi watavutiwa kuja kumsikiliza. Wanaosema JK akae nchini ashughulikie matatizo ya ndani, huenda wana hoja, lakini, kwa mtazamo wangu, si rahisi kutenganisha mambo ya ndani na ya nje. Pengine kwa kujishughulisha na mambo ya nje Rais Kikwete anajenga mazingira mazuri ya kutusaidia kwa mambo ya ndani. Vile vile Tanzania ina viongozi wengi au watu wengi ambao tunawaita viongozi. Hao wanafanya kazi gani? Kwani ni lazima awepo JK kuwaelekeza watu wa wilayani au mkoani wajibu wao? Je tunamhitaji rais aje kuwahamasisha watu wazoe taka taka mitaani, au waendeshe magari kwa uangalifu? Tunao viongozi wengi, kuanzia mtaani hadi kwenye ngazi ya Taifa. Wanafanya nini, na wanashindwa nini mpaka awepo rais?
  Watanzania tumezoea kukaa vijiweni na kutoa lawama kwa wengine. Nayachukulia malamiko kuhusu safari za nje za JK kwa msingi huo. Kama kila mwananchi na kiongozi angewajibika pale alipo, nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini hii tabia ya kumlaumu rais na kumtaka awepo nchini kutuelekeza namna ya kusafisha mitaro iliyoziba ni visingizio vya waTanzania ambao wanapenda zaidi kukaa vijiweni na kukosoa kuliko kuwajibika.
  Joseph L. Mbele
  1520 St. Olaf Avenue
  Northfield MN 55057
  Phone: 507 403 9756
   
 14. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Big up kwa Professor Mbele hapo juu!

  Swala lingine ambalo bahati mbaya limemuangukia JM Kikwete ni kwamba haya maskandali mengi yake ni ya nyuma ila yameibuka kipindi chake. BoT, EPA na yule mdogo wake EPA etc ni ufisadi ambao umeanza kufanyika zamani sana na pengine tangia enzi sa Mwinyi. I think its unfortunate that wakati wake wa uongozi mambo yote haya yamefumaka utadhani septic tank limejaa na kuanza kuvuja.

  Maybe in someone else term will all his foreign trips pay a huge dividend.

  I like this: "Watanzania tumezoea kukaa vijiweni na kutoa lawama kwa wengine. Nayachukulia malamiko kuhusu safari za nje za JK kwa msingi huo. Kama kila mwananchi na kiongozi angewajibika pale alipo, nchi yetu ingekuwa mbali. Lakini hii tabia ya kumlaumu rais na kumtaka awepo nchini kutuelekeza namna ya kusafisha mitaro iliyoziba ni visingizio vya waTanzania ambao wanapenda zaidi kukaa vijiweni na kukosoa kuliko kuwajibika." Joseph L. Mbele
   
 15. m

  mamah Member

  #15
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Umesahau???? Mabilioni ya JK.. Tehee tehe...............
   
 16. Iteitei Lya Kitee

  Iteitei Lya Kitee JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 589
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mmmh kutabasamu kibrazameni na kuvaa suti nzito!!
  Kuvaa travota mguuni na pia kutoa mahari ya mtoto anaeoa!!
  Kuenda google na kumshika mkono Obama
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sanasana, serikali ya awamu hii imebaki ikikamilisha miradi iliyanzishwa na Mkapa. Kuna uwezekano hata hivyo kuwa mpaka mwisho wa muhula huu utakapofikia, baadhi ya miradi itakuwa haijakamilika. Pia kuna wasi wasi kwamba serikali ya awamu hii inawezxa isianzishe mrado wowote mkubwa wa aidha barabara, umeme au maji
   
 18. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  Haya ya BWM sidhani kama tunapaswa kujivunia sana;
  1. Hiyo miradi myekundu yote imetokana na pesa za kuomba-omba zilizotokana na kodi za wenzetu wanaowajibika kwenye nchi zao.
  2. Lakini, angalau BWM alikuwa na mipango, JK mpango wake mkuu ni mmoja tu, kupita-pita kwenye maofisi ya viongozi wengine na kuomba-omba bila aibu kama vile waTZ hawawezi kufanya lolote bila misaada.
  3. JK amesingizia kila siku kuwa anazunguka ulimwengu mzima kutafuta wawekezaji, je wako wapi?
  4. Je amefanikiwa kwa kiasi gani kuvuta wawekezaji akilinganisha na BWM aliyetengenezea mikakati yake Dar na wawekezaji wakamfuata, licha ya mapungufu yake?
  Kwa kifupi ni kuwa BWM alizungukwa na wanaojua kazi na wakamsaidia kwenye awamu yake ya kwanza.

  Awamu yake ya mwisho ndio akajizamisha kwenye wizi ambao alianzia mwishoni mwa awamu ya kwanza lakini mazuri aliyokuwa ameanzisha yalikwishashika mizizi na kuzaa matunda licha ya kuzungukwa na magugu (ufisadi) aliyopanda.

  JK badala ya kuandaa mahali pa wawekezaji kufanyia kazi na kuliandaa taifa, amezurura-zurura mpaka dakika za mwisho (2005-2009), na sasa hana cha kuonyesha na badala yake anatafuta cha kusema kwa kwenda kuzindua miradi aliyoanzisha mwenzake.

  JK lazima aondoke, maana kashindwa miaka 5 aliyopewa afanye kazi. Kwa hiyo hakuna haja ya kupewa miaka 5 mingine ya kujitajirisha.
   
 19. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli hana chochote cha kujisifu kama KIONGOZI hii inatuaminisha kwamba kuna genge linaongoza nchi yeye kama kivuli...wanalotaka ndilo linalofanyika na si vinginevyo..Ila naona kama anazidi kuzeeka kuliko muda tatizo ninini? au kutembeza bakuli
   
 20. Baridijr

  Baridijr Member

  #20
  Jun 17, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna kitu chochote ambacho JK amekifanya na hatafanya lolote la kukumbukwa katika nchi hii
   
Loading...