Kikwete alivyovutia wawekezaji Italia, kupigia debe mapinduzi ya kilimo Afrika

Apr 27, 2006
26,588
10,364
::Makala za Uchumi Jumatano Nov 07, 2007

•Kikwete alivyovutia wawekezaji Italia,kupigia debe mapinduzi ya kilimo Afrika

Habari Zinazoshabihiana
• Siku ya Chakula Duniani na kauli mbiu ya chakula ni haki 16.10.2007 [Soma]
• Uchumi Tanzania unaweza kukua hesabu zikizingatiwa 05.09.2007 [Soma]
• Mikakati ya kumkomboa mkulima, mfugaji kiuchumi 13.03.2007 [Soma]

*Mkurugenzi WFP amsifu kwa kuisemea Afrika
*Rais Ujerumani amuunga mkono kuhifadhi mazingira
*Aeleza fursa tele za uwekezaji, Italia kumsaidia

HIVI karibuni, Rais Jakaya Kikwete alizuru Italia, Vatican na Ufaransa ambako pamoja na mambo mengine, alitumia fursa hiyo kuisemea Tanzania na Afrika kuhusu mapinduzi katika kilimo na kuhifadhi mazingira na kuvutia wawekezaji. Mwandishi Wetu, GODFREY LUTEGO aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari walioandamana na Rais katika msafara huo anaeleza katika makala yake ya pili, mwito wa Rais kuhusu mabadiliko katika kilimo na alivyovutia wawekezaji Italia.

WAKATI akijinadi katika kampeni za kuwania urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM mwaka 2005, Rais Jakaya Kikwete alitumia kauli mbiu ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania akiamini Tanzania yenye neema tele inawezekana. Tangu aingine madarakani, Rais Kikwete amekuwa akihangaika usiku na mchana kutimiza ahadi yake hiyo kwa Watanzania licha ya jitihada zake hizo kuathiriwa na majanga ya ukame, njaa, kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, umeme kukatika. Pamoja na yote hayo, Rais anaonekana hajachoka na wiki mbili zilizopita alienda Italia kuithibitisha dunia kuwa, alipania, bado amepania na ataendelea kupania kuwaletea Watanzania, maisha bora kama alivyowaahidi kama si leo, basi miaka ijayo kutokana na miradi mbalimbali anayoipigia debe yenye kulenga kuboresha maisha ya wananchi kwani kauli yake ilikuwa thabiti.

Alienda Italia kufanya nini ?

Wakati baadhi ya wananchi na hasa viongozi wa vyama wa siasa vya upinzani wakiendelea kuhoji safari zake za nje, Rais Kikwete ameendelea kwenda huko nje kuonesha safari hizo si za mambo binafsi bali ni za kuwatumikia Watanzania wote. Akiwa Italia, Rais Kikwete alipata fursa ya kuhutubia mkutano wa 27 wa Shirika la Kilimo duniani (FAO) makao makuu ya FAO, Rome katika maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani ambayo mwaka huu ujumbe wake ni Haki ya chakula kwa wote. Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliwataka wahisani wasaidie kuboresha kilimo akiamini ndicho msingi mkuu wa ukombozi. Alitaja baadhi ya matatizo yanayosababisha dhamira ya maisha bora kwa wote iwe na kigugumizi na kuziomba nchi wahisani zisaidie kuyaondoa kwani Serikali pekee haiwezi. Rais alisema kwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini ambako kilimo ndio chanzo kikuu cha ajira na riziki na kilimo ndio kinachochangia asilimia 45 ya pato la Taifa (GDP). "Ni wazi kuwa kama kilimo barani Afrika na Tanzania kikiboreshwa, kitawezesha kuwepo kwa uzalishaji chakula
zaidi na kuondoa umaskini, " alisema katika hotuba yake. Hata hivyo, alionya, lengo la kuboresha kilimo Afrika ambacho ni lengo la kwanza la mpango wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG) kuondoa njaa na umaskini, kikichangia asilimia 30 ya GDP na asilimia 40 ya mauzo ya bidhaa za nje kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara linaweza lisifikiwe.

Kwa nini malengo hayawezi kufikiwa:

Kuna matatizo mengi lakini baadhi ni kutegemea kilimo cha mvua ambacho Rais alisema kutokana na ukame, kilimo kimeathirika na kusababisha wakulima wavune mazao kidogo hivyo kuwepo haja ya kupunguza kilimo cha kutegemea mvua. Mbali ya umwagiliaji, Rais Kikwete alitaka matumizi ya sayansi na teknolojia katika kilimo yaongezwe kwani pamoja na jitihada za tangu uhuru kuboresha kilimo, bado mambo si mazuri kwani sehemu nyingi bado kilimo cha jadi cha matumizi ya jembe la mkono la tangu enzi za Yesu bado ndio kinatumika. Maeneo mengi bado yanatumia zana hizo kutokana na kukosa matrekta na plau za kukokotwa na ng'ombe kwa sababu ya bei kubwa za matrekta lakini pia baadhi ya maeneo kutokuwa na maksai wa kuvuta majembe ya kukokotwa. Rais alitaka pia Afrika iongeze jitihada katika utafiti na maendeleo ya kilimo na kujenga uwezo wa kuzalisha mbegu bora zaidi za mazao na kuzitawanya kwa wakulima mapema huku kwani utumiaji mbegu zisizo na ubora hupunguza tija. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakulima wa Tanzania wanatumia wastani wa kilo nane za mbolea kwa kila hekta kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha na Uholanzi ambako wakulima hutumia kilo 578 kwa hekta na mkulima wao kuvuna zaidi.
Alisema ili kufanikisha wakulima kupata mbolea na kuitumia zaidi, kuna haja ya kuwapa ruzuku na kuleta mageuzi ya uchumi Afrika kuzingatia utoaji ruzuku na madawa ya kuulia wadudu.
Kwa kukosa madawa ya kuua wadudu katika magugu, katika mazao wakati yakimea au yakivunwa, wakulima wengine wamejikuta wakipata hasara kubwa na hivyo kuendelea kuwa maskini kutokana na kupata kipato kidogo. Hata hivyo, Rais alisema, madawa hayo hayawezi kusaidia bila mpango wa huduma za ugani kwa wakulima kwani imebainika kutokuwepo kwake kunaathiri maendeleo ya kilimo cha kisasa kwani wakulima wanaendelea kulima kwa mbinu za kizamani. Kutokana na hayo, Rais alisema, wataalam wa ugani wa kuwafundisha kilimo cha kisasa, mbinu na teknolojia yake wanahitajika kupitia mpango wa mapinduzi ya kilimo Afrika.
Kwa mujibu wa hotuba yake, ukosefu wa mikopo kutoka benki na taasisi nyingine za kifedha ni eneo lingine linalokwamisha maendeleo ya wakulima kutokana na mabenki mengi kutokuwa tayari kuwakopesha kwa madai ni hatari kwani hawana amana. Hayo na mambo mengine ndiyo yanaumiza wakulima wadogo wadogo kwani hukosa pembejeo na huduma nyingine ambazo zingewazezesha kupanua kilimo chao na kuboresha maisha yao. Tatizo la masoko ya mazao ya wakulima lililo katika nchi nyingi ni eneo lingine linalosumbua wakulima kwani hawajui wakauze wapi mavuno yao na kupata bei muafaka inayolingana na thamani ya mazao yao kwani uzoefu umeonesha kuwa wamekuwa hawapati soko la uhakika na wanapunjwa bei zake. Changamoto nyingine katika kuendeleza kilimo ni miundombinu inayoathiri uuzaji wa mazao ya kilimo Afrika ambapo sehemu kusiko na miundombinu mizuri, haziendelei kwa kukosa fursa ya kuzalisha zaidi kwani mazao hayafiki sokoni, wakulima hawapanui kilimo kwa kukosa pembejeo na huduma za ugani.

Nchi zitafanikiwa vipi kujikomboa:

Ili ziweje kujikomboa, Rais Kikwete alitaka nchi za Afrika zisaidiwe kuboresha kilimo chake kiwe cha kisasa kwa kubuni mipango na kupewa misaada ya kiufundi ambayo hazina, ziajiri maofisa ugani, kujenga miundombinu ya kisasa na masoko.
Aliishukuru FAO kwa kusaidia kuendeleza kilimo Tanzania na nchi nyingine duniani na kutoa rai iwezeswhe zaidi na nchi wahisani ziitikie mwito wa FAO kutaka miradi iwezeshwe ili iweze kutekelezwa kuondoa njaa na umaskini kila mtu aishi. Tanzania inapata dola bilioni 2.5 kutoka FAO katika Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) ulioanza 2006 ukiwa ni mwanzo wa maendeleo ya kilimo Tanzania hivyo kilichobaki ni kuutekeleza vyema na raslimali zikiwepo,kilimo kitaboreka.
Rais alisema Tanzania itaendeleza kilimo ikishirikiana na FAO.

Kikwete aungwa mkono:

Jitihada za Rais Kikwete kutaka Watanzania na wananchi wa Afrika kwa jumla kupata maisha bora kupitia kilimo ziliungwa mkono na watu mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa FAO. Rais Horst Koelhler wa Ujerumani na pia Mwakilishi wa Papa, Monsinyori Renatus Volante, mchezaji wa zamani wa Italia, Roberto Baggio nao katika nyakati tofauti walimuunga mkono haja ya chakula zaidi kuzalishwa ili kuondoa njaa duniani.
Monsinyori alisoma salamu maalum za Papa Benedict XVI. Rais wa Ujerumani yeye aliungana na Rais Kikwete kupiga vita umaskini na njaa Afrika na duniani kote kwa jumla akionya vita, migogoro na machafuko ya kisiasa vinapaswa kuepukwa kwani vinachangia kurudisha nyuma maendeleo makubwa yaliyofikiwa na nchi kuwaondolea wananchi umaskini na njaa. Akihutubia mkutano huo pia, Dkt. Horst Koehler alisema mapambano dhidi ya njaa lazima pia yajumuishe mikakati ya kuzuia vita na migogoro kwani vita ikitokea, huharibu maendeleo yaliyofikiwa na nchi kwa miaka mingi nyuma. Rais huyo alisema Shirika la kimataifa la Oxfam linakadiria kuwa vita huzigharimu nchi za Afrika zaidi ya dola bilioni 18 kwa mwaka na asilimia 15 ya pato lake la uchumi na ndio maana Jumuiya ya Afrika (AU) na NEPAD zimesema suluhisho kuu ni kuzuia vita kutokea na kuleta na kusimamia amani ili nchi husika ziwe na usalama ziweze kuzalisha na kuondoa njaa.
Kwa mujibu wa Rais huyo wa moja ya mataifa makubwa, amani peke yake bila uwiano mzuri wa kiuchumi na biashara hautasaidia hivyo kuna haja kuwepo kwa mfumo mzuri wenye uwiano sawa wa biashara kwani uliopo sasa uliwekwa na nchi zilizoendelea, zenye viwanda na hakuna ubishi kuwa watu wengi duniani wa nchi zilizoendelea, wamenufaika na mfumo huo. Alisema walionufaika ni nchi zilizoendelea ambazo zinadhibiti soko la dunia hivyo suala la msingi la kujadili ni kuzipatia nchi zote haki sawa ya kushiriki na kunufaika na soko la dunia kwani nchi zinazoendelea, za dunia ya tatu bado zinaminywa. Rais huyo alisema tabia ya nchi tajiri kutoa ruzuku kwa wakulima wao hasa kwa mazao ya kuuza nje hasa ya kilimo inazifanya nchi maskini kushindwa kushindana katika soko. Alitoa mfano wa nyanya ya kopo kutoka nchi tajiri inavyoua soko la nyanya ya Senegal kwa kuwa itauzwa rahisi kutokana na gharama za kuitengeneza kuwa chini kwa sababu ya ruzuku ambayo Serikali ya nchi tajiri inawapa wakulima wake. Ili kuondoa hali hiyo, Rais huyo alipendekeza kuwe na mfumo mpya wa biashara wa dunia wenye mwelekeo wa maendeleo kwa wote bila ubaguzi ambao utaruhusu masoko ya nchi tajiri yawe wazi kwa bidhaa kutoka nchi maskini na ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa humo upunguzwe ili maskini nao wawekeze huko. Alisema kunahitajika mfumo wa biashara unaozingatia hali halisi na mahitaji ya nchi maskini zinazoendelea na kwamba lazima raslimali za nchi hizo zinufaishe watu wake.

Furaha ya Ujerumani:

Rais huyo wa Ujerumani alisema anafurahi mauzo ya bidhaa kwenye biashara sawia kwa Ujerumani yaliongezeka kwa asilimia 50 mwaka jana. "Tukinunua bidhaa kutoka nchi maskini, wakulima wa nchi zile wanapata fedha zaidi kuliko wangeuza soko la dunia, " alisema. Kwa mujibu wa Kiongozi huyo, ili kuweka uwiano mzuri wa mataifa yaliyoendelea, uchumi unaokua na nchi maskini zinazoendelea utakaodumisha dhamira ya dunia moja yenye usawa, kunahitajika Umoja wa Mataifa (UN) wenye nguvu na imara kiutendaji kwani ndio unaoweka mikakati ya maendeleo.
Je, UN itafanikishaje hilo. Rais huyo alisema ni kwa Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono mabadiliko yaliyoanzishwa na Katibu Mkuu wa zamani wa UN, Dkt. Koffi Annan kuhusu masuala ya maendeleo, amani, haki za binadamu kwa wanasiasa kuyatekeleza akiamini linawezekana wakubwa wakiamua. Alisema mengi yanaweza kufanyika kwa kuzifanya taasisi zote zilizo chini ya UN kufanya kazi zake kama chombo kimoja na hivyo akatoa changamoto kwa Shirika la Kazi Duniani (ILO), la biashara (WTO) na taasisi za fedha kushirikiana na nyingine. Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kuwa, wana jukumu la kufanya mabadiliko yanayoendelea kufanywa FAO yafanikiwe na akaitaka FAO ijikite katika jukumu lake kuu la utoaji taarifa na utaalam wa kilimo na chakula, irekebishe utoaji maamuzi yake na uendeshaji menejimenti yake ikubalike kwa UN na nchi wanachama, iboreshe uhusiano wake na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na ule wa kilimo na chakula (IFAD).
Alisifu jitihada za NEPAD kuimarisha demokrasia na utawala bora Afrika katika jitihada zake za kupambana na umaskini katika nchi za Afrika kwani masuala hayo ni ya msingi katika kuweka sera nzuri za uchumi zinazozingatia maslahi ya wananchi kuondoa umaskini. Alitaka nchi tajiri kusaidia jitihada za nchi hizo kwa kushirikiana na NEPAD. Pia aliisisifu NEPAD kwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya vijijini na kilimo kwa kujua wengi wa watu hasa wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la sahara wako vijijini. Alitaka lengo kuu la vita dhidi ya njaa liwe kuhakikisha watu wana chakula cha kuzalisha wao au maeneo ya karibu mambo yanayohitaji, mashine za kisasa za kulimia, teknolojia, mikopo, miundombinu, masoko na umilki ardhi wa uhakika na si kunyangànywa ardhi. Aliungana na Rais Kikwete kuzungumzia haja ya udhibiti wa uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira ambao Afrika na jumuiya ya kimataifa haujafanikiwa katika hilo ili kuwezesha mazingira yalindwe kwani uharibifu ukiachwa uendelee, mafuriko, ukame yatazidi. Alisema nchi tajiri ndio zinachangia zaidi kuharibu mazingira kutokana na hewa chafu kutoka viwandani na hivyo zina wajibu mkubwa zaidi wa kupambana na uharibifu huo kuupunguza. Alisema Umoja wa Ulaya (EU) wakati Ujerumani ikiwa Rais wa EU ilijaribu kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na
lengo sasa ni kuishusha hadi asilimia 20 mwaka 2020.

Je, jitihada za Kikwete zilizaa matunda

Je, katika ziara hiyo Italia, kilio cha Rais Kikwete kilizaa matunda na kuthibitisha kuwa ziara zake si za kupoteza wakati na raslimali za Watanzania kama wapinzani wanavyodai. Jibu ni ndiyo. Rais Kikwete aliweza kushawishi kwa vitendo na maneno ya kwenye hotuba yake, wahisani mbalimbali, FAO yenyewe na pia Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Aliikuna WFP hadi ikaahidi kuwasaidia wakulima kupata masoko ya uhakika, mikopo, bima na wanafunzi kula shuleni yote ikiwa imelenga kuboresha maisha ya Watanzania 2008. Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Bibi Josette Sheeran alimweleza Rais Kikwete mjini Rome kuwa alivutiwa na hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa 27 wa Siku ya Chakula Duniani ulioandaliwa na FAO na kufanyika makao makuu ya FAO.

Kilichofanya Mkurugenzi WFP aguswe na Kikwete

Yako mambo mengi ambayo Tanzania kama nchi imefanya na kuikosha WFP na FAO kwa jumla na nchi nyingine wahisani katika suala zima la mchakato wa maendeleo kama vita dhidi ya rushwa, hali ya usalama wa nchi kuwa shwari, kupanuka kwa wigo wa demokrasia, kuimarika kwa miundombinu ya barabara na njia nyingine za mawasiliano, kukuza kiwango cha elimu n.k. Lakini mbali ya hayo, Mkurugenzi wa WFP, Bibi Sheeran alionesha kuguswa na kufurahishwa zaidi na jinsi Rais Kikwete alivyoguswa na matatizo ya wakulima na alivyoonesha nia ya kuyaondoa akiwa ni mmoja wa viongozi wachache Afrika walioonesha dhamira hiyo ya kusaidia wananchi wake. Mkurugenzi huyo alisema alipokutana na Rais Kikwete na ujumbe wake uliokuwa na mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe na wa Chakula na Kilimo, Bw. Stephen Wassira kuwa, alikuwa amezoea kuona matatizo mengi ya Afrika yakisemwa na watu wa nje wakiwemo watu mashuhuri mbalimbali, akina Bonno wanaoguswa nayo. Hata hivyo, alishangaa kumwona Rais Kikwete kwa ujasiri mkubwa akieleza matatizo yanayokwamisha maendeleo ya Afrika na kuyaainisha vyema akiomba msaada wa nchi wahisani na taasisi mbalimbali zilizojikita kuondoa umaskini duniani. Kufuatia kukoshwa kwake na hotuba ya Rais Kikwete, Mkurugenzi huyo alisema, katika kuunga mkono jitihada za Rais huyo kuanzia mwakani, WFP itaiweka Tanzania katika mpango wa majaribio wa kuondoa umaskini na kukuza elimu.
Katika mpango huo, alisema WFP itawawezesha wakulima kulima mazao zaidi na kuuza zaidi kwa kuwapa mikopo, bima na kuwawezesha kupata masoko ya uhakika ya mazao yao na kuyasafirisha kufuatia kuwepo miundombinu bora kutoka shambani, sokoni, viwandani na hii itamaanisha kuwa watu hao sasa watakuwa na maisha bora aliyowaahidi Rais Kikwete 2005.
Mpango huo utakaoanzishwa pia Ghana unalenga kuvunja nira ya umaskini. Wakulima wataondokana na hatari ya kukosa chakula na mazao ya biashara kwa kuzalisha mazao kwa kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua tu na kuathiriwa na ukame na kufaidika na bima ukitokea moto, ukame, mafuriko. Kwa mujibu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa WFP, ndani ya mpango huo, kutakuwa pia na mpango wa kuwapa chakula (angalau uji), wanafunzi wawapo shule ili waweze kushika vyema masomo darasani bila kuathiriwa na njaa na uchovu. Katika kufanikisha mpango huo, mwaka huu watazieleza nchi wahisani, G8 wasaidie kuufanikisha kwani wakifanya hivyo watasaidia elimu na mkulima kuondoa umaskini unaomkabili.
Kwa mujibu waBibi Sheeran, inakadiriwa kila mtoto atatumia dola za Marekani senti 10 (sh. 120) kwa siku kwa kunywa uji.
Tanzania tayari ina mpango wa kulisha wanafunzi wake shuleni ambapo zaidi ya shule 300 Manyara, Dodoma na Arusha zinatoa chakula kwa watoto. Japan ilianza mpango kama huo wa kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni tangu mwaka 1890.
Kwa kuangalia haraka haraka, mpango wa WFP ni mgeni lakni kimsingi, ni mpango uliokuwa umeanishwa katika mpango wa elimu ya kujitegema enzi za uongozi wa Mwalimu Nyerere.
Wakati huo, karibu kila shule ilikuwa na mradi wa kilimo ambapo wanafunzi walikuwa wanalima mazao ya biashara kama pamba, kahawa, na chakula kama mahindi, mtama, uwele, mhogo, mpunga kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wake na ya biashara kwa ajili ya kuuza na kutunisha mfuko wa shule. Ni mfuko huo uliotumika kusaidia kuziba nakisi ya bajeti ya Serikali katika kununua samani, vifaa vya michezo, tiba na kugharamia usafiri wa walimu shuleni kwa idhini ya Kamati za shule. Ni vipi mpango huo ulikufa au kufifia, ndio changamoto. Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alimtaka Rais Kikwete amhakikishie nia ya Seriali kuunga mkono na kusimamia mpango huo jambo ambalo Rais alilifanya akithibitisha nia ya Serikali yake kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere kuendeleza mazuri aliyoacha ukiwemo mpango huo wa kuwezesha mashule. Rais Kikwete alisema mpango huo utasaidia Tanzania kufanikisha ujumbe wa mwaka huu wa FAO wa Haki ya kupata chakula kwani kila mtu, mkulima na watoto atapata chakula. Bibi Sheeran alisema wameamua kuanzisha mpango huo baada ya kuona wakulima katika nchi nyingi duniani na hasa Afrika wanakosa masoko ya kuuza mazao yao, miundombinu ya kuyasafirisha hadi sokoni na wanaathiriwa na njaa na ukame kwa kutegemea kilimo cha mvua badala ya umwagiliaji.

Kikwete apinga WFP kununulia chakula wakimbizi nje

Alisema WFP itaendelea kusaidia Tanzania kupambana na njaa, ukame, mafuriko na wakimbizi na kuweka mipango ya dharula ya kupambana nayo. Rais Kikwete alimweleza Tanzania haifurahishwi na mpango wa WFP kununua chakula nchi za nje kwa ajili ya wakimbizi wakati kuna mazao mengi ya wakulima nchini ambayo yangenunuliwa, wangenufaika. Huu ni ujasiri wa aina yake ambao Rais kama kiongozi wa nchi ameounesha kwa wahisani. Alisema haileti maana Tanzania kuendelea kupokea wakimbizi na kuwapa hifadhi lakini WFP iwalishe kwa kununua chakula cha kutoka nchi za nje na jirani. Katika kuweka mambo sawa, Rais alitaka kuanzia sasa WFP iwe inanunua chakula kwenye ghala la Hifadhi ya Chakula ya Taifa (SGR) ambalo lina tani 20,000 za akiba ambazo zikinunuliwa, SGR nayo itanunua nafaka za wakulima nchini na hivyo kuwaondolea umaskini na kuleta maisha bora kwa Mtanzania.
Ingawa Mkurugenzi Mtendaji huyo hakutoa jibu la papo hapo kuhusu changamoto hiyo ya Rais, ni wazi hilo likitekelezwa, litasaidia kuwakomboa wakulima wa Tanzania kwa kuwa watakuwa na uhakika wa moja ya masoko, wataweza kuwapa watoto wao, elimu kwa kulipia gharama mbalimbali za elimu. Mpaka sasa Tanzania bado inahifadhi zaidi ya wakimbizi 500,000 Kigoma, Kagera idadi ambayo inamaanisha kuwa, kama wakulima watapewa fursa hiyo ya kuwalisha chakula, wakulima zaidi ya 500,000 na familia zao watanufaika pia. Lakini jitihada za Rais Kikwete hazikuishia kwenye kupiga debe la kutaka mabadiliko katika kilimo tu ili kuwasaidia wakulima kupata maisha bora bali alitumia muda wake adhimu pia kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali za biashara.
Hatua hiyo ilithibtisha jinsi gani ana dhamira ya kweli ya kuleta maisha bora kwa kila mtu kulingana na eneo lake kadri fursa zinavyopatikana, muda kuruhusu licha ya kelele za wapinzani akithibitisha usemi kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji na msemo wa wahenga kuwa mtoto acha kulia, acha watu waone wenyewe hivyo anatenda, watu waamue.
Ni lini watu wataona Rais Kikwete anafanya nini anapokwenda nje. Ni suala la muda. Kuna mambo yatakayochukua muda mfupi na mengine muda mrefu kulingana na itifaki, mawasiliano, mashauriano, utafiti, raslimali, miundombinu na dhamira.
Hata hivyo, la haraka ambalo kila mtu ameliona na ama kulisikia ni dhamira ya Italia kama nchi kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo ambayo imeoneshwa na wafanyabiashara wa huko na kusisitizwa na Serikali yao.
 
Mnyonge mnyongeni, lakini haki tumpe pia maana hapa JF tunafahamika sana kwa vichwa makini, kwenye hili tumpe haki yake,

Ila tuendelee kumkaba koo kwenye la mafisadi, pamoja na kwamba amesema kuna vyombo vya dola vinalishughulikia, anahitaji kuwaongeza speed, lakini kwa hili haki yake apewe, at least safarii hii ya Italy, haikuwa kutalii kama tulivyoambiwa.
 
*Mkurugenzi WFP amsifu kwa kuisemea Afrika
*Rais Ujerumani amuunga mkono kuhifadhi mazingira
*Aeleza fursa tele za uwekezaji, Italia kumsaidia

Hapa tu ndio tatizo la Kikwete, anatafuta kusifiwa na watu wa nje wakati wananchi wake wakifa kwa njaa. Hivi sifa za nje kwa Mobutu, na madikteta wengine ziliwasaidia vipi raia wa nchi hizo?

... Tangu aingine madarakani, Rais Kikwete amekuwa akihangaika usiku na mchana kutimiza ahadi yake hiyo kwa Watanzania licha ya jitihada zake hizo kuathiriwa na majanga ya ukame, njaa, kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, umeme kukatika.

Rais yeyote akiingia madarakani lazima ategee matukio kama haya na ajiandae kukabiliana nayo. Inaonekana kikwete hakujua kuwa Tanzania ina ukame na majanga kabla hajachaguliwa kuwa rais.

Pamoja na yote hayo, Rais anaonekana hajachoka na wiki mbili zilizopita alienda Italia kuithibitisha dunia kuwa, alipania, bado amepania na ataendelea kupania kuwaletea Watanzania, maisha bora kama alivyowaahidi kama si leo, basi miaka ijayo kutokana na miradi mbalimbali anayoipigia debe yenye kulenga kuboresha maisha ya wananchi kwani kauli yake ilikuwa thabiti.

yani kikwete amekwenda italia kuithibitia dunia kuhusu kazi yake aliyochaguliwa kufanya? no wonder kuna mtu hapa alipendekeza JK agombee nafasi UN or somewhere kama zipo maana naona anajali sana dunia inasema nini!

Wakati baadhi ya wananchi na hasa viongozi wa vyama wa siasa vya upinzani wakiendelea kuhoji safari zake za nje, Rais Kikwete ameendelea kwenda huko nje kuonesha safari hizo si za mambo binafsi bali ni za kuwatumikia Watanzania wote.

Kwenda nje kuonyesha kuwa anawatumikia watanzania?

Akiwa Italia, Rais Kikwete alipata fursa ya kuhutubia mkutano wa 27 wa Shirika la Kilimo duniani (FAO) makao makuu ya FAO, Rome katika maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani ambayo mwaka huu ujumbe wake ni Haki ya chakula kwa wote. Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliwataka wahisani wasaidie kuboresha kilimo akiamini ndicho msingi mkuu wa ukombozi.

Kuhutubia mikutano ya nje ndio kazi aliyochaguliwa kufanya? Vipi kuhusu migodi ya madini anayoigawa bure kwa wakoloni?

Alitaja baadhi ya matatizo yanayosababisha dhamira ya maisha bora kwa wote iwe na kigugumizi na kuziomba nchi wahisani zisaidie kuyaondoa kwani Serikali pekee haiwezi. Rais alisema kwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini ambako kilimo ndio chanzo kikuu cha ajira na riziki na kilimo ndio kinachochangia asilimia 45 ya pato la Taifa (GDP). "Ni wazi kuwa kama kilimo barani Afrika na Tanzania kikiboreshwa, kitawezesha kuwepo kwa uzalishaji chakula
zaidi na kuondoa umaskini, "

Wakati nchi zote zilizoendelea zinapunguza idadi ya wananchi wake wanaojihusisha na kilimo (ECON 061}, kilaza wetu yeye anasifia vile asilimia 80 inajihusisha kwa kilimo na anataka kukeep hiyo namba hapo?

alisema katika hotuba yake. Hata hivyo, alionya, lengo la kuboresha kilimo Afrika ambacho ni lengo la kwanza la mpango wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG) kuondoa njaa na umaskini, kikichangia asilimia 30 ya GDP na asilimia 40 ya mauzo ya bidhaa za nje kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara linaweza lisifikiwe.

.......

Kuna matatizo mengi lakini baadhi ni kutegemea kilimo cha mvua ambacho Rais alisema kutokana na ukame, kilimo kimeathirika na kusababisha wakulima wavune mazao kidogo hivyo kuwepo haja ya kupunguza kilimo cha kutegemea mvua. Mbali ya umwagiliaji, Rais Kikwete alitaka matumizi ya sayansi na teknolojia katika kilimo yaongezwe kwani pamoja na jitihada za tangu uhuru kuboresha kilimo, bado mambo si mazuri kwani sehemu nyingi bado kilimo cha jadi cha matumizi ya jembe la mkono la tangu enzi za Yesu bado ndio kinatumika. Maeneo mengi bado yanatumia zana hizo kutokana na kukosa matrekta na plau za kukokotwa na ng'ombe kwa sababu ya bei kubwa za matrekta lakini pia baadhi ya maeneo kutokuwa na maksai wa kuvuta majembe ya kukokotwa. Rais alitaka pia Afrika iongeze jitihada katika utafiti na maendeleo ya kilimo na kujenga uwezo wa kuzalisha mbegu bora zaidi za mazao na kuzitawanya kwa wakulima mapema huku kwani utumiaji mbegu zisizo na ubora hupunguza tija. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakulima wa Tanzania wanatumia wastani wa kilo nane za mbolea kwa kila hekta kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha na Uholanzi ambako wakulima hutumia kilo 578 kwa hekta na mkulima wao kuvuna zaidi.
Alisema ili kufanikisha wakulima kupata mbolea na kuitumia zaidi, kuna haja ya kuwapa ruzuku na kuleta mageuzi ya uchumi Afrika kuzingatia utoaji ruzuku na madawa ya kuulia wadudu.
Kwa kukosa madawa ya kuua wadudu katika magugu, katika mazao wakati yakimea au yakivunwa, wakulima wengine wamejikuta wakipata hasara kubwa na hivyo kuendelea kuwa maskini kutokana na kupata kipato kidogo. Hata hivyo, Rais alisema, madawa hayo hayawezi kusaidia bila mpango wa huduma za ugani kwa wakulima kwani imebainika kutokuwepo kwake kunaathiri maendeleo ya kilimo cha kisasa kwani wakulima wanaendelea kulima kwa mbinu za kizamani. Kutokana na hayo, Rais alisema, wataalam wa ugani wa kuwafundisha kilimo cha kisasa, mbinu na teknolojia yake wanahitajika kupitia mpango wa mapinduzi ya kilimo Afrika.
Kwa mujibu wa hotuba yake, ukosefu wa mikopo kutoka benki na taasisi nyingine za kifedha ni eneo lingine linalokwamisha maendeleo ya wakulima kutokana na mabenki mengi kutokuwa tayari kuwakopesha kwa madai ni hatari kwani hawana amana. Hayo na mambo mengine ndiyo yanaumiza wakulima wadogo wadogo kwani hukosa pembejeo na huduma nyingine ambazo zingewazezesha kupanua kilimo chao na kuboresha maisha yao. Tatizo la masoko ya mazao ya wakulima lililo katika nchi nyingi ni eneo lingine linalosumbua wakulima kwani hawajui wakauze wapi mavuno yao na kupata bei muafaka inayolingana na thamani ya mazao yao kwani uzoefu umeonesha kuwa wamekuwa hawapati soko la uhakika na wanapunjwa bei zake. Changamoto nyingine katika kuendeleza kilimo ni miundombinu inayoathiri uuzaji wa mazao ya kilimo Afrika ambapo sehemu kusiko na miundombinu mizuri, haziendelei kwa kukosa fursa ya kuzalisha zaidi kwani mazao hayafiki sokoni, wakulima hawapanui kilimo kwa kukosa pembejeo na huduma za ugani.

haya yote yatafanikiwa sio kwa kufanya umatonya nje na kujililia bali kwa kutunza kilichopo na sio kuuza nchi kwa bei ya katasha kama anachoendelea kufanya!

..
Hatua hiyo ilithibtisha jinsi gani ana dhamira ya kweli ya kuleta maisha bora kwa kila mtu kulingana na eneo lake kadri fursa zinavyopatikana, muda kuruhusu licha ya kelele za wapinzani akithibitisha usemi kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji na msemo wa wahenga kuwa mtoto acha kulia, acha watu waone wenyewe hivyo anatenda, watu waamue.

kwa hiyo anakwenda nje ili kuwakomoa wapinzani au ndio maana gani hapa!

Ni lini watu wataona Rais Kikwete anafanya nini anapokwenda nje. Ni suala la muda. Kuna mambo yatakayochukua muda mfupi na mengine muda mrefu kulingana na itifaki, mawasiliano, mashauriano, utafiti, raslimali, miundombinu na dhamira. Hata hivyo, la haraka ambalo kila mtu ameliona na ama kulisikia ni dhamira ya Italia kama nchi kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo ambayo imeoneshwa na wafanyabiashara wa huko na kusisitizwa na Serikali yao.

Only in Tanzania ndio watu wanajisifia kufanya umatonya. Ama kweli nilikuwa natafuta kitu cha kusifia katika serikali ya JK ila baada ya kusoma hiki kitabu cha propaganda sasa nimeona kuwa the guy hana idea of what anafanya. Watu wanaomba misaada kwa kujificha, this guy anasherehekea kuomba misaada, misaada ambayo hata akikaa bongo wazungu wataileta tu kama "walivyoileta" karne ya 18 na kugeuza afrika kuwa koloni lao!
 
Kikwete alivyovutia wawekezaji Italia,kupigia debe mapinduzi ya kilimo Afrika

Bado sijamaliza kusoma lakini maswali mengi yameenea kichwani!
I wonder what mugabe is thinking? How can he do that? First ugandas foreign minister[sic] and now Italy?
Na mimi nikajiuliza
Mapinduzi ya kilimo wakati land yetu inauzwa kushoto kulia? Mkulima huyo anayetaka mapinduzi haya ni nani?:confused:
Anyways naendelea kusoma hapa ili nipate kufungua ubongo!
 
huko italia si ndio kwanza kaenda na unataka uone maendeleo hapo hapo mkuu au ? nadhani subira ndio kitu kitakachotufanya tuseme mazuri/mabaya kutokana na matokeo ya alichovutia mkuu wetu ! lets wait on this one !
 
Mkuu Marshal unafikiri mapinduzi ya kilimo yatakuwa solved na hao wazungu? sana sana wanatucheka tuu na kutuona hatuna akili na sijaona deal yeyote ya maana hapo aliyofanya na hao wazungu zaidi ya hotuba,najua nimekuwa harsh hapo kwa JK lakini ukweli ndio huo.
ngoja nikuambie tufanye nini ili mapinduzi ya kilimo yafanyike

1)Ipe value ardhi kwa kutunga sheria ili watu waweze kuchukulia mikopo Bank and other financial insititution.

2)Ondoa tax kwenye kilimo kuanzia mbolea mpaka matractor(nafikiri tayari hapa wamejitahidi)

3)Serikali inabidi yenyewe imwage pesa za kutosha kwa watakao kuwa na nia ya kilimo sio kusubiri mabank

4)Mwaga pesa nyingi kwenye research kwenye vyuo kama SUA au kwa mikoa ya kusini anzisha reseach centers ya mahindi na mazao mengine kutokana na zone na wawe responsible moja kwa moja kwa wakulima

5)somesha na ajiri wataalam wetu na wengine ajiri toka nje watusaidie

6)Anzisha one point kama ile investment center ya wawekezaji ambapo wakulima wanaweza kupata information zote kuanzia upatikanaji wa ardhi,mikopo,masoko,wataalam wa kilimo,research & data za mazao yote yanayolimwa Tanzania,hali ya hewa na legal services zote za kuanza kilimo.

7)hakikisha umeme na barabara zinafika katika hizo sehemu zilizotengwa kwa kilimo la sivyo hakuna mtu atapoteza muda wake kumwaga billions huku akijua hakuna usafiri wala umeme wa kuhifadhi & process kitakachozalishwa

...yako mengi lakini haya yanaweza kusaidia na tunaweza kujifanyia wenyewe na tukaacha kutumia our hard earning dollar kuagiza michele yenye sumu.
 
.Kwani hii kitu haipo?
2)Ondoa tax kwenye kilimo kuanzia mbolea mpaka matractor(nafikiri tayari hapa wamejitahidi)

I].Wajanja walitumia nafasi hii kuleta mashine zingne na bidhaa za kuuzwa rejareja![/I]

3)Serikali inabidi yenyewe imwage pesa za kutosha kwa watakao kuwa na nia ya kilimo sio kusubiri mabank
.Twenty eight million pounds I presume!!

4)Mwaga pesa nyingi kwenye research kwenye vyuo kama SUA au kwa mikoa ya kusini anzisha reseach centers ya mahindi na mazao mengine kutokana na zone na wawe responsible moja kwa moja kwa wakulima
.Quite possible...lakini siyo nyingi hizo!;)

5)somesha na ajiri wataalam wetu na wengine ajiri toka nje watusaidie
.Wapo wengi from awamu ya kwanza to present...Wanajinufaisha, sidhani kama asilimia kubwa itarudi!

6)Anzisha one point kama ile investment center ya wawekezaji ambapo wakulima wanaweza kupata information zote kuanzia upatikanaji wa ardhi,mikopo,masoko,wataalam wa kilimo,research & data za mazao yote yanayolimwa Tanzania,hali ya hewa na legal services zote za kuanza kilimo.
.There was Coopertaives? What were their functions?
7)hakikisha umeme na barabara zinafika katika hizo sehemu zilizotengwa kwa kilimo la sivyo hakuna mtu atapoteza muda wake kumwaga billions huku akijua hakuna usafiri wala umeme wa kuhifadhi & process kitakachozalishwa

.Hapa dole tupu! Same mfano mzuri
...yako mengi lakini haya yanaweza kusaidia na tunaweza kujifanyia wenyewe na tukaacha kutumia our hard earning dollar kuagiza michele yenye sumu.

Ni kweli kuna mengi. ndio kwanza tumemaliza kutambaa, tumesimama sasa na kujaribu kubalance...baby steps will follow!
 
1.
Only in Tanzania ndio watu wanajisifia kufanya umatonya. Ama kweli nilikuwa natafuta kitu cha kusifia katika serikali ya JK ila baada ya kusoma hiki kitabu cha propaganda sasa nimeona kuwa the guy hana idea of what anafanya. Watu wanaomba misaada kwa kujificha, this guy anasherehekea kuomba misaada, misaada ambayo hata akikaa bongo wazungu wataileta tu kama "walivyoileta" karne ya 18 na kugeuza afrika kuwa koloni lao!

Mkuu Mwafrika,

Heshima mbele, Tanzania tulianza kuomba toka enzi za Mwalimu, bajeti yetu toka enzi hizo inachangiwa 40% na wafadhili, kati hizo 40%, 5% ni kwa ajili ya vyama vya siasa, upinzani included, sijawahi kusikia upinzani wakikataa ruzuku za kupewa na wafadhili, kwenye uchaguzi wa mwisho wa urais Chadema walipewa hela ngapi na Conservative wa UK? au u-Matonya unaishia tu kwenye taifa kusaidiwa na wazungu 40% za bajeti toka tupate uhuru?

2.
Mkuu Marshal unafikiri mapinduzi ya kilimo yatakuwa solved na hao wazungu? sana sana wanatucheka tuu na kutuona hatuna akili na sijaona deal yeyote ya maana hapo aliyofanya na hao wazungu zaidi ya hotuba,najua nimekuwa harsh hapo kwa JK lakini ukweli ndio huo.

Mkuu Koba, you somehow seeems to make some sense among all, lakini bado una-fall short, kwa sababu the big question linapaswa kuwa ni mapinduzi ya aina gani ya kilimo tunahitaji Afrika, licha ya Tanzania?

Mapinduzi ya kilimo in Afrikan style, au in European style?

3.
ngoja nikuambie tufanye nini ili mapinduzi ya kilimo yafanyike

1)Ipe value ardhi kwa kutunga sheria ili watu waweze kuchukulia mikopo Bank and other financial insititution.

Kwenye ardhi na value na kukopesha wananchi, ukweli ni kwamba ndio kwanza tumeanza kulivalia njuga na kuna some progress kwenye hilo, tena kwa kuanza tumeanza na uwezo mkubwa kipesa nchini, kama viongozi mbali mbali wa ccm na upinzani, ndio maana benki yetu kama NSSF imeweza kuwakopesha mapesa mengi sana kina Mengi, Sumaye, Freeman, Idrisa, na Cheyo kuna viongozi kama Mzindakaya ambao pia wamepewa mikopo mizito sana na kuweza kufungua ranchi, sasa huu ni mwanzo tu tuko kwenye majaribio, baadaye tutahamia kwa wananchi wa kati, na mwishowe wa chini kabisa, kumbuka ni miaka michache tu iliyopita tulikuwa chini ya siasa ya ujamaa na kujitegemea ya Mwalimu, ambapo haya yalikuwa ni ndoto ya mwenda wazimu, we are making a progress kwenye hilo na sidhani kama awamu ya nne ina anything to do na hilo, ninaaamini haya ni mapinduzi ya kitaifa kiuchumi kufuatilia wakati tulionao,

4. 2)Ondoa tax kwenye kilimo kuanzia mbolea mpaka matractor(nafikiri tayari hapa wamejitahidi)

Kwenye hili la pili la kuondoa taxes kwenye kilimo, mbolea, na matractor, tunaongea lugha moja, kuwa wanajitahidi ukilinganisha na tukikotoka, mimi nafikiri kwa kuanzia ni haya yako mawili yenye umuhimu.

Ahsante Mkuu.
 
Koba
Senior Member JF Expert

5)somesha na ajiri wataalam wetu na wengine ajiri toka nje watusaidie

Mkuu Wangu Koba,

Serikali ya Kikwete, haiko mbali sana kuwasikiliza wananchi kama wewe, wenye michango mizito kwa taifa lao, kwenye hili la wataalamu inajitahidi pole pole kujaribu, kama ulivyoshauri, ona hapa chini:-

::Habari za Tanzania Jumatano Nov 07, 2007 Imetolewa mara ya mwisho: 09.10.2007 0918 EAT

.JK azindua Mfuko kugharimia mafunzo ya watendaji wakuu

RAIS Jakaya Kikwete amezindua Mfuko kwa ajili ya kugharimia mafunzo ya watendaji wakuu serikalini, yenye lengo la kuboresha utendaji wa Serikali, ili uendane na uchumi wa soko na zama za utandawazi. Akihutubia kikao cha Watendaji Wakuu wa Kampuni na Taasisi Tanzania, kabla ya uzinduzi huo Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema uamuzi wa Serikali kuingia kwenye mfumo wa uchumi wa soko unahitaji mabadiliko ya fikra kwa watumishi wa Serikali.

"Tulikuwa na miaka 23 ya uchumi wa kupanga, ambapo Serikali ilikuwa inaendesha kila kitu," alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa kipindi hicho watumishi wa Serikali walifundishwa kuibana sekta binafsi. Alibainisha kuwa mabadiliko ya fikra za watumishi wa Serikali, yanachukua muda ingawa kumekuwa na mafanikio mazuri ya utendaji katika sekta ya umma. Mafunzo hayo yanatarajiwa kugharimu zaidi ya dola milioni 2 za Marekani zitakazotolewa kwa ushirikiano kati ya Serikali, kikao cha Watendaji Wakuu wa Tanzania na Benki ya Dunia (WB).

Akizungumza katika kikao hicho muda mfupi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Fedha, Bibi Zakiah Meghji, kiongozi wa kikao hicho Bw. Ali Mufuruki, alisema mafunzo hayo yatatolewa kwa watendaji wakuu serikalini, wenye vyeo vya ukatibu mkuu. Watendaji hao wanaotarajia kuanza mafunzo Februari mwakani, watalazimika kuingia darasani kwa muda kabla ya kutoka nje ya darasa na kutembelea baadhi ya nchi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Naye Waziri Meghji alisema Serikali imejiandaa kutoa mchango wake kwenye mafunzo hayo kwa lengo la kuboresha na kuimarisha menejimenti katika sekta ya umma.

1.

kwenye uchaguzi wa mwisho wa urais Chadema walipewa hela ngapi na Conservative wa UK? au u-Matonya unaishia tu kwenye taifa kusaidiwa na wazungu 40% za bajeti toka tupate uhuru?

Labda utuambie wewe mkuu inawezekana unaijua CHADEMA vizuri zaidi kuliko wanachadema wenyewe! CHADEMA ni chama pekee kilichochapisha hadi kwenye magazeti taarifa za mapato na matumizi ya kampeni zake za uchaguzi wa CCM 2005. Hatukuona senti yeyote ikitoka Conservatives. Hili limeshajibiwa na viongozi wote wakuu wa CHADEMA hadi hapo kwenye forum. CCM hadi leo kimya kwa sababu wanajua hela zao za kampeni walituibia hela zetu kupitia BoT. Sasa hilo la Conservatives tueleze wewe inawezekana una ukweli kuliko viongozi wetu wa CHADEMA, tupe data mkuu.

On a serious note kuhusu post yako, wananchi hawamkuchagua Kikwete kwa kuwa ni bingwa wa kuwaomba misaada kwa wazungu na wala hii haikuwa moja ya sifa zake. Kama tungetaka hili tungembakisha Mkapa. Mkapa ndiye anayejulikana duniani kwa kuwa na PR nzuri na wazungu hadi akafutiwa madeni lukuki, sio Kikwete. Ni aibu kumpa credit Rais wa nchi kisa eti ameweza kushawishi misaada ya wazungu, tena kaahidiwa halafu na shirika la FAO! No, hili tutalikataa. Wewe tueleze hapa katika ahadi zake 72 alizotoa katika uchaguzi wa 2005, ameshatekeleza asilimia gani na ana mipango gani ya kutekeleza zingine.

Attitude inayoonyeshwa kwenye post yako ndiyo iliyowafanya wananchi wetu sasa waanze kukaa tu wasubiri kuletewa maendeleo. Rais wetu kwa kusifiwa na watu kama nyie anafikiri ataweza kuwafanyia wananchi kila kitu kwa misaada ya wazungu, matokeo yake hawezi kufanya chochote na wazungu wataendelea kumuahidi hadi 2010! Mfano mzuri kila siku anahaidi kujenga barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Mwanza na watu watapita kwa Taxi, akiahidi hili, serikali yake imeshindwa kikamilisha ujenzi wa barabara ya Sam Nujoma ambaye ni chini ya KM 5 katika kipindi cha miaka miwili aliyokaa madarakani!

The bottom line mkuu ni kuwa: ni aibu kumpa rais credit on the basis ya kuaidiwa misaada na wazungu. Idd Amin, Mobutu Sesko, Sadam Huseein na Kamuzu Banda-ni baadhi ya Marais waliopendwa sana na kupewa misaada lukuki na wazungu, tunakumbuka sana hili hadi leo.
 
..hayavunji mfupa!

..mkuu ES,kama tukitaka ku-quote yaliyosemwa na mheshimiwa tutashindwa hata pa kuyaweka hapa!

..kitu cha maana ni kuonyesha au kubainisha yale yaliyoanza kufanyiwa kazi!kumbuka"hoja hujengwa kwa mifano hai"

..nimeona umeelezea sehemu juu ya kilwa road,ndio ni mfano mzuri[juu ya utendaji wa serikali]ila misplaced!hiyo kazi si ya hii serikali ni ya iliyopita!hata ile ya sam nujoma!

..challenge zipo nyingi mkuu!maneno mengi hayatasaidia,vitendo zaidi vinahitajika!
 
Ila tuendelee kumkaba koo kwenye la mafisadi, pamoja na kwamba amesema kuna vyombo vya dola vinalishughulikia,

..haya ndio maneno!maana huwezi sema kuwa unahifadhi kubwa ya chakula ulichovuna,wakati unajua wazi ghalani kuna kila aina ya wadudu[mchwa,panya,dumuzi,n.k]

at least safari hii ya Italy, haikuwa kutalii kama tulivyoambiwa.

..it's too early to say!i hope its not!but you know what?kazi kubwa iko hapahapa nchini!infrastructure zetu bado hoi,na hivyo zina-limit ukuaji wa maendeleo!
 
..it's too early to say!i hope its not!but you know what?kazi kubwa iko hapahapa nchini!infrastructure zetu bado hoi,na hivyo zina-limit ukuaji wa maendeleo!

Wakuu mimi siamini kuwa safari za nnje zinaweza kweli kuleta wawekezaji hapa nchini. Ndio kuna umuhimu wa kujitangaza lakini sio kwa nnjia hiyo. Kuvutia wawekezaji kunaanzia huku nyumbani kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kuwepo na soft and hard infrustractures kama vile, bara bara, human resources, umeme, sheria nzuri, kusiwepo na rushwa ukisajili kampuni husumbuliwi, mifumo mizuri ya kodi, masoko etc.

Wawekezaji ni wanatafuta faida, nio maana wanaitwa wajasiria mali. Na mjasiria mali ni mtu anayeweza kuona mlango pale wengine wanaona ni ukuta. Sasa wawekezaji wengi wao wanaangalia indicators na mazingira ya kuwekeza ili waweze kuwa na return ya pesa zao na si kuwa ni nini raisi kasema. Jamani wawekezaji wanamambo mengi wanayoangalia jaribuni kusoma report ya doing busness ambayo wawekezaji wengi wanaisoma na kuevaluate mazingira ya uwekezaji. [media]http://www.doingbusiness.org/Documents/CountryProfiles/TZA.pdf[/media]
 
..when was this report released?i can see its a latest one!

..au ndio uzuri wa JF,vitu hupatikana motomoto!
 
Mkuu hii imekuwa released siku si nyingi mkuu hapa JF unapata mambo yote mkuu. Ni report muhimu sana hiyo mzee wawekezaji huwa wanaiamini japo mimi huwa siamini sana data za WB.

..data za WB,inategemea unataka fanya nini?kama ni kuwekeza you'll need to do a thorough market reseach!lakini kama we ni mkurugenzi fulani katika multinational fulani,unaweza tumia hizo kuwapa mabwana wadogo kibarua cha kuangalia viability ya mradi katika nchi fulani!

..nchi wahisani hutumia hizo kujengea policy zao towards us!hasa za misaada,ambayo in real sense si misaada bali mazingaombwe!
 
Ni kweli mkuu na ndio maana mimi nasema sisi badala ya kusafiri kutafuta wawekezaji kila mahali tuimarishe mazingira ya ndani kwanza. Bara bara nzuri, reli nzuri, Bandari ya Tanga, Dar na Ntwara zi fanye kazi, kuwepo na umeme wa uhakika si wa mgao, mazingira mazuri ya taasisi za fedha na insuarance, tupambane na rushwa na kuwa na uongozi bora katika ngazi zote, tuelimishe watu wetu na huduma nzuri za afya wapate, tudumishe amani yetu, airport nzuri, mfumo mzuri wa mabenk etc.

Nakuapia wala hatuna haja ya kutalii dunia nzima kuomba watu waje wawekeze bali watu watamiminika kuomba nafasi za kuwekeza. Kwani nchi kama China, Honkong na sasa hivi Vetnam wanazunguka kuomba FDI? ni kuweka mazingira mazuri tuu kuvutia. Waswahili wasema Chema chajiuza kizuri cha jitembeza (sikumbuki tena methali) ila ndio hali halisi tusijidangane na kusafiri na mamia ya watu eti kuomba wawekezaji waje.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom