Field Marshall ES
R I P
- Apr 27, 2006
- 12,622
- 1,235
::Makala za Uchumi Jumatano Nov 07, 2007
Kikwete alivyovutia wawekezaji Italia,kupigia debe mapinduzi ya kilimo Afrika
Habari Zinazoshabihiana
Siku ya Chakula Duniani na kauli mbiu ya chakula ni haki 16.10.2007 [Soma]
Uchumi Tanzania unaweza kukua hesabu zikizingatiwa 05.09.2007 [Soma]
Mikakati ya kumkomboa mkulima, mfugaji kiuchumi 13.03.2007 [Soma]
*Mkurugenzi WFP amsifu kwa kuisemea Afrika
*Rais Ujerumani amuunga mkono kuhifadhi mazingira
*Aeleza fursa tele za uwekezaji, Italia kumsaidia
HIVI karibuni, Rais Jakaya Kikwete alizuru Italia, Vatican na Ufaransa ambako pamoja na mambo mengine, alitumia fursa hiyo kuisemea Tanzania na Afrika kuhusu mapinduzi katika kilimo na kuhifadhi mazingira na kuvutia wawekezaji. Mwandishi Wetu, GODFREY LUTEGO aliyekuwa mmoja wa waandishi wa habari walioandamana na Rais katika msafara huo anaeleza katika makala yake ya pili, mwito wa Rais kuhusu mabadiliko katika kilimo na alivyovutia wawekezaji Italia.
WAKATI akijinadi katika kampeni za kuwania urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM mwaka 2005, Rais Jakaya Kikwete alitumia kauli mbiu ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania akiamini Tanzania yenye neema tele inawezekana. Tangu aingine madarakani, Rais Kikwete amekuwa akihangaika usiku na mchana kutimiza ahadi yake hiyo kwa Watanzania licha ya jitihada zake hizo kuathiriwa na majanga ya ukame, njaa, kupanda kwa bei za mafuta ya petroli, umeme kukatika. Pamoja na yote hayo, Rais anaonekana hajachoka na wiki mbili zilizopita alienda Italia kuithibitisha dunia kuwa, alipania, bado amepania na ataendelea kupania kuwaletea Watanzania, maisha bora kama alivyowaahidi kama si leo, basi miaka ijayo kutokana na miradi mbalimbali anayoipigia debe yenye kulenga kuboresha maisha ya wananchi kwani kauli yake ilikuwa thabiti.
Alienda Italia kufanya nini ?
Wakati baadhi ya wananchi na hasa viongozi wa vyama wa siasa vya upinzani wakiendelea kuhoji safari zake za nje, Rais Kikwete ameendelea kwenda huko nje kuonesha safari hizo si za mambo binafsi bali ni za kuwatumikia Watanzania wote. Akiwa Italia, Rais Kikwete alipata fursa ya kuhutubia mkutano wa 27 wa Shirika la Kilimo duniani (FAO) makao makuu ya FAO, Rome katika maadhimisho ya Siku ya Chakula duniani ambayo mwaka huu ujumbe wake ni Haki ya chakula kwa wote. Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliwataka wahisani wasaidie kuboresha kilimo akiamini ndicho msingi mkuu wa ukombozi. Alitaja baadhi ya matatizo yanayosababisha dhamira ya maisha bora kwa wote iwe na kigugumizi na kuziomba nchi wahisani zisaidie kuyaondoa kwani Serikali pekee haiwezi. Rais alisema kwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini ambako kilimo ndio chanzo kikuu cha ajira na riziki na kilimo ndio kinachochangia asilimia 45 ya pato la Taifa (GDP). "Ni wazi kuwa kama kilimo barani Afrika na Tanzania kikiboreshwa, kitawezesha kuwepo kwa uzalishaji chakula
zaidi na kuondoa umaskini, " alisema katika hotuba yake. Hata hivyo, alionya, lengo la kuboresha kilimo Afrika ambacho ni lengo la kwanza la mpango wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG) kuondoa njaa na umaskini, kikichangia asilimia 30 ya GDP na asilimia 40 ya mauzo ya bidhaa za nje kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara linaweza lisifikiwe.
Kwa nini malengo hayawezi kufikiwa:
Kuna matatizo mengi lakini baadhi ni kutegemea kilimo cha mvua ambacho Rais alisema kutokana na ukame, kilimo kimeathirika na kusababisha wakulima wavune mazao kidogo hivyo kuwepo haja ya kupunguza kilimo cha kutegemea mvua. Mbali ya umwagiliaji, Rais Kikwete alitaka matumizi ya sayansi na teknolojia katika kilimo yaongezwe kwani pamoja na jitihada za tangu uhuru kuboresha kilimo, bado mambo si mazuri kwani sehemu nyingi bado kilimo cha jadi cha matumizi ya jembe la mkono la tangu enzi za Yesu bado ndio kinatumika. Maeneo mengi bado yanatumia zana hizo kutokana na kukosa matrekta na plau za kukokotwa na ng'ombe kwa sababu ya bei kubwa za matrekta lakini pia baadhi ya maeneo kutokuwa na maksai wa kuvuta majembe ya kukokotwa. Rais alitaka pia Afrika iongeze jitihada katika utafiti na maendeleo ya kilimo na kujenga uwezo wa kuzalisha mbegu bora zaidi za mazao na kuzitawanya kwa wakulima mapema huku kwani utumiaji mbegu zisizo na ubora hupunguza tija. Kwa mujibu wa Rais Kikwete, wakulima wa Tanzania wanatumia wastani wa kilo nane za mbolea kwa kila hekta kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha na Uholanzi ambako wakulima hutumia kilo 578 kwa hekta na mkulima wao kuvuna zaidi.
Alisema ili kufanikisha wakulima kupata mbolea na kuitumia zaidi, kuna haja ya kuwapa ruzuku na kuleta mageuzi ya uchumi Afrika kuzingatia utoaji ruzuku na madawa ya kuulia wadudu.
Kwa kukosa madawa ya kuua wadudu katika magugu, katika mazao wakati yakimea au yakivunwa, wakulima wengine wamejikuta wakipata hasara kubwa na hivyo kuendelea kuwa maskini kutokana na kupata kipato kidogo. Hata hivyo, Rais alisema, madawa hayo hayawezi kusaidia bila mpango wa huduma za ugani kwa wakulima kwani imebainika kutokuwepo kwake kunaathiri maendeleo ya kilimo cha kisasa kwani wakulima wanaendelea kulima kwa mbinu za kizamani. Kutokana na hayo, Rais alisema, wataalam wa ugani wa kuwafundisha kilimo cha kisasa, mbinu na teknolojia yake wanahitajika kupitia mpango wa mapinduzi ya kilimo Afrika.
Kwa mujibu wa hotuba yake, ukosefu wa mikopo kutoka benki na taasisi nyingine za kifedha ni eneo lingine linalokwamisha maendeleo ya wakulima kutokana na mabenki mengi kutokuwa tayari kuwakopesha kwa madai ni hatari kwani hawana amana. Hayo na mambo mengine ndiyo yanaumiza wakulima wadogo wadogo kwani hukosa pembejeo na huduma nyingine ambazo zingewazezesha kupanua kilimo chao na kuboresha maisha yao. Tatizo la masoko ya mazao ya wakulima lililo katika nchi nyingi ni eneo lingine linalosumbua wakulima kwani hawajui wakauze wapi mavuno yao na kupata bei muafaka inayolingana na thamani ya mazao yao kwani uzoefu umeonesha kuwa wamekuwa hawapati soko la uhakika na wanapunjwa bei zake. Changamoto nyingine katika kuendeleza kilimo ni miundombinu inayoathiri uuzaji wa mazao ya kilimo Afrika ambapo sehemu kusiko na miundombinu mizuri, haziendelei kwa kukosa fursa ya kuzalisha zaidi kwani mazao hayafiki sokoni, wakulima hawapanui kilimo kwa kukosa pembejeo na huduma za ugani.
Nchi zitafanikiwa vipi kujikomboa:
Ili ziweje kujikomboa, Rais Kikwete alitaka nchi za Afrika zisaidiwe kuboresha kilimo chake kiwe cha kisasa kwa kubuni mipango na kupewa misaada ya kiufundi ambayo hazina, ziajiri maofisa ugani, kujenga miundombinu ya kisasa na masoko.
Aliishukuru FAO kwa kusaidia kuendeleza kilimo Tanzania na nchi nyingine duniani na kutoa rai iwezeswhe zaidi na nchi wahisani ziitikie mwito wa FAO kutaka miradi iwezeshwe ili iweze kutekelezwa kuondoa njaa na umaskini kila mtu aishi. Tanzania inapata dola bilioni 2.5 kutoka FAO katika Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) ulioanza 2006 ukiwa ni mwanzo wa maendeleo ya kilimo Tanzania hivyo kilichobaki ni kuutekeleza vyema na raslimali zikiwepo,kilimo kitaboreka.
Rais alisema Tanzania itaendeleza kilimo ikishirikiana na FAO.
Kikwete aungwa mkono:
Jitihada za Rais Kikwete kutaka Watanzania na wananchi wa Afrika kwa jumla kupata maisha bora kupitia kilimo ziliungwa mkono na watu mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wa FAO. Rais Horst Koelhler wa Ujerumani na pia Mwakilishi wa Papa, Monsinyori Renatus Volante, mchezaji wa zamani wa Italia, Roberto Baggio nao katika nyakati tofauti walimuunga mkono haja ya chakula zaidi kuzalishwa ili kuondoa njaa duniani.
Monsinyori alisoma salamu maalum za Papa Benedict XVI. Rais wa Ujerumani yeye aliungana na Rais Kikwete kupiga vita umaskini na njaa Afrika na duniani kote kwa jumla akionya vita, migogoro na machafuko ya kisiasa vinapaswa kuepukwa kwani vinachangia kurudisha nyuma maendeleo makubwa yaliyofikiwa na nchi kuwaondolea wananchi umaskini na njaa. Akihutubia mkutano huo pia, Dkt. Horst Koehler alisema mapambano dhidi ya njaa lazima pia yajumuishe mikakati ya kuzuia vita na migogoro kwani vita ikitokea, huharibu maendeleo yaliyofikiwa na nchi kwa miaka mingi nyuma. Rais huyo alisema Shirika la kimataifa la Oxfam linakadiria kuwa vita huzigharimu nchi za Afrika zaidi ya dola bilioni 18 kwa mwaka na asilimia 15 ya pato lake la uchumi na ndio maana Jumuiya ya Afrika (AU) na NEPAD zimesema suluhisho kuu ni kuzuia vita kutokea na kuleta na kusimamia amani ili nchi husika ziwe na usalama ziweze kuzalisha na kuondoa njaa.
Kwa mujibu wa Rais huyo wa moja ya mataifa makubwa, amani peke yake bila uwiano mzuri wa kiuchumi na biashara hautasaidia hivyo kuna haja kuwepo kwa mfumo mzuri wenye uwiano sawa wa biashara kwani uliopo sasa uliwekwa na nchi zilizoendelea, zenye viwanda na hakuna ubishi kuwa watu wengi duniani wa nchi zilizoendelea, wamenufaika na mfumo huo. Alisema walionufaika ni nchi zilizoendelea ambazo zinadhibiti soko la dunia hivyo suala la msingi la kujadili ni kuzipatia nchi zote haki sawa ya kushiriki na kunufaika na soko la dunia kwani nchi zinazoendelea, za dunia ya tatu bado zinaminywa. Rais huyo alisema tabia ya nchi tajiri kutoa ruzuku kwa wakulima wao hasa kwa mazao ya kuuza nje hasa ya kilimo inazifanya nchi maskini kushindwa kushindana katika soko. Alitoa mfano wa nyanya ya kopo kutoka nchi tajiri inavyoua soko la nyanya ya Senegal kwa kuwa itauzwa rahisi kutokana na gharama za kuitengeneza kuwa chini kwa sababu ya ruzuku ambayo Serikali ya nchi tajiri inawapa wakulima wake. Ili kuondoa hali hiyo, Rais huyo alipendekeza kuwe na mfumo mpya wa biashara wa dunia wenye mwelekeo wa maendeleo kwa wote bila ubaguzi ambao utaruhusu masoko ya nchi tajiri yawe wazi kwa bidhaa kutoka nchi maskini na ushuru kwa bidhaa zinazoingizwa humo upunguzwe ili maskini nao wawekeze huko. Alisema kunahitajika mfumo wa biashara unaozingatia hali halisi na mahitaji ya nchi maskini zinazoendelea na kwamba lazima raslimali za nchi hizo zinufaishe watu wake.
Furaha ya Ujerumani:
Rais huyo wa Ujerumani alisema anafurahi mauzo ya bidhaa kwenye biashara sawia kwa Ujerumani yaliongezeka kwa asilimia 50 mwaka jana. "Tukinunua bidhaa kutoka nchi maskini, wakulima wa nchi zile wanapata fedha zaidi kuliko wangeuza soko la dunia, " alisema. Kwa mujibu wa Kiongozi huyo, ili kuweka uwiano mzuri wa mataifa yaliyoendelea, uchumi unaokua na nchi maskini zinazoendelea utakaodumisha dhamira ya dunia moja yenye usawa, kunahitajika Umoja wa Mataifa (UN) wenye nguvu na imara kiutendaji kwani ndio unaoweka mikakati ya maendeleo.
Je, UN itafanikishaje hilo. Rais huyo alisema ni kwa Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono mabadiliko yaliyoanzishwa na Katibu Mkuu wa zamani wa UN, Dkt. Koffi Annan kuhusu masuala ya maendeleo, amani, haki za binadamu kwa wanasiasa kuyatekeleza akiamini linawezekana wakubwa wakiamua. Alisema mengi yanaweza kufanyika kwa kuzifanya taasisi zote zilizo chini ya UN kufanya kazi zake kama chombo kimoja na hivyo akatoa changamoto kwa Shirika la Kazi Duniani (ILO), la biashara (WTO) na taasisi za fedha kushirikiana na nyingine. Aliwaambia washiriki wa mkutano huo kuwa, wana jukumu la kufanya mabadiliko yanayoendelea kufanywa FAO yafanikiwe na akaitaka FAO ijikite katika jukumu lake kuu la utoaji taarifa na utaalam wa kilimo na chakula, irekebishe utoaji maamuzi yake na uendeshaji menejimenti yake ikubalike kwa UN na nchi wanachama, iboreshe uhusiano wake na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na ule wa kilimo na chakula (IFAD).
Alisifu jitihada za NEPAD kuimarisha demokrasia na utawala bora Afrika katika jitihada zake za kupambana na umaskini katika nchi za Afrika kwani masuala hayo ni ya msingi katika kuweka sera nzuri za uchumi zinazozingatia maslahi ya wananchi kuondoa umaskini. Alitaka nchi tajiri kusaidia jitihada za nchi hizo kwa kushirikiana na NEPAD. Pia aliisisifu NEPAD kwa kutoa kipaumbele kwa maendeleo ya vijijini na kilimo kwa kujua wengi wa watu hasa wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la sahara wako vijijini. Alitaka lengo kuu la vita dhidi ya njaa liwe kuhakikisha watu wana chakula cha kuzalisha wao au maeneo ya karibu mambo yanayohitaji, mashine za kisasa za kulimia, teknolojia, mikopo, miundombinu, masoko na umilki ardhi wa uhakika na si kunyangànywa ardhi. Aliungana na Rais Kikwete kuzungumzia haja ya udhibiti wa uchafuzi wa hali ya hewa na mazingira ambao Afrika na jumuiya ya kimataifa haujafanikiwa katika hilo ili kuwezesha mazingira yalindwe kwani uharibifu ukiachwa uendelee, mafuriko, ukame yatazidi. Alisema nchi tajiri ndio zinachangia zaidi kuharibu mazingira kutokana na hewa chafu kutoka viwandani na hivyo zina wajibu mkubwa zaidi wa kupambana na uharibifu huo kuupunguza. Alisema Umoja wa Ulaya (EU) wakati Ujerumani ikiwa Rais wa EU ilijaribu kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na
lengo sasa ni kuishusha hadi asilimia 20 mwaka 2020.
Je, jitihada za Kikwete zilizaa matunda
Je, katika ziara hiyo Italia, kilio cha Rais Kikwete kilizaa matunda na kuthibitisha kuwa ziara zake si za kupoteza wakati na raslimali za Watanzania kama wapinzani wanavyodai. Jibu ni ndiyo. Rais Kikwete aliweza kushawishi kwa vitendo na maneno ya kwenye hotuba yake, wahisani mbalimbali, FAO yenyewe na pia Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Aliikuna WFP hadi ikaahidi kuwasaidia wakulima kupata masoko ya uhakika, mikopo, bima na wanafunzi kula shuleni yote ikiwa imelenga kuboresha maisha ya Watanzania 2008. Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Bibi Josette Sheeran alimweleza Rais Kikwete mjini Rome kuwa alivutiwa na hotuba aliyoitoa kwenye mkutano wa 27 wa Siku ya Chakula Duniani ulioandaliwa na FAO na kufanyika makao makuu ya FAO.
Kilichofanya Mkurugenzi WFP aguswe na Kikwete
Yako mambo mengi ambayo Tanzania kama nchi imefanya na kuikosha WFP na FAO kwa jumla na nchi nyingine wahisani katika suala zima la mchakato wa maendeleo kama vita dhidi ya rushwa, hali ya usalama wa nchi kuwa shwari, kupanuka kwa wigo wa demokrasia, kuimarika kwa miundombinu ya barabara na njia nyingine za mawasiliano, kukuza kiwango cha elimu n.k. Lakini mbali ya hayo, Mkurugenzi wa WFP, Bibi Sheeran alionesha kuguswa na kufurahishwa zaidi na jinsi Rais Kikwete alivyoguswa na matatizo ya wakulima na alivyoonesha nia ya kuyaondoa akiwa ni mmoja wa viongozi wachache Afrika walioonesha dhamira hiyo ya kusaidia wananchi wake. Mkurugenzi huyo alisema alipokutana na Rais Kikwete na ujumbe wake uliokuwa na mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe na wa Chakula na Kilimo, Bw. Stephen Wassira kuwa, alikuwa amezoea kuona matatizo mengi ya Afrika yakisemwa na watu wa nje wakiwemo watu mashuhuri mbalimbali, akina Bonno wanaoguswa nayo. Hata hivyo, alishangaa kumwona Rais Kikwete kwa ujasiri mkubwa akieleza matatizo yanayokwamisha maendeleo ya Afrika na kuyaainisha vyema akiomba msaada wa nchi wahisani na taasisi mbalimbali zilizojikita kuondoa umaskini duniani. Kufuatia kukoshwa kwake na hotuba ya Rais Kikwete, Mkurugenzi huyo alisema, katika kuunga mkono jitihada za Rais huyo kuanzia mwakani, WFP itaiweka Tanzania katika mpango wa majaribio wa kuondoa umaskini na kukuza elimu.
Katika mpango huo, alisema WFP itawawezesha wakulima kulima mazao zaidi na kuuza zaidi kwa kuwapa mikopo, bima na kuwawezesha kupata masoko ya uhakika ya mazao yao na kuyasafirisha kufuatia kuwepo miundombinu bora kutoka shambani, sokoni, viwandani na hii itamaanisha kuwa watu hao sasa watakuwa na maisha bora aliyowaahidi Rais Kikwete 2005.
Mpango huo utakaoanzishwa pia Ghana unalenga kuvunja nira ya umaskini. Wakulima wataondokana na hatari ya kukosa chakula na mazao ya biashara kwa kuzalisha mazao kwa kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua tu na kuathiriwa na ukame na kufaidika na bima ukitokea moto, ukame, mafuriko. Kwa mujibu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa WFP, ndani ya mpango huo, kutakuwa pia na mpango wa kuwapa chakula (angalau uji), wanafunzi wawapo shule ili waweze kushika vyema masomo darasani bila kuathiriwa na njaa na uchovu. Katika kufanikisha mpango huo, mwaka huu watazieleza nchi wahisani, G8 wasaidie kuufanikisha kwani wakifanya hivyo watasaidia elimu na mkulima kuondoa umaskini unaomkabili.
Kwa mujibu waBibi Sheeran, inakadiriwa kila mtoto atatumia dola za Marekani senti 10 (sh. 120) kwa siku kwa kunywa uji.
Tanzania tayari ina mpango wa kulisha wanafunzi wake shuleni ambapo zaidi ya shule 300 Manyara, Dodoma na Arusha zinatoa chakula kwa watoto. Japan ilianza mpango kama huo wa kutoa chakula kwa wanafunzi shuleni tangu mwaka 1890.
Kwa kuangalia haraka haraka, mpango wa WFP ni mgeni lakni kimsingi, ni mpango uliokuwa umeanishwa katika mpango wa elimu ya kujitegema enzi za uongozi wa Mwalimu Nyerere.
Wakati huo, karibu kila shule ilikuwa na mradi wa kilimo ambapo wanafunzi walikuwa wanalima mazao ya biashara kama pamba, kahawa, na chakula kama mahindi, mtama, uwele, mhogo, mpunga kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wake na ya biashara kwa ajili ya kuuza na kutunisha mfuko wa shule. Ni mfuko huo uliotumika kusaidia kuziba nakisi ya bajeti ya Serikali katika kununua samani, vifaa vya michezo, tiba na kugharamia usafiri wa walimu shuleni kwa idhini ya Kamati za shule. Ni vipi mpango huo ulikufa au kufifia, ndio changamoto. Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alimtaka Rais Kikwete amhakikishie nia ya Seriali kuunga mkono na kusimamia mpango huo jambo ambalo Rais alilifanya akithibitisha nia ya Serikali yake kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere kuendeleza mazuri aliyoacha ukiwemo mpango huo wa kuwezesha mashule. Rais Kikwete alisema mpango huo utasaidia Tanzania kufanikisha ujumbe wa mwaka huu wa FAO wa Haki ya kupata chakula kwani kila mtu, mkulima na watoto atapata chakula. Bibi Sheeran alisema wameamua kuanzisha mpango huo baada ya kuona wakulima katika nchi nyingi duniani na hasa Afrika wanakosa masoko ya kuuza mazao yao, miundombinu ya kuyasafirisha hadi sokoni na wanaathiriwa na njaa na ukame kwa kutegemea kilimo cha mvua badala ya umwagiliaji.
Kikwete apinga WFP kununulia chakula wakimbizi nje
Alisema WFP itaendelea kusaidia Tanzania kupambana na njaa, ukame, mafuriko na wakimbizi na kuweka mipango ya dharula ya kupambana nayo. Rais Kikwete alimweleza Tanzania haifurahishwi na mpango wa WFP kununua chakula nchi za nje kwa ajili ya wakimbizi wakati kuna mazao mengi ya wakulima nchini ambayo yangenunuliwa, wangenufaika. Huu ni ujasiri wa aina yake ambao Rais kama kiongozi wa nchi ameounesha kwa wahisani. Alisema haileti maana Tanzania kuendelea kupokea wakimbizi na kuwapa hifadhi lakini WFP iwalishe kwa kununua chakula cha kutoka nchi za nje na jirani. Katika kuweka mambo sawa, Rais alitaka kuanzia sasa WFP iwe inanunua chakula kwenye ghala la Hifadhi ya Chakula ya Taifa (SGR) ambalo lina tani 20,000 za akiba ambazo zikinunuliwa, SGR nayo itanunua nafaka za wakulima nchini na hivyo kuwaondolea umaskini na kuleta maisha bora kwa Mtanzania.
Ingawa Mkurugenzi Mtendaji huyo hakutoa jibu la papo hapo kuhusu changamoto hiyo ya Rais, ni wazi hilo likitekelezwa, litasaidia kuwakomboa wakulima wa Tanzania kwa kuwa watakuwa na uhakika wa moja ya masoko, wataweza kuwapa watoto wao, elimu kwa kulipia gharama mbalimbali za elimu. Mpaka sasa Tanzania bado inahifadhi zaidi ya wakimbizi 500,000 Kigoma, Kagera idadi ambayo inamaanisha kuwa, kama wakulima watapewa fursa hiyo ya kuwalisha chakula, wakulima zaidi ya 500,000 na familia zao watanufaika pia. Lakini jitihada za Rais Kikwete hazikuishia kwenye kupiga debe la kutaka mabadiliko katika kilimo tu ili kuwasaidia wakulima kupata maisha bora bali alitumia muda wake adhimu pia kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali za biashara.
Hatua hiyo ilithibtisha jinsi gani ana dhamira ya kweli ya kuleta maisha bora kwa kila mtu kulingana na eneo lake kadri fursa zinavyopatikana, muda kuruhusu licha ya kelele za wapinzani akithibitisha usemi kelele za chura hazimzuii ng'ombe kunywa maji na msemo wa wahenga kuwa mtoto acha kulia, acha watu waone wenyewe hivyo anatenda, watu waamue.
Ni lini watu wataona Rais Kikwete anafanya nini anapokwenda nje. Ni suala la muda. Kuna mambo yatakayochukua muda mfupi na mengine muda mrefu kulingana na itifaki, mawasiliano, mashauriano, utafiti, raslimali, miundombinu na dhamira.
Hata hivyo, la haraka ambalo kila mtu ameliona na ama kulisikia ni dhamira ya Italia kama nchi kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ya maendeleo ambayo imeoneshwa na wafanyabiashara wa huko na kusisitizwa na Serikali yao.