Kikwete alivyoshangiliwa Bungeni leo inamaanisha nini?

Ina maanisha...., wamjengoni wengi bila kujali vyama vyao vya kisiasa na itikadi, walikuwa "WAPIGA DILI", ndani na nje ya mjengo.

Mstaafu hakuwa na muda na watu wa aina hiyo, ilimradi yake yanamnyookea, aliona mengine awaachie wenyewe.

Au kwa lugha nyepesi, mstaafu alikuwa kama mtoa riziki ambaye yeye alipojimegea chake, akaona ngoja jukumu hili niwaachie wataka riziki wenyewe waamue wafanye mgawanyo huo, basi ikawa mwenye nguvu anajikatia tu anavyojisikia. Hao wanaoshangilia leo mjengoni ni miongoni mwa wale waliokuwa na nguvu.

Nitakuwa nimeeleweka tu maana hamna namna...
 
Back
Top Bottom