Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.

Sasa ilikuwa hivi,
Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombewengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwawingi wakati huohuo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.

Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwamengi mno na mazao yametapakaa mashambani,. akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.

Aliendelea kufanya hivyokwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....

Sasa bwana ,,kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa raisi kipindi hicho JK Nyerere.

Katika barua hiyo akaandika lawama nyiingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwakuwa navunja miiko ya uongozi na mambo mengine meengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)...

Basi bwana, akamalizia mwisho kwakujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa rais wa nchi wakati huo!......

Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.

Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu eaisi kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni maMbo yenu kayamalizeni hukohuko".

Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yakee...., sasa siku mija alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia rais!!....

Sayore akaisoomaaa we akashangaa mno!! na akafura kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...

Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....

Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwauliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na saemekinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna mkuu akiwemo Kikwette!!!

Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa mkwere...

Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...

Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yuile mmasai! akatetemeka macho yakamtoka lip! kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani......

Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogo kabisa kuingia barabara ya kuu...

Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER, hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake......

Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama... lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!!

Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....

Kwa hisani ya jf maktaba
Makaburi kama haya yanamwitaji
"The undertaker" .
Naomba niombe kauli kwa bibie FaizaFoxy. Kama atakua na lolote LA kuchangia hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadaye Kikwetu alichaguliwa kuwa Rais,
Tupe yatokanayo.
Uhusiano wa Sayore na Kikweti wakati wa Urais wake ulikuaje?
 
Wakuu:
Hii inawezekana kuwa ni riwaya.
Afisa yeyote wa jeshi (commissioned/non commissioned) hana mamlaka ya kuwasiliana na CiC pasipo na kupitia kwa CDF vinginevyo ni kukiuka sheria. Lakini sio mbaya kuisoma riwaya hii.
 
Wakuu:
Hii inawezekana kuwa ni riwaya.
Afisa yeyote wa jeshi (commissioned/non commissioned) hana mamlaka ya kuwasiliana na CiC pasipo na kupitia kwa CDF vinginevyo ni kukiuka sheria. Lakini sio mbaya kuisoma riwaya hii.
Sawa Mkuu
 
Back
Top Bottom