Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa msukosuko! | Page 14 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa msukosuko!

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Mzizi wa Mbuyu, Feb 25, 2011.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.

  Sasa ilikuwa hivi,
  Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombe wengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwa wingi wakati huo huo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.

  Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwa mengi mno na mazao yametapakaa mashambani akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.

  Aliendelea kufanya hivyo kwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....

  Sasa bwana kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! Sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa Rais kipindi hicho JK Nyerere.

  Katika barua hiyo akaandika lawama nyingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwa kuwa inavunja miiko ya uongozi na mambo mengine mengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)...

  Basi bwana, akamalizia mwisho kwa kujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa Rais wa nchi wakati huo!......

  Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.

  Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu eaisi kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni mambo yenu kayamalizeni hukohuko".

  Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yake. Sasa siku moja alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

  Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia Rais!!

  Sayore akaisoomaaa we akashangaa mno!! Na akafura kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...

  Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....

  Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwauliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na saemekinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna mkuu akiwemo Kikwette!!!

  Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa mkwere...

  Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...

  Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yuile mmasai! akatetemeka macho yakamtoka lip! kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani......

  Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogo kabisa kuingia barabara ya kuu...

  Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER, hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake......

  Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama... lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!!

  Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....

  **Ndugu zangu hiki ni kisa cha ukweli kwa 100%, inawezekana uandishi wangu ukawa na upungufu, lakini niemekipata kutoka watu mbalimbali waliowahi kuwa karibu sana na mkasa huu.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #261
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  kumbe rais wetu MKUDA? Ndo Maana Liyumba anakiona cha mtemakuni
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #262
  Sep 9, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kweli uandishi wako una mapungufu, Usa River na Monduli ziko mbali sana, ... au ulitaka kumaanisha Mto wa Mbu?
   
 4. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #263
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nyani haoni ********hebu pia tujikumbushe wakati slaa alipoondoka kanisani na kuukucha upadre wa kanisa katoliki,unajua sababu? ilikuwa kama hivi,kwanza alianza kwa kumuweka kimada rose kasili mtoto wa kimbulu hali ya kuwa sheria za kikanisa ambapo ana PHD yake zinakataza padre padre kuwa na mke.

  Sababu ya pili aliiba pesa za chama cha vipofu Tanzania zaidi ya shilingi milioni mia saba zilizotolewa na shirika la world vision tanzania kwa ajili ya kuwasaidia vipofu nchini jamaa akaiba pesa na mwenzake ambaye yeye alirudi kaniisani akaomba radhi akasamehewa na slaa akakimbilia CCM kuomba kugombea ubunge, lakini kumbe CCM chini ya mzee mwinyi walishamstukia huyu jamaa ni jambazi na anakuja ndani ya chama kutaka kuchakachua wakamnyima nafasi.

  Kilichojiri baada ya pale akakimbilia chadema ambacho hakikuwa na network kama ilivyo hivi sasa na akapewa nafasi ya kuwakilisha,mungu si athmani akashinda! toka ameingia bungeni mwaka 1995 - 2006 hakuwa akisikika kama yupo pale,baada ya kashfa zake za kijangili kuibuliwa kanisani na wanaccm naye akaona aanze kujifanya ana uchungu na taifa hili wakati hana mbele wala nyuma, eeeeeee Mungu Mwenyezi wa mbingu na nhi,tuepushe na fitna hii inayoitwa slaa.

  Kama aliweza kukusaliti wewe kanisani na mbele zako vipi asiweze kutusaliti sisi wadanganyika tena mbele zako? ni nani asojua sababu za chadema kutomrushia madongo rostam pale Igunga? ni kwa sababu kuna ukweli zile pesa za kifisadi mlizozikosa za kagoda sasa zinaisaidia chadema kwenye uchaguzi kwani kuna bif baina ya rostam na akina nape! habari ndo hiyo
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #264
  Sep 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,885
  Trophy Points: 280
  Umemaliza? haya nenda kalale maana naona viroba vya leo vimekuzidi uwezo.
   
 6. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #265
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Uliko taja ni mbali zaidi labda Ngarenaro ya chini ambayo ipo karibu sana na ARUSHA AIRPORT.
   
 7. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #266
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Kwa taarifa tu ni kwamba Sayore ulikuwa anatumia rasilimali za jeshi kufanikisha kilimo hicho.
   
 8. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #267
  Apr 1, 2014
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,363
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Huyu JK sijui nani atampa adhabu kwa kosa alilowatenda watanzania kwa kutoa maoni yake binafsi kwenye bunge la katiba badala ya kuyatoa kwa wakati kwenye tume ya Warioba akidanganya anakwenda kuzindua bunge maalum la katiba!

  JK mnafki hana mfano!
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #268
  Apr 1, 2014
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Jk anapaswa kujibu khoja au mtoto wake amsaidie. Kimya maana yake ni kuafiki.
   
 10. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #269
  Apr 3, 2014
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,363
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Bila shaka ni ukweli kwani isingekuwa kweli Kurugenzi ya Habari ya ikulu wangeshakanusha tangu 2011 habari hii ilipotoka!!
   
 11. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #270
  Dec 4, 2016
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,333
  Likes Received: 2,980
  Trophy Points: 280
  Mambo Yalikuwa Mazito Sana Yaani Duh Chupuchupu
   
 12. Kaka

  Kaka JF-Expert Member

  #271
  Dec 7, 2016
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 705
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 80
  Mkuu,

  Mheshimiwa Rais wa awake ya tano amewataka wampelekee malalamiko yao alipomuweka na askari magereza.

  Kaka ...
   
 13. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #272
  Dec 10, 2016
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Kwa Tanzania ya sasa..Hakuna mwanasiasa anayemfikia JK kwa siasa
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #273
  Dec 28, 2016
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Huwezi kuongoza taasisi ya umma na baadaye kufanya biashara na taasisi hiyo. Hapo Sayore alikiuka ethics za uongozi na vilevile misingi ya Ujamaa. Hivyo Kikwete alikuwa sahihi kabisa.
   
 15. jerrytz

  jerrytz JF-Expert Member

  #274
  Jan 9, 2017
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 5,693
  Likes Received: 3,114
  Trophy Points: 280
  Ulikuwa Monduli wakati JK anaandika barua.
  Ulikuwepo Dar wakati Nyerere anapokea barua na kuisoma.
  Ulikuwepo Ikulu wakati Nyerere anampa barua Mkuu wa Majeshi
  Ulikuwepo Ngome -wakati mkuu wa majeshi anampa barua Sayore
  Ulikuwepo Monduli Sayore alipoitisha kikao
  Ukamwona JK akitembea porini mpak USA river
  Ukamwona akipata lift kwenye gari ya ushirika
  Ulikuwepo alipofika Dar.....
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #275
  Apr 20, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  Nasisimka jamani, nikamateni jamani, wasije wakaniteka kina BASHITE na Duterte
   
 17. Deadbody

  Deadbody JF-Expert Member

  #276
  Apr 22, 2017
  Joined: May 30, 2015
  Messages: 2,776
  Likes Received: 3,979
  Trophy Points: 280
  H
  Kali hii
   
 18. intermediate

  intermediate JF-Expert Member

  #277
  Apr 22, 2017
  Joined: Nov 17, 2014
  Messages: 231
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  hahaha mkwere mpuuzi sana
   
 19. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #278
  May 8, 2017
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 16,927
  Likes Received: 60,386
  Trophy Points: 280
  Aiseee
   
 20. n

  niah JF-Expert Member

  #279
  May 20, 2017
  Joined: Sep 26, 2015
  Messages: 3,248
  Likes Received: 3,472
  Trophy Points: 280
  Nimesoma huu uzi nikitokea kwenye uzi wa barua ya Malima kujiuzuru. Duh.
   
 21. Ip man 3

  Ip man 3 JF-Expert Member

  #280
  May 20, 2017
  Joined: May 29, 2016
  Messages: 471
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 80
  Duuu
   
Loading...