Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

hakika historia ni somo zuri sana. huyo ndiye JK tunayemjua..... asingekimbia yangemtokea puani.

Hilo ni wazi kabisa ni mtu wa kuyaona mambo ila kuyaweka hadharani hawezi kabisa na ndio mpaka leo ni mtu wa kuyaweka majungu na kuyafanyia kazi ni bure khaaaaa hiyo ni aibuuuuu sana. yeye sia alikuwa Mjeda basi angeyakabili kijeda sasa kumbe ule woga anao mpaka huku yeye ni rais??

Kuna vitu wakuu mnanifanya niwadharau kwani mnakosa kuwa na ile title inayosema nyie ni great thinkers.

Jiulizeni maswali halafu mjijibu :-

a. Je tuseme kweli kimetokea swali la kujiuliza ni je JK alikosea kuandika barua kwenda kwa mwajiri wa mkuu wa chuo? Au hamfahamu definition ya whistleblowers?

b. Yupi mzalendo kati ya Sayore na JK kwasababu Sayore alikuwa anatumia madaraka yake for his own benefit. Akiwauzia chuo chakula na maziwa wakati yeye ndio mlipaji mwenyewe kama mkuu wa chuo. Huu si ndio ufisadi wenyewe? akijipandishia bei na kuongeza idadi nani angelihoji?

c. Mnaodai kuwa Nyerere aliliacha suala hilo jeshini sio kwamba aliona ni majungu na fitina mmejiuliza alitaka na kupendelea uadilifu ufanyike? Why kwasababu kama ni kweli huyu mkuu alitakiwa kuondolewa ila evidence ziko wapi kuprove hilo jambo? ikiwa ni kweli basi hiyo ni sababu moja wapo Nyerere hafai kuwa kiongozi kwasababu si mzalendo na aliruhusu ufisadi uendelee.
 
Wakuu manjua kuwa JK ana ID humu ya ukweli tokea akiwa waziri enzi za Mkapa sio mzaha na bado huwa anaitumia mara kwa mara kweli JF kiboko mpaka muheshimiwa presidaa ni memba wake!
 
kama hicho kisa ni cha kweli basi naona jk alikuwa mzalendo zamani,.may be alitumia inappropriate channel kulingana na standard za jeshi,
baada ya pale naona mkwere aliapa kuifisidi hii nchi mpaka tukome,..hii story has been told half,..haiwezekani mtu alete info ya kizalendo afu apotezewe lazima there was more than that.
mkwere alikuwa snitch AKA informer,
kwa story ilivyoelezewa niko upande wake atleast kwa kipindi kile sio leo na tuquestion busara ya mwalimu kwa hilo...
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Haiingii akilini mtu sijui Kapteni wa jeshi aandike barua kwa rais hahahaha bado sana!!!
 
Mkuu unaonyesha kichwa yako inamemory ndogo sana mpaka unakwenda kwa budget.
Naweza amini story kwa kuwa kuna mifano mingi ya Mkwere ambayo inaonyesha jamaa hakuanza fitna leo wala jana.
Yupo wapi Steven Mashishanga nenda kamuone morogoro mzee alivyochoka kwa kumsupport Sumaye wapi Philip Mangula katibu mkuu CCm kipindi cha mkapa hakumsupport JK sasa anaendesha baloon lililochoka Iringa, na wengi wa wanazuoni wanasema katika kosa alilofanya Mkwere CCM ni kumpiga chini Mangula mtu aliyeweza kudumisha nidhamu chamani.

Fuatilia stori ya Professa Mahalu na kesi yake ya ubadhirifu wa pesa kule ubalozini Italia na safari ya Kikwete Italy pindi Mahalu akiwa balozi na baada ya kikwete kurudi kesi ikashonwa ili kumkomoa Mahalu. so binafsi naweza amini kwani inaendana na visasi na fitna nyingi, ikumbukwe Kikwete alikuwa mkufunzi so maya be alidhani anaweza pandishwa cheo but hakufuata Military Chain of Command

Kama Mahalu ni msafi si itajulikana tu si kesi ipo mahakamani??? Mbona dogo una majungu sana
 
Kuna vitu wakuu mnanifanya niwadharau kwani mnakosa kuwa na ile title inayosema nyie ni great thinkers.

ikiwa ni kweli basi hiyo ni sababu moja wapo Nyerere hafai kuwa kiongozi kwasababu si mzalendo na aliruhusu ufisadi uendelee.

hawa ni wale wale kama sio JK mwenyewe au jamaa wenye ubongo mufilisi kama yeye...ambaye hatambui kuwa nyerere ni BABA WA TAIFA......

KIFUPI kauli yako haijadiliki.....
 
..JF kunapatikana kila data..!niliwahi kusema humu, na nina rudia tena historia za watu zinawafanya wawe hivyo walivyo...ndicho ninachoamini.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Mwalimu aliweza kumshughulikia mpambe wake wa harusi (best man) na waziri wake wa nchi za nje, Oscar Kambona hadi akakimbia nchi kwa sababu ya tuhuma za ubepari. Nadhani suala la Sayore lilikuwa dogo sana kwake.

Best man hakuwa jeshi lakini Sayore angeweza kuorganise kumuondoka kwake. Unadhani yeye hakutafakari yote hayo?

Furthermore, alimuogopa best man wake kwa vile alikuwa na mvuto zaidi kuliko yeye. Wakati wa Army mutiny best man ndiyo alisikilizwa na wanajeshi kwa hivyo jamaa akaingia hofu. Soma declassified CIA reports.
 
Sio hayo tu kafanya mengi sana hata kupora mademu wa rafiki zake enzi hizo kwa mzee mmoja maaeneo ya meada pub sinza..

Sasa kama wakina mama walikuwa wanajigonga gonga kwa kupenda vyeupe na yeye hapitiwi na sketi mbele ulitaka afanye nini?

Tunaona hata leo hii kwenye forum kuna wakina dada wanajitangazia wanataka wachumba weupe.
 
Mkuu una ushaidi na hilo?let the man rest in peace Dude......Uwezi kupata umaarufu kwa kutoa a cheap crap like this.....Think Big Buddy!

Let him rest in peace indeed !! Lakini ukweli ndio huo na laiti mwanae asingekuwa fisadi kama baba yake angecollaborate taarifa hii!! Sasa ukitaka amini la sivyo kalagha baho!!
 
Nadhani hapa tunazungushana maneno tu; si kuna profesa aliyeandika biography ya JK hivi karibuni na inaonekana ni kama official biography? Hakuna mtu mwenye hicho kitabu ambaye anaweza kutuambia inasemwa nini kuhusu kuondoka kwa JK Monduli?
 
Wakuu manjua kuwa JK ana ID humu ya ukweli tokea akiwa waziri enzi za Mkapa sio mzaha na bado huwa anaitumia mara kwa mara kweli JF kiboko mpaka muheshimiwa presidaa ni memba wake!

el toro, wewe ndo JK nini?, kwani huko monduli hapakuwa na vikao vya menejiment?, kwa nini hakulitaarifu jeshi bali kamwandikia rais?, unataka kuhararisha kuwa jeshini hapakuwa na uwazi?. Huyu ni mtu hatari.
 
Very interesting story!
Huyu jamaa ndivyo alivyo hasa.

Hii stori ilitakiwa ichapishwe kwenye Gazeti mojawapo linalotoka weekly kama Mwanahalisi au Raia Mwema ili watu wapate ''The other side of the coin" kuhusu Mkwere.

Unajua Mwalimu J.K.Nyerere alikuwa HATAKI UNAFIKI, MAJUNGU NA UMBEYA.Hii ilikuwa ni komesha kwa Mkwere.Kwa akili ya Mkwere alifikiri akipeleka huo umbeya kwa Mwalimu basi yeye angelipewa Ukuu wa Chuo cha Monduli.

Lakini siyo kwa Mwalimu bana!!!
 
Nadhani hapa tunazungushana maneno tu; si kuna profesa aliyeandika biography ya JK hivi karibuni na inaonekana ni kama official biography? Hakuna mtu mwenye hicho kitabu ambaye anaweza kutuambia inasemwa nini kuhusu kuondoka kwa JK Monduli?

Labda uangalie CV yake hapa chini....nadahni alipata demotion 1986...pengine kwa sababu hiyo
2005-???? President,URT
1995-2005Minister for Foreign Affairs and International Cooperation
1995-2005Member of Parliament for Chalinze Constituency
1994-1995 Minister for Finance
1990-1995 Member of Parliament for Bagamoyo Constituency
1990-1994 Minister for Energy, Minerals and Water Development
1988-1990Deputy Minister for Energy and Minerals
1986-1988 Nachingwea and Masasi Districts (CCM) District Secretary
1983-1986 Political Commissar Tanzania Military Academy in Monduli
1981-1983 Tabora CCM Regional Secretary
1980-1981Administrative officer CCM Headquarters
1977-1980 Deputy Secretary of CCM, Zanzibar
1976-1977Singida Regional Secretary of TANU
1975-1976Deputy Regional Secretary of Tanganyika African National Union (TANU) in Singida
 
Ukiangalia hiyo demotion ya mwaka 1986 (kutoka katibu wa chama wa mkoa hadi kuwa katibu wa chama wa wilaya, unaweza kujiuliza maswali mengi sana!
 
Back
Top Bottom