Kikwete alivyoondoka Monduli chuo cha Jeshi kwa misukosuko

Ni halali katika zama zake, hakukuwa na sheria iliyokataza hilo.



ni wazi hujalisoma Azimio la Arusha, hakuna mahali ambapo azimio lilikataza hilo.


`


Azimio la arusha lilikataza kuchanganya biashara na utumishi wa umma. Mtu mwenye pesa ilikuwa ni number one disqualification.
 
Kikwete huwa haongelei ..sana maisha yake ya nyuma ya mwaka 1990...haongelei sana role yake jeshini...especially role yake vitani ..ambayo ukikaa na askari yeyote jambo la kwanza ni kujivunia histria yake ya mapigano...dunia nzima askari hiyo ndiyo fahari yao ..

AS of General Sayore yule jamaa uaskari upo kwenye damu...hata sasa ambako anazidi miaka 70 yuko as fit as ever...he walks 10 km daily kwenye Golf course.....anajivunia uaskari wake na hata waliokuwa chini yake wanasema ni askari anayependa nidhamu na anayechukia ugoi goi.......alikuwa hapendi tabia ya maafisa kufuga vitambi.....na watu kama kina Brigadier Karubi waliokuwa na vitambi enzi zake walikuwa wanamkoma wanapokutana kwenye retreat ya wakubwa wa jeshi....kwani alihakikisha kila asubuhi anamka saa 11. ..na kuanza route march na mchaka mchaka....kijeshi mkuu akishaamka atakachofanya wote inabidi mfuate....mabregadier na makanali wenye vitambi walikuwa wanamkoma ...
Kitu kingine tofauti ni kuwa huyu mzee hafichi kutumia majani....thats why macho yake hawezi kuacha kuwa nyekundu...but that kitu jeshini ni kawaida sana...ila yeye hafichi!!!

Historia ya Kikwete sidhani kama kwenye kile kitabu alichoandikiwa na profesa wa marekani ameeleza yote hata nitakitafuta.....kwakuwa zaidi ya maisha yake ya jeshini kutokuwa na la kujivunia ...tutapenda kujuwa kilichomfanya KATIBU MTENDAJI WA CCM- DAUD MWAKAWAGO ...akamshusha cheo JK...Ambaye alikuwa afisa wa ngazi za juu makao makuu ya chama kwa kuazia Kisiwandui na baadaye Lumumba idara ya usalama ya chama[alipofanya kazi na mrema ].

DAUD MWAKAWAGO alimchusha cheo toka makao makuu hadi kwenda kuwa katibu wa wilaya ..Singida,Tabora...etc Ilikuwa demotion ya hali ya juu ..wakati huo akiwa CAPT.jakaya...na Baadaye akaondolewa kwenye chama kwenda kuwa Mkufunzi wa jeshi mondoli ..baada ya kuwa amehudhuria kozi ya company comander na kupewa umeja........

Baadaye ndio akaondoka jeshini kwa yale yaliyoandikwa hapa....na kurudi Lumumba ambapo inaelezwa mzee kawawa alimsaidia na kumpeleka tena wilayani masasi ,lindi...kuwa tena katibu wa wilaya[fikirieni enzi hizo ..graduate ,na tena major .]..kazi ya makatibu wa wilaya wengi walikuwa darasa la saba...kina SALOME nYIti et al......

Kitu pekee ambacho kikwete anakiri kwenye historia yake ni namna WAZIRI MKUU WARIOBA alivyomsaidia kumuondoa porini...wakati anazindua kitabu kile anakiri hili......anasema ni warioba ambaye alikuwa ameenda kusini kuweka kambi kwa ajili ya mafuriko ya miaka ya 1988...alimkuta Kikwete Lindi ..na akamuonea huruma ...hasa kutokana na kukumbuka alikuwa makao makuu ya chama hadi kwenda kuwa katibu wa wilaya ...na akijuwa wazi kuwa anayo elimu inayotosha ..aliporudi DAR alimfuata mzee mwinyi na kumuomba ampe Kikwete ubunge wa Taifa.......mzee mwinyi alikubali ushauri wa mzee warioba ..akampa kikwete ubunge wa Taifa na unaibu wazir wa nishati na madini kumsaidia mzee Al noor kassam....hapo ndio ukawa mwanzo wa Maj. Kikwete kurudi mjini..na historia yake mpya ilianzia hapo....nadhani pia na kiumri akili zilikuwa zimepoa kiasi..ni wazi ujana wake ndio ulikuwa unamletea matatizo labda.......akiwa naibu waziri wa nishati mwaka 1990..ndipo alipopandishwa cheo jeshini na kuwa LT.COLONEL....that was obvious kwa kuwa tayari alikuwa na influence ...lakini hakupanda akiwa kwenye active fire.....bali ilikuwa kisiasa zaidi....mwaka 1992 wakati siasa ilivyoondolewa jeshini LT.COL kikwete aliamua kwa hiari kustaaafu jeshi!

Mkuu umenena vema, na pia ikumbukwe kuwa Mwinyi hakumpa kazi JK moja kwa moja, alimwambia aende kwanza kwa Mwalimu akamuombe msamaha kwa kuanzisha fagio la chuma amabalo pamoja na mambo mengine lilikuwa na lengo la kumuondoa mzee Kawawa kwenye chama eti ni mmoja kati ya viongozo mzigo. JK alienda kwa Mwalimu kumuomba msamaha, mwalimu alimsamehe lakini baada ya kumtukana sana sana!! kwamba" wewe ninani hata usema kawawa hafai!? kijana mnafiki sana wewe habari zako zote ninazo. nani wewe ! Mwalimu alifoka mno nasikia ..........lakini Mwinyi alimtahadharisha mapema kwama akikufokea wewe kakae kimya tu...na kuendelea kuomba msamaha....
Kweli Mwalimu alimsamehe JK akapata kazi......lakini nadhani wenyewe mnaona tabia yake ilivyo.....
 
Sio hayo tu kafanya mengi sana hata kupora mademu wa rafiki zake enzi hizo kwa mzee mmoja maaeneo ya meada pub sinza..
 
Ngoja nikamtishie Mkwere kidogo ikulu, najua ni muoga atakimbia kama alivyo awahi kwao Msoga kwa mguu na kumuachia kiti cha uraisi anayestahili, Dk Slaa.
 
mkwere fitna si utani!!! kosa kubwa ni kwamba watanzania tumekuwa hatutumii historia kujifunza...kumwingiza jk ikulu for two consecutive terms ni maafa!
 
Hivi kwa nini JK hakushitakiwa kwa kosa la AWOL (Absent without Official Leave) kwa mujibu wa juzuu za JWTZ?

Juzuu za jwtz hazina kipengele cha kufungua mashtaka kwa kosa la AWOL huwezi kumshtaki mtu ambaye hujui yupo wapi. Je kama amekufa mahali mkahesabiana na kukuta hayupo? Kinachofanyika ni kwamba mtu asipoonekana kambini kwa muda wa miezi 3 baada ya juhudi zote za kumtafuta ikiwemo kuwasiliana na mrithi wake kushindikana, inaundwa bodi ya inquiry na inahitimisha AWOL na kumfuta kwenye nguvu ya kikosi na jeshi. Tena kuacha au kutoroka jeshi sio gross misconduct kama alivyosema mtu mmoja ni kama vile kupoteza askari au ofisa vitani tu. Kinachoangaliwa ni kwamba anafanya nini baada ya kuacha jeshi asije akaingia kwenye vikundi vya uasi tu!

So kwa hili inawezekana kbs ukaondoka kwa AWOL na ukafanya kazi nyingine au ukaapply kazi nyingine kama utaweza kupita kwenye vetting system inayohusika. Kama system haiangalii background au iko corrupted atapata tu nafasi yoyote
 
Kighoma Malima alikufa kwa mshituko baada ya kuwapa misamaha ya kodi wahindi lukuki wakimuahidi kuwa fedha wamemuwekea ulaya , kwenda kucheki account ya VIJISENTI vyake akakuta hakuna kitu; basi mzaramo alikuwa amefuatana na mwali wake ikabidi AFE!!
Mkuu una ushaidi na hilo?let the man rest in peace Dude......Uwezi kupata umaarufu kwa kutoa a cheap crap like this.....Think Big Buddy!
 
Ni kweli niliwahi kuadithiwa na General Mmoja Mstaafu kwa sasa ,wakati wa kampeni za "urahisi"mwaka 2005
 
alikuwa luteni kanali alipotoka monduli na hakupanda tena mpaka leo ni luteni kanali...cheo above next kwa meja

kikwete ameondoka monduli akiwa major....na hata alipoteuliwa ubunge wa taifa na uwaziri mara ya kwanza alikuwa ni major.....huo u lt col. Alipata mwaka 90/91 ..kabla tu ya mfumo wa vyama vingi kuanza....mwaka 92..alipostaafu rasmi jeshini
 
Mkuu umenena vema, na pia ikumbukwe kuwa Mwinyi hakumpa kazi JK moja kwa moja, alimwambia aende kwanza kwa Mwalimu akamuombe msamaha kwa kuanzisha fagio la chuma amabalo pamoja na mambo mengine lilikuwa na lengo la kumuondoa mzee Kawawa kwenye chama eti ni mmoja kati ya viongozo mzigo. JK alienda kwa Mwalimu kumuomba msamaha, mwalimu alimsamehe lakini baada ya kumtukana sana sana!! kwamba" wewe ninani hata usema kawawa hafai!? kijana mnafiki sana wewe habari zako zote ninazo. nani wewe ! Mwalimu alifoka mno nasikia ..........lakini Mwinyi alimtahadharisha mapema kwama akikufokea wewe kakae kimya tu...na kuendelea kuomba msamaha....
Kweli Mwalimu alimsamehe JK akapata kazi......lakini nadhani wenyewe mnaona tabia yake ilivyo.....

Aisee!
Kama hizi habari ni za kweli basi JF ni kiboko! Nimebaki mdomo wazi jinsi watu walivyo na details
 
Kweli kwenye jamii forum kuna watoto, wafitini, mabinafsi na mabeberu ya kisasa. Yaani mtu alikua anapinga utumwa nyie mnasema mfitini? kama mnachuki binafsi msilete humu, siasa haina urafuki wala undugu kwa sasa mnaweka chuki against JK but kumbuka atakuja Mbowe au Slaa vizuri tu siku akimess up wote mtamchukia binafsi and this is what is happening in Libya.

Tuwe makini sana na tunapotoa comments zetu na tusilete story za vijiweni humu JF. Nikukumbushe tu kuwa JK alimaliza mafunzo yake vyema kabisa (alihitimu). Pia kumbuka kwa kipindi kile shimbo hakuwa Monduli fuatilia vizuri historia ya shimbo, na unapomuita Pimbi maana yake unajiita mwenyewe pimbi mdogo. Kimbuka wakati ule ilikua ukitoka nnje ya kambi ukiacha walinzi wa kambi kulikua na wanyama wakali kama simba na chui katika pori linalozunguka kambi hiyo hata leo kuna ushahidi wa kutosha kuhusu hilo.
je wakati huo wamasai walikuwa wakiishi wapi?mbona hawakuliwa wakaisha?umakini wako uko wapi?ukweli JK ni mwongo na mnafiki ndio maana anadai haijui Dowans mbele ya umma, nyuma ya pazia anaruhusu ilipwe mabilioni
 
Inamaana alitoka Jeshini?na ni kwa nini Julius ambae alikua Amiri Jeshi Mkuu ampekazi nyuingine?tunaomba maelezo ilikuaje akapewa kazi nyingine?
 
Mimi nadhani kwa hali ya wakati ule si ajabu alikuwa sahihi.Sometimes maisha yanahitaji kujipendekeza ili utoke ukikalia ukimya ndo hayo mwenzio rais sasa.Nyerere mwenyewe hiyo ndo ilikuwa sera yake kwani unadhani utaifishaji ulifanywa kwa msingi gani? Angalia viongozi matajiri wanavyotunyasanyasa sasa hivi ukisema una njaa wanakushangaa
 
So mkwere licha ya kuhudhuria mafunzo ya kijeshi monduli hakuwahi kumaliza na kuwa-commissioned Officer?? Huenda ndio maana amekuwa legelege haiwezekani eti Kanali wa jeshi akawa kama mkwere hata sauti tu haionyeshi kama alikuwa mwanajeshi......Kweli Tanzania tumekula hasara sio mchezo.
 
Kipindi hicho mkuu wa chuo alikuwa Gideon Sayore, Kikwete alikuwa ni mmoja wakufunzi wa siasa chuoni hapo.

Sasa ilikuwa hivi,
Mzee Sayore alikuwa anafuga ng'ombewengi pamoja kufanya shughuli za kilimo kwawingi wakati huohuo akiwa mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli.

Hivyo basi baada ya kuona ng'ombe wanatoa maziwamengi mno na mazao yametapakaa mashambani,. akaamua kuwa awe analiuzia jeshi mazao kama vile maharage na mahindi pamoja na maziwa na nyama kutoka kwenye mifugo yake.......na pesa anachukua yeye mwenye mazo.

Aliendelea kufanya hivyokwa kipindi kirefu tu.. ikiwa ni kama sehemu yake ya maisha....

Sasa bwana ,,kumbe Kikwette (JK) ilikuwa inamuuma sana sana, yaani mno! sasa haieleweki kama ilikuwa kweli ni kwa uzalendo ua wivu tu....akaandika barua kwa raisi kipindi hicho JK Nyerere.

Katika barua hiyo akaandika lawama nyiingi mno na majungu mengi sana dhidi ya Sayore, akimwita bepari, bwenyenye, mnyonyaji n.k huku akisema hafai kuwa mkuu wachuo hicho kwakuwa navunja miiko ya uongozi na mambo mengine meengi (si mnamjua JK anavyojua kupiga fitna!)...

Basi bwana, akamalizia mwisho kwakujiandika jina lake na sahihi yake huku akijiita mzalendo kamili barua ikapostiwa ikiwa imeadresiwa kwa rais wa nchi wakati huo!......

Mwalimu, aliipata barua ile aliifungua akaisomaaaa kisha akapiga hesabu zake....sijui aliwaza nini mzee yule, akaihifadhi ile barua ikaa sana ofini kwake bila kuchukua uamuzi wowote.

Siku moja alipokuja mkuu wa majeshi wakati huo "General Mtukula" (David Musuguli) ofisini kwa Mwalimu eaisi kipindi hicho, mwalimu akampa ile barua kutoka kwa Kikwete "akisema hayo ni maMbo yenu kayamalizeni hukohuko".

Basi bwana ile barua Mkuu wa majeshi alikaa nayo muda hivi kwenye makabrasha yakee...., sasa siku mija alikuja Mkuu wa chuo cha kijeshi Monduli(Sayore) Dar es salaam kufanya shughuli za kikazi akaenda hadi ofisini kwa Mkuu wa majeshi.

Baada ya shughuli kwisha na Sayore akiwa anajiandaa kwenda Monduli Mkuu wa majeshi alimwita, akampa ile barua ya Kikwete aliyomwandikia rais!!....

Sayore akaisoomaaa we akashangaa mno!! na akafura kwa hasira yule mmasai...., akuliza mwalimu kasemaje? Akaambiwa mwalimu kasema yamalizeni wenyewe!!.... Akasema naam, na akaondoka na ile barua hadi Monduli...

Alipofika tu yule mmasai aliitisha kikao cha wakufunzi wote na wakuu wengine pale chuoni, wakati wanajikusanya kwenda kwenye chumba cha mkutano yeye aliamua kwenda kutoa copy ile barua ya Kikwete, kopi nyingi idadi sawa na wajumbe wa mkutano ule....

Alipoingia mkutanoni akawaona wakuu na wakufunzi wote wameketi wakimsubiri wajue alicho waitia,.. akaanza kwa kuwauliza..jamani kama kuna mtu ana matatizo, au anaona kuna jambo haliendi sawa anyooshe mkono na saemekinacho mkereketa......watu wote wakawa kimya huku wengine wakisema hamna mkuu akiwemo Kikwette!!!

Basi bwana, tumalizie mkasa huu wa mkwere...

Sayore akaanza kuwagawia zile nakala (copies) za ile barua ya Kikwete kwenda kwa rais akawagawia wooote including Kikwete!!! Huku yule mmasasi Sayore akiwa amefura kwa hasira, macho mekunduuu! Akagonga ngumi juu ya meza kwa hasira na kusema someni hiyo barua!! kisha akatoka na kusema anakuja muda si mrefu...

Hapo Kikwete akajua kifo chake kimefika, akikumbuka macho ya yuile mmasai! akatetemeka macho yakamtoka lip! kwa woga!.. na wenzie wakamwanzishia zogo mle ndani......

Alichokifanya ni kuondoka haraka pale kikaoni wenzie wakajua bado yupo chuoni, kumbe safari ya Dar ikawa imeanza...!! Jamaa alitembea uchochoroni kwa muda mrefu sana huku akiogo kabisa kuingia barabara ya kuu...

Mashuhuda wanasema yule bwana akaja kupanda lift ya gari za vyama vya ushirika maeneo ya USA RIVER, hakukumbuka kubeba mzigo wowote!! Just imagine kutoka Monduli hadi hapo jamaa aliteseka sana... lakini yeye hakujali, cha muhimu ilikuwa kusalimisha maisha yake......

Basi huo ndiyo ukawa mwisho wa JK Monduli,........... hukurudi akaja Dar na kupangiwa kazi nyingine na chama... lakini alikuwa anamlaani sana Nyerere eti kwanini alimfanyia vile!!

Hicho ndicho chanzo cha JK kumchukia mwalimu na kugoma katakata kumwita baba wa taifa hadi leo! Yeye humwita mzee Nyrere tu au mwalimu baasi...na mara chache akiwa nje ya nchi humwita 'Father of our Nation', lakini ni pale anapotaka kupigiwa makofi kwa nukuu za Mwalimu....

**Ndugu zangu hiki ni kisa cha ukweli kwa 100%, inawezekana uandishi wangu ukawa na upungufu, lakini niemekipata kutoka watu mbalimbali waliowahi kuwa karibu sana na mkasa huu...
Hv ni kweli/? ndio maana ht uraisi alisema,bado!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom