Makanyaga
JF-Expert Member
- Sep 28, 2007
- 10,339
- 6,855
WOS,
Kama umeelewa somo, tunaambiwa kwamba JK alitoroka kwenye kikao baada ya Mkuu SAYORE kugawa barua(ya FITNA)) kwenye kikao akiacha wazitazame, na yeye (sayore)kutoka nje.
JK alitambua ambacho kingefuatia... hivyo aliamua kutoroka KWA KUPITA NJIA ZAKUJIFICHA!(hapo ndio kwenye ishu)..
Asingeweza kufuata barabara, maana alijua angeshikwa, kama wewe umeshawahi kufika Monduli, utaijua ile barabara ya kutoka Monduli kikosini hadi kuikamata barabara kuu ilivyonyooka, na hivyo asingewahi kuimaliza angeshikwa fasta, na option ya kupanda gari ndio usiongelee, maana asingeenda mbali, lakini pia magari ya kule yote yalikuwa ni ya kijeshi(hasa kwa enzi zile).
Chakufanya ilikuwa ni kukatiza kwa njia za porini...Zipo njia nyingi san kutoka Monduli kwenda mjini Arusha bila kufuata barabara!
Na tunaposema porini, si lazima iwe MSITU....NI NJIA YOYOTE ISIYOKUWA OFFICIAL, hivyo usitafute msitu hapo.
LAKINI UKUMBUKE PIA JK alikuwa Mwanajeshi, hivyo ujue alikuwa amehitimu masomo ya kijeshi kama MM(Mbinu za Medani etc), ambapo KUTEMBEA PORINI NI ISHU KAMA CHAI TU, na sehemu kubwa ya mafunzo inafanyikia huko...Hivyo hakuna sababu ya njia ZOZOTE kukutana, kama unavyotaka wewe iwe, wajeshi hawahitaji njia nyoofu!
Hivyo sioni uzito wa hoja yako ya kushangaa jiografia ya Arusha na kutembea Porini.
Unachekesha mno halafu una hoja sana. hufai!