Kikwete alivyomfunga mdomo Membe sakata la rada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete alivyomfunga mdomo Membe sakata la rada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PISTO LERO, Aug 8, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  • ALISEMA ANGEWATAJA WATUHUMIWA, RAIS AKASEMA HAKUNA USHAHIDI, WABUNGE WAPINGA MJADALA KUFUNGWA, WASEMA WAHUSIKA WAPO, WASHTAKIWE

  Waandishi Wetu, Dar na Dodoma | Mwananchi

  KAULI iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba hakuna ushahidi wa kuwashtaki watuhumiwa rushwa ya rada, inaonekana kumfunga mdomo Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye aliwahi kuahidi kwamba angewataja watuhumiwa hao.

  Rais Kikwete alipokutana na wakuu wa vyombo vya habari wiki iliyopita, alisema Serikali inashindwa kuwashtaki waliotuhumiwa katika suala hilo kutokana ukweli kwamba hata Uingereza walikana Kampuni ya BAE Systems kutoa rushwa na badala yake wakasema ilikosea katika kuandika hesabu zake.

  Wakati Rais Kikwete akisema hakuna ushahidi wa kuwashtaki watuhumiwa wa rushwa ya rada, tayari Membe alikuwa amesema watuhumiwa wapo, anawajua na aliahidi kwamba angewataja bungeni.

  Hata hivyo, Membe aliyewasilisha Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya wizara yake bungeni juzi, alishindwa kutekeleza ahadi yake licha ya kutakiwa kufanya hivyo na baadhi ya wabunge, wakiongozwa na Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Ezekia Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana (Chadema).

  Juzi, kabla Membe hajasoma hotuba yake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alitoa taarifa rasmi ya Serikali bungeni kuhusu suala hilo na alisema kuwa, hakuna mtuhumiwa wa rada anayeweza kupelekwa mahakamani na kutamka kwamba mjadala kuhusu suala hilo umefungwa rasmi.

  "Hata Uingereza iliyochunguza suala hilo imeeleza bayana kwamba hakuna rushwa na katika hatua hiyo, Serikali haiwezi kumfikisha mtu yeyote mahakamani," alisema Chikawe.

  Kauli hiyo ya Serikali inaonekana kuwakera baadhi ya wabunge ambao jana waliliambia gazeti hili kwamba wanashangazwa na jinsi Serikali ilivyomaliza na kufunga mjadala wa ufisadi wa rada, hali kukiwa na kila dalili kwamba wapo Watanzania waliohusika katika ufisadi huo.

  Kauli za wabunge
  Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema: "Ushahidi wa kwanza ni fedha zilizorejeshwa kwa sababu Watanzania walilipa zaidi. Kama kuna fedha zililipwa zaidi, iweje asipatikane mtu wa kuchukuliwa hatua. Tulivyoelezwa ni kuwa vyombo vya uchunguzi vilikuwa vinachunguza suala hili, sasa tunashangaa kuelezwa kuwa hakuna uchunguzi unaoendelea."

  Alihoji kama fedha zaidi ya Sh70 bilioni zililipwa zaidi, kwa nini waliohusika na uzembe huo wasichukuliwe hatua?

  Alisema kama fedha za nchi zimelipwa zaidi,
  inawezekana kulikuwa na ufisadi au uzembe na hayo yote yanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangala alisema kuwa, amefurahishwa na msimamo wa mawaziri katika suala hilo ingawa haamini kama ungekosekana ushahidi wa kumnasa aliyehusika.

  "Siamini kama ilishindikana kupata ushahidi, ninachokiona ni kwamba hakukuwa na juhudi za kuhakikisha unapatikana ushahidi na wahusika waliamua jambo hili liende kama lilivyo.

  Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema atamwandikia rasmi Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 46 ili waziri atakiwe kujibu kwa ukweli na kuacha kutetea ukiukwaji wa sheria.

  Alisema Waziri Chikawe alitoa taarifa potofu kuwa makubaliano yaliyoidhinishwa na Mahakama ya Uingereza Desemba 21, 2010 yanaifanya Serikali ya Tanzania ishindwe kuchukua hatua za kisheria dhidi ya ufisadi huo, akisema wakati ripoti ya Kamati ya Bunge la Uingereza ya
  Maendeleo ya Kimataifa kuhusu uchunguzi wa uhalifu wa fedha ya Novemba 14, 2011 ilisisitiza wahalifu wa ufisadi huo wachukuliwe hatua za kisheria.

  Pia alisema madai ya waziri huyo kuwa Serikali ya Uingereza haikuwa tayari kutoa ushahidi na ushirikiano, hayana ukweli kwa akirejea msimamo wa Serikali hiyo uliotolewa Agosti 6, 2012.

  Mbunge huyo alisema Waziri Chikawe hakujibu kikamilifu swali lake la jana asubuhi pale alipohoji kwa nini Serikali isichukue hatua za kisheria dhidi ya uzembe, matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu uchumi na kuisababishia hasara Serikali kama ilivyofanya kwa mawaziri na watendaji wa Serikali waliofikishwa mahakamani kuhusu tuhuma hizo.

  "Bila hata kupelekewa ushahidi wa rushwa anaodai waziri, mazingira ya mashtaka dhidi ya madai hayo na mengine ya ukiukwaji wa sheria yapo kwenye ripoti za Serikali yenyewe za nyakati mbalimbali," alisema.

  Mnyika alisema Serikali isipotangaza kuendelea na uchunguzi na kufungua mashtaka itabainika kuna ubaguzi katika uchukuaji wa hatua na mafisadi wakubwa wanalindwa.
  Kutokana na msimamo wa Serikali ya Uingereza, Mnyika alimtaka Rais Kikwete kurekebisha majibu yake aliyoyatoa kwa wahariri na kuagiza vyombo vya dola viendelee kuchukua hatua.


  Kauli ya JK Ikulu
  Utata kuhusu suala hilo ulianza kuibuliwa na Rais Kikwete aliposema Ikulu kwamba Serikali imeshindwa kuwafungulia watu mashtaka ya rada kutokana na kukosekana ushahidi ambao ulitarajiwa kutoka Uingereza.

  Alisema Serikali inashindwa kuwashtaki waliotuhumiwa katika suala hilo kutokana na mazingira yaliyojengwa nchini Uingereza yakionyesha kwamba Tanzania haiwezi kupata ushahidi wowote kuhusu suala hilo.

  "Sasa hapo sisi tunaanzia wapi, maana kwenye asili ya tukio hili, wanasema hakuna rushwa, kwa hiyo wanasheria wetu tukiwauliza nao wanahoji kwamba tunaanzia wapi katika suala hili," alisema Kikwete.

  Ahadi ya Membe
  Mara kwa mara Membe amenukuliwa akisema baada ya Serikali kupata chenji ya rada, lazima ijisafishe kwa kuhakikisha watuhumiwa wanafikishwa mahakamani. Membe alisema watuhumiwa wa rada wapo na lazima Serikali ijisafishe kwa kuhakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria.

  Juni mwaka huu, Membe alisema akiona kimya kinazidi kuhusu watuhumiwa wa rushwa katika kashfa ya rada, atawataja bungeni.

  Alinukuliwa akisema kila aliyehusika na biashara hiyo ya rada ametajwa na kuwekwa picha yake katika kitabu cha, ‘The Shadow World-Inside the Global Arms Trade,' kilichoandikwa na mwandishi wa Afrika Kusini, Andrew Feinstein.

  Alisema atawataja kwa sababu kimya chao tangu kutoka kwa kitabu hicho kinamaanisha kwamba wanahofia kukanusha.  Membe alisema kitabu hicho chenye kurasa 672, kina sura nzima inayozungumzia suala la rada akitaja kwamba, imeandikwa kwenye ukurasa wa 218 na 219.... "Ukienda ukurasa wa 285 utakuta wanaeleza namna fedha zilivyoibwa," alisema. Hata hivyo, juzi alishindwa kuwataja baada ya Waziri Chikawe kuzima suala hilo.


  Kutokana na msimamo wake huko, alijikuta katika shinikizo la kutakiwa kuwataja watuhumiwa hao juzi, wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka 2012/13.

  Wenje kwa upande wake, alisema kambi hiyo inaendelea kuhoji ni kwa nini mpaka sasa watuhumiwa wa kashfa hiyo wanaendelea kutembea vifua mbele bila kuchukuliwa hatua.

  Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rachel Mashishanga alimtaka Membe kuwataja watuhumiwa hao kwa kuwa amesema mara kwa mara kwamba anawajua... "Waziri Membe alipata kueleza anawafahamu watuhumiwa wa kashfa hiyo ni vyema akawataja ili jamii iwatambue." Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa naye alimtaka Membe kufanya hivyo kwa kuwataja watu waliohusika katika kashfa hiyo.

  Kashfa ya rada
  Kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa na Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Silaha ya BAE Systems ya Uingereza, ilianza mwaka 2000 na imekuwa ikiibuka mara kwa mara.

  Ilimfanya aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Clare Short wakati wa Serikali ya Waziri Mkuu Tony Blair, kujiuzulu akipinga Uingereza kuuzia nchi maskini kama Tanzania rada hiyo kwa bei kubwa.

  Kashfa hiyo kwa muda mrefu pia imekuwa ikitajwa kumhusisha aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge ambaye pia aliwahi kukutwa na kiasi cha Sh1.2 bilioni, kisiwani Jersey ambazo Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza, ilikuwa ikichunguza kama zilikuwa na uhusiano na biashara hiyo.

  Pia kuna kesi ya rada katika Mahakama ya Kisutu huku Polisi ikiendelea kumtafuta aliyekuwa dalali wa biashara hiyo, Sailesh Vithlan ambaye anatuhumiwa kushawishi na kuhonga baadhi ya maofisa wa juu na wanasiasa nchini ili wanunue rada hiyo.

  Hata hivyo, tayari Serikali imekwishapokea Pauni 29 milioni za malipo ya fidia kwa Serikali ya Tanzania na imekubaliwa kwamba fedha hizo zitatumika kununua vitabu na madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.
   
 2. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Another DHAIFU episode!! Hakuna ushahidi wa RADA ila kuna ushahidi kwa kesi ya akina Mramba na Yona...

  Kazi ya polisi ni kutafuta ushahidi kama unavyotafutwa kwa aliyemteka dr Uli

  Kweli DhAIFU ni janga la kitaifa na
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Aug 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Alimfunga mdomo kwasababu na yeye ni mtuhumiwa, nadhani angetajwa na yeye pia
   
 4. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  si watajeni kama mnawajua?
   
 5. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  You can do better than that !
   
 6. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  unachosha watu ndugu
   
 7. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna baadhi yetu tumetokea kutowa maneno zidi ya kauli ya Rais alipozungumzia masuala ya Rada na kusema:

  'Serikali inashindwa kuwashtaki waliotuhumiwa katika suala hilo kutokana ukweli kwamba hata Uingereza walikana Kampuni ya BAE Systems kutoa rushwa na badala yake wakasema ilikosea katika kuandika hesabu zake.'

  Tanzania imebarikiwa, kubarikiwa kwa nchi maana yake wananchi wafaidike na hiyo baraka iliyokuwepo au iliyokuwemo ,tuangalie malala miko ya wa Tanzania utasikia kauli inayosema wageni wanakuja hapa na kuchukuwa mali za nchi yetu ,huku sie wenywe tunakufa na umasikini, tusiwalaumu wageni kabla ya kujiangalia sisi wenywe wapi tunafanya makosa pia umasikini uliokuwapo ukiwa wa nchi au mtu au watu ni sisi wenye ,hivi wangapi kati yetu tunajinasibu sie ni WAZALENDO?

  Leo unapewa nafasi katika serekali au shirika lolote lile au wazifa wowote ule halafu unashidwa kuitumia nafasi hiyo? tunabaki kujipachika majina na kujiita Wazalendo,tunashindwa hata kuangalia wazalendo wa kweli wanavyotumia madaraka na mali ya nchi tunayojinasibia kuwa ni yetu soteumewahi kujiuliza katika wakati wowote ule inakuwaje wachache ndio wenye kula matunda ya uzalendo?

  Maneno ya Rais yanalenga pande mbili ya kwanza hao waliokwisha kula hiyo chenji ndio wamesha pita kwa maana nyingine yamesha kwisha hayo ,jee umejiuliza mara ngapi matokeo yenye mfano wa hili la rada yamekuwa yakitokea na mwisho wake humalizikia vipi?

  Upande wa pili ni kutuamsha mie na wewe tuliolala kimawazo usingizi wa fofofo (kifo) na saha zangu kwa wanao jiita wazalendo endelea kujita wazalendo lakini kumbuka kama umebahatika au ije itokee umebahatika kupewa nafasi usije ukafanya makosa na kushindwa kuitumia nafasi hiyo kama wanavyoitumia viongozi wetu au walivyoitumia wanunuzi wa rada au wanaosaini mikataba ya nchi utakuja kujuta siku za mbele.
   
 8. m

  malaka JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  We wa wapi?
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Watajwe mara ngapi? na ushahidi uko wazi kabisa hata kichaa anajua...anachoongopa Kikwete ni kwasasababu na yeye yumo, ndiyo maana Chenge alisema kwa kiburi kabisa kuwa nalizo nazo yeye ni vijisenti tu...
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Jamani watanzania mbona tunarudishana kulekule?? ifike sehemu tuwe tunajiridhisha tu, hatuwezi tukasubiri eti Mr. DHAIFU awataje watu ambao tayari keshawapa na vyeo tena vikubwa. Ukweli ni kwamba hawa watu walishakubaliana kulindana LIWALO NA LIWE. cha kufanya hapa tujipangeni kuwapiga chini 2015 au kabla ya hapo halafu tuwapeleke kortini. watatajana tu. hii staili ya kumuuliza mwizi kama ameiba huku unamchekea unategemea atakubali kweli?? NASHAURI TUTUMIE NGUVU NYINGI KUWAPA WATU ELIMU YA URAIA WAJUE WANAVYONYONYWA RASILIMALI ZA TAIFA LAO NA HAWA WAKOLONI WEUSI. WATAKAPOELEWA ITAKUWA RAHISI KUWAONDOA MADARAKANI NA KUWAFIKISHA KORTINI.
   
 11. M

  Maseto JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Wadau,
  Katika hali isiyo ya kawaida gazeti la serikali "Daily News' la tarehe 8.8.2012 limeandika kuwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania amethibisha kuwa makubaliano kati ya SFO na BAE ya kutokuwashitaki waliohusika na ufisadi wa kuuziana rada ya Tanzania hayafungi nchi nyingine yoyote ile.Balozi huyu aliongeza kuwa Tanzania inaweza kufanya uchunguzi kama kawaida na wao (Uingireza) watatoa ushirikiano.
  Si kawaida kwa gazeti hili kuandika taarifa inayoenda kinyume na msimamo wa serikali.
  Kwa sababu ya ushamba wangu nimeshindwa kukopi taarifa hiyo kama ilivyo na kuiweka hapa.Naomba msaada.

  SASA SERILKALI IACHE VISINGIZIO,IANZE KAZI YA KUWAWAJIBISHA AKINA CHENGE
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu Maseto hii ni nchi mkuu wa nchi anasema hivi waziri wake anasema hivi katibu mkuu nae anasema hivi
  hakuna mwenye uhakika habari ipi ni sahihi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nipe hilo gazeti nikusaidie!
   
 14. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Maseto

  Ulikishindwa hiki hapa!

  BAE radar scandal culprits face prosecution  THE government can still investigate corruption allegations in the controversial sale of radar to Tanzania by a British arms company - BAE Systems over a decade ago.

  The British High Commission in Tanzania clarified yesterday that the agreement between the UK's Serious Fraud Office (SFO) and BAE regarding the radar is not binding on any other state and therefore does not preclude investigations in Tanzania that could lead to prosecutions. The SFO and BAE reached a deal two years ago for the latter to effect 30 million pound sterling payment to settle a bribery investigation by SFO, for failure to keep proper accounting records of the radar sale.

  "The British government has always made clear that we would cooperate with the Tanzanian authorities in their investigation and prosecution of possible offences under Tanzanian law in relation to the BAE radar issue", the High Commission said in a statement posted on its website. The statement added that report of the IDC (UK parliament's International Development Committee) enquiry into Financial Crime and Development (November 15, 2011) welcomed "the Government of Tanzania's plans to bring individuals before the courts."

  The IDC also noted that it "is essential that all those involved in financial crime are dealt with appropriately." It reaffirmed the British Government's commitment to work alongside the government of Tanzania in tackling corruption. Meanwhile, Justice and Constitutional Affairs Minister, Mattias Chikawe has reiterated that anyone with credible evidence anywhere in the world to assist government prosecute local culprits of the overpriced BAE Systems radar purchase over a decade ago, should come forward.

  Mr Chikawe said while responding to Ubungo lawmaker, John Mnyika's argument that it's untrue that a British court ruled that after payment of over 70bn/- penalty, no one from the company can be prosecuted.

  "We can still prosecute these people locally and it's untrue that the British judge gave anyone immunity after payment of the penalty," Mr Mnyika argued as lawmakers questioned the sincerity of the government's commitment to fight high level graft while some culprits of the radar deal are holding positions of authority in Parliament.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  dawa ni kuipiga chini hii serikali dhaifu, halafu ndo tuwapeleke kortini hawa wezi. kwa sasa itakuwa ngumu maana wao ndo wanatoa amri. wakitoka madarakani hakyanani tutawageuza tunavyotaka kwa mujibu wa sheria. tusitunishe sana mishipa ya shingo kwa sasa kwani watendelea tu kutu-enjoy.
   
 16. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Akili yako imefikia hapo hivyo siyo ajabu
   
 17. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  rada ilkua wakati wa mkapa...nani waziri wa fedha anajulikana, nani waziri mkuu aliyetetea ununuzi kwa nguvu anajulikana ......nani alikua waziri wa sheria na mwanasheria mkuu wote wanajulikana ....sasa membe yana mnataka amtaje nani? mambo mengine uzushi...
   
 18. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,946
  Likes Received: 1,505
  Trophy Points: 280
  Kwanza pia watajwe wale nguli waliowekewa vijisenti vya rushwa kule kwenye benki Uswisi mbona tunataka issu isahaulike Kikwete aseme bana au nako hakuna ushahidi
   
 19. MKANKULE

  MKANKULE JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 422
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  hicho kitu ndugu yangu kisashau kabisa kwenye serikali dhaifu,labda waanze kuchunguzwa baada ya kikwete kuondoka madarakani.tuwe na subira bado miaka 2 na ushee tu wataanza kuchunguzwa.
   
 20. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2012
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Napenda nikuongezee kwamba kama ni Serikali ya CCM itakayoendelea kuwa madarakani sahau kabisa hiyo habari (kwenye nyekundu). Utamaduni wa ulaji na kulindana haukuanzia kwa Kikwete na hautaishia kwake kama CCM (ambayo ni chombo dhahiri kabisa cha wizi mkubwa wa kimfumo/kiserikali) itaendelea kutawala. Kinachowaunganisha ndani ya chama hicho ni fursa tu za kuhomola; Sumaye alijisahau kidogo akatoa siri hiyo huko nyuma. Usibabaishwe na kesi za akina Mramba na Mahalu. Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Weak point wanaodandia gari hilo kwa mbele kama akina Maranda na akina Liyumba ndio wa kutolewa kafara uzito ukizidi.
   
Loading...