Kikwete aliuwezaje huu usanii wa "hata mi mwenyewe ndo nalisikia saa hizi"?

chapwa24

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
1,115
2,000
Enzi za JK kulikuwa kunaibuka Agenda tata sana mwenyewe anasafiri zake kama mwezi watu wanaongea wanapambana wao kwa wao kila mtu anakuwa na mtizamo wake. Siku anarejea waandishi kibao airport wanamuuliza Mh hili suala vipi anawajibu hata mwenyewe ndo nalisikia saa hii

Dah nimemkumbuka Mzee Jakaya sometime alikuwa anaepusha shari kwa usanii tu, kumbe anawachora tu . Sisi wengine kinatushinda nini tukisemwa na kukosolewa tunachukia kabisa na kuamua kupotezana kabisa.
mzee alikuwa na uwezo sana kustahimili mikiki
 

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
2,862
2,000
Mwanamke hajawahi kujiamini hata siku moja, Ukimpinga anadhañi ni kwa sababu ya jinsia yake.mama yenu hajiamini na ni kilaza
Angekua hajiamini na kilaza kwa hizi kelele zenu za week nzima angeshaamrisha Abubakar aachiwe, kapiga zake kimya anaendelea na mishe zake za kuwatumikia waTZ, nyie tukaneni hadi mchoke, Abubakar sasa yupo Segerea na anaweza kula 30yrs or maisha kabisa. Endeleeni na matusi yenu, hayana impact yeyote kwake na kwa wananchi
 

kajekudya

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
1,551
2,000
JK Kiongozi anyejiamini

Waliomfuata baada yake wako very insecure

Mmoja akaamuru Lissu amiminiwe risasi auawe

Mwingine kampa Mbowe kesi ya Ugaidi

Yaani wanatumia miguvu miiingi badala ya kujibu hoja kwa hoja
Asanteni Sana. Comment zenu ziwe fupi fupi hivi hivi ila mwishoni muwe mnaongeza tule tuneno JK ni dhaifu na nchi ipo OutoPilot.
Mstuone hatuna kumbukumbu enyi wanaserengeti.
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,259
2,000
Enzi za JK kulikuwa kunaibuka Agenda tata sana mwenyewe anasafiri zake kama mwezi watu wanaongea wanapambana wao kwa wao kila mtu anakuwa na mtizamo wake. Siku anarejea waandishi kibao airport wanamuuliza Mh hili suala vipi anawajibu hata mwenyewe ndo nalisikia saa hii

Dah nimemkumbuka Mzee Jakaya sometime alikuwa anaepusha shari kwa usanii tu, kumbe anawachora tu . Sisi wengine kinatushinda nini tukisemwa na kukosolewa tunachukia kabisa na kuamua kupotezana kabisa.
Hivyi yule Ulimboka aling'olewa meno,kucha,kwenye utawala gani?
Hivyi Mwakyembe alinyonyoka nywele enzi zipi?
Vipi Mwangosi ilikuwa utawala wa Jiwe?
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,471
2,000
Swali gumu kwa Kikwete: FEDHA ZA ESCROW NI MALI YA SERIKALI AU SINGASINGA NA RUGEMALILA? hatoweza kujibu hadi anaingia kaburini.
Mbona alijibu kuwa si fedha za serikali.
Za mdau anayepaswa kulipwa na TANESCO.
Alisema kimsingi zile pesa serikali(TANESCO) ililipa mapema wakati wakisubiria mahakama iseme nani anastahili kulipwa kutokana na kazi au huduma iliyofanyika tayari.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,984
2,000
Sasa kwanini Ruge na Singasinga wakamatwe?
Wakati wewe unashangaa kukamatwa, mimi nashangaa ushahidi kutokamilika wakati zimeshapita takribani Siku 1470 tangu wafikishwe mahakamani!!

Yaani kesi ya kiofisi, inayohusisha pesa zilizokuwa benki kuu... pesa ambazo katu haziwezi kutoka bila nyaraka lakini zikiwa zimepita zaidi ya siku 1450 bado wanatuambia uchunguzi hujakamilika!!!
 

Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
6,135
2,000
Unaikumbuka ile ya Escrow, nchi nzima inamsubiri Rais atoke kwenye matibabu ya tezi dume Marekani ili atoe neno lake..

Akafika Airport akaongea kuhusu ugonjwa wake ulivyoanza, alivyoiaga familia yake, alivyopokelewa na kutibiwa Marekani, kisha akaaga na kuelekea Ikulu, hakutaja neno Escrow hata mara moja..
Angetaja kivipi wakati yeye ndiye angekuwa mhusika mkuu?
 

mambio

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,363
2,000
JK Kiongozi anyejiamini

Waliomfuata baada yake wako very insecure

Mmoja akaamuru Lissu amiminiwe risasi auawe

Mwingine kampa Mbowe kesi ya Ugaidi

Yaani wanatumia miguvu miiingi badala ya kujibu hoja kwa hoja
Mwingine akaamua Dr Ulimboka ang'olewe meno, mwingine akaamua mwangosi apigwe bomu, mwingine tena akawavunja kina Dr Slaa mikono na Lipumba kishushiwa mkong'oto havy.
Yaan ni tafarani tu!
Kweli Mkwere ni mwanasiasa bora sanaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom