Kikwete aliuwezaje huu usanii wa "hata mi mwenyewe ndo nalisikia saa hizi"?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,106
2,000
Enzi za JK kulikuwa kunaibuka Agenda tata sana mwenyewe anasafiri zake kama mwezi watu wanaongea wanapambana wao kwa wao kila mtu anakuwa na mtizamo wake. Siku anarejea waandishi kibao airport wanamuuliza Mh hili suala vipi anawajibu hata mwenyewe ndo nalisikia saa hii

Dah nimemkumbuka Mzee Jakaya sometime alikuwa anaepusha shari kwa usanii tu, kumbe anawachora tu . Sisi wengine kinatushinda nini tukisemwa na kukosolewa tunachukia kabisa na kuamua kupotezana kabisa.
 

captain dunga

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
209
500
Unaikumbuka ile ya Escrow, nchi nzima inamsubiri Rais atoke kwenye matibabu ya tezi dume Marekani ili atoe neno lake..

Akafika Airport akaongea kuhusu ugonjwa wake ulivyoanza, alivyoiaga familia yake, alivyopokelewa na kutibiwa Marekani, kisha akaaga na kuelekea Ikulu, hakutaja neno Escrow hata mara moja..
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,119
2,000
Unaikumbuka ile ya Escrow, nchi nzima inamsubiri Rais atoke kwenye matibabu ya tezi dume Marekani ili atoe neno lake..

Akafika Airport akaongea kuhusu ugonjwa wake ulivyoanza, alivyoiaga familia yake, alivyopokelewa na kutibiwa Marekani, kisha akaaga na kuelekea Ikulu, hakutaja neno Escrow hata mara moja.
JK Kiongozi anyejiamini

Waliomfuata baada yake wako very insecure

Mmoja akaamuru Lissu amiminiwe risasi auawe

Mwingine kampa Mbowe kesi ya Ugaidi

Yaani wanatumia miguvu miiingi badala ya kujibu hoja kwa hoja
 

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,106
2,000
Unaikumbuka ile ya Escrow, nchi nzima inamsubiri Rais atoke kwenye matibabu ya tezi dume Marekani ili atoe neno lake..

Akafika Airport akaongea kuhusu ugonjwa wake ulivyoanza, alivyoiaga familia yake, alivyopokelewa na kutibiwa Marekani, kisha akaaga na kuelekea Ikulu, hakutaja neno Escrow hata mara moja..

Kwa nini
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
24,226
2,000
Kuna siku waandishi wa habari walimbana kwamba wananchi wanasema wewe Mzee wewe unasafiri safiri saana.. akachekaaaa akawaambia hivi nyie mshafuga mbwa? kawaida ya mbwa hutembea huko na huko walau akipata fupa apelete wakagawane na waanae ili siku ipite.

akawauliza tena swali lingine....kama hamna basi niacheni nikapumzike safari ilikuwa ndefu saana.

Huyo ndiye JK Mzee wa stress free.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
umesoma mpaka mwisho lakini?
kakwambia utajua wewe Gwajima gani. Kama ni Gwajima mvaa scarf ya bandera au Gwajima mchungaji.
Kwahiyo unataka kumaanisha Gwajima yule anaetembea kutegemeana na uelekeo wa upepo?!

Gwajima wote ni wa kupuuzwa tu!!!

And in fact, Wanasiasa wote, hususani kama Wanasiasa wenyewe ni wa Tanzania, na Wanasiasa wa Tanzania wenyewe hususani kama ni wa CCM, man, hao wote ni wa kupuuzwa tu!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom