Kikwete alipoteza nafasi nzuri ya kujijengea heshma!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete alipoteza nafasi nzuri ya kujijengea heshma!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Papa D, Nov 21, 2010.

 1. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Baada ya wabunge wa Chadema kususia hotuba ya JK, mheshimiwa wetu alikosa diplomasia rahisi ambayo ingewaweka CHADEMA mtegoni!! Ningekuwa mimi ndo JK siku hiyo ya tukio ningeongea kama ifuatavyo:-
  Ndugu zangu nimeshtushwa na baadhi ya wabunge kuondoka ukumbini kwani kuondoka kwao kumefanya wananchi wanaowawakilisha wasipate uwakilishi stahiki!! Mimi Kama Raisi wa Jamhuri ya TZ nisingependa kuona baadhi ya Raia wa nchi hii wakitengwa kwenye mijadala inayohusu masuala ya maisha yao kwa namna yeyote ile. Kwa kuwa Mimi ni Rais wa Watanzania wote nahitaji kutatua dukuduku la kila Mtanzania bila kujali Dini, itikadi, rangi wala kabila! Mh. Spika, kwa idhini yako ningependa waheshimiwa walioondoka wafikishiwe ujumbe kwamba, Napendekeza Wateue wawakilishi watatu hadi sita ili nikutane nao kwa ajili ya kufahamu kiini cha tatizo, tukizungumze, tupange mikakati ya kuboresha kisha kupata muafaka. Mh. Spika naamini unawafahamu walioondoka na uwakilishi wao.
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwani wao ni akina nani mpaka awaombe? kutokuwepo kwao kumepunguza nini kwenye hotuba yake? Hiyo ilikuwa ni ishara tosha kwa wapiga kura wao kuwa wabunge waliowachagua kwenda kuwawakilisha wamewasaliti.
  Eti hawamtambui rais!!!!!!!
  Hivi kweli chadema wangeshinda pangekalika hapa nchini?
  Ndo maana wamekazana tu kuwa waliibiwa kura lakini leteni basi matokeo yakweni kwani na nyinyi mna copy, hamtaki kuleta, mmekazana tu mmeibiwa. what shame is this? Aggghhhhh.
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  wala asiwaite kwani kipindi cha kampeni kilishaisha, Rais ni cheo chenye shughuli nyingi zinazoratibiwa, basi kama ni hivyo hata kwenye misafara yake angesimama akienda ikulu na kuuliza wapita njia wanamatatizo gani?
  Ametumia diplomasia kama unavyoiita tena ya juu mle ndani kuna watu wana vichwa mwezi wa Februari tarehe 8 utawasikia kwani hata na wale waliogoma kuhudhuria angewafuata kuwauliza mbona leo hamkuja kunisikiliza.
  Mwache atulie Bunge litaamua, kama Katiba mpya ndani ya siku 100 njia zipo na zinakuja sio ki-vile
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Nov 23, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Huyo jamaa hahitaji Heshima broda! Kikwete anakazi moja tu ya kuwanyonya watanzania kama kupe!
   
 5. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  JK hawezi kufikiria fasta hivo. Hapo mpaka akaulize mabosi wake afanye nini!
   
 6. M

  MOMO Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mkuu naomba kutofautiana nawe katika hili. Kufanya hivyo kwangu ingekuwa ni unafki wa hali ya juu kwani sababu iliyowafanya wabunge wa CHADEMA kuondoka ndani ya Bunge ilikuwa ni wazi.
   
Loading...