Kikwete aliposema "Sijawahi kuona mchapakazi kama Lowassa" alimaanisha nini?

Anaanza kumsafishaa ili akimtangaza kuwa wazirii watu washishangae ........maana ndilo sharti lake alilopewa ..lazima amsafishe kwa urais 2015...
 
Lowasa ana matatizo yake ya kuchakachua mahela ya wananchi fasta fasta, lakini ni mtendaji mzuri kuliko Pinda-Anagalia kipindi chake wakurugenzi wa halmashauri mbofumbofu walivyokuwa na wakati mgumu, sasa hivi jamaa wana kwiba bila aibu na maendeleo hakuna!
 
Pumbafu yake, na ufisadi wote alioufanya bado anaonekana kuwa mchapakazi? Kweli Ufisadi upo mwingi kwenye nchi yetu. Fisadi boss, fisadi mchapakazi
 
EL Hafai kuwa kiongozi na Mwalimu Nyerere alishawahi kulisema hili. Ananuka UFISADI mkubwa na kwa sasa yeye na RA ndio wanaoiongoza nchi kwa "remote".

EL alimwambia Sitta kwamba hatakuwa Speaker wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano na kweli hajawa. Na wamemweka Speaker wao watakayemwamlia cha Kufanya ndugu Anne Makinda. Wanafanya ufisadi wanapata pesa nyingi ambazo wanazitumia kuwamaliza WAPAMBANAJI WA UFISADI; huku wakimtumia Makamba kama kuwadi wao mkubwa.

EL anajua fika alichokuwa anawafanyia Ma-DC wakati akiwa waziri wa maji na umwagiliaji. Makamba ndiye kibaraka mkubwa wa Mafisadi papa wanaoyumbisha nchi.

Na chini ya Uongozi wa CCM nchi hii haiwezi kuondoa rushwa na ufisadi uliyokubuhu kwani kwa CCM ufisadi ndio namba one qualification ya kuwa kiongozi.
 
Lowasa ana matatizo yake ya kuchakachua mahela ya wananchi fasta fasta, lakini ni mtendaji mzuri kuliko Pinda-Anagalia kipindi chake wakurugenzi wa halmashauri mbofumbofu walivyokuwa na wakati mgumu, sasa hivi jamaa wana kwiba bila aibu na maendeleo hakuna!
mkuu nakuunga mkono unajua Pinda amekuwa kama msukule tuuu anapelekwapelekwa tuu! LOWASA ni mchapakazi mzuri ila WIZI! jizi kishenzi!
 
Nadhani bila mafisadi nchi hii haitakuwepo, hayo ndio mawazo ya watu wa rangi ya kijani, kwao rushwa ni mpaka kwa balozi wa nyumba kumi kumi.
 
jaman tujue kwamba kila mtu ana mazuri na mabaya yake na mtu afanyapo baya mzuri yote hufutika....bt tuangalie shilingi kwa pande zote jaman..
 
Mie nafikiri kuwa anaweka mazingira ya kumbeba1 Tusubiri tuone! Lojiki iko hivi:
Analiambia Bunge "Baraza la mawaziri litakuwa na wachapa kazi',
Anaendelea kuwaeleza wananchi: "Lowasa ni mchapakazi"
Kwa hiyo anataka kuueleza Ulimwengu, 'msishangae kumwona Lowassa kwenye baraza la mawaziri (licha ya kutolewa baruti miaka michache iliyopita"
 
nawezekana ni mchapa kazi illeee si unajua yeye na Jk walikuwa wakipigana vikumbo wanapotembelea wilaya zenye ma-DC kama yule aliyemteua hivi karibuni wanajuana kwa ''uchapa kazi" wao
 
Watu wa kanda ya ziwa ni mashahidi! Shinyanga na Kahama. Walipata maji kwa hisani ya EL na kama angelikuwa yungali uwazirini basi maji yangekuwa dom!!! Tusichojua ni alipata kiasi gani % :teeth: Kabisa akirudi kwenye uwaziri namuunga mkono
 
nawezekana ni mchapa kazi illeee si unajua yeye na Jk walikuwa wakipigana vikumbo wanapotembelea wilaya zenye ma-DC kama yule aliyemteua hivi karibuni wanajuana kwa ''uchapa kazi" wao

Duh! Hilo nalo nenoooo!
 
Lowasa ana matatizo yake ya kuchakachua mahela ya wananchi fasta fasta, lakini ni mtendaji mzuri kuliko Pinda-Anagalia kipindi chake wakurugenzi wa halmashauri mbofumbofu walivyokuwa na wakati mgumu, sasa hivi jamaa wana kwiba bila aibu na maendeleo hakuna!

Mimi nachojua Lowasa ni mbadhilifu na sikubaliani na comparison yako ya Lowasa na Pinda sababu sielewi ni namna gani umelinganisha utendaji wa watu hao wawili. Wakati wa Lowassa mfumo wa serikali za mitaa pamoja na Waziri wake alikuwa ule ule unaotumika wakati wa Pinda? Waziri husika alihusika vipi kwa utendaji mzuri au mbaya wa hizo halmashauri? Kama ni suala na chain of command, kwa maana ya kwamba Waziri Mkuu anawajibika kwa utendaji wa Waziri husika na Halmashauri husika, basi kwa misingi hiyo hiyo ya chain oa command Rais Kikwete abebe lawama. Kwa kifupi naona comparison uliyotumia ya Lowasa na Pinda kwa hii sababu ha Hamlashauri inaweza inaweza kuleta conclusions za haraka haraka ambazo zinaweza zisiwe na usahihi. Kumbuka kuna mambo mengine ambayo Pinda atakuwa ameyafanya vizuri kuliko Lowasa kwa hiyo kigezo kisiwe hizo Hamlashauri tu (ingawa kweli kama una ushahidi kama nilivyosema hapo juu, hiki kinaweza kuwa kigezo kimoja wapo vile vile). Uchapa kazi mzuri wa serikali unaenda na maamuzi mazuri ya public interest. Kama mtu anafanya maamuzi na kibadhirifu hata akilala kazini akifanya kazi haisaidii sababu huyo si mchapa kazi!!
 
Kuchapa kazi anachapa aswaaa huko kwao kwani kukoje?ye si mbunge bwana wa monduli au?
 
Back
Top Bottom