Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi siku 1 baada ya Luhanjo kuamua kumrudisha Jairo

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Kwa mujibu wa TBC taifa raisi Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi juu ya Jairo asubuhi ya tarehe 25 na baada ya kuisoma aliamuru Jairo asirudi kazini hadi yeye mwenyewe rais atakapoamua namna muafaka ya kufanya hivo.

Taarifa ya Ikulu inasisitiza kuwa rais hakushinikizwa na mtu yeyote kuamua Jairo asirudi kazini. Itakumbukwa kuwa Luhanjo alikutana na waandishi asubuhi ya tarehe 24 na kutangaza kumrudisha kazini.

Niishie hapo, tu maana nimepata kichefuchefu niliposikia habari hiyo. So ngoja nikatapike kwanza.
 
Kwa mujibu wa tbc taifa raisi Kikwete alipokea taarifa ya uchunguzi juu ya Jairo asubuhi ya tarehe 25 na baada ya kuisoma aliamuru Jairo asirudi kazini hadi yeye mwenyewe rais atakapoamua namna muafaka ya kufanya hivo. Taarifa ya ikulu inasisitiza kuwa rais hakushinikizwa na mtu yeyote kuamua Jairo asirudi kazini. Itakumbukwa kuwa Luhanjo alikutana na waandishi asubuhi ya tarehe 24 na kutangaza kumrudisha kazini. Niishie hapo, tu maana nimepata kichefuchefu niliposikia habari hiyo. So ngoja nikatapike kwanza.

Hawa jamaa wa Ikulu ni vilaza kweli kwani wanafikiria wananchi wa leo ndio wale wa mwaka 1961!! Hawa wa leo HAWADANGANYIKI!
 
Hakuna Kiongozi hapa hivi mkisema alipata Taarifa siku ya Trh 25 does men Rais huwa hajui lolote linaloendelea hapa Tanzania mpaka apelekewe loh hiyo ni hatari...hata bibi yangu ana miaka 80 alikua anajua na anaishi Kijijini kwetu sembuse Rais!!!
 
wapendwa,

hii ni rubish!! luhanjo hana ubavu wa kumsimammisha wala kumrudisha kazini Jairo wala katibu mkuu wa wizara nyingine yoyote bila ridhaa ya rais. Wasitudanganye hao, walikuwa na mawasiliano mazuri tu. Wamepima upepo ndio wakaamua watoke hivyo.

TZ tuna kazi kubwa sana katika uongozi wetu

Tusiache kuliombea taifa letu
 
Wanaanza kusafishana? Kama ni hivyo mbona JK hajamchukulia huyo Mbena mkabila hatua mahsusi?
 
TAARIFA YENYEWE NDIO HII




UNITEDREPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATEOF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
[h=4]Fax: 255-22-2113425[/h]
PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
[h=5][/h]




TAARIFAYA UFAFANUZI

Tarehe 21 Julai,mwaka huu, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi Bwana Phillemon Luhanjo,akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma,alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara yaNishatai na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzialiokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake.


Bwana Luhanjoalichukua hatua ya kumsimamisha Bw. Jairo kufuatia tuhuma zilizokuwazimeelekezwa dhidi yake na baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kuhusuMakadirio na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka2011/12 katika kikao cha Bunge kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2011.


Katika mjadalahuo, baadhi ya wabunge walihoji uhalali wa Wizara kuomba michango yafedha kutoka kwenye Taasisi zilizoko chini ya usimamizi wake ilikusaidia Bajeti ya Wizara hiyo kupita kwa urahisi.


Kufuatia hatuahiyo ya kumsimamisha kazi Bw. Jairo, Katibu Mkuu Kiongozi alimwombaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bwana LudovickUtouh kufanya ukaguzi maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhumahizo.


Tarehe 9 Agosti,mwaka huu, 2011, Bw. Utouh aliwasilisha Ripoti yake kwa Katibu MkuuKiongozi, na tarehe 23, Agosti, 2011, Katibu Mkuu Kiongoziakiambatana na Bw. Utouh alitangaza mbele ya waandishi wa habarimatokeo ya ukaguzi huo maalum na uchunguzi wa awali juu ya tuhumadhidi ya Bw. Jairo.


Katika Ripoti yakembele ya waandishi wa habari, Bw. Utouh alihitimisha:
"Ukaguzi maalum haukuthibitisha kuwepo kwa usahihi wa tuhumazilizotolewa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.David Kitundu Jairo."

Kufuatia Ripotihiyo ya Bw. Utouh, Katibu Mkuu Kiongozi naye aliwaambia waandishi wahabari:
"Matokeoya uchunguzi huo ni kwamba tuhuma zilizotolewa Bungeni tarehe 18Julai, 2011, hazikuweza kuthibitika. Kutokana na matokeo haya yauchunguzi wa awali, mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu, Nishati na Madini, Bwana David Kitundu Jairo, sitaweza kuendelea nahatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na Hati yaMashitaka kwa sababu Bwana David Kitundu Jairo, hajapatikana na kosala kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa Taarifa ya UkaguziMaalum."

Alihitimisha:"
Kufuatiamatokeo ya taarifa hii ya awali na kwa mamlaka niliyonayo kwa mujibuwa Sheria Na. 8 ya Utumishi Umma ya Mwaka 2002 na kanuni zake zaMwaka 2003, NINAAMURU BWANA DAVID KITUNDU JAIRO AREJEE KAZINI KUANZIASIKU YA JUMATANO, TAREHE 24 AGOSTI, 2011."

KURUGENZI YAMAWASILIANO YA RAIS, IKULU,inapenda kutoa ufafanuzi kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguziya CAG na uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu suala hilo asubuhi yatarehe 25 Agosti, 2011, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliamua kuwa Ndugu Jairo asirudikazini mpaka kwanza yeye Rais atapoamua namna gani ya kurudi kazini,lini na wapi.

Katibu MkuuKiongozi alifikisha uamuzi huo wa Rais kwa Ndugu David Jairo ambayemapema asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameripoti kazini. Ndugu Jairoalitii uamuzi huo wa Rais.


Tunapendakusisitiza kuwa Mheshimiwa Rais hawaja kigeugeu kwa sababu alifanyauamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu MkuuKiongozi. Na uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia sualahilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge.Pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamishaWaziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya tarehe 25, 2011.


Aidha, tunapendakufafanua zaidi kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ametimiza wajibu wakeipasavyo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Katibu Mkuu kwa mujibu waSheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Rais, kwaupande wake, ametumia madaraka yake kama Mamlaka ya Ajira ya KatibuMkuu. Hakuna suala la kujichanganya wala ukigeugeu ndani ya Serikali kuhusu suala hili.


Mwisho.

Imetolewana Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dares Salaam.
26Agosti, 2011
 
Rais wetu ni matatizo na janga km vile ukimwi, mafuriko, kukosa umeme etc. Ndiyo maan watu waishamzadharau siku nyingi nakumbuka alishatoa amri ya kuvunjwa uzio pale jangwani lakini hadi leo mabati yapo.

Walompotosha wanamng'ong'a.
 
Tunapendakusisitiza kuwa Mheshimiwa Rais hawaja kigeugeu kwa sababu alifanyauamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu MkuuKiongozi. Na uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia sualahilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge.Pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamishaWaziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya tarehe 25, 2011.
Aidha, tunapendakufafanua zaidi kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ametimiza wajibu wakeipasavyo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Katibu Mkuu kwa mujibu waSheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Rais, kwaupande wake, ametumia madaraka yake kama Mamlaka ya Ajira ya KatibuMkuu. Hakuna suala la kujichanganya wala ukigeugeu ndani ya Serikalikuhusu suala hili.


Ndg taarifa hii siyo sahii, siku ya kwanza Luhanjo alimrudisha kazini, siku ya pili Jairo akarejea kazini, na siku hiyo Mh Zitto akatoa hoja na kuboreshwa na Mh Olesendeka hili kuunda tume.

Siku ya tatu Rais kwa kupitia waziri mkuu akajibu swali la Mh Mbowe kuwa Jairo kasimamishwa, Je, kauli hipi imetangulia? Wabunge? Au Rais? Rais kapima kauli ya wabunge?

Swari langu Luhanjo akuwasiliana na Rais kabla ya kutoa taarifa hiyo?

USANII MPAKA LINI?
 
Kwa maelezo toka IKULU ni kuwa kila mteule wa Rais ni rais pale alipo na hivyo anaweza kufanya maamuzi yoyote pale alipo bila kumshirikisha mwenye nchi (rais). Hii inachefua zaidi ... Ndo maana tuna mafisadi kama kina EL, RA, AC na wengine ambao ndo wanaoendesha nchi hii na jamaa akila biscuit tu pale ikulu. Iliwahi kudokezwa na king of kings ... walijadili sasa wanapotezea ...



quote_icon.png
By King of Kings
UPDATES: 25/8/2011

Ikulu ya cheza picha la kihindi! Jana baada ya mkuu wa kaya kurudi magogoni kilikalika kikao na bwana Luhanjo akatoa taarifa ya kikao chake na akina Jairo na ikajadiliwa hali ya mambo bungeni!
Moja ya nilichokitafsiri ni kuwa Ikulu na Bungu wanatofautiana sana juu ya Jairo!
Maamuzi ya kikao cha usiku wa jana ni kuwa kwakuwa mda wa Luhanjo kustaafu ulishafika na mpaka leo yupo kwa hisani ya mkuu wa kaya basi walizuge taifa kuonyesha umma kuwa ikulu imesikitishwa na maamuzi ya Luhanjo hivyo imemtimua kazi!
Wazo hilo alilito Luhanjo mwenyewe, japo kikwete alisita kidogo lakini Luhanjo alifafanua jinzi mbinu hii itakavyo badili upepo na hali ya mambo itakuwa shwari ndipo mkuu wa kaya akakubali wazo hilo!

Spika wa bunge aliwasiliana na mkuu wa kaya mida ya saa nne na dk kumi na akamueleza dhamira ya bunge kuomba ushauri:
1. Nani awaweke katika kamati
2. Nini wakifanye hao wanakamati

Mkuu wa kaya akaomba kuwa ngoja atulize kichwa kwanza atatoa dokezo!!
Kikubwa msitegemee jipya kutoka ktk kamati hiyo kwakuwa inateuliwa na ikulu!
Last edited by Jason bourne; Today at 08:15 AM.​





 
Luhanjo alimsimamisha jairo au alimpa likizo?hii taarifa iliandikwa wakati wamechanganyikiwa na bado mtaandika sana taarifa za ovyoovyo mwaka huu!this is dotcom generation hatudanganyiki
 
Ata basic management principles zinawashinda?
Yaani your junior atoe maamuzi mazito kama ya kumrudisha Jairo wewe uliyemteua haujui?
Kweli ili ni janga kwa Taifa
 
TAARIFA YENYEWE NDIO HII

TAARIFAYA UFAFANUZI
Tunapendakusisitiza kuwa Mheshimiwa Rais hawaja kigeugeu kwa sababu alifanyauamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu MkuuKiongozi. Na uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia sualahilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge.Pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamishaWaziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya tarehe 25, 2011.
Aidha, tunapendakufafanua zaidi kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ametimiza wajibu wakeipasavyo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Katibu Mkuu kwa mujibu waSheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma. Mheshimiwa Rais, kwaupande wake, ametumia madaraka yake kama Mamlaka ya Ajira ya KatibuMkuu. Hakuna suala la kujichanganya wala ukigeugeu ndani ya Serikalikuhusu suala hili.
Mwisho.
Imetolewana Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
Dares Salaam.
26Agosti, 2011

Kawaida huwa siyo mwimbaji lakini taarifa hii naona imekoleza chorus ya KIGEUGEU, KIGEUGEU ... KIGEUGEU ...
Naomba mwenye clip atuwekee hapa ili tusherehekee maamuzi ya ikulu.
 
Back
Top Bottom