Kikwete alipitia dirishani, sasa kaamua kulifunga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete alipitia dirishani, sasa kaamua kulifunga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 11, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,818
  Trophy Points: 280
  Kikwete alipitia dirishani, sasa kaamua kulifunga?

  Mwandishi Maalum
  Raia Mwema
  Machi 10, 2010
  YANAWEZA kusemwa mengi kuhusu jitihada binafsi anazozifanya Rais Jakaya Kikwete kushupalia Sheria mpya ya Gharama za Uchaguzi. Sheria hii yaweza kupata saini yake ya kuiridhia wakati wowote wiki hii.

  Ni moja ya sheria atakayoiwekea saini; huku akichekelea moyoni jinsi alivyomudu kuwafunga midomo waliokuwa wakali kuikosoa bungeni, na hata kutishia kutopitisha muswada wake.

  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete

  Kutokana na mazoea mabaya yaliyozoeleka, wanasiasa wengi wanahoji kama kweli Rais Kikwete amedhamiria kukomesha rushwa ya uchaguzi au anazuga kama ambavyo amekuwa anafanya katika mambo mengi mengine.

  Wanaohoji hivyo wana sababu moja kubwa; nayo ni kwamba Rais Kikwete ni tunda la rushwa ya uchaguzi. Ni tunda la matumizi mabaya na makubwa ya uchaguzi. Iweje leo aone njia iliyomwingiza madarakani ni mbaya?

  Kwa misingi ya kawaida ya uchaguzi, Rais Kikwete asingeweza kushinda uchaguzi mwaka 2005. Milango ya kuingia Ikulu ilikuwa imefungwa kabisa! Hakuwa na fedha binafsi. Chama hakikuwa na fedha kwa ajili yake tu (walikuwa wagombea 11 wa CCM).

  Isitoshe, hakuwa na uzoefu wala rekodi iliyozidi wagombea wengine katika medani za utendaji. Timu yake ya kampeni ilisigina maadili na kanuni za CCM ili kumpitisha (vitisho, kashfa kwa wenzake, kufuru ya fedha, na hata ‘ugaidi’ mamboleo dhidi ya Mwenyekiti wa chama wa wakati ule).

  Habari zinasema Kamati ya Maadili na Nidhamu iliandaa taarifa dhidi ya Kikwete na watu wake, na kwa mujibu wa “Waraka wa Butiku”, taarifa hiyo ilipuuzwa ama kwa Mwenyekiti kuogopa vitisho vya mtandao au basi tu Mwenyekiti alitumia rungu lake. Wengine wanasema na kuamini kwamba kama taarifa hiyo ingesomwa, milango ya Ikulu ingefungwa kwa Kikwete.

  Sababu hizi zote na nyingine zisizofahamika, zaweza kuthibitisha ukweli kuwa milango ya kuingilia Ikulu kwa Kikwete ilikuwa imefungwa, lakini alifanikiwa kuingia kwa kupitia dirishani – dirisha (rushwa ya uchaguzi) lililokuwa limesahaulika kufungwa na walinzi!

  Kwa njia ya dirisha hilo, Kikwete akaingia Ikulu. Wanaohoji dhamira ya Kikwete katika kusukuma mbele sheria hii ya kudhibiti fedha chafu wakati wa uchaguzi, wanamwona Kikwete ana roho mbaya kwa sababu aliponea kwenye tundu la sindano kwa kupitishwa dirishani, lakini baada ya kuingia ndani ameamua kuziba lile dirisha ili wengine wasiingie.

  Kwa maana hiyo basi, chini ya utawala wa Kikwete, milango na madirisha imefungwa kwa wanasiasa wanaopenda kununua uongozi na kuimiliki demokrasia kwa kutumia nguvu ya fedha.

  Swali la msingi hapa ni kama Kikwete anayo nguvu ya dhamiri (moral authority) kusimamia sheria hii? Mashaka ni mengi kuliko matumaini.
  Kwa nini? Kwanza, Kikwete amechafuliwa sana na rushwa ya uchaguzi. Mwaka 1995 alipojaribu, kwa mara ya kwanza, kugombea nafasi ya urais, alitumia “jeuri ya fedha” ya rafiki yake Edward Lowassa, kukodisha ndege na kukusanya saini za wadhamini kwa muda mfupi sana kuliko wagombea wengine.

  Jeuri hiyo ya fedha aliipata wapi wakati hakuwa tajiri? Alikoipata, tunaweza kuona leo hii anavyogwaya mbele ya waliompa fedha! Pili, hana rekodi ya kusimamia mambo magumu katika maisha yake.
  Waswahili wanamwita “muungwana” kwa kutanabahisha kuwa hawezi kufanya mambo magumu yanayoumiza nafsi yake au rafiki zake. Wanaompenda, au tuseme wanaonufaikanaye, wanadai ana utu. Lakini utu huo ni wa ajabu; kwani unaacha raslimali za nchi ziliwe na wachache; huku mamilioni ya masikini wakiteketea kwa umasikini na kukosa haki zao za msingi.

  Tatu, Kikwete ameshuhudia chaguzi za jumuia za chama kuanzia wilaya, mikoa hadi taifa zikighubikwa na rushwa chafu mbele yake, na hata nyingine kusindikizwa na watoto wake! Hakufanya kitu. Alikaa kimya - dalili tosha kwamba rushwa katika chaguzi za chama si kitu kinachosumbua nafsi yake.

  Tumeona maamuzi yake binafsi; hasa pale alipojikuta watoa rushwa wawili maswahiba wake wakileta rufaa mbele yake, na yeye kuishia kugwaya na kuamua kuwapa nafasi nyingine za uongozi ili kuepusha mgogoro mkubwa ambao ungetokana na yeye kufanya maamuzi magumu.

  Kwa kifupi, inahitaji ujasiri wa pekee kulipiga teke titi lililokunyonyesha. Hivi sasa kamati yake kuu ya chama chake CCM, imejazwa wajumbe waliongia kwa kutumia nguvu ya fedha, na inatia shaka kama Kamati Kuu hii inaweza kusimamia sheria hii kwa uchaguzi wa ndani wa chama chake.

  Mmoja wa wajumbe hao wa Kamati Kuu ya CCM ameniambia, wakati naandika makala hii, kuwa: “Tulivyopita sisi kuingia Kamati Kuu, ndivyo alivyopita yeye kuingia Ikulu; itakuwa ajabu mwizi kumkamata mwizi mwenzie”.

  Usemi huu unanikumbusha usemi mwingine wa mkubwa mmoja nchini aliyesema: “JK hawezi kumdhalilisha aliyemwingiza Ikulu, akapona. Anatafuta laana?” Msemaji huyu aliyasema haya pale alipoulizwa ni nini kitatokea endapo Kikwete atatoa kibali cha kukamatwa watuhumiwa wa Kagoda Agriculture waliokwapua bilioni 40 ili kunusuru ushindi wa CCM mwaka 2005.

  Sheria ya kuthibiti fedha chafu katika chaguzi zetu inapokelewa kwa furaha na faraja kwa wapenda haki wote nchini. Hata hivyo, inapungukiwa na mambo makuu matatu, si katika maudhui yake, bali katika miundo mbinu yake.

  Kwanza, watekelezaji wake wanapungukiwa na uadilifu. Hili ni wazi kuwa, mkandamizaji wako wa jana hawezi kuwa mkombozi wako wa leo. CCM iliyoingia madarakani kwa rushwa haiwezi kuiondoa rushwa ikabaki madarakani.

  CCM inayoshikilia dola, haiwezi kuiruhusu dola kuikamata CCM pale itakapotaka kutekeleza kauli mbiu ya “CCM Itatawala Milele” kwa gharama zozote. Mifano iko wazi, na wa karibuni ni huu mnyukano kati ya Bunge na Serikali kuhusu kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea.

  Serikali inajua fika Dk. Hosea ana udhaifu kadhaa kiutendaji na wabunge wanataka aondolewe Takukuru, lakini haiwezi kamwe kumgusa na CCM ikapona maana, baba huyu anayo mafaili ya kila mmojawao ya wakati wa uchaguzi.

  Suluhisho la mnyukano huu halitakaa liwe zuri kwa Dk. Hosea mwenyewe; maana tuliwahi kuyaona ya aina hiyo huko nyuma.
  Kwa kifupi, unaweza kusema hivi: Sheria ya kudhibiti fedha chafu wakati wa uchaguzi ni nzuri, lakini watekelezaji ni “mashetani”.

  Pili, katika hali ambayo Mahakama, Bunge, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Takukuru, na Tume ya Uchaguzi vinakosa uhuru kamili katika kutekeleza majukumu yake, ni vigumu kuona ni jinsi gani sheria hii itafanya kazi.

  Hivi kweli inawezakana vyombo vikapitisha uamuzi unaomnyima mgombea wa CCM nafasi ya kugombea? Mbona mafaili ya Takukuru yanayowatuhumu wanasiasa wa CCM sharti yapelekwe kwanza Ikulu?

  Mbona mahakimu kabla hawajaamua hatima yao kwanza wawasiliane na wakuu wa wilaya? Mbona hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu mgombea binafsi inapigwa danadana na hakuna lolote?

  Katika nchi ambamo utawala wa sheria unafanya kazi, Mkuu wa Dola angewajibishwa kwa kuchelewesha hukumu ya namna hiyo! Mpaka hapa niseme, utekelezaji wa sheria yoyote hutegemea sana utashi na uhuru wa taasisi na vyombo vya dola vilivyotajwa katika sheria hiyo kuwa vitatekeleza sheria hiyo. Kwa Tanzania, hatunavyo, na vilivyopo, havina utashi wala uhuru.

  Tatu, demokrasia imefinywa hata ndani ya chama tawala. Mbinyo huu wa demokrasia ndani ya chama tawala hauwezi kuruhusu uwepo wa demokrasia nje ya chama hiki. Hivi sasa wakubwa wamenuniana na hawaambiani ukweli kuhusu uhuru walionao wana CCM kugombea nafasi ya urais mwaka huu.
  Mizengwe imewekwa kuzuia hilo. Atakayediriki kugombea amepewa wiki moja kutimiza masharti; huku Kikwete akiondolewa sharti hilo. Kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kumwezesha mgombea Kikwete apite bila kupingwa; huku akiwaacha wengine wakiwa wamenuna!
  Sababu inayotolewa ni eti huu ni “utaratibu na utamaduni wa ndani ya Chama”, lakini wanaosema hivyo, hawatoi maelezo ya kwa nini utaratibu wa kubadilishana kati ya Bara na Visiwani haufuatwi tena na hakuna anayeruhusiwa kuhoji.

  Ingekuwa bora kama Kikwete angeacha kipindi hiki cha pili kwa mgombea wa Visiwani ili kuonyesha nia njema ya kudumisha Muungano kwa kutumia “utaratibu na utamaduni wa ndani ya chama chetu”.

  Mwisho, ikiwa kweli Kikwete anayo nia njema ya kukomesha rushwa katika chaguzi za Tanzania, namshauri kwa nia njema afanye mawili ya msingi. Kwanza, akiri wazi na hadharani kuwa hata yeye ni tunda la rushwa katika chaguzi, na aeleze masikitiko yake kuhusu jambo hilo.
  Wote tunajua kuwa si yeye binafsi alifanya hivyo; bali ni mfumo batili uliokithiri ndani ya chama chake, na yeye binafsi hakuwa na ubavu wa kukataa mikakati hiyo. Hili litamsafisha na kumpa nguvu itoshayo kusimamia sheria hii mpya.

  Pili, kama mkuu wa nchi, atamke na kuwa tayari kumkataa mgombea yeyote wa CCM atayebainika kutumia fedha; hata kama kwa kufanya hivyo ushindi utaenda chama cha upinzani.

  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kufanya hivyo. Tangu yeye hatujaona mfano wake; kwamba linapofika suala la uadilifu, itikadi na ukereketwa wa chama, vinawekwa mbali. Basi JK atamke kuwa ni heri chama cha upinzani kichukue nafasi endapo mla rushwa wa CCM anaelekea kuchukua ushindi wa kununua.

  Litakuwa tamko la kimapinduzi na litafungua milango kwa waadilifu kuingia katika ofisi za umma. Hapatakuwapo tena haja ya watu kupitishwa madirishani. Tamko hili, litalizima lile lisemalo, “CCM bila rushwa haiwezekani”.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Imetulia hii!
   
 3. F

  Fataki Senior Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu, siyo kwamba kaamua kulifuga hilo dirisha, bali kuliondoa kabisa kwa kuweka matofali na zege.
   
 4. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kazi kwelikweli
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  aliyeko ndani hataki walio nje waingia kama alivyoingia yeye..
   
 6. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naam Raia mwema, koleo si kijiko kikubwa Kudos!
   
 7. d

  damn JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kuweka tofauli na zege? Mkuu, nina mashaka, huu unaweza kuwa usanii mwingine. Pengine kila atakayegombea ambaye hayuko katika kundi lake, ataonekana kuwa na pesa chafu, yawezekana kuna watu anataka kuwabana.

  Who knows inawezekana wenye uhusiano na MNF, na akina butiku, unaukumbuka ule mdahalo walivyoubeza wapambe wake?
   
 8. K

  Kabengwe JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 242
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwandishi amechambua vizuri na ninamuunga mkono kwa kusema sheria ya uchaguzi iliyopitishwa hivi karibuni ni nzuri sana kwa ustawi wa utawala bora hapa nchi.

  Kwa Rais kujitokeza mbele ya umma na kukiri kwamba aliingia madarakani kwa rushwa si jambo rahisi. Na sema hvyo kwasababu baada ya kutamka hvyo, kuna mambo mengi yatafuata na mengi yatakuwa ni ya kisheria ambapo inawezekana akahitajika kujiuzulu! Sidhani kama yupo tayari kwa hilo.

  Nadhani kwa Rais kuweza ku-implement vzr, inatakiwa hii sheria ianze kutumika kwenye uchaguzi wa NEC-CCM. Huo ndio utakuwa mwanzo mzuri pekee wa sheria hii kuwa na makali, coz ukishapata decision makers ambao wameingia madarakani kwa haki, huku chini wote watafuata! Ila hii ni kama Rais ana nia ya kweli kuhakikisha Utawala bora unaimarishwa nchi! Na waziri wa utawala bora anafaa kuwa Magufuli sio huyu tulie nae kwasasa!
   
 9. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kikwete alipitia dirishani,

  sasa kaamua kulifunga?

  Mwandishi Maalum​
  Machi 10, 2010 [​IMG]
  YANAWEZA kusemwa mengi kuhusu jitihada binafsi anazozifanya Rais Jakaya Kikwete kushupalia Sheria mpya ya Gharama za Uchaguzi. Sheria hii yaweza kupata saini yake ya kuiridhia wakati wowote wiki hii.
  Ni moja ya sheria atakayoiwekea saini; huku akichekelea moyoni jinsi alivyomudu kuwafunga midomo waliokuwa wakali kuikosoa bungeni, na hata kutishia kutopitisha muswada wake.
  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete
  Kutokana na mazoea mabaya yaliyozoeleka, wanasiasa wengi wanahoji kama kweli Rais Kikwete amedhamiria kukomesha rushwa ya uchaguzi au anazuga kama ambavyo amekuwa anafanya katika mambo mengi mengine.
  Wanaohoji hivyo wana sababu moja kubwa; nayo ni kwamba Rais Kikwete ni tunda la rushwa ya uchaguzi. Ni tunda la matumizi mabaya na makubwa ya uchaguzi. Iweje leo aone njia iliyomwingiza madarakani ni mbaya?
  Kwa misingi ya kawaida ya uchaguzi, Rais Kikwete asingeweza kushinda uchaguzi mwaka 2005. Milango ya kuingia Ikulu ilikuwa imefungwa kabisa! Hakuwa na fedha binafsi. Chama hakikuwa na fedha kwa ajili yake tu (walikuwa wagombea 11 wa CCM).
  Isitoshe, hakuwa na uzoefu wala rekodi iliyozidi wagombea wengine katika medani za utendaji. Timu yake ya kampeni ilisigina maadili na kanuni za CCM ili kumpitisha (vitisho, kashfa kwa wenzake, kufuru ya fedha, na hata ‘ugaidi’ mamboleo dhidi ya Mwenyekiti wa chama wa wakati ule).
  Habari zinasema Kamati ya Maadili na Nidhamu iliandaa taarifa dhidi ya Kikwete na watu wake, na kwa mujibu wa “Waraka wa Butiku”, taarifa hiyo ilipuuzwa ama kwa Mwenyekiti kuogopa vitisho vya mtandao au basi tu Mwenyekiti alitumia rungu lake. Wengine wanasema na kuamini kwamba kama taarifa hiyo ingesomwa, milango ya Ikulu ingefungwa kwa Kikwete.
  Sababu hizi zote na nyingine zisizofahamika, zaweza kuthibitisha ukweli kuwa milango ya kuingilia Ikulu kwa Kikwete ilikuwa imefungwa, lakini alifanikiwa kuingia kwa kupitia dirishani – dirisha (rushwa ya uchaguzi) lililokuwa limesahaulika kufungwa na walinzi!
  Kwa njia ya dirisha hilo, Kikwete akaingia Ikulu. Wanaohoji dhamira ya Kikwete katika kusukuma mbele sheria hii ya kudhibiti fedha chafu wakati wa uchaguzi, wanamwona Kikwete ana roho mbaya kwa sababu aliponea kwenye tundu la sindano kwa kupitishwa dirishani, lakini baada ya kuingia ndani ameamua kuziba lile dirisha ili wengine wasiingie.
  Kwa maana hiyo basi, chini ya utawala wa Kikwete, milango na madirisha imefungwa kwa wanasiasa wanaopenda kununua uongozi na kuimiliki demokrasia kwa kutumia nguvu ya fedha.
  Swali la msingi hapa ni kama Kikwete anayo nguvu ya dhamiri (moral authority) kusimamia sheria hii? Mashaka ni mengi kuliko matumaini.
  Kwa nini? Kwanza, Kikwete amechafuliwa sana na rushwa ya uchaguzi. Mwaka 1995 alipojaribu, kwa mara ya kwanza, kugombea nafasi ya urais, alitumia “jeuri ya fedha” ya rafiki yake Edward Lowassa, kukodisha ndege na kukusanya saini za wadhamini kwa muda mfupi sana kuliko wagombea wengine.
  Jeuri hiyo ya fedha aliipata wapi wakati hakuwa tajiri? Alikoipata, tunaweza kuona leo hii anavyogwaya mbele ya waliompa fedha! Pili, hana rekodi ya kusimamia mambo magumu katika maisha yake.
  Waswahili wanamwita “muungwana” kwa kutanabahisha kuwa hawezi kufanya mambo magumu yanayoumiza nafsi yake au rafiki zake. Wanaompenda, au tuseme wanaonufaikanaye, wanadai ana utu. Lakini utu huo ni wa ajabu; kwani unaacha raslimali za nchi ziliwe na wachache; huku mamilioni ya masikini wakiteketea kwa umasikini na kukosa haki zao za msingi.
  Tatu, Kikwete ameshuhudia chaguzi za jumuia za chama kuanzia wilaya, mikoa hadi taifa zikighubikwa na rushwa chafu mbele yake, na hata nyingine kusindikizwa na watoto wake! Hakufanya kitu. Alikaa kimya - dalili tosha kwamba rushwa katika chaguzi za chama si kitu kinachosumbua nafsi yake.
  Tumeona maamuzi yake binafsi; hasa pale alipojikuta watoa rushwa wawili maswahiba wake wakileta rufaa mbele yake, na yeye kuishia kugwaya na kuamua kuwapa nafasi nyingine za uongozi ili kuepusha mgogoro mkubwa ambao ungetokana na yeye kufanya maamuzi magumu.
  Kwa kifupi, inahitaji ujasiri wa pekee kulipiga teke titi lililokunyonyesha. Hivi sasa kamati yake kuu ya chama chake CCM, imejazwa wajumbe waliongia kwa kutumia nguvu ya fedha, na inatia shaka kama Kamati Kuu hii inaweza kusimamia sheria hii kwa uchaguzi wa ndani wa chama chake.
  Mmoja wa wajumbe hao wa Kamati Kuu ya CCM ameniambia, wakati naandika makala hii, kuwa: “Tulivyopita sisi kuingia Kamati Kuu, ndivyo alivyopita yeye kuingia Ikulu; itakuwa ajabu mwizi kumkamata mwizi mwenzie”.
  Usemi huu unanikumbusha usemi mwingine wa mkubwa mmoja nchini aliyesema: “JK hawezi kumdhalilisha aliyemwingiza Ikulu, akapona. Anatafuta laana?” Msemaji huyu aliyasema haya pale alipoulizwa ni nini kitatokea endapo Kikwete atatoa kibali cha kukamatwa watuhumiwa wa Kagoda Agriculture waliokwapua bilioni 40 ili kunusuru ushindi wa CCM mwaka 2005.
  Sheria ya kuthibiti fedha chafu katika chaguzi zetu inapokelewa kwa furaha na faraja kwa wapenda haki wote nchini. Hata hivyo, inapungukiwa na mambo makuu matatu, si katika maudhui yake, bali katika miundo mbinu yake.
  Kwanza, watekelezaji wake wanapungukiwa na uadilifu. Hili ni wazi kuwa, mkandamizaji wako wa jana hawezi kuwa mkombozi wako wa leo. CCM iliyoingia madarakani kwa rushwa haiwezi kuiondoa rushwa ikabaki madarakani.
  CCM inayoshikilia dola, haiwezi kuiruhusu dola kuikamata CCM pale itakapotaka kutekeleza kauli mbiu ya “CCM Itatawala Milele” kwa gharama zozote. Mifano iko wazi, na wa karibuni ni huu mnyukano kati ya Bunge na Serikali kuhusu kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea.
  Serikali inajua fika Dk. Hosea ana udhaifu kadhaa kiutendaji na wabunge wanataka aondolewe Takukuru, lakini haiwezi kamwe kumgusa na CCM ikapona maana, baba huyu anayo mafaili ya kila mmojawao ya wakati wa uchaguzi.
  Suluhisho la mnyukano huu halitakaa liwe zuri kwa Dk. Hosea mwenyewe; maana tuliwahi kuyaona ya aina hiyo huko nyuma.
  Kwa kifupi, unaweza kusema hivi: Sheria ya kudhibiti fedha chafu wakati wa uchaguzi ni nzuri, lakini watekelezaji ni “mashetani”.
  Pili, katika hali ambayo Mahakama, Bunge, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Takukuru, na Tume ya Uchaguzi vinakosa uhuru kamili katika kutekeleza majukumu yake, ni vigumu kuona ni jinsi gani sheria hii itafanya kazi.
  Hivi kweli inawezakana vyombo vikapitisha uamuzi unaomnyima mgombea wa CCM nafasi ya kugombea? Mbona mafaili ya Takukuru yanayowatuhumu wanasiasa wa CCM sharti yapelekwe kwanza Ikulu?
  Mbona mahakimu kabla hawajaamua hatima yao kwanza wawasiliane na wakuu wa wilaya? Mbona hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu mgombea binafsi inapigwa danadana na hakuna lolote?
  Katika nchi ambamo utawala wa sheria unafanya kazi, Mkuu wa Dola angewajibishwa kwa kuchelewesha hukumu ya namna hiyo! Mpaka hapa niseme, utekelezaji wa sheria yoyote hutegemea sana utashi na uhuru wa taasisi na vyombo vya dola vilivyotajwa katika sheria hiyo kuwa vitatekeleza sheria hiyo. Kwa Tanzania, hatunavyo, na vilivyopo, havina utashi wala uhuru.
  Tatu, demokrasia imefinywa hata ndani ya chama tawala. Mbinyo huu wa demokrasia ndani ya chama tawala hauwezi kuruhusu uwepo wa demokrasia nje ya chama hiki. Hivi sasa wakubwa wamenuniana na hawaambiani ukweli kuhusu uhuru walionao wana CCM kugombea nafasi ya urais mwaka huu.
  Mizengwe imewekwa kuzuia hilo. Atakayediriki kugombea amepewa wiki moja kutimiza masharti; huku Kikwete akiondolewa sharti hilo. Kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kumwezesha mgombea Kikwete apite bila kupingwa; huku akiwaacha wengine wakiwa wamenuna!
  Sababu inayotolewa ni eti huu ni “utaratibu na utamaduni wa ndani ya Chama”, lakini wanaosema hivyo, hawatoi maelezo ya kwa nini utaratibu wa kubadilishana kati ya Bara na Visiwani haufuatwi tena na hakuna anayeruhusiwa kuhoji.
  Ingekuwa bora kama Kikwete angeacha kipindi hiki cha pili kwa mgombea wa Visiwani ili kuonyesha nia njema ya kudumisha Muungano kwa kutumia “utaratibu na utamaduni wa ndani ya chama chetu”.
  Mwisho, ikiwa kweli Kikwete anayo nia njema ya kukomesha rushwa katika chaguzi za Tanzania, namshauri kwa nia njema afanye mawili ya msingi. Kwanza, akiri wazi na hadharani kuwa hata yeye ni tunda la rushwa katika chaguzi, na aeleze masikitiko yake kuhusu jambo hilo.
  Wote tunajua kuwa si yeye binafsi alifanya hivyo; bali ni mfumo batili uliokithiri ndani ya chama chake, na yeye binafsi hakuwa na ubavu wa kukataa mikakati hiyo. Hili litamsafisha na kumpa nguvu itoshayo kusimamia sheria hii mpya.
  Pili, kama mkuu wa nchi, atamke na kuwa tayari kumkataa mgombea yeyote wa CCM atayebainika kutumia fedha; hata kama kwa kufanya hivyo ushindi utaenda chama cha upinzani.
  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kufanya hivyo. Tangu yeye hatujaona mfano wake; kwamba linapofika suala la uadilifu, itikadi na ukereketwa wa chama, vinawekwa mbali. Basi JK atamke kuwa ni heri chama cha upinzani kichukue nafasi endapo mla rushwa wa CCM anaelekea kuchukua ushindi wa kununua.
  Litakuwa tamko la kimapinduzi na litafungua milango kwa waadilifu kuingia katika ofisi za umma. Hapatakuwapo tena haja ya watu kupitishwa madirishani. Tamko hili, litalizima lile lisemalo, “CCM bila rushwa haiwezekani”.

  Source: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2118
   
 10. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..hawa walikuwa na nafasi ya kulaani rushwa ya CCM-Mtandao tangu wakati wa chaguzi za 1995,2000,na 2005, lakini waliamua kukaa kimya.

  ..nakubaliana na maoni yao, lakini nadhani hawa sasa wanasukumwa zaidi na chuki binafsi.

  ..nimeona wanamtaka JK awaombe radhi wa-Tanzania kwa kushiriki rushwa ktk chaguzi zilizopita. nashauri waandishi wa gazeti la raia mwema nao waombe radhi kwa kutokukemea rushwa ya wanamtandao ktk chaguzi zilizopita.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..haya mambo yalikuwa yakifanywa na wanamtandao tangu mwaka 1995. sasa hawa kina Jenerali Ulimwengu na Johnson Mbwambo walikuwa wapi wakati wote huo wanakuja kusema leo 15 years later?
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Mar 11, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  It is very true jamaa alipitia dirishani kupitia kule Kagoda na sasa anataka kujifanya dirisha limefungwa na halifunguki.lakini kuna la zaidi jamaa anachokilenga.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  ndio maana wengine tuliuliza..aliyekwisha chafuka aweza kusafisha wengine bila yeye mwenyewe kujisafisha?
   
 15. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  "Hivi kweli inawezakana vyombo vikapitisha uamuzi unaomnyima mgombea wa CCM nafasi ya kugombea?"-Raia Mwema

  Watanzania ni vema wakaelewa kuwa, nia ya hii sheria ni kuwadhibiti Wasio wa JK, ndani na nje ya CCM.

  Ni nani anayefikiri kuwa hii sheria itamgusa RA?
   
 16. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwa kifupi makala hii inatuambia kuwa sheria hii haitekelezeki kwani walioitunga wako 'GUILTY' kwa makosa hayo hayo. Hii sheria ni sugarcoat yenye nia ya kuuhadaa ulimwengu tu kuwa uongozi huu unayo nia ya kupambana na rushwa. Uongozi uliowekwa na UFISADI daima utalindwa na UFISADI. Lakini kwa kuwa wenye busara walishasema UFALME ULIOJENGWA KWENYE MISINGI YA UOVU DAIMA UTAANGUSHWA NA UOVU HUO si ajabu UFISADI HUO ukawa ndo shimo litakalouzika utawala huu. Ndo maana kwa kutambua hilo viongozi wanaanza kutapa tapa kwa kuweka sheria .... sheria ambazo kimsingi hazitatekelezeka kwani wanaotakiwa kuzitekeleza ni WAVUNJA SHERIA WAZOEFU NA WALIOKUBUHU WAKIONGOZWA NA MKUU WAO!

  Sasa hivi mbiu zimeanza kupigwa. KALAMU ZILE ZILE ZILIZOKUWA ZIKITUAMINISHA KUWA TUMEPATA KIFAA SASA ZIMEGEUZWA UPANDE WA PILI NA ZINASEMA KINYUME CHAKE.

  Hapa ndo patamu......
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Mar 11, 2010
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Usishangae 2015 akalifungua/zibua ili kumpata atakayelifunga/ziba 2020. ndo mchezo huo, mambo ya ajabu kabisa!
   
 18. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kikwete ni jasiri kwani ninavyojua mimi hata huyo mwandishi hasingeweza hata kurudisha pazia tuu la hilo dirisha sembuse kulifunga na kutia zege!Tumpe sifa mzee Kikwete kwa hilo,ongera baba!
   
 19. J

  JB Member

  #19
  Mar 12, 2010
  Joined: Jul 28, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bubu, Hii article imetulia.

  To be honest siamini kama serikali ya JK imemaanisha kuondoa tatizo la rushwa katika chaguzi za Tanzania ambalo kila kukicha linazidi kushika kasi kama moto wa nyika.
  Inawezekana hii itatumika kama fimbo kwa wabaya wake ili kuwamaliza kisiasa ukizingatia kuwa mfuatiliaji/mtekelezaji wa hii sheria ni Takukuru ambayo inaripoti ikulu moja kwa moja.
   
 20. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kama waandishi walihongwa ili wampambe JK na kuwachafua wagombea wengine,huo ni uthibitisho kuwa waandishi wetu ni wala rushwa na kama tujuavyo wale waandishi ndio leo wanajipambanua ni wapambanaji wa vita dhidi ya rushwa kwa nini tusiamini kuwa sasa wamepata Tajiri mwengine aliepanda dau ili wamchafue JK.kila siku wanaimba JK alihonga sasa wataje hayo makundi yaliyohongwa ili tuyajue tujitenge nayo (najua waandishi watakuwa Included kwenye hii LIST OF SHAME).Pengine waandishi wanaipinga hii sheria kwa kuwa wanajua Rizki yao mwaka huu imeota mbawa.
   
Loading...