Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl. Nyerere, Sehemu ya tatu (3)

GARETHBALE

Member
Dec 22, 2013
76
332
HAWA NDIO WATU WATANO WANAOUNDA KUNDI LA "WANAMTANDAO"

Asalaam aleykum,
Tumsifu Yesu Kristo,
Wakubwa zangu shikamooni na wadogo zangu marhaba.

Nichukue fursa hii kuwashukuru wasomaji wa simulizi hizi zihusuzo wasifu wa mwanasiasa Bernard Kamilius Membe(BM)mwenye asili ya kabila la Wamwera kutoka mkoa wa Lindi kanda ya Kusini.

Hadi sasa katika simulizi hizi ambazo zimejikita kwenye kuelezea mambo ambayo wengi hawayafahamu kuhusu mwanasiasa huyu nguli niliyoyapa jina la "series" yenye "episodes" nyingi zitakazowekwa zote mpaka ziishe na leo tupo "episode" ya tatu.

Katika "episode" iliyopita niliahidi kuandika kuhusu "mtandao".Na nikauliza je inafahamika kwamba "mtandao" ulikuwa na watu watano tu?.Ni kina nani hao?.Ilikuwaje wakaungana na nani aliasisi wazo la kuunda "mtandao"?.Endelea kufuatana nami katika "episode" hii.

Baada ya Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kupokea majibu ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kutoka kwa Ndg.Bernard Kamilius Membe juu ya swali lake kama vijana wanaruhusiwa kuomba ridhaa ya chama katika kuwania urais wa nchi alimshirikisha suala lile marehemu Mzee Samweli John Sitta.

Alifanya hivi kwasababu Mzee Samweli John Sitta alikuwa ni mtu wake wa karibu katika harakati zake za kisiasa.Lakini pia ukongwe katika chama na utumishi wa umma vilichangia kwa Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kuamini katika ushauri wa Mzee Samweli John Sitta.

Mzee Samweli John Sitta alikubaliana na wazo la Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya uamuzi wake wa kuwania urais wa nchi.Na aliunga mkono suala la kumtuma Ndg.Bernard Kamilius Membe kumuuliza Mwl.Julius Kambarage Nyerere kama nao vijana wagombee.Ila akamshauri zaidi kwamba Mwl.Julius Kambarage Nyerere akirejea nchini kutoka katika ziara zake basi waende Msasani kuzungumza naye ili wapate baraka zake ana kwa ana.

Na ukweli Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliporejea nchini Tanzania Mzee Samweli John Sitta na Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete waliomba mihadi ya kuonana naye.Aliridhia na wao kwenda kumwona.Majibu ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere hayakubadilika.Yalikuwa ni yaleyale kama aliyomjibu Ndg.Bernard Kamilius Membe akiwa nchini Canada.

Wakati huo waliokuwa wakitajwa kuutaka urais kupitia CCM miongoni mwao ni Mzee Samweli John Malecela na Mzee Cleopa David Msuya.Mzee Benjamin William Mkapa hakuwa maarufu sana miongoni mwao.

Safari ya kuusuka "mtandao" ikaanza rasmi.Ikawa ni fursa pia kwa Ndg.Edward Ngoyai Lowassa ambaye kwa wakati huo naye alikuwa mteule wa nafasi ya ubunge akitokea katika utumishi wa umma kama Mkurugenzi Mkuu wa AICC jijini Arusha.

Tofauti na mwenzake Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete yeye(Lowassa) alikuwa anapambana kivyake.Japo kama ilivyo kwa Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete naye(Lowassa) alijikita kwenye turufu ya ujana.Hii turufu ilikuwa na nguvu mno kwa wakati ule ndani ya CCM na mitaani.

Na huu ndio wakati ambao mwanasiasa kutokea mkoa wa Tabora Rostam Abdulrasool Aziz alikuwa ana muda mfupi tangu aingie bungeni kupitia uchaguzi mdogo jimbo la Igunga.Alikuwa na urafiki na Ndg.Edward Ngoyai Lowassa sio Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Samweli John Sitta wala Ndg.Bernard Kamilius Membe.

Pilikapilika za kujipanga na uchukuaji fomu,kutafuta wadhamini na kukampeni zilipopamba moto ikambidi Ndg.Bernard Kamilius Membe aombe likizo serikalini ili aje ajiunge na katika kundi la kumsaidia Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete.

Uamuzi huu haukuwa mrahisi sana.Ulihatarisha ajira yake serikalini na ukizingatia kwa wakati ule alikuwa bado ni mtumishi wa "ofisi nyeti".

Inasemekana kwamba kabla ya kuomba likizo alizungumza na Mwl.Julius Kambarage Nyerere ili na yeye apate baraka zake.Na hii ni kwasababu kwa wakati ule Mwl.Julius Kambarage Nyerere alikuwa bado na nguvu kubwa katika chama,serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.Likizo ilipatikana na alirudi nchini akitokea Canada.Makazi yake kwa muda wote wa kampeni ikawa ni Palm Beach Hotel ya jijini Dar es salaam.

Uamuzi wa kuchukua likizo ili ajiunge na Mzee Samweli John Sitta kumsaidia Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete ulimletea matatizo kwa baadhi ya watu hususani watumishi wenzake katika "ofisi nyeti" na jamii ya watu wa Kusini kwa ujumla.Wengi hawakumwelewa.Wale wa "ofisi nyeti" walishangazwa na uamuzi wa yeye kuomba likizo ili ashiriki shughuli za kisiasa tena kwakuwa upande tofauti na aliyekuwa bosi wake.Kwa wachache wasiojua ni kwamba Mzee Benjamin William Mkapa alikuwa bosi wa Ndg.Bernard Kamilius Membe kwasababu ya uwaziri wake wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa wakati ule ambao Ndg.Bernard Kamilius Membe alipohamishiwa kwa mara ya kwanza ubalozini nchini Canada.

Lakini pia watu wa Kusini hawakumwelewa Ndg.Bernard Kamilius Membe kwasababu alionekana kumpinga Mzee Benjamin William Mkapa ambaye pia ni mtu wa Kusini.Hii ilimfanya hata Mzee Maokola Majogo kumfuata Ndg.Bernard Kamilius Membe na kumhoji ni kwanini anapingana na mwenzake wa Kusini.Kwa Ndg.Bernard Kamilius Membe hii kwake haikuwa hoja,alisimamia msimamo wake kuwa yeye anamuunga mkono Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete na hawezi kubadilika.Kwake yeye siasa haikuwa suala la ukanda bali umoja na mshikamano wa taifa.

Kutokana na uwepo wa Ndg.Edward Ngoyai Lowassa na Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa vijana pekee waliotangaza nia ya kugombea urais ikashauriwa waungane.Ndipo wakachukua fomu pamoja na kuzunguka pamoja kutafuta wadhamini kama kanuni za CCM zinavyotaka.Kabla ya kuitwa "mtandao" wakapachikwa jina la kundi maarufu la muziki nchini Marekani liitwalo Boys 2 Men.Wakatumia ndege ndogo waliyokodi kuzungukia mikoa yote nchini na kurejesha fomu pamoja.

Mchakato wa kuchambua fomu za wagombea kabla ya kuchuja majina na kuteua machache yatakayopigiwa kura na NEC ili kumpata mgombea mmoja ulianza.Jina la Ndg.Edward Ngoyai Lowassa lilikatwa.Mzee Samweli John Sitta akaja na wazo la kuongeza nguvu katika kundi la Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumwita Ndg.Edward Ngoyai Lowassa na kumwomba awape watu wake wanaomuunga mkono.Ndipo ikaamuliwa sasa kuwe na kundi kuu la watu watano tu watakaoendesha kampeni za Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete likisaidiana na kundi jingine dogo ambalo litasaidia kuzungukia wajumbe wengine ambao hawa watu watano hawawezi kuwafikia.

Ndipo ikaunganishwa nguvu ya Mzee Samweli John Sitta(Mwenyekiti),Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete(Mgombea),Ndg.Bernard Kamilius Membe(Mpanga mikakati),Rostam Abdulrasool Aziz(Mweka Hazina)na Ndg.Edward Ngoyai Lowassa(Katibu).

Lile kundi dogo lililokuwa na jukumu la kusaidia hawa watu watano ambao ndio "wanamtandao" wakuu liliongozwa na Mzee Mohamed Abdulaziz pamoja na marehemu Kapt.John Komba.Kundi hili lilishindwa kumshawishi Dk.Anthony Mwandu Diallo kujiunga nao.Alipofuatwa aliwajibu kuwa tayari Mzee Benjamin William Mkapa kashamwomba amsaidie katika kampeni hivyobasi hawezi kuacha kumuunga mkono.

Kampeni zilipamba moto.Dodoma haikukalika."Wanamtandao" walijipanga vyema.Walitoa ushindani mkubwa ambao ulimfanya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kutumia nguvu ya ziada kuwadhibiti.Hii ni kwasababu aliamini katika uwezo wa Mzee Benjamin William Mkapa kwa wakati ule."Wanamtandao" walijitosheleza kwa mikakati,walikuwa na watu,walikuwa na vitendea kazi na walijua kushawishi.Na ndio maana wajuzi wa masuala ya siasa waliokuwepo miaka ile wanasema Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete alishinda katika kura za maoni ila tu Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliingilia kati kwasababu kwa nyakati zile aliona nchi ilihitaji mtu aina ya Mzee Benjamin William Mkapa.

Na ikumbukwe kuwa katika mchuano ule kulitokea sintofahamu baina ya mgombea wa "wanamtandao" na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa wakati ule marehemu Mzee Lawrence Gama.Yote hii ilikuwa katika kuwadhibiti "wanamtandao" ambao walizitawala kampeni mwanzo mwisho.

Baada ya uamuzi wa CCM kumteua Mzee Benjamin William Mkapa "wanamtandao" walikubaliana na matokeo.Walivunja kundi lao na kuunganisha nguvu ya kumsaidia Mzee Benjamin William Mkapa ambaye nje ya chama chao alikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mwanasiasa mkongwe Augustine Lyatonga Mrema na msomi Prof.Ibrahim Haruna Lipumba.

"Wanamtandao" Ndg.Edward Ngoyai Lowassa alienda kugombea ubunge jimbo la Monduli mkoani Arusha,Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete alienda kugombea ubunge jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani,Ndg.Bernard Kamilius Membe alirejea kibaruani ubalozini nchini Canada,Rostam Abdulrasool Aziz alienda kutetea nafasi yake ya ubunge jimbo la Igunga mkoa wa Tabora pamoja na Mzee Samweli John Sitta aliyerejea Urambo Mashariki kutetea nafasi yake ya ubunge pia.

Lile kundi dogo lililokuwa likiwasaidia "wanamtandao" nalo likaungana na wanachama wengine wa CCM kumsaidia Mzee Benjamin William Mkapa.Na huu ndio ukawa mwanzo wa uhai wa "wanamtandao" kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005."Mtandao" haukufa.Zaidi ulijiongezea wafuasi kila kulipokucha.Nina imani nimeeleweka.

Kuhusu "wanamtandao" mwaka 1995 naomba niishie hapa."Episodes" zijazo nitaelezea walivyorejea kwa kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya katika kampeni za mwaka 2005.

Swali:Je Kikwete ni ndugu wa damu na Membe?

Tuungane pamoja kesho muda kama huu....
 
Mtandao hauna nafasi tena miaka hii mnataka turudishe tenda genge la mafisadi ikulu sizani kama itatokea!

Katika mambo nilimuona Kikwete alifanya jambo ni kutoruhusu ili kundi liendelee kutamba baada ya kuzunguka na kufanya ufisadi wa kutisha kwenye serikali yake.
 
Ndio maana katika kura za maoni Magufuli alipata bahati ya kuiwakilisha CCM, katika chaguzi ya 2015 na hii yote ni baada ya wana mtandao kushindwa kuelewana, viongozi wa juu wakaamua kuwavunja madume mawili "Membe" na "Lowassa" maana hata Jakaya alishindwa kufanya maamuzi na hapo ndipo bahati ikamdondokea JPM.

Na ndio maana JPM hata kwenye ziara zake haishiwi kumpongeza Mkapa, maana pasipo yeye asingekanyaga Jengo Jeupe, hata yale maamuzi ya kuwakata Lowasa na Membe ni hasira za Mzee Mkapa kwa hao vijana enzi za kinyang'anyiro cha nani asismame katika kugombea uraisi 1995, maana vijana walipa hofu kwelikweli na kama ulivyosema JK ndio ilibidi asimame badala ya Mkapa.

Hadi sasa najiuliza ilikuwaje hawa maswahiba mawili walishindwa kuelewana 2015 hadi kufikia mtandao wao kuvunjwa, nasubili episodes nyingine mkuu..
 
Safi sana, haya mambo ndo tunayoyataka hapa JF

Kwa kuongezea tu, Baada ya JK na watu wake kwenda msasani kwa mwalimu, walimkuta mwalimu na watu pale anaongea nao, baada ya kusikiliza nia yao na kuwabariki wakagombee.

Hata hivyo mwalimu alikuwa na wazo tofauti kichwani, akakata shauri la kwenda Dodoma kuthibiti nguvu yao maana aligundua kuwa bila kuwadhibiti wangechukua nchi!

Hata kwenye kupiga kura ndani ya CCM kati ya BWM na JK, Mwalimu alifanya kampeni ya kuandika vimemo kwa mkono wake akiwaomba wajumbe wa Zanzibar wamuunge mkono BWM.

Lakini ukiacha hilo, baada ya JK kumgalagaza Msuya na BWM kwenye round ya hao watatu, Mwalimu alivunja kanuni za CCM kwa kulazimisha kura zipigwe kati ya BWM na JK wakati kitu hicho hakikuwemo ktk kanuni, Yaani ilipaswa JK atangazwe tu kuwa mgombea maana yeye ndo aliibuka kidedea dhidi ya wote kwenye mkutano mkuu
 
Mtoa mada ni either anadanganya kwa kuwa 1995 hakuwa matured kuweza kujua yaliyokuwa yanatokea

Au kalishwa matango pori nae kwa kuwa hana kumbukumbu nzuri kaamua nae kuja na hoja nyepesi ili kutimiza hadaa kwa faida yake binafsi au ya aliemtuma.

Mwaka 1995 Benjamin Mkapa alikuwa Waziri wa Elimu ya Juu; Sayansi ya teknolojia na hivyo hakuwa boss wa Membe kama hoja inavyopambwa.

1995 Edward Lowasa alikuwa Waziri wa ardhi na nyumba. Na hakuwa AICC. Edward alikuwa AICC 1989/90. Kutujuza hapa kuwa mwaka 1995 kuwa EL alikuwa boss wa AICC ni hadaa ya mchana peupe.

Kama haya machache ambayo watu wazima tunakumbuka bila kutumia google; si ajabu hata hayo "yanayodaiwa ni mazungumzo na Mwl JKN" yakawa kamba.

Bora ungetafuta watu wazima ili kuwa na facts ili unapodanganya, basi uongo unakuwa karibu sana na ukweli.
 
At least wakati huo kumpata mgombea kulienda kwa ushawishi na mbinu za kisiasa kisha hakukuwa na chuki.
Bahati mbaya kwa sasa hata kutangaza unataka kugombea tayari unatafutiwa visa, utatukanwa sana, utaonekana sio mzalendo na hata kutishiwa kifo.
CCM sio ile tena ya hoja au ujanja ujanja bali hii imebaki ya "kuimba kama kasuku" sifa za mtawala kiasi hata angetembea uchi atasifiwa kuwa Kaunda suti imempendeza.
Hakuna hoja ni viroja tuu, chama hiki pamoja na kuwa kilianza kuwa hovyo miaka kama 20 iliyopita lakini ndani ya hii mitatu au minne kimekuwa zaidi hovyo hovyo na sio chama cha siasa bali genge LA uhalifu.
 
Wakongwe kama Poise, tunakuelewa hoja yako nimeona threads nyingi humu vijana vinadanganya ila kwa sababu wala pumba ni wengi hawawezi kuchanganua kati ya mchanga na ulezi.
 
Ukirudi usisahau kujibu hili swali
Kitu gani kilimpoteza kwenye ulingo wa siasa mzee Samwel John Sitta kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005?
 
Kingine ambacho nimesahau kuweka record sawa.
Mtoa mada pia anafanya upotoshaji wa kujua wa bila kujua.

Mwaka 1995 kati ya wagombea watatu wa mwisho waliopigiwa kura na mkutano mkuu CCM walikuwa ni
Lt. Col. Jakaya Mrisho Kikwete (Waziri wa Fedha wakati huo)
Mhe. Benjamin W. Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia)
Mhe. Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais)

Kama nilivyopangilia; JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na Mkapa then Msuya akawa wa 3.

Kwa kuwa katiba ya CCM iko wazi, mjumbe anaepata zaidi ya asilimia 51 ya wajumbe anapita moja kwa moja. Ndiyo maana JK alipopata wingi wa kura zaidi ya 51% mwaka 2005, akasema "safari hii kura zimetosha"

Hakuna aliemfanyia mizengwe JK 1995; unless kama kuna jambo ambalo mtoa mada analo alete ushahidi. Ila katiba na taratibu za CCM zinafahamika. Na kwa wale tuliokuwepo tukifuatilia, tunasikitika kuona mtu ana hadaa mchana peupe.

Muandishi, nakushauri ufanye homework. Ili hata kama unadanganya basi uongo wako usiwe too obvious.

JF ni great thinkers forum. It is very shameful to write white lies
 
.
Kingine ambacho nimesahau kuweka record sawa.
Mtoa mada pia anafanya upotoshaji wa kujua wa bila kujua.

Mwaka 1995 kati ya wagombea watatu wa mwisho waliopigiwa kura na mkutano mkuu CCM walikuwa ni
Lt. Col. Jakaya Mrisho Kikwete (Waziri wa Fedha wakati huo)
Mhe. Benjamin W. Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia)
Mhe. Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais)

Kama nilivyopangilia; JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na Mkapa then Msuya akawa wa 3.

Kwa kuwa katiba ya CCM iko wazi, mjumbe anaepata zaidi ya asilimia 51 ya wajumbe anapita moja kwa moja. Ndiyo maana JK alipopata wingi wa kura zaidi ya 51% mwaka 2005, akasema "safari hii kura zimetosha"

Hakuna aliemfanyia mizengwe JK 1995; unless kama kuna jambo ambalo mtoa mada analo alete ushahidi. Ila katiba na taratibu za CCM zinafahamika. Na kwa wale tuliokuwepo tukifuatilia, tunasikitika kuona mtu ana hadaa mchana peupe.

Muandishi, nakushauri ufanye homework. Ili hata kama unadanganya basi uongo wako usiwe too obvious.

JF ni great thinkers forum. It is very shameful to write white lies
 
HAWA NDIO WATU WATANO WANAOUNDA KUNDI LA "WANAMTANDAO"

Asalaam aleykum,
Tumsifu Yesu Kristo,
Wakubwa zangu shikamooni na wadogo zangu marhaba.

Nichukue fursa hii kuwashukuru wasomaji wa simulizi hizi zihusuzo wasifu wa mwanasiasa Bernard Kamilius Membe(BM)mwenye asili ya kabila la Wamwera kutoka mkoa wa Lindi kanda ya Kusini.

Hadi sasa katika simulizi hizi ambazo zimejikita kwenye kuelezea mambo ambayo wengi hawayafahamu kuhusu mwanasiasa huyu nguli niliyoyapa jina la "series" yenye "episodes" nyingi zitakazowekwa zote mpaka ziishe na leo tupo "episode" ya tatu.

Katika "episode" iliyopita niliahidi kuandika kuhusu "mtandao".Na nikauliza je inafahamika kwamba "mtandao" ulikuwa na watu watano tu?.Ni kina nani hao?.Ilikuwaje wakaungana na nani aliasisi wazo la kuunda "mtandao"?.Endelea kufuatana nami katika "episode" hii.

Baada ya Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kupokea majibu ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kutoka kwa Ndg.Bernard Kamilius Membe juu ya swali lake kama vijana wanaruhusiwa kuomba ridhaa ya chama katika kuwania urais wa nchi alimshirikisha suala lile marehemu Mzee Samweli John Sitta.

Alifanya hivi kwasababu Mzee Samweli John Sitta alikuwa ni mtu wake wa karibu katika harakati zake za kisiasa.Lakini pia ukongwe katika chama na utumishi wa umma vilichangia kwa Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kuamini katika ushauri wa Mzee Samweli John Sitta.

Mzee Samweli John Sitta alikubaliana na wazo la Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete juu ya uamuzi wake wa kuwania urais wa nchi.Na aliunga mkono suala la kumtuma Ndg.Bernard Kamilius Membe kumuuliza Mwl.Julius Kambarage Nyerere kama nao vijana wagombee.Ila akamshauri zaidi kwamba Mwl.Julius Kambarage Nyerere akirejea nchini kutoka katika ziara zake basi waende Msasani kuzungumza naye ili wapate baraka zake ana kwa ana.

Na ukweli Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliporejea nchini Tanzania Mzee Samweli John Sitta na Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete waliomba mihadi ya kuonana naye.Aliridhia na wao kwenda kumwona.Majibu ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere hayakubadilika.Yalikuwa ni yaleyale kama aliyomjibu Ndg.Bernard Kamilius Membe akiwa nchini Canada.

Wakati huo waliokuwa wakitajwa kuutaka urais kupitia CCM miongoni mwao ni Mzee Samweli John Malecela na Mzee Cleopa David Msuya.Mzee Benjamin William Mkapa hakuwa maarufu sana miongoni mwao.

Safari ya kuusuka "mtandao" ikaanza rasmi.Ikawa ni fursa pia kwa Ndg.Edward Ngoyai Lowassa ambaye kwa wakati huo naye alikuwa mteule wa nafasi ya ubunge akitokea katika utumishi wa umma kama Mkurugenzi Mkuu wa AICC jijini Arusha.

Tofauti na mwenzake Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete yeye(Lowassa) alikuwa anapambana kivyake.Japo kama ilivyo kwa Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete naye(Lowassa) alijikita kwenye turufu ya ujana.Hii turufu ilikuwa na nguvu mno kwa wakati ule ndani ya CCM na mitaani.

Na huu ndio wakati ambao mwanasiasa kutokea mkoa wa Tabora Rostam Abdulrasool Aziz alikuwa ana muda mfupi tangu aingie bungeni kupitia uchaguzi mdogo jimbo la Igunga.Alikuwa na urafiki na Ndg.Edward Ngoyai Lowassa sio Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete,Mzee Samweli John Sitta wala Ndg.Bernard Kamilius Membe.

Pilikapilika za kujipanga na uchukuaji fomu,kutafuta wadhamini na kukampeni zilipopamba moto ikambidi Ndg.Bernard Kamilius Membe aombe likizo serikalini ili aje ajiunge na katika kundi la kumsaidia Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete.

Uamuzi huu haukuwa mrahisi sana.Ulihatarisha ajira yake serikalini na ukizingatia kwa wakati ule alikuwa bado ni mtumishi wa "ofisi nyeti".

Inasemekana kwamba kabla ya kuomba likizo alizungumza na Mwl.Julius Kambarage Nyerere ili na yeye apate baraka zake.Na hii ni kwasababu kwa wakati ule Mwl.Julius Kambarage Nyerere alikuwa bado na nguvu kubwa katika chama,serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.Likizo ilipatikana na alirudi nchini akitokea Canada.Makazi yake kwa muda wote wa kampeni ikawa ni Palm Beach Hotel ya jijini Dar es salaam.

Uamuzi wa kuchukua likizo ili ajiunge na Mzee Samweli John Sitta kumsaidia Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete ulimletea matatizo kwa baadhi ya watu hususani watumishi wenzake katika "ofisi nyeti" na jamii ya watu wa Kusini kwa ujumla.Wengi hawakumwelewa.Wale wa "ofisi nyeti" walishangazwa na uamuzi wa yeye kuomba likizo ili ashiriki shughuli za kisiasa tena kwakuwa upande tofauti na aliyekuwa bosi wake.Kwa wachache wasiojua ni kwamba Mzee Benjamin William Mkapa alikuwa bosi wa Ndg.Bernard Kamilius Membe kwasababu ya uwaziri wake wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kwa wakati ule ambao Ndg.Bernard Kamilius Membe alipohamishiwa kwa mara ya kwanza ubalozini nchini Canada.

Lakini pia watu wa Kusini hawakumwelewa Ndg.Bernard Kamilius Membe kwasababu alionekana kumpinga Mzee Benjamin William Mkapa ambaye pia ni mtu wa Kusini.Hii ilimfanya hata Mzee Maokola Majogo kumfuata Ndg.Bernard Kamilius Membe na kumhoji ni kwanini anapingana na mwenzake wa Kusini.Kwa Ndg.Bernard Kamilius Membe hii kwake haikuwa hoja,alisimamia msimamo wake kuwa yeye anamuunga mkono Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete na hawezi kubadilika.Kwake yeye siasa haikuwa suala la ukanda bali umoja na mshikamano wa taifa.

Kutokana na uwepo wa Ndg.Edward Ngoyai Lowassa na Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kuwa vijana pekee waliotangaza nia ya kugombea urais ikashauriwa waungane.Ndipo wakachukua fomu pamoja na kuzunguka pamoja kutafuta wadhamini kama kanuni za CCM zinavyotaka.Kabla ya kuitwa "mtandao" wakapachikwa jina la kundi maarufu la muziki nchini Marekani liitwalo Boys 2 Men.Wakatumia ndege ndogo waliyokodi kuzungukia mikoa yote nchini na kurejesha fomu pamoja.

Mchakato wa kuchambua fomu za wagombea kabla ya kuchuja majina na kuteua machache yatakayopigiwa kura na NEC ili kumpata mgombea mmoja ulianza.Jina la Ndg.Edward Ngoyai Lowassa lilikatwa.Mzee Samweli John Sitta akaja na wazo la kuongeza nguvu katika kundi la Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumwita Ndg.Edward Ngoyai Lowassa na kumwomba awape watu wake wanaomuunga mkono.Ndipo ikaamuliwa sasa kuwe na kundi kuu la watu watano tu watakaoendesha kampeni za Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete likisaidiana na kundi jingine dogo ambalo litasaidia kuzungukia wajumbe wengine ambao hawa watu watano hawawezi kuwafikia.

Ndipo ikaunganishwa nguvu ya Mzee Samweli John Sitta(Mwenyekiti),Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete(Mgombea),Ndg.Bernard Kamilius Membe(Mpanga mikakati),Rostam Abdulrasool Aziz(Mweka Hazina)na Ndg.Edward Ngoyai Lowassa(Katibu).

Lile kundi dogo lililokuwa na jukumu la kusaidia hawa watu watano ambao ndio "wanamtandao" wakuu liliongozwa na Mzee Mohamed Abdulaziz pamoja na marehemu Kapt.John Komba.Kundi hili lilishindwa kumshawishi Dk.Anthony Mwandu Diallo kujiunga nao.Alipofuatwa aliwajibu kuwa tayari Mzee Benjamin William Mkapa kashamwomba amsaidie katika kampeni hivyobasi hawezi kuacha kumuunga mkono.

Kampeni zilipamba moto.Dodoma haikukalika."Wanamtandao" walijipanga vyema.Walitoa ushindani mkubwa ambao ulimfanya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kutumia nguvu ya ziada kuwadhibiti.Hii ni kwasababu aliamini katika uwezo wa Mzee Benjamin William Mkapa kwa wakati ule."Wanamtandao" walijitosheleza kwa mikakati,walikuwa na watu,walikuwa na vitendea kazi na walijua kushawishi.Na ndio maana wajuzi wa masuala ya siasa waliokuwepo miaka ile wanasema Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete alishinda katika kura za maoni ila tu Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliingilia kati kwasababu kwa nyakati zile aliona nchi ilihitaji mtu aina ya Mzee Benjamin William Mkapa.

Na ikumbukwe kuwa katika mchuano ule kulitokea sintofahamu baina ya mgombea wa "wanamtandao" na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa wakati ule marehemu Mzee Lawrence Gama.Yote hii ilikuwa katika kuwadhibiti "wanamtandao" ambao walizitawala kampeni mwanzo mwisho.

Baada ya uamuzi wa CCM kumteua Mzee Benjamin William Mkapa "wanamtandao" walikubaliana na matokeo.Walivunja kundi lao na kuunganisha nguvu ya kumsaidia Mzee Benjamin William Mkapa ambaye nje ya chama chao alikabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mwanasiasa mkongwe Augustine Lyatonga Mrema na msomi Prof.Ibrahim Haruna Lipumba.

"Wanamtandao" Ndg.Edward Ngoyai Lowassa alienda kugombea ubunge jimbo la Monduli mkoani Arusha,Ndg.Jakaya Mrisho Kikwete alienda kugombea ubunge jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani,Ndg.Bernard Kamilius Membe alirejea kibaruani ubalozini nchini Canada,Rostam Abdulrasool Aziz alienda kutetea nafasi yake ya ubunge jimbo la Igunga mkoa wa Tabora pamoja na Mzee Samweli John Sitta aliyerejea Urambo Mashariki kutetea nafasi yake ya ubunge pia.

Lile kundi dogo lililokuwa likiwasaidia "wanamtandao" nalo likaungana na wanachama wengine wa CCM kumsaidia Mzee Benjamin William Mkapa.Na huu ndio ukawa mwanzo wa uhai wa "wanamtandao" kuelekea uchaguzi wa mwaka 2005."Mtandao" haukufa.Zaidi ulijiongezea wafuasi kila kulipokucha.Nina imani nimeeleweka.

Kuhusu "wanamtandao" mwaka 1995 naomba niishie hapa."Episodes" zijazo nitaelezea walivyorejea kwa kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya katika kampeni za mwaka 2005.

Swali:Je Kikwete ni ndugu wa damu na Membe?

Tuungane pamoja kesho muda kama huu....
Hujatwambia bado Lowassa alipoulizwa na Mwalimu we kijana hizi mali umezipata wapi na ile kauli maaru ''kama mnampenda kampikieni chai'' tatizo unaandika tu kutaka kumpa ujiko Membe .
 
Kingine ambacho nimesahau kuweka record sawa.
Mtoa mada pia anafanya upotoshaji wa kujua wa bila kujua.

Mwaka 1995 kati ya wagombea watatu wa mwisho waliopigiwa kura na mkutano mkuu CCM walikuwa ni
Lt. Col. Jakaya Mrisho Kikwete (Waziri wa Fedha wakati huo)
Mhe. Benjamin W. Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia)
Mhe. Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais)

Kama nilivyopangilia; JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na Mkapa then Msuya akawa wa 3.

Kwa kuwa katiba ya CCM iko wazi, mjumbe anaepata zaidi ya asilimia 51 ya wajumbe anapita moja kwa moja. Ndiyo maana JK alipopata wingi wa kura zaidi ya 51% mwaka 2005, akasema "safari hii kura zimetosha"

Hakuna aliemfanyia mizengwe JK 1995; unless kama kuna jambo ambalo mtoa mada analo alete ushahidi. Ila katiba na taratibu za CCM zinafahamika. Na kwa wale tuliokuwepo tukifuatilia, tunasikitika kuona mtu ana hadaa mchana peupe.

Muandishi, nakushauri ufanye homework. Ili hata kama unadanganya basi uongo wako usiwe too obvious.

JF ni great thinkers forum. It is very shameful to write white lies

Hakuna mahali katika katiba ya CCM palipotaka mgombea apate 51%. Hiyo hoja aliibuka nayo Nyerere papo kwa papo mkutanoni from nowhere baada ya mgombea wake yaani BWM na Msuya kuwa wamegaragazwa na JK kwenye round ya kwanza.
Mmoja wa watu waliosimama kuhoji hiyo hoja ya mwalimu kwa kupoint out kuwa haikuwemo kwenye kanuni za chama aliondolewa fasta sana mkutanoni na watu wa Security.
 
Ndio maana katika kura za maoni Magufuli alipata bahati ya kuiwakilisha CCM, katika chaguzi ya 2015 na hii yote ni baada ya wana mtandao kushindwa kuelewana, viongozi wa juu wakaamua kuwavunja madume mawili "Membe" na "Lowassa" maana hata Jakaya alishindwa kufanya maamuzi na hapo ndipo bahati ikamdondokea JPM.

Na ndio maana JPM hata kwenye ziara zake haishiwi kumpongeza Mkapa, maana pasipo yeye asingekanyaga Jengo Jeupe, hata yale maamuzi ya kuwakata Lowasa na Membe ni hasira za Mzee Mkapa kwa hao vijana enzi za kinyang'anyiro cha nani asismame katika kugombea uraisi 1995, maana vijana walipa hofu kwelikweli na kama ulivyosema JK ndio ilibidi asimame badala ya Mkapa.

Hadi sasa najiuliza ilikuwaje hawa maswahiba mawili walishindwa kuelewana 2015 hadi kufikia mtandao wao kuvunjwa, nasubili episodes nyingine mkuu..
mbona rais magufuli kuna siku alisema bila kikwete asingekua rais?..nikwamba alipata nafasi ile(si kwa bahati mbaya) kwa kuwa anatoka kanda ya ziwa(wasukuma,wanyamwezi,wakurya,wahaya),kanda amabayo kama hutoishika basi hushindi uchaguzi,na pia alionekana ndiye anayeaaminika(msafi) kwa wananchi kwa kipindi kile neno ufisadi limeshika hatamu,rais wa nchi hii hawezi kupatikana kwa nbahati mbaya hivyo kama unavyodhani
 
Kingine ambacho nimesahau kuweka record sawa.
Mtoa mada pia anafanya upotoshaji wa kujua wa bila kujua.

Mwaka 1995 kati ya wagombea watatu wa mwisho waliopigiwa kura na mkutano mkuu CCM walikuwa ni
Lt. Col. Jakaya Mrisho Kikwete (Waziri wa Fedha wakati huo)
Mhe. Benjamin W. Mkapa (Waziri wa Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia)
Mhe. Cleopa Msuya (Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais)

Kama nilivyopangilia; JK aliongoza kwa kura akifuatiwa na Mkapa then Msuya akawa wa 3.

Kwa kuwa katiba ya CCM iko wazi, mjumbe anaepata zaidi ya asilimia 51 ya wajumbe anapita moja kwa moja. Ndiyo maana JK alipopata wingi wa kura zaidi ya 51% mwaka 2005, akasema "safari hii kura zimetosha"

Hakuna aliemfanyia mizengwe JK 1995; unless kama kuna jambo ambalo mtoa mada analo alete ushahidi. Ila katiba na taratibu za CCM zinafahamika. Na kwa wale tuliokuwepo tukifuatilia, tunasikitika kuona mtu ana hadaa mchana peupe.

Muandishi, nakushauri ufanye homework. Ili hata kama unadanganya basi uongo wako usiwe too obvious.

JF ni great thinkers forum. It is very shameful to write white lies
huku mtaani wanadai eti jk aliingizwa tu kukata nguvu za prof malima,maana wajumbe wa ccm wengi walikua wa dini ya malima,kwa kuwa bara na visiwani wanatoa idadi sawa ya wajumbe...tatizo jk na wenzake wakagonga kampeni la maana,wakapitiliza
 
Hujatwambia bado Lowassa alipoulizwa na Mwalimu we kijana hizi mali umezipata wapi na ile kauli maaru ''kama mnampenda kampikieni chai'' tatizo unaandika tu kutaka kumpa ujiko Membe .

Hizi ngonjela zinaandikwa na Membe mwenyewe kujipa ujiko!!!
 
At least wakati huo kumpata mgombea kulienda kwa ushawishi na mbinu za kisiasa kisha hakukuwa na chuki.
Bahati mbaya kwa sasa hata kutangaza unataka kugombea tayari unatafutiwa visa, utatukanwa sana, utaonekana sio mzalendo na hata kutishiwa kifo.
CCM sio ile tena ya hoja au ujanja ujanja bali hii imebaki ya "kuimba kama kasuku" sifa za mtawala kiasi hata angetembea uchi atasifiwa kuwa Kaunda suti imempendeza.
Hakuna hoja ni viroja tuu, chama hiki pamoja na kuwa kilianza kuwa hovyo miaka kama 20 iliyopita lakini ndani ya hii mitatu au minne kimekuwa zaidi hovyo hovyo na sio chama cha siasa bali genge LA uhalifu.
Imepangwa wagombea wataokaochukua fomu ya urais ya chama chakavu 2020 watatekwa .
 
Back
Top Bottom