Kikwete alimtuma Membe kwa Mwl Nyerere, Sehemu ya nne (4)

GARETHBALE

Member
Dec 22, 2013
76
400
JE KIKWETE NA MEMBE NI NDUGU WA KUZALIWA TUMBO MOJA?

Nichukue fursa hii kuwashukuru wasomaji,wakosoaji,wauliza maswali na watoa maoni wote wa jukwaa hili kwa kila ninachoandika na kukiweka humu.

Ikumbukwe kwamba dhumuni kuu la simulizi hizi ni kuwajulisha watu juu ya wasifu au historia ya mwanasiasa nguli Bernard Kamilius Membe.Ambayo kwa pengine sio kila mtu anaijua au anamjua vilivyo mwanasiasa huyu.

Ndio maana katika simulizi hizi nikaamua kuzipa jina "series" ambayo itabebwa na "episodes" tofauti zenye kuelezea matukio muhimu ambayo yana mvuto wa kipekee katika safari yake ya utumishi wa umma na kisiasa pia.

Katika "episode" iliyopita ambayo ilielezea kuhusu "wanamtandao" niliona baadhi ya wasomaji wakihoji kuhusu masuala kadhaa ambayo hawakuyaelewa au pengine labda sikuyaweka.

Nitatoa ufafanuzi katika masuala mawili yaliyojitokeza ambayo moja sikueleweka nilimaanisha nini niliposema kwamba Benjamin William Mkapa alikuwa kuwa bosi wa Bernard Kamilus Membe wakati akihamia katika ubalozi wetu nchini Canada na lingine nilikumbushwa kuwa walioingia tatu bora kwenye kura za maoni walikuwa ni Jakaya Mrisho Kikwete,Benjamin William Mkapa na David Cleopa Msuya.

Nitafafanua kama ifuatavyo kabla ya kuendelea na "episode" ya leo:

Kwanza kwa manufaa ya wote ambao hawafahamu hili suala la Benjamin William Mkapa kuwa bosi wa Bernard Kamilius Membe akiwa ubalozini nchini Canada iko hivi:

Benjamin William Mkapa ana historia ya kuwa waziri wa mambo ya nje mara mbili.

Kwanza aliteuliwa uwaziri wa mambo ya nje mwaka 1977-1980 kisha akabadilishwa wizara hadi mwaka 1984-1990 aliporejeshwa tena wizara ya mambo ya nje.

Hoja ya ubosi wa Benjamin William Mkapa kwa Bernard Kamilius Membe inakuwa na mashiko kwasababu kuna kipindi Bernard Kamilius Membe alikuwa mshauri wa masuala ya usalama(wa ndani na nje)wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Na ndio huo wakati Benjamin William Mkapa alikuwa waziri wa mambo ya nje na kupelekea kufanya kazi kwa karibu na Bernard Kamilius Membe.

Kuhusu suala la majina ya walioingia kwenye tatu bora mwaka 1995 ni ukweli walikuwa Jakaya Mrisho Kikwete,Benjamin William Mkapa na David Cleopa Msuya.Mimi hawa wote niliwataja katika "episode" iliyopita kuwa walichukua fomu na waligombea.Japo ni ukweli sikuwataja kama waliingia tatu bora lakini sio kwa makusudi bali nilijikita kwenye kuonesha kuwa ushindani mkubwa ulikuwa ni kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Benjamin William Mkapa.

Baada ya kufafanua hayo basi naomba sasa nirejee kwenye dhima kuu ya "episode" ya leo.

Leo nitazungumzia juu ya maneno yaliyosikika sana miaka kadhaa nyuma kuhusu kuwepo undugu wa damu baina ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe.Maneno haya yalishika kasi kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2013-2015 na hata baada ya hapo hadi leo wapo wanaoamini juu ya maneno haya.

Nini msingi mkuu wa maneno haya?Ni siasa au kutojua chimbuko la Bernard Kamilius Membe?Mimi nitasaidia majibu.Msingi mkuu wa maneno haya ni siasa na kutokujua chimbuko la Bernard Kamilius Membe.Vyote vinaenda pamoja.

Nitaanza na sababu ya kwanza ambayo ni siasa:

Kama mjuavyo Bernard Kamilius Membe ana hulka ya ukimya.Ukimya huu ni wa tabia yake halisi lakini pia imechangiwa zaidi na kazi yake katika "ofisi nyeti" ambayo usiri na ukimya ni sehemu ya maisha ya kila siku ya mtumishi wa ofisi hiyo.

Hii ilipelekea watu wengi hata wale walio karibu na yeye kuanzia 2000-2012 kutoelewa kama alikuwa na wazo la kugombea urais.Hakuweka wazi mipango yake kwasababu bado aliamini katika kujipima na kutekeleza majukumu aliyoaminiwa na bosi wake(Jakaya Mrisho Kikwete).

Ilipofika mwaka 2012 wakati wa uchaguzi wa ndani CCM ndipo kundi kubwa la kumpinga Bernard Kamilius Membe liliibuka likiongozwa na mwanasiasa kijana Hussein Bashe ambaye kwasasa ndio Naibu Waziri wa kilimo na mbunge wa Nzega Mjini.Hussein Bashe alikuwa mtekelezaji wa mkakati wa "Godfathers" wake ambao ni Edward Ngoyai Lowassa na Rostam Abdulrasool Aziz.

Kwanini hawa walimkamia sana Bernard Kamilius Membe asishinde uchaguzi wa ndani mwaka 2012!?Jibu ni kwamba walitaka kuvunja historia ya rais wa nchi kutokea wizara ya mambo ya nje lakini kama ilivyokuwa kwa Jayaka Mrisho Kikwete na Benjamin William Mkapa.Sababu ya pili ni sakata la Richmond lililomwondoa Edward Ngoyai Lowassa katika uwaziri mkuu.Sababu ya tatu ni hoja ya kuvua gamba ya CCM.Katika "episodes" zijazo nitaelezea sababu hizi tatu kwanini mahasimu wa Bernard Kamilius Membe walizitumia kama "payback" kwake katika kummaliza kisiasa.Waliposhindwa ndio wakaibuka na hoja ya undugu wake wa damu na Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika suala la pili lilipolekea watu kuaminishwa kuwa yeye ana undugu wa damu na Jakaya Mrisho Kikwete ni kutokujulikana haswa kwa chimbuko lake.Ndio maana hapo mwanzo katika "episode" hii nilitaja kuwa suala la siasa na hili la kutojulikana haswa kwa chimbuko lake.

Kuhusu chimbuko lake ni kwamba Bernard Kamilius Membe ni mtu wa Kusini.Kabila lake ni Mmwera wanaotokea mkoa wa Lindi.Kijijini kwao panaitwa Rondo.Tarafa yao inaitwa Chiponda.

Ni mtoto wa pili kati ya watoto saba kwa baba Anthony Ntachile na mama Cecilia Membe.Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Roman Katoliki.

Kaka yake mkubwa ambaye kwasasa ni marehemu aliitwa Simon,mdogo wake anayemfuatia ambaye naye ni marehemu aliitwa Ester-huyu kama Bernard na yeye alikuwa mwanasiasa na hadi umauti unamfika alikuwa Diwani wa viti maalum wa CCM kata ya Mbagala.Wadogo zake wengine ni Consolatha aishiye mkoani Tanga,Steven aishiye nchini Canada,Tasilo na Castro waishio mkoani Lindi.

Mnaweza kujiuliza ni kwanini anatumia ubini wa Membe na sio Ntachile!?Hii sio tu kwake bali ni kwa Wamwera wote.Ni utamaduni wa Wamwera kutumia majina yenye ubini wa mama zao.Hakuna Mmwera duniani anayetumia ubini wa baba yake.Labda tu pale inapotokea mama ni wa kabila lingine ndio mtoto hutumia jina la baba yake ambaye ni Mmwera.

Ndio maana watoto wake(Bernard Kamilius Membe)wanatumia ubini wake.Ni kwasababu mama yao ni mwenyeji wa mkoani Ruvuma wilaya ya Nyasa kwahiyo hana chimbuko la umwerani.

Bernard Kamilius Membe ana ndoa takatifu na mkewe Dorcas Richard.Wamebarikiwa watoto watatu ambao ni Cecilia Bernard Membe(mwenye shahada ya uzamili kwenye fani ya mawasiliano),Richard Bernard Membe(mwenye shahada ya masuala ya kompyuta)na Denis Bernard Kamilius Membe(anayesubiri kufanya mitihani yake ya kidato cha nne mwaka huu).

Bernard Kamilius Membe kama alivyokuwa Edward Ngoyai Lowassa na alivyo Balozi mstaafu Jaka Ng'wabi Mwambi kwa Jakaya Kikwete naye ni rafiki mkubwa wa Jakaya Mrisho Kikwete.Urafiki wao ulianzia miaka ya 1970s wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mtumishi wa CCM ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania mkoani Arusha kwenye chuo cha Monduli.

Chimbuko la urafiki wao lilitokana na masuala ya kikazi.Ambapo kuna wakati jeshini kulikuwa na matatizo baina ya Mkuu wa Chuo cha Monduli(jina nalihifadhi) na Jakaya Mrisho Kikwete.Msuguano wao ulipelekea Mkuu wa Chuo cha Monduli kuandika taarifa mbaya dhidi ya Jakaya Mrisho Kikwete na kuiwasilisha Ikulu.

Wakati huo rais wa nchi ni Mwl.Julius Kambarage Nyerere.Baada ya kuipata na kuisoma taarifa ile Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliagiza timu ya watu kadhaa kwenda mkoani Arusha katika Chuo cha Monduli ili kufanya uchunguzi juu ya yale yanayosomeka ndani ya taarifa ile dhidi ya Jakaya Mrisho Kikwete.

Timu hiyo ilikuwa ya watu kutoka katika "ofisi nyeti" lakini Bernard Kamilius Membe hakuwepo miongoni mwao.Mkuu wa Chuo cha Monduli alijua ujio wa timu ile lakini mlalamikiwa Jakaya Mrisho Kikwete hakujua uwepo wa taarifa mbaya dhidi yake wala uwepo wa timu ya watu kutoka Dar es salaam walioagizwa na Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuchunguza yaliyomo kwenye taarifa hiyo.

Kosa la kiufundi lililofanyika na timu ile pengine kwa kujua au kutokujua ni kusikiliza upande mmoja(mtoa tuhuma na mwandishi wa taarifa)na kutosikiliza na upande unaolalamikiwa katika ile taarifa kisha nao wakaandaa taarifa yao na kuiwasilisha Ikulu kwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuisoma taarifa ya timu aliyoituma hakuridhika nayo.Akafanya maamuzi ya kumtuma Bernard Kamilius Membe tena akiwa peke yake kwenda mkoani Arusha katika Chuo cha Monduli ili kufanya uchunguzi upya na kumpelekea taarifa.

Mwl.Julius Kambarage Nyerere alichukua maamuzi hayo kwasababu kuu mbili.Kwanza Bernard Kamilius Membe alikuwa ni mmoja kati ya wahitimu bora wa mafunzo(kozi)ya shughuli za "ofisi nyeti" katika "intake" yao lakini pia alikuwa hana muda mrefu tangu atoke nchini Uingereza katika kozi na mafunzo maalum yaliyoendeshwa na shirika la ujasusi la Scotland Yard.

Baada ya Bernard Kamilius Membe kuwasili mkoani Arusha alifanya utaratibu wa kufika na kuongea na Mkuu wa Chuo cha Monduli na kufanya uchunguzi wake kutokana na njia alizozijua yeye mwenyewe na baada ya kukusanya taarifa alimtafuta na Jakaya Mrisho Kikwete na kuzungumza naye na kupata taarifa aliyoitaka.Sio Mkuu wa Chuo Cha Monduli au Jakaya Mrisho Kikwete mwenyewe aliyejua kama Bernard Kamilius Membe kaonana na wote.Alionana nao wote maeneo tofauti na mida tofauti na siku tofauti.Kazi yake haikuacha alama ya kujulikana kwa yeyote yule baina ya Mkuu wa Chuo Cha Monduli au Jakaya Mrisho Kikwete.

Kilichomshangaza Jakaya Mrisho Kikwete ni uwepo wa masuala ambayo ni mageni masikioni mwake.Lakini Mkuu wa Chuo cha Monduli yale masuala hayakuwa mageni kwake ila tu hakujua kama Jakaya Mrisho Kikwete atafikiwa na Bernard Kamilius Membe.Aliamini ingekuwa kama mwanzo.

Na huu ndio ukawa mwanzo mkuu wa mahusiano ya karibu kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe na mawasiliano baina yao yakawa makubwa sana hata baada ya Bernard Kamilius Membe kurejea Dar es salaam.

Alipowasili jijini Dar es salaam Bernard Kamilius Membe aliandika taarifa yake na kuiwasilisha Ikulu kwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kama ilivyopaswa.Moja ya maamuzi ya kukumbukwa yaliyotokana na taarifa hii iliyoandaliwa na Bernard Kamilius Membe ni uamuzi wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kutenganisha shughuli za kijeshi na kisiasa.Na ndio ukawa mwanzo mzuri kwa Jakaya Mrisho Kikwete kuacha jeshi,kuingia mazima katika siasa na kutimiza ndoto zake kuanzia nafasi za utumishi wa chama hadi urais wa nchi.

Hakukuwa,hakujawahi kuwa na hakuna uhusiano wa kidamu kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe.Mmoja ni Mkwere wa Pwani na mwingine ni Mmwera wa Lindi.Urafiki wao ulipelekea wao kuishi kama familia tangu miaka ile hadi leo hii.Kila mmoja ana mchango mkubwa katika maisha ya mwenzake.

Kwa wasiojua ni kwamba hata siku Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara ya kwanza anateuliwa kuwa mbunge alikuwa Dar es salaam kikazi(kazi za chama)na alifikia Sea View nyumbani kwa Bernard Kamilius Membe mahali ambapo alikuwa akifikia kila anapokuja Dar es salaam kikazi.Na hata alipotaka kwenda Chalinze kuwasalimia wazazi na ndugu zake alitumia gari ya Bernard Kamilius Membe.

Huu ndio ukweli kuhusu mahusiano ya hawa maswahiba wawili.Kwa undani zaidi itaelezewa vizuri katika kitabu cha Bernard Kamilius Membe kiitwacho "This is my profile" ambacho kitakuwa katika lugha ya kiingereza na kiswahili.

"Episode" ijayo nitaelezea kwa ufupi mambo kumi ya kipekee usiyoyajua kuhusu Bernard Kamilius Membe.

Tukutane tena kesho muda kama huu.......
 
mwakajingatky

JF-Expert Member
May 30, 2018
552
1,000

Ngoja nikufollow mkuu...

By the way,una uhusiano gani na membe? (sababu unavijua vitu vingi harafu vya ndani)

Harafu pia huyo mkuu wa jeshi,monduli si amewahi kuwa katibu mkuu wa ccm?
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,005
2,000
Umeandika, ''Na huu ndio ukawa mwanzo mkuu wa mahusiano ya karibu kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe na mawasiliano baina yao yakawa makubwa sana hata baada ya Bernard Kamilius Membe kurejea Dar es salaam''.

Kama ulichokiandika ni kweli basi hii paragraph yako pamoja na kwanza umeandika ili kuonyesha ukaribu wa Mzee Kikwete na Bernard Membe ulivyoanza lakini ambacho umekiibua kinaonyesha kazi aliyoifanya Membe ilikuwa na dosari kwa sababu huwezi kwenda kutafuta ukweli kwa mshukiwa wa jambo fulani halafu hapo hapo mkaanza urafiki wa kudumu. Hili ni kosa kubwa katika kazi za upelelezi (prefessional ethics).

Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa alichofanya Membe ni kwenda kumueleza/kumtonya Mzee Kikwete kilichofanyika nyuma yake na nani alichokifanya dhidi yake. Kwa maana nyingine hakwenda kutafuta ukweli bali alienda ''kumtonya'' kinachoendelea na awe makini ndio maana wakawa ''marafiki wa karibu'' baada ya ulichokisema Membe kuandika repoti chanya kwa upande wa Kikwete!

Makosa kama haya aliyofanya Membe ya kujenga urafiki wa kudumu na mtuhumiwa ambaye hakupaswa hata ajue unafanya nini yanaonekana ni madogo lakini kwenye fani ya usalama ni makosa makubwa sana ambayo yanamwondolea sifa ya kuwa mwajiriwa wa kitengo cha usalama!

Unanikumbusha tukio moja nchini uingereza ambao mpelelezi alitumwa kwenda kumpeleleza mama mmoja lakini wakati anafanya kazi hiyo wakawa marafiki wa karibu mpaka wakawa wanafanya mapenzi. Baadaye alimaliza kazi yake ya kumpeleleza na kukabidhi kwa maofisa waliomtuma. Yule mama baadaye alikamatwa na kupelekwa mahakamani lakini kesi ilipoanza ikagundulika kuwa alichikifanya ni kinyume cha maadili ya kazi na kesi ikatupiliwa mbali.

Baada ya wakuu wake wa kazi kugundua mahakamani mfanyakazi wao (mpelelezi)) alikuwa anafanya mpaka mapenzi na mtuhumiwa, waliamua kumfukuza kazi kwa sababu alichokifanya ni kinyume na misingi ya kazi (code of ethics).
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,526
2,000
Safi sana mleta mada.

Jiwe kasamehe Trilion 424 tulizoibiwa na ACACIA kwenye madini yetu, pesa anbazo zingeweza kujenga SGR zaidi ya 10, na kupiga lami barabara za wilaya zote, kujenga Vyuo vya ufundi kila wilaya nchini na kujenga hospitali za rufaa za hadhi ya Muhimbili kila mkoa nchini na chenji nyingi tu ikabaki!

2020 Twende na Membe, Jasusi mwenye uchungu na nchi kama yeye hawezi kufanya kosa kama hilo!
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
2,479
2,000
Umeandika, ''Na huu ndio ukawa mwanzo mkuu wa mahusiano ya karibu kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe na mawasiliano baina yao yakawa makubwa sana hata baada ya Bernard Kamilius Membe kurejea Dar es salaam''.

Kama ulichokiandika ni kweli basi hii paragraph yako pamoja na kwanza umeandika ili kuonyesha ukaribu wa Mzee Kikwete na Bernard Membe ulivyoanza lakini ambacho umekiibua kinaonyesha kazi aliyoifanya Membe ilikuwa na dosari kwa sababu huwezi kwenda kutafuta ukweli kwa mshukiwa wa jambo fulani halafu hapo hapo mkaanza urafiki wa kudumu. Hili ni kosa kubwa katika kazi za upelelezi (prefessional ethics).

Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa alichofanya Membe ni kwenda kumueleza/kumtonya Mzee Kikwete kilichofanyika nyuma yake na nani alichokifanya dhidi yake. Kwa maana nyingine hakwenda kutafuta ukweli bali alienda ''kumtonya'' kinachoendelea na awe makini ndio maana wakawa ''marafiki wa karibu'' baada ya ulichokisema Membe kuandika repoti chanya kwa upande wa Kikwete!

Makosa kama haya aliyofanya Membe ya kujenga urafiki wa kudumu na mtuhumiwa ambaye hakupaswa hata ajue unafanya nini yanaonekana ni madogo lakini kwenye fani ya usalama ni makosa makubwa sana ambayo yanamwondolea sifa ya kuwa mwajiriwa wa kitengo cha usalama!
mkuu hii ni hoja na tuna haki ya kuijadili ,na majadiliano haya yatawaliwe na FACTS sio mihemko,msome vizuri ili kumwelewa mtoa hoja,HAKUONGEA NA JK ili kumtonya,aliongea naye ili kupata his side of story,ni lazima tuelewe kuna TWO sides of any story,kwa hiyo mchunguzi alipoondoka Arusha alikuwa tayari ana two sides of story,akaandika ripoti yake na mapendekezo yake ILA ni RAIS tu ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuamua,don't shot the messenger pls.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,005
2,000
mkuu hii ni hoja na tuna haki ya kuijadili ,na majadiliano haya yatawaliwe na FACTS sio mihemko,msome vizuri ili kumwelewa mtoa hoja,HAKUONGEA NA JK ili kumtonya,aliongea naye ili kupata his side of story,ni lazima tuelewe kuna TWO sides of any story,kwa hiyo mchunguzi alipoondoka Arusha alikuwa tayari ana two sides of story,akaandika ripoti yake na mapendekezo yake ILA ni RAIS tu ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuamua,don't shot the messenger pls.
Mkuu;
Rais Nyerere hakumtuma ili kwenda kutafuta marafiki bali alimtuma ili kufanya kazi tena ya SIRI bila mtuhumiwa/watuhumiwa kujua. Hii siyo kazi kama mtu anayenda kutafuta wateja wa biashara!

Kwa nini unadhani Membe hakuanzisha urafiki wa karibu pia na upande wa pili (Mkuu wa chuo)? Kwa nini wakawa marafiki wa karibu baada tu ya Membe kurudi Dar es Salaam?

Jaribu kuangalia hili suala kwa upana zaidi na sio kujikita kwenye dhumuni la mada pekee!

Kitendo hiki alichokifanya Membe alipaswa kuchukuliwa hatua za kinidhani kwa kosa la code of ethics.
 
aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,100
2,000
Kuna vitu unajitajidi ila vingins haupo sahihi ama ulipewa habari kwa kukwepesha mambo fulani
Siasa jeshini hajatenganisha nyerere amekuja kutenganisha rais mwinyi kama unakumbukumbu mwaka 1992 ndipo lilifanyika gwaride rasmi la kuwaaga walioamua kufuata upande wa siasa na kitoka kwenye jeshi (picha ya kikwete na kinana wakiwa na vazi lajeshi)
 
Adili

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
3,142
2,000
mkuu hii ni hoja na tuna haki ya kuijadili ,na majadiliano haya yatawaliwe na FACTS sio mihemko,msome vizuri ili kumwelewa mtoa hoja,HAKUONGEA NA JK ili kumtonya,aliongea naye ili kupata his side of story,ni lazima tuelewe kuna TWO sides of any story,kwa hiyo mchunguzi alipoondoka Arusha alikuwa tayari ana two sides of story,akaandika ripoti yake na mapendekezo yake ILA ni RAIS tu ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuamua,don't shot the messenger pls.
"Shoot"
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
9,525
2,000
Mkuu;
Rais Nyerere hakumtuma ili kwenda kutafuta marafiki bali alimtuma ili kufanya kazi tena ya SIRI bila mtuhumiwa/watuhumiwa kujua. Hii siyo kazi kama mtu anayenda kutafuta wateja wa biashara!

Kwa nini unadhani Membe hakuanzisha urafiki wa karibu pia na upande wa pili (Mkuu wa chuo)? Kwa nini wakawa marafiki wa karibu baada tu ya Membe kurudi Dar es Salaam?

Jaribu kuangalia hili suala kwa upana zaidi na sio kujikita kwenye dhumuni la mada pekee!

Kitendo hiki alichokifanya Membe alipaswa kuchukuliwa hatua za kinidhani kwa kosa la code of ethics.

Mkuu kitu ninachokiona kuna mahala labda hukuelewa..
Wapelelezi wa kwanza walihoji upande mmoja, Membe alihoji pande mbili. Wale wamwanzo hawakutenda haki kwa JK ndio maana JKN alimtuma Membe ilikubalance story.. Urafiki ulikuja baadaye baada ya JK kugundua Membe alimtendea haki( hata ungekuwa wewe ungefanya hivyo kwa mtu aliyekuwa mwema na kutenda haki kwako, waliokwenda mwanzo hawakutenda haki nafikiri JK alivyojua baadaye ndio urafiki ukaja hapo)
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,767
2,000
Safi sana mleta mada.

Jiwe kasamehe Trilion 424 tulizoibiwa na ACACIA kwenye madini yetu, pesa anbazo zingeweza kujenga SGR zaidi ya 10, na kupiga lami barabara za wilaya zote, kujenga Vyuo vya ufundi kila wilaya nchini na kujenga hospitali za rufaa za hadhi ya Muhimbili kila mkoa nchini na chenji nyingi tu ikabaki!

2020 Twende na Membe, Jasusi mwenye uchungu na nchi kama yeye hawezi kufanya kosa kama hilo!
Ohoooo !!!
 
jnhiggins

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
1,622
2,000
bila shaka mwandishi ni Benard Membe, mzee tuondolee balaa hili mlilotuletea 2015, pia usijekutugeuka pindi utakapokalia kiti cha ufalme,
uguswe unuke!
Mwandishi sio Bernard Membe, ila ni mtu ambaye anamfahamu Membe au walifanyakazi pamoja. Kwasababu angekuwa ni Membe ndio mwandishi basi hizi habari za Monduli ambazo ni kweli, angeziweka vizuri sana na pia kuna mambo ambayo mwandishi hayajui vizuri
 
Ukana Shilungo

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
2,968
2,000
JE KIKWETE NA MEMBE NI NDUGU WA KUZALIWA TUMBO MOJA?

Nichukue fursa hii kuwashukuru wasomaji,wakosoaji,wauliza maswali na watoa maoni wote wa jukwaa hili kwa kila ninachoandika na kukiweka humu.

Ikumbukwe kwamba dhumuni kuu la simulizi hizi ni kuwajulisha watu juu ya wasifu au historia ya mwanasiasa nguli Bernard Kamilius Membe.Ambayo kwa pengine sio kila mtu anaijua au anamjua vilivyo mwanasiasa huyu.

Ndio maana katika simulizi hizi nikaamua kuzipa jina "series" ambayo itabebwa na "episodes" tofauti zenye kuelezea matukio muhimu ambayo yana mvuto wa kipekee katika safari yake ya utumishi wa umma na kisiasa pia.

Katika "episode" iliyopita ambayo ilielezea kuhusu "wanamtandao" niliona baadhi ya wasomaji wakihoji kuhusu masuala kadhaa ambayo hawakuyaelewa au pengine labda sikuyaweka.

Nitatoa ufafanuzi katika masuala mawili yaliyojitokeza ambayo moja sikueleweka nilimaanisha nini niliposema kwamba Benjamin William Mkapa alikuwa kuwa bosi wa Bernard Kamilus Membe wakati akihamia katika ubalozi wetu nchini Canada na lingine nilikumbushwa kuwa walioingia tatu bora kwenye kura za maoni walikuwa ni Jakaya Mrisho Kikwete,Benjamin William Mkapa na David Cleopa Msuya.

Nitafafanua kama ifuatavyo kabla ya kuendelea na "episode" ya leo:

Kwanza kwa manufaa ya wote ambao hawafahamu hili suala la Benjamin William Mkapa kuwa bosi wa Bernard Kamilius Membe akiwa ubalozini nchini Canada iko hivi:

Benjamin William Mkapa ana historia ya kuwa waziri wa mambo ya nje mara mbili.

Kwanza aliteuliwa uwaziri wa mambo ya nje mwaka 1977-1980 kisha akabadilishwa wizara hadi mwaka 1984-1990 aliporejeshwa tena wizara ya mambo ya nje.

Hoja ya ubosi wa Benjamin William Mkapa kwa Bernard Kamilius Membe inakuwa na mashiko kwasababu kuna kipindi Bernard Kamilius Membe alikuwa mshauri wa masuala ya usalama(wa ndani na nje)wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Na ndio huo wakati Benjamin William Mkapa alikuwa waziri wa mambo ya nje na kupelekea kufanya kazi kwa karibu na Bernard Kamilius Membe.

Kuhusu suala la majina ya walioingia kwenye tatu bora mwaka 1995 ni ukweli walikuwa Jakaya Mrisho Kikwete,Benjamin William Mkapa na David Cleopa Msuya.Mimi hawa wote niliwataja katika "episode" iliyopita kuwa walichukua fomu na waligombea.Japo ni ukweli sikuwataja kama waliingia tatu bora lakini sio kwa makusudi bali nilijikita kwenye kuonesha kuwa ushindani mkubwa ulikuwa ni kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Benjamin William Mkapa.

Baada ya kufafanua hayo basi naomba sasa nirejee kwenye dhima kuu ya "episode" ya leo.

Leo nitazungumzia juu ya maneno yaliyosikika sana miaka kadhaa nyuma kuhusu kuwepo undugu wa damu baina ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe.Maneno haya yalishika kasi kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2013-2015 na hata baada ya hapo hadi leo wapo wanaoamini juu ya maneno haya.

Nini msingi mkuu wa maneno haya?Ni siasa au kutojua chimbuko la Bernard Kamilius Membe?Mimi nitasaidia majibu.Msingi mkuu wa maneno haya ni siasa na kutokujua chimbuko la Bernard Kamilius Membe.Vyote vinaenda pamoja.

Nitaanza na sababu ya kwanza ambayo ni siasa:

Kama mjuavyo Bernard Kamilius Membe ana hulka ya ukimya.Ukimya huu ni wa tabia yake halisi lakini pia imechangiwa zaidi na kazi yake katika "ofisi nyeti" ambayo usiri na ukimya ni sehemu ya maisha ya kila siku ya mtumishi wa ofisi hiyo.

Hii ilipelekea watu wengi hata wale walio karibu na yeye kuanzia 2000-2012 kutoelewa kama alikuwa na wazo la kugombea urais.Hakuweka wazi mipango yake kwasababu bado aliamini katika kujipima na kutekeleza majukumu aliyoaminiwa na bosi wake(Jakaya Mrisho Kikwete).

Ilipofika mwaka 2012 wakati wa uchaguzi wa ndani CCM ndipo kundi kubwa la kumpinga Bernard Kamilius Membe liliibuka likiongozwa na mwanasiasa kijana Hussein Bashe ambaye kwasasa ndio Naibu Waziri wa kilimo na mbunge wa Nzega Mjini.Hussein Bashe alikuwa mtekelezaji wa mkakati wa "Godfathers" wake ambao ni Edward Ngoyai Lowassa na Rostam Abdulrasool Aziz.

Kwanini hawa walimkamia sana Bernard Kamilius Membe asishinde uchaguzi wa ndani mwaka 2012!?Jibu ni kwamba walitaka kuvunja historia ya rais wa nchi kutokea wizara ya mambo ya nje lakini kama ilivyokuwa kwa Jayaka Mrisho Kikwete na Benjamin William Mkapa.Sababu ya pili ni sakata la Richmond lililomwondoa Edward Ngoyai Lowassa katika uwaziri mkuu.Sababu ya tatu ni hoja ya kuvua gamba ya CCM.Katika "episodes" zijazo nitaelezea sababu hizi tatu kwanini mahasimu wa Bernard Kamilius Membe walizitumia kama "payback" kwake katika kummaliza kisiasa.Waliposhindwa ndio wakaibuka na hoja ya undugu wake wa damu na Jakaya Mrisho Kikwete.

Katika suala la pili lilipolekea watu kuaminishwa kuwa yeye ana undugu wa damu na Jakaya Mrisho Kikwete ni kutokujulikana haswa kwa chimbuko lake.Ndio maana hapo mwanzo katika "episode" hii nilitaja kuwa suala la siasa na hili la kutojulikana haswa kwa chimbuko lake.

Kuhusu chimbuko lake ni kwamba Bernard Kamilius Membe ni mtu wa Kusini.Kabila lake ni Mmwera wanaotokea mkoa wa Lindi.Kijijini kwao panaitwa Rondo.Tarafa yao inaitwa Chiponda.

Ni mtoto wa pili kati ya watoto saba kwa baba Anthony Ntachile na mama Cecilia Membe.Dini yake ni mkristo wa dhehebu la Roman Katoliki.

Kaka yake mkubwa ambaye kwasasa ni marehemu aliitwa Simon,mdogo wake anayemfuatia ambaye naye ni marehemu aliitwa Ester-huyu kama Bernard na yeye alikuwa mwanasiasa na hadi umauti unamfika alikuwa Diwani wa viti maalum wa CCM kata ya Mbagala.Wadogo zake wengine ni Consolatha aishiye mkoani Tanga,Steven aishiye nchini Canada,Tasilo na Castro waishio mkoani Lindi.

Mnaweza kujiuliza ni kwanini anatumia ubini wa Membe na sio Ntachile!?Hii sio tu kwake bali ni kwa Wamwera wote.Ni utamaduni wa Wamwera kutumia majina yenye ubini wa mama zao.Hakuna Mmwera duniani anayetumia ubini wa baba yake.Labda tu pale inapotokea mama ni wa kabila lingine ndio mtoto hutumia jina la baba yake ambaye ni Mmwera.

Ndio maana watoto wake(Bernard Kamilius Membe)wanatumia ubini wake.Ni kwasababu mama yao ni mwenyeji wa mkoani Ruvuma wilaya ya Nyasa kwahiyo hana chimbuko la umwerani.

Bernard Kamilius Membe ana ndoa takatifu na mkewe Dorcas Richard.Wamebarikiwa watoto watatu ambao ni Cecilia Bernard Membe(mwenye shahada ya uzamili kwenye fani ya mawasiliano),Richard Bernard Membe(mwenye shahada ya masuala ya kompyuta)na Denis Bernard Kamilius Membe(anayesubiri kufanya mitihani yake ya kidato cha nne mwaka huu).

Bernard Kamilius Membe kama alivyokuwa Edward Ngoyai Lowassa na alivyo Balozi mstaafu Jaka Ng'wabi Mwambi kwa Jakaya Kikwete naye ni rafiki mkubwa wa Jakaya Mrisho Kikwete.Urafiki wao ulianzia miaka ya 1970s wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mtumishi wa CCM ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania mkoani Arusha kwenye chuo cha Monduli.

Chimbuko la urafiki wao lilitokana na masuala ya kikazi.Ambapo kuna wakati jeshini kulikuwa na matatizo baina ya Mkuu wa Chuo cha Monduli(jina nalihifadhi) na Jakaya Mrisho Kikwete.Msuguano wao ulipelekea Mkuu wa Chuo cha Monduli kuandika taarifa mbaya dhidi ya Jakaya Mrisho Kikwete na kuiwasilisha Ikulu.

Wakati huo rais wa nchi ni Mwl.Julius Kambarage Nyerere.Baada ya kuipata na kuisoma taarifa ile Mwl.Julius Kambarage Nyerere aliagiza timu ya watu kadhaa kwenda mkoani Arusha katika Chuo cha Monduli ili kufanya uchunguzi juu ya yale yanayosomeka ndani ya taarifa ile dhidi ya Jakaya Mrisho Kikwete.

Timu hiyo ilikuwa ya watu kutoka katika "ofisi nyeti" lakini Bernard Kamilius Membe hakuwepo miongoni mwao.Mkuu wa Chuo cha Monduli alijua ujio wa timu ile lakini mlalamikiwa Jakaya Mrisho Kikwete hakujua uwepo wa taarifa mbaya dhidi yake wala uwepo wa timu ya watu kutoka Dar es salaam walioagizwa na Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuchunguza yaliyomo kwenye taarifa hiyo.

Kosa la kiufundi lililofanyika na timu ile pengine kwa kujua au kutokujua ni kusikiliza upande mmoja(mtoa tuhuma na mwandishi wa taarifa)na kutosikiliza na upande unaolalamikiwa katika ile taarifa kisha nao wakaandaa taarifa yao na kuiwasilisha Ikulu kwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Baada ya Mwl.Julius Kambarage Nyerere kuisoma taarifa ya timu aliyoituma hakuridhika nayo.Akafanya maamuzi ya kumtuma Bernard Kamilius Membe tena akiwa peke yake kwenda mkoani Arusha katika Chuo cha Monduli ili kufanya uchunguzi upya na kumpelekea taarifa.

Mwl.Julius Kambarage Nyerere alichukua maamuzi hayo kwasababu kuu mbili.Kwanza Bernard Kamilius Membe alikuwa ni mmoja kati ya wahitimu bora wa mafunzo(kozi)ya shughuli za "ofisi nyeti" katika "intake" yao lakini pia alikuwa hana muda mrefu tangu atoke nchini Uingereza katika kozi na mafunzo maalum yaliyoendeshwa na shirika la ujasusi la Scotland Yard.

Baada ya Bernard Kamilius Membe kuwasili mkoani Arusha alifanya utaratibu wa kufika na kuongea na Mkuu wa Chuo cha Monduli na kufanya uchunguzi wake kutokana na njia alizozijua yeye mwenyewe na baada ya kukusanya taarifa alimtafuta na Jakaya Mrisho Kikwete na kuzungumza naye na kupata taarifa aliyoitaka.Sio Mkuu wa Chuo Cha Monduli au Jakaya Mrisho Kikwete mwenyewe aliyejua kama Bernard Kamilius Membe kaonana na wote.Alionana nao wote maeneo tofauti na mida tofauti na siku tofauti.Kazi yake haikuacha alama ya kujulikana kwa yeyote yule baina ya Mkuu wa Chuo Cha Monduli au Jakaya Mrisho Kikwete.

Kilichomshangaza Jakaya Mrisho Kikwete ni uwepo wa masuala ambayo ni mageni masikioni mwake.Lakini Mkuu wa Chuo cha Monduli yale masuala hayakuwa mageni kwake ila tu hakujua kama Jakaya Mrisho Kikwete atafikiwa na Bernard Kamilius Membe.Aliamini ingekuwa kama mwanzo.

Na huu ndio ukawa mwanzo mkuu wa mahusiano ya karibu kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe na mawasiliano baina yao yakawa makubwa sana hata baada ya Bernard Kamilius Membe kurejea Dar es salaam.

Alipowasili jijini Dar es salaam Bernard Kamilius Membe aliandika taarifa yake na kuiwasilisha Ikulu kwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kama ilivyopaswa.Moja ya maamuzi ya kukumbukwa yaliyotokana na taarifa hii iliyoandaliwa na Bernard Kamilius Membe ni uamuzi wa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kutenganisha shughuli za kijeshi na kisiasa.Na ndio ukawa mwanzo mzuri kwa Jakaya Mrisho Kikwete kuacha jeshi,kuingia mazima katika siasa na kutimiza ndoto zake kuanzia nafasi za utumishi wa chama hadi urais wa nchi.

Hakukuwa,hakujawahi kuwa na hakuna uhusiano wa kidamu kati ya Jakaya Mrisho Kikwete na Bernard Kamilius Membe.Mmoja ni Mkwere wa Pwani na mwingine ni Mmwera wa Lindi.Urafiki wao ulipelekea wao kuishi kama familia tangu miaka ile hadi leo hii.Kila mmoja ana mchango mkubwa katika maisha ya mwenzake.

Kwa wasiojua ni kwamba hata siku Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara ya kwanza anateuliwa kuwa mbunge alikuwa Dar es salaam kikazi(kazi za chama)na alifikia Sea View nyumbani kwa Bernard Kamilius Membe mahali ambapo alikuwa akifikia kila anapokuja Dar es salaam kikazi.Na hata alipotaka kwenda Chalinze kuwasalimia wazazi na ndugu zake alitumia gari ya Bernard Kamilius Membe.

Huu ndio ukweli kuhusu mahusiano ya hawa maswahiba wawili.Kwa undani zaidi itaelezewa vizuri katika kitabu cha Bernard Kamilius Membe kiitwacho "This is my profile" ambacho kitakuwa katika lugha ya kiingereza na kiswahili.

"Episode" ijayo nitaelezea kwa ufupi mambo kumi ya kipekee usiyoyajua kuhusu Bernard Kamilius Membe.

Tukutane tena kesho muda kama huu.......
MKUU aksante kwa madini uliyoshusha!👏👏
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom