Kikwete alimtaja MAALIM Seif wa zenji kishabiki?

Mwana wa Mungu

JF-Expert Member
Aug 14, 2008
1,004
1,195
Jamani, naomba kuuliza kwa wale wanaofahamu maana halisi ya "MAALIM", kwasababu kwa wale waliomsikiliza kikwete, aliitaja hiyo Maalim kiushabiki fulani hivi sasa mimi sikumuelewa. sina maana mbaya lakini kutu kinachonifanya niwe na dukuduku lazima nikiseme...kwasababu kwa kuongea kauli ile, ilionyesha kama vile anafanya ushabiki wa kidini vile...kuna mtu aliisikia vizuri ile kauli jamani? ili tumrekebishe huyu Rais aliyepitishwa na ccm?
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,072
1,195
jamani, naomba kuuliza kwa wale wanaofahamu maana halisi ya "maalim", kwasababu kwa wale waliomsikiliza kikwete, aliitaja hiyo maalim kiushabiki fulani hivi sasa mimi sikumuelewa. Sina maana mbaya lakini kutu kinachonifanya niwe na dukuduku lazima nikiseme...kwasababu kwa kuongea kauli ile, ilionyesha kama vile anafanya ushabiki wa kidini vile...kuna mtu aliisikia vizuri ile kauli jamani? Ili tumrekebishe huyu rais aliyepitishwa na ccm?

sijui unachoongea hapa ni nini!!!!!!!
 
Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
0
Jamani, naomba kuuliza kwa wale wanaofahamu maana halisi ya "MAALIM", kwasababu kwa wale waliomsikiliza kikwete, aliitaja hiyo Maalim kiushabiki fulani hivi sasa mimi sikumuelewa. sina maana mbaya lakini kutu kinachonifanya niwe na dukuduku lazima nikiseme...kwasababu kwa kuongea kauli ile, ilionyesha kama vile anafanya ushabiki wa kidini vile...kuna mtu aliisikia vizuri ile kauli jamani? ili tumrekebishe huyu Rais aliyepitishwa na ccm?
Jirekebishe kwanza wewe na hizo hisia zako.
 
DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
195
Kwani hujui ni kazi yake kuhubiri udini? Ana uhubiri na kuutekeleza yeye ndiyo kinara -angekuwa siyo kinara si angeagiza rashidi shamte akamatwe aliyetumwa na riddhwan kutuma ujumbe wa udini -yeye ndio mdini hajaanza leo.
 
Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
0
Maalim kapewa shavu, wenzake wanakula UDUVI NA UROJO kwa kwenda mbele.

Hawa ni kama ile methali isemayo " waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba" lao moja muda ulikuwa haujafika tu.

Miaka hii mitano watatukamua kisawa sawa tukaze buti tu, maana ni mauaji ya taratibu haya tunakabiliana nayo.

Hao wanaoshabikia sisiemu sasa hivi utaona wanaanza kukunja sura zao muda si mrefu pale jua litakapozidi kuchoma hadi ktk mifupa.

Kuanzia sasa tutegemee yafuatayo:
1. mfumuko mkubwa wa bei za vitu na kupanda kwa gharama za maisha.
2. hali ya maisha kuendelea kudidimia siku hadi siku hasa kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini.
3. Kupanda kwa gharama za usafiri, umeme na maji na hata kodi za nyumba.
4. kupanda bei ya vinywaji na hasa bia ingawa idadi ya wanywaji itazidi kuongezeka siku hadi siku. n.k

Hayo ni machache tu yapo zaidi
 
Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,072
1,195
maalim kapewa shavu, wenzake wanakula uduvi na urojo kwa kwenda mbele.

Hawa ni kama ile methali isemayo " waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba" lao moja muda ulikuwa haujafika tu.

Miaka hii mitano watatukamua kisawa sawa tukaze buti tu, maana ni mauaji ya taratibu haya tunakabiliana nayo.

Hao wanaoshabikia sisiemu sasa hivi utaona wanaanza kukunja sura zao muda si mrefu pale jua litakapozidi kuchoma hadi ktk mifupa.

Kuanzia sasa tutegemee yafuatayo:
1. Mfumuko mkubwa wa bei za vitu na kupanda kwa gharama za maisha.
2. Hali ya maisha kuendelea kudidimia siku hadi siku hasa kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini.
3. Kupanda kwa gharama za usafiri, umeme na maji na hata kodi za nyumba.
4. Kupanda bei ya vinywaji na hasa bia ingawa idadi ya wanywaji itazidi kuongezeka siku hadi siku. N.k

hayo ni machache tu yapo zaidi

kama kupanda kwa bei ya pombe itasaidia watu kufa polepole, ni afadhali naipande maanake hatutaki taifa la walevi!!!!
 
junior2008

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
528
0
Jamani, naomba kuuliza kwa wale wanaofahamu maana halisi ya "MAALIM", kwasababu kwa wale waliomsikiliza kikwete, aliitaja hiyo Maalim kiushabiki fulani hivi sasa mimi sikumuelewa. sina maana mbaya lakini kutu kinachonifanya niwe na dukuduku lazima nikiseme...kwasababu kwa kuongea kauli ile, ilionyesha kama vile anafanya ushabiki wa kidini vile...kuna mtu aliisikia vizuri ile kauli jamani? ili tumrekebishe huyu Rais aliyepitishwa na ccm?

Mwana wa mungu unaweza kufafanua vizuri alitaja MAALIM wakati anaongelea nini? Usidhani kila mmoja alisikiliza kwahiyo tuhabarishe kidogo ili tuweze kuchangia labda kama unataka kujua maana tu ya neno MAALIM
 
Mtoto wa Kishua

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
834
225
JK kama alikua na ushabiki wa dini hilo sijui, ila kama Muislamu mpenda dini yake, lazima atakua anapenda watu wenye imani yake ,haswa ukizingatia amekuzwa kwa kuamini Usilamu ndio jibu la kufuka peponi, hapo sioni tatizo.

Kutajwa kwa Maalim Seif ,sidhani kama alikua analenga udini zaidi, nadhani alikua anapiga dogo kwa CHADEMa kwamba hata wakitoka nje na kumpinga, yeye teari ni raisi na wako pamoja na chama cha upinzani.

Viongozi wajuu wa serikali ya JK kuwa waislamu hilo na dhani halina udini, maana Ukiangalia isingewezekana kupata makamu wa raisi toka Zanzibar akawa Mkristo. kajaribu ku balance kwa kumteua waziri mkuu wa dini nyingine.
 
Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502

Kwani Zanzibar hakuna wakristo?
 
MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
0
Wakati wenzetu wanajadili na kutafuta njia za maendeleo, sisi bado tumekwama kwenye uislamu/ukristo, ubara/uzanzibari, upemba/uunguja, uchaga/unyamwezi, udodoma/U-mbeya, mpaka wapi?

Watanzania tuna matatizo, leo hii nimesoma habari moja baadhi ya Wazanzibari wanahisi kuchaguliwa Wazanzibari kwenye baraza la
Muungano kuna lengo la kuzidi kukandamiza Zanzibar, hapa kuna wenginge wanalalamika kuna Wazanzibari wengi katika baraza la Muungano, wakati wapo wengine wanalalamika kuwa kuna mikoa haikutoa waziri. Tutafikia wapi?

Ninaheshimu mawazo ya wengine, ninalowaomba Watanzania wenzangu, hasa hapa pahali pa "Great Thinkers", tujadili yale yakuliletea taifa maendeleo, mabadiliko na tuwachane na ushabiki wa vijiweni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom