Kikwete alienda Ujerumani lini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,541
40,173
Jamani, nasikia JK alikwenda ujerumani na kurudi kimya kimya... na zaidi alienda kuliona dege letu la Airbus, je ni kweli au ni tetesi mitaani.
 
naona watu wlilalamika sana kuhusu afari zake, sasa ikulu wameacha kuwambia watu kuhusu safari za raisi nje ya nchi
 
Nakumbuka mara ya mwisho, alikwenda kwa uchunguzi wa afya kama miezi sita iliyopita, kumbe ameenda tena karibuni?

Hizo zitakuwa habari mpya weka dataz mkuu, najua kuwa unazo ndio maana umeanza....!
 
vyanzo vyangu vinadokeza kuwa ijumaa alitimkia Ujerumani na kurudi mapema jana sijui ni kweli kiasi gani. Najua alikuwa aende kwenye ile ziara ndefu lakini akamuachia Karume
 
Mmezidi kumfuata fuata hivyo wameamua kutowaambia. Lakini kama wamefanya hivyo litawatokea puani.
 
Mwanakijiji,
Navyoelewa mimi ni kwamba alitakiwa kwenda Ujarumani lakini kawakilishwa na Karume kutokana na ujio wa Bush...
 
vyanzo vyangu vinadokeza kuwa ijumaa alitimkia Ujerumani na kurudi mapema jana sijui ni kweli kiasi gani. Najua alikuwa aende kwenye ile ziara ndefu lakini akamuachia Karume

Dar mpaka Ujerumani kwa kale kaG5 ni masaa mangapi? Alafu hiyo ndege iliondoka kwenye hangar lake au alitumia ndege ya kukodi
 
Hata mtu kama ana kasafari kake ka private mnataka muambiwe? mwishowe hata akienda msalani mtataka mjuwe, duhh.
 
Hata mtu kama ana kasafari kake ka private mnataka muambiwe? mwishowe hata akienda msalani mtataka mjuwe, duhh.

Safari gani hizo za private ambazo wananchi wa Tanzania hawastahili kuzijua!? hebu fafanua
 
Ni kweli alienda na Bush alilisema hilo kwenye dinner jana akamshukuru "For cutting short your trip in Germany"
sasa mbona vituko! Ameamua ku-sneak off? Huu ni utoto na unaonyesha that this prez is spineless. Kama anajua anachokifanya ni sahihi, basi angeenda waziwazi bila kuficha, badala ya kutoroka kama mwizi!
Na kwa wale ambao wanajaribu kumtetea, this was not a private visit of an individual , yeye ni prez of URTz kwa hiyo the people have a right to know prez wao yuko nchini au la. Sasa kaamka kaona u-Vasco da Gama ni mbaya sasa anataka kuleta usiri. Huyo mpambe wake Membe aliyekuwa anawani u-Vasco da gama sijui ana nini la kusema!?
 
ni Kweli Jamaa Aliondoka Kwenda Kuangalia Lile Cancer La Atcl Linaloingia Muda Si Mrefu Na Pia Kuna Ambazo Wametoa Order Zinakuja 2014,,,pundamilia Analifahamu Hilo....
pia Kuna Mikwara Wa Kuotota Gurantee Kwa Hili Linalokuja Hivyo Ameenda Kuangalia Ni Kweli Au Lah.......
mwenyezi Mungu Ailaze Atcl Mahali Pema Peponi.....hiyo Ndege Ni Mdebedo Mtupu,,,mimi Niko Usa Nimepata Ma Data Yake Analiza Kama Mtanzania ,mwenye Mapenzi Mema,,,,,kama Watatoa Hiyo Gurantee Basi Huu Ni Ufisadi Mwingine Mkubwa ,,,,na Jk Atakuwa Mtuhumiwa Mkuuu....kwanini Kila Sehemu Tulie Sie Tu Njamani Watanznaia,,,,madini Wanachukua Makopo Tunaletewa...we Jakaya Angalia Vixzuri Hili......juzi Wapendwa Nimepata Dondoo Baada Ya Jamaa Kulipua Swala La Madege Mabovu Mheshimiwa Mattaka Kawahakikishia Anafanya Redenders Na Kaapa Anawatimua Wote Wliohusika,,,na Cha Kuhuzunisha Tunasikia Walikaa Na Chama Cha Wafanyakazi Akaulizwa Sababu Za Kuwapunguza ,,,akasema Watu Wengi Wakambana Ndipo Alipokuja Kwemada,.,,alipokuwa Akiingia Aliambiwa Na Waziri Chenge Hapo Kuna Majungu Na Kuna Watu Wanaojidai Kampuni Yao Wakimsumbua Awafukuzie Mbali....kamati Za Maadili Bungeni Huyu Ndie Chenge Alierudi Tena Je Ni Haki Hiii???wana Jf Tunaomba Ma Lawyer Kuwasaidia Hawa Ndugu,,na Kikao Inasemekna Akikavunjika,,,ndugu Zanguni Si Mchukue Rebate Kama Sisi Mje Uku Kula Kuku,,,muachane Na Hayo Matatizo
 
Hivi Rais angepata ajali au tukio lolote baya kutokea na kumsababishia kurudi Watanzania wangeelewa? Hii habari ya yeye kwenda Ujerumani niliandika wiki kadhaa nilipoibua sakata la ATC. Serikali kumpa Karume aongoze msafara kule Ujerumaini ilikuwa danganya toto.. Waandishi hawana budi kuuliza "Inakuwaje Rais atoroke kimya kimya"...
 
Kinachoumiza hizi banana republic za kwetu ni lack of transparency! Yaani tunafanya mambo kienyeji mno! Sasa imagine huyo ni mkuu wa kaya!! atamkemea kweli afisa anayeenda likizo binafsi kijijini Maswa au Magu na VX ya walipa kodi?

Kwa wale wanaoshangaa kwa nini watu hapa wanafuatilia hili swala, its simple, huyu bwana is traveling on our names and pay check kama taifa! anaunguza kodi zetu, kwa hiyo tunahaki ya kujua hili! Umeshaona mtu anauliza Mkapa au Sumaye yuko wapi? its non of our business....sisi anayetuhusu ni yule anayetumia kodi zetu! Jamani pesa hii ni ya raia zaidi ya million 38! Huoni Bush anaandamana na msululu wa press? unafikiri anapenda? ni kwa sababu anatumia kodi za wa-USA na kwa hiyo wana haki ya kujua what he is doing huko aliko!
 
maalim ..hiyo ndio gharama ya kuwa kiongozi..your whole life become under scrutiny!!!!

Hapa ndipo naipendea JF,

Mambo yanafanyika sirini, vyombo vya habari haviandiki, lakini JF kama kawaida yake inatupatia habari zikiwa bado jikoni. Hivi sababu ni nini ya kwenda kimya kimya? hii imeanza kama ile ya kusaini mkataba wa buzwagi hotelini.....

wana JF.... kaeni mkao wa kula, another skandali in making
 
Rais Kikwete alienda kuangalia ndege yetu mpya ya Airbus kwenye Jiji la Hamburg nchini Ujerumani. Cha kushangaza na kushtua ni kuwa wakati huo huo Rais wa Zanzibar Bw. Amani Karume alikuwa nchini Ujerumani akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara wa Kitanzania wapatao hamsini hivi. Karume alichukua nafasi hiyo baada ya JK kutingwa na ujio wa Bush. Kinachoshangaza ni jinsi gani JK ilimbidi aende tu... hata kimya kimya.. sasa lingetokea huko tungeambiwa Rais alikuwa anaenda wapi?
 
Back
Top Bottom