Kikwete akumbana na zomeazomea Mbeya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete akumbana na zomeazomea Mbeya...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wa mmoja, Aug 31, 2010.

 1. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete jana aliendelea na mikutano yake ya kampeni katika mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya ambapo wananchi walimpa matumaini makubwa ya ushindi lakini wagombea ubunge wawili walizomewa.

  Kikwete aliwasili mkoani Mbeya jana na kuanzia kampeni zake kwenye mji mdogo wa Tunduma ambao uko mpakani mwa Zambia na ambao una pilikapilika nyingi za wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hiyo jirani.

  Tofauti na mikutano mingine ya kampeni katika majimbo mbalimbali ambayo ameshatembelea kwenye kampeni zake, Kikwete alikumbana na hali isiyo ya kawaida wakati alipowanadi kwa nyakati tofauti wagombea hao wa majimbo ya Nkasi Kusini, Desderius Nipata na wa Mbozi Kusini, Lucas Siyame.

  Tukio la kwanza la kuzomea lilitokea kwenye Uwanja wa Kate, ulio katika Kata ya Kate ambako wananchi walizomea baada ya mgombea wa Jimbo la Nkasi kuwataka wampigie kura Kikwete.

  Lakini alipoanza kuomba wananchi hao wampigie kura na yeye ili afanye kazi na Kikwete, wananchi hao walianza kumzomea.


  Source: Mwananchi 30/08/2010
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,135
  Trophy Points: 280
  atajiju...........hiyo ni rasharasha tu mvua yenyewe bado...
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Vyombo vya habari havitaki kuitangaza hii.
   
 4. Wa mmoja

  Wa mmoja Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio havitaki,vingi vinaogopa!
  But naona mwananchi wamekuwa wabishi kidogo,hivi karibuni mwandishi wao alipigwa pini kuufwata msafara wa kikwete kuelekea kwenye kampeni za CCM!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Zomea zomea itaendelea hadi kwenye upigaji wa kura
   
Loading...