Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Nimesoma hiyo story ya magazetini kuhusu maelezo ya balozi wa marekani kuwa serikali ya Kikwete haijawasiliana na serikali ya Marekani kuhusu suala la Balali kurejeshwa nyumbani. Nimesoma pia ile story ya wizara ya mambo ya nje wakijikoroga kuwa wao sio wanaotakiwa kumtaka Balali arudi nyumbani bali ni wizara ya fedha ndiyo inatakiwa kufanya hivi (what a moronic excuse!).
Haya yote yanadhihirisha wazi kuwa serikali ya Kikwete haina mpango wa kumtaka Balali arudi nyumbani kusimamia kesi ya wizi wa pesa za BoT unaomkabili (kulingana na maelezo ya serikali). Wakati serikali ya Kikwete imetoa miezi sita kwa waliohusika na wizi huu kukimbia nchi na kuficha mali zao (huku pia wakisubiria kuona kama Balali atakufa) oooopsss kuipa bodi ya BoT kufanya uchunguzi wa wizi wa BoT, hotuba ya waziri Meghji bungeni kuhusu wizi huu inaonyesha kuwa mengi sana yanataka kufichwa hapa ili kuwafunika wahusika wakuu wa wizi huu - Mkapa, Mramba, Mgonja, Rostam Aziz, na sasa mkuu wa kaya mwenyewe Kikwete.
Inabidi sasa Kikwete akubali kuhusika na wizi huu wa BoT na ajiengue kabisa katika kuendesha uchunguzi huku akiruhusu tume huru ya bunge ifanye uchunguzi wa kila kilichotokea huko BoT na uchunguzi huu urudishwe kwa miaka kumi nyuma kwa kuanza na madai ya Mrema yalifanyiwa uchunguzi na kina Oyombe (mb-Rorya) na wengine.
Inabidi sasa Kikwete akubali kuhusika na wizi huu moja kwa moja na akubali kuwa ushindi wake wa "kishindo" dhidi ya wapinzani wake ndani ya ccm na ule mkuu ni flawed na inabidi taratibu zifanyike za kuwa na uchaguzi mwingine wa haki.
Inabidi sasa Kikwete akubali kuhusika na wizi huu na pia aombe msamaha kwa wapinzani wake wa ndani ya ccm kina Malecela, Sumaye, Salim Ahmed Salim na wengine wote aliotumia pesa za wizi na vyombo vya habari vichafu vya mkoloni na mwizi Rostam Aziz kuwachafua ili ashinde kwa "kishindo"
Raisi Kikwete, chagua kufanya kitu chema mapema kabla jehanam haijashushwa juu yako kutoka kwa vilio vya wazazi na ndugu wanaopoteza watoto wao na mama zao kwa kukosa madawa huku wewe ukitumia mabilioni kusafiri na kufanya personal shoping zako kwa pesa za wizi!