Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Rais Kikwete ambaye sasa hivi yuko Ethiopia alichepukia Libya kwa ziara ya siku moja ya kikazi. Katika taarifa ya habari ya saa mbili TBC wametangaza sababu ya Rais kwenda Libya na kufanya mazungumzo na Ghadaffi (pichani) kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Bernard Membe:
"alienda kuzungumza na Ghaddafi, ili kujua ni jinsi gani Afrika ya Magharibi wamejiandaa kupokea wadhifa wa Uenyekiti wa AU hapo Februari mwakani wakati zamu ya Tanzania itakapofikia kikomo".
Hayo ndiyo maelezo pekee yaliyotolewa na kurusha na TBC. Nikakaa chini na kujiuliza "well najua tuna Gulfstream na anaweza akachepukia mahali pengine popote, lakini kwenda kuuliza swali yaweza kuwa sababu ya kutosha"? Nikaendelea kujiuliza "si angejaribu angalau angejalibu kuomba kitu kama ilivyokawaida?"
Yawezekana kuna sababu nyingine lakini hiyo ndiyo iliyotangazwa so msinijie juu bure!
lakini nikakumbuka kuwa yawezekana simu za Ikulu hazifanyi kazi au haziko secure enough; Na nilipokumbuka email nikagundua kuwa hata email yao haifanyi kazi hadi wanatumia ya yahoo.com na yawezekana hawakutaka kufanya hivyo maana Muammar angewadhania ni Wanigeria wanajarimu kumuingiza mjini.
Nikajisemea.. "it is good to be a President"..