BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,889
Kikwete akilegea CCM imekwisha
Waandishi Wetu, Dar & Dodoma Oktoba 31, 2007
Raia Mwema
Mkutano Mkuu wa CCM
KUTANO Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unafanyika baadaye wiki hii, Dodoma, huku chama hicho kikikabiliwa na mgawanyiko mkubwa pengine kushinda yote iliyopata kuwapo huko nyuma, na hofu ya kujitokeza kwa kura za itifaki kama ilivyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2002, wachunguzi wamesema.
Kimsingi mkutano huo utahitimisha uchaguzi ambao umekuwa ukiendelea ndani ya chama hicho ambao nao unatajwa kuwa chanzo cha mgawanyiko wa dhahiri hasa baada ya kuwapo tayari mgawanyiko katika maeneo mengi katika ngazi za wilaya na mkoa.
Tayari CCM imekwisha kupata uongozi wake toka chini hadi ngazi ya mikoa unaoingia ndani ya Halmashauri Kuu (NEC). Unaosubiriwa kufahamika pamoja, ndio unaotarajiwa kukiendesha chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano hadi mwaka 2012.
Habari za ndani ya CCM ambazo Raia Mwema imezipata zinasema kwamba kuna mabadiliko ya kiutaratibu yaliyofanywa na vikao vya juu vya CCM ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kupiga kura katika makundi ya mikoa badala ya kwenda mbele katika masanduku isipokua kwa uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake.
Kwa mujibu wa habari hizo, utaratibu huo pamoja na utamaduni wa wagombea kutoruhusiwa kuwa na wawakilishi wakati wa kuhesabu kura, unazidisha hofu ya kuwapo kwa kura za itifaki kama ilivyokua katika uchaguzi wa mwaka 2002 ambao viongozi wa juu wa Chama na Serikali walipata kura nyingi na wale ambao hawakutakiwa walipata kura chache.
Kwa kweli tunahofia kutokea kwa matokeo kama ya mwaka 2002 ambayo vigogo walipata kura nyingi na wale ambao walionekana kama hawatakiwi walipata kura chache na wengine kuangushwa kabisa. Unakumbuka Jakaya Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Edward Lowassa, akiwa Waziri wa Maji walipata kura chache huku Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana, Emmanuel Nchimbi, alishindwa, anasema mgombea mmoja wa CCM na kuendelea:
Na mwaka huu sisi wadogo najua hatutapona kabisa maana hali tunavyoijua katika hili kundi la kifo la wagombea 20 tayari kuna wenzetu wana kura zao za itifaki halafu watafuatiwa na wale wenye uwezo wa kifedha ambao wamefanya kampeni kubwa zaidi na kutoa fedha nyingi.
CCM imekwishakutangaza watu ambao ndio watakaosimamia uchaguzi huo wakiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samuel Sitta akisaidiwa na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho.
Maspika hao wanasaidiwa pamoja na watu wengine, Mweka Hazina wa CCM, Rostam Aziz na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana, Emmanuel Nchimbi, wote wakiwa wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho.
Habari kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari nchini kote ambazo zimelifikia gazeti la Raia Mwema, zimekuwa zikisema kwamba kumekuwapo hekaheka huko kutokana na ziara za wanaotaka kuchaguliwa katika hatua hii ya mwisho ili waingie katika NEC.
Hilo ni kundi kubwa la wagombea wapatao 59 ambao kati yao ni 20 tu watakaopitishwa. Kundi hilo lina kila aina ya vigogo, wengi wao wakiwa ni wenye nyadhifa za sasa za uwaziri na wengine ni ambao ama walikuwa mawaziri au walikuwa na vyeo kwenye chama na au katika serikali iliyopita ya Benjamin Mkapa.
Aidha, wengi katika kundi hili ni walewale walioingizwa kwenye NEC kupitia mchujo huohuo uchaguzi uliopita, na kwa hiyo safari hii, ni kana kwamba mchezo unajirudia baada ya miaka mitano.
Waliomo katika kundi hilo ni Amos Makala, Dk. Baanda Salim, Jackson Msome, Arbogast Dogodogo, James Nsekela, Costantine Kanyasu, Amos Siyantemi. Mohamed Mkumba. Profesa Idris Mtulia, Profesa Samwel Wangwe na Andrew Chenge.Wengine ni Edward Lowassa, Abdulrahman Kinana, Novatus Makunga, Tarimba Abbas, Filbert Bayi, Shy-Rose Bhanji, Juma Kapuya, Hamida Kilua, Lucas Kisasa, John Komba, Makongoro Mahanga, Yusuf Makamba, Mahamed Mamoon, Wilson Masilingi, Benard Membe, William Ngeleja, Kingunge Ngombale- Mwiru na Salim Khamis.
Wengine ni Pared Kaduga, John Chiligati, Paschal Mabiti, Abeid Mwinyimsa, Charles Kagonji, Dk Ibrahim Msengi, Hassan Ngwilizi, Said Masoud Fundikira, Hashim Twakyondo na Nicholas Zacharia.
Kundi hilo lina wagombea wengine kama David Mathayo David, Aggrey Mwanri, David Holela, Isdore Shirima, Stephen Wassira, Christopher Mwita Gachuma, Enock Chambier, Maurus Mhimbira, Profesa David Mwakyusa na Emmanuel Mwambulukutu.
Wengine wanaogombea kuwa wajumbe wa NEC ni Frederick Sumaye, Siwajibu Clavery, William Lukuvi, Jaka Mwambi, Job Ndugai, George Simbachawe, Abdul Adam Sapi Mkwawa, Uhahula Frank Uhahula, Dk. Diodrus Kamala na Said Kilahama.
Wakati huo, Sumaye, aliyekuwa Waziri Mkuu, aliongoza akiwa na kura 1546 kati ya kura 1677 zilizopigwa. Alikuwa akifuatiwa na Philip Mangula aliyepata kura 1524.
Mangula alikuwa Katibu Mkuu, majuzi aliwania nafasi ya NEC kutoka Iringa akabwagwa vibaya katika kura zilizopigwa na karibu watu walewale ambao miaka mitano iliyopita walimpa ushindi wa pili.
Katibu Mkuu huyo wa zamani wa CCM ameiambia Raia Mwema katika mahojiano maalumu kwamba kushindwa kwake kupata kura kunatokana na msimamo wake wa kukataa kuhonga.
Katika moja ya nukuu zake anasema: akaniambia kuwa ilikuwa muhimu kwangu kwenda kuwasalimia (wajumbe) kwa kuwapa angalau soda. Nikamjibu kuwa kama ni salamu za kujuliana hali tu, nilikuwa tayari, lakini si salamu za kupeana soda.
Nikamwonyesha kipeperushi chenye maelezo yangu binafsi. Akanikejeli kuwa wajumbe hawataki hayo siku hizi. Akasema mtindo huo umepitwa na wakati, hivyo nijirekebishe. Nikakataa, na mambo yakabaki hivyo.
Wao hivi sasa wanasema wanataka vipeperushwa, si vipeperushi. Hii ndiyo hulka ya wapiga kura wetu wa sasa. CCM ya sasa sicho chama kile ambacho kiliongozwa na Mwalimu (Julius Kambarage Nyerere).
Nilikataa kwa sababu kwangu ninaamini kuwa ni mwiko kuhonga. Kufanya hivyo ni mwiko. Nikifanya hivyo nitakuwa ninalikosea kanisa langu ambalo naliamini. Mahojiano hayo na Mangula yemachapishwa kwa kirefu kuanzia ukurasa wa 13 wa toleo hili.
Washindi wengine katika uchaguzi huo wa mwaka 2002, kwa mujibu wa kura zao ni: Msome (1474), Kinana (1329), Kingunge (1312), Makamba (1311), Ngwilizi (1263), Komba (1244), Kapuya (1155), Sarungi (1002), Paul Kimiti (957), Jakaya Kikwete (911), Lukuvi (846), Dk Masumbuko Lamwai (820), Lowassa (808), Charles Keenja (782), Shirima (708), Stephen Mashishanga (707), Ahmed Shabiby (699) na Profesa Mtulia.
Ukiwaondoa Dk Lamwai, Keenja, Shabiby na Mashishanga ambao safari hii wamesusa, na Kikwete ambaye sasa ni Mwenyekiti, wengine waliosalia katika washindi wa kwanza 20 ambao ndio wanaotakiwa kupita, wamo.
Walioshindwa katika kundi hilo, wengine ambao wamejaribu bahati yao safari hii pia, ni Masilingi (643), Profesa Mwakyusa (592), Christopher ole Sendeka (554), Edgar Maokola- Majogo (549), Dk Pius Ngwandu (527), Sebastian Chale (507), Mussa Nkhangaa (499) na Suleiman Sadiq (482).
Wengine ni Leonidas Gama (476), Mohamed Seif Malinda (431), Mwanri (415) Theodos Kasapira (408), Dk. Msengi (381), Mwambi (340), Hamza Mwenegoha (325), Mateo Qares (305), Gerald Guninita (281), George Mlawa (278), Athman Mfutakamba (259) na Profesa Henry Mgombelo (243).
Wagombea wengine walikuwa ni Bernard Mbakileki (239), Neema Masawe (230), Kamuga Edward Budegeye (225), Joe Shengena (213), James Jijanda (199), Dk Fadhili Omar (186), Gulzar Sabil (185) na Brigedia Jenerali mstaafu Mwilipanga Lupembe (181).
Wengine walikuwa ni Paulo Laizer (178), Dk Cuthbert Mhilu (162), Dauda Kalumuna (128), Honorius Mmavele (127) Zainuddin Adamjee (123), Kasinje Hamidu (117), Cuthbert Semdiga (114), Paul Ghemela (101), Javan Masimami na aliyefunga mlango akiwa Stanley Sabuni (92).
Uchaguzi huo unafanyika huku kukiwa na kutokuelewana hata katika mikoa ambayo, kwa asili, imekuwa ni shwari.Makovu ya makundi yaliyokuwa yakipambana katika mchakato wa kuwania urais ndani ya CCM mwaka 2005 ndiyo ambayo, wachunguzi wa mambo wanasema yatakuwa yakichukua nafasi katika uchaguzi huu wa mwishoni mwa wiki.
Tangu baada ya uchaguzi huo, mahusiano ya makundi hayo, kwa mfano, mkoani Mbeya yamekuwa mabaya na mara kadhaa CCM imetuma ujumbe huko, chini ya Kinana, kujaribu kutafuta suluhu.
Huko kundi la mgombea nafasi ya urais ambaye hakufanikiwa, Profesa Mwandosya, limekuwa likipambana na la Tom Mwangonda, Mbunge wa Kuteuliwa, ambaye alipambana na Mwandosya na kisha kushindwa hivi karibuni katika kuwania ujumbe wa NEC Mkoa. Mbeya limekuwa eneo linalofukuta, hata hivyo, suluhu inaelekea kuwa mbioni kupatikana kama ziara ya wiki iliyopita ya Waziri Mkuu Lowassa ilivyoshuhudia. (Soma safu ya Yatokanayo: Uk. 9).
Hali hiyo ya mvutano imeshuhudiwa pia mkoani Mwanza, ambako makundi ya wagombea wawili, Anthony Diallo na Raphael Chegeni, yameacha mpasuko.
Jirani ya Mwanza, mgawanyiko mkubwa uko mkoani Mara, ambako tofauti zilizoshindikana kusuluhishwa zilisababisha NEC kufuta ugombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa.
Mwenyekiti wa muda mrefu, Chambiri, safari hii alikuwa apambane na Gachuma katika nafasi hiyo, lakini ugombea wao umefutwa na wote wameingizwa katika kutafuta nafasi hizo 20.
Lakini pengine hali ilivyo mkoani Arusha ndiyo ambayo inaeleza zaidi kiwango cha migongano kilivyokua ndani ya CCM kutokana na kuenguliwa kwa wagombea wawili ambao walikamatwa kwa tuhuma za rushwa. Walioenguliwa ni pamoja na Elisa Mollel na Lekule Laizer.
Akijaribu kutibu majeraha hayo ya Arusha, hivi karibuni, Rais Kikwete alikemea tabia ya baadhi ya watu kujifanya wapelelezi, waendesha mashitaka na mahakama, akimaanisha kwamba suala la kina Mollel na Laizer lilikuwa bado halijafanyiwa uamuzi na hivyo hadi wakati huo hawakuwa na hatia.
Wote wawili wana nguvu za kutosha mkoani humo ndani ya CCM na kuenguliwa kwao kumeacha tofauti ambazo kama hazitasuluhishwa mapema na kwa makini, mtazamo wa jamii ya Mkoa wa Arusha juu ya CCM utakuwa umeathirika kiasi cha kutosha.
Ukicha masuala ya uchaguzi, shutuma za ufisadi dhidi ya Serikali ya CCM na kushindwa kwa dhahiri kwa baadhi ya wanaoshutumiwa kwa uoza huo kujibu hoja nako hakuielezi vyema CCM miongoni mwa wanajamii.
Japo baadhi ya wanaotuhumiwa wametishia kwenda mahakamani, ukweli ni kwamba hawawezi kuthubutu kufika huko ambako kuna uwezekano mkubwa wa matendo yao ya nyuma wakiwa waajiriwa kwingine yataanikwa.
Inashangaza kwamba baada ya tuhuma za ufisadi, baadhi yao wamesema wanakwenda mahakamani. Wanakwenda kutafuta suluhisho la tatizo la kisiasa mahakamani? Hii inashangaza. Hawa si wanasiasa. Hawajui kwamba huko kila kitu chao kitaanikwa. Na baadhi huko nyuma walifukuzwa kazi kwa masuala hayahaya ya ufisadi, anasema mchambuzi mmoja.
Shinikizo la hoja ya wapinzani la ufisadi limeifanya Serikali nzima kufanya ziara ya mikoani ambako inaelezwa kwamba mawaziri wanaeleza uzuri wa Bajeti ya mwaka huu ambayo nayo ilipingwa sana.
Habari, hata hivyo, zinasema kwamba ziara hizo hazihusiani kabisa na suala la Bajeti, bali zimelenga kuzima moto wa vilio vya ufisadi na kuwafanyia kampeni za ujumbe wa NEC baadhi ya vigogo ndani ya Serikali na kwa mawaziri wanaowania nafasi hiyo muhimu ndani ya CCM. Ukiacha masuala hayo ya uchaguzi, Mkutano Mkuu unatarajiwa pia kupitia mapendekezo ya mabadiliko katika katiba ya CCM.
Mabadiliko yanayopedekezwa ni pamoja na kuwa na Bunge lenye uwakilishi unaolingana wa asilimia 50 wa wabunge wanaume na wanawake kama ambavyo imependekezwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Jambo jingine litakalozingatiwa na Mkutano Mkuu ni nafasi ya Makamu Mwenyekiti, inayoshikiliwa sasa na John Malecela.
Malecela hakuwania nafasi ya u- NEC na kuna kila dalili kwamba anaweza kubadilishwa. Baadhi ya majina ambayo yamekuwa yakitajwa ni ya pamoja na Pius Msekwa na mkewe, Anna Abdallah; Sumaye, Kinana na wengine wanamtaja hata Mangula, wote wakionekana kutokua ndani ya kundi maarufu la wanamtandao lililotajwa kusaidia ushindi wa Rais Kikwete.
Malecela amekalia umakamu kwa kipindi kirefu na dhahiri kwa hali ya mambo ilivyo kurejea kwake katika nafasi hiyo kuna utata. Wakati ule wa awamu ya tatu, inaelezwa, kwamba ilihitaji nguvu ya ziada ya Mwenyekiti Mkapa kutetea uteuzi wake, japo baadaye ilikuja kuonekana kuwa nafasi hiyo ilistahili mtu kama Malecela.
Nafuu, pengine ya Malecela (hata kama akiukosa umakamu) na wazee wenzake kama Cleopa Msuya, imo katika sehemu ya mabadiliko ya katiba ya CCM yanayopendekezwa ya kuwafanya wazee kama hao kuwa wanachama wa kudumu wa NEC.
Kwa sasa wanachama hao dumu ni pamoja na Rashidi Kawawa, Mwinyi, Mkapa na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk Salmin Amour.