Kikwete akikutana na hawa simanzi humtoka ghafla, Pax tecum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete akikutana na hawa simanzi humtoka ghafla, Pax tecum

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, May 1, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kuna rika fulani ya watu hasa watoto, kuna watu wenye maisha ya mfumo fulani wa maisha na wengineo mnaojua mtu ukiwa katika kufikiria mambo mazito yenye kukuchefua au kuumiza ubongo, unajikuta kufarijika na kupata amani na maono mapya moyoni. Ukweli ndo huo, tujitahidi kupata nafasi ya kukutana na watu wa aina hiyo au kutembelea chekechea baada ya bongo kuchoshwa na mengi ya kukanganya utajisikia mtu umepata utulivu na amani isiyo kawaida, hata kama ni ya muda lakini inakuongezea siku za kuishi kadiri ya wanasayansi na wanasaikolojia.
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwanini?
   
 3. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kuanzisha Thread tuwe tunalipia ili kupunguza pumba kama hizi,au lianzishwe jukwaa la thread pendwa maana title na kilichomo kama chu.pi na kofia (mbalimbali)!
   
 4. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #4
  May 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,491
  Likes Received: 4,764
  Trophy Points: 280
  thapotii
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unaweza kuona pumba, lakini jaribu kutafakari maudhui ya mleta habari. Na ukiangalia sana kisaikolojia unaweza kugundua kitu cha msingi kwa watu walio na mambo mengi yanayoumiza ubongo hadi hawapati nafasi ya kuwa na watu ambao muda kidogo wanaokutana wanawapa mpozo wa kuondoa wingu zito linalosumbua kichwani.

  Mfano wengie huamua kwenda huko porini na kuanza kutafakari mengi yanayojia huko, ndege wazuri, wanyama pori wanavyofurahia himaya yao, mito yenye maji maangavu yanayotiririka sehemu ambayo haijaathirika kimazingira, mimea na maua mbalimbali yanavyopamba pori hadi unatamani mazingira hayo yangekuzunguka unakoishi.

  Tatizo wengi wetu hupuuza vitu vidogo kama hivyo kwani ndivyo kisaikolojia vinamwongezea mtu uhai na furaha ya maisha ingawa ni kwa muda, lakini unajisikia kupunguza mawimbi yaliyokuwa yanakusonga na kupata nguvu mpya, faraja na hata fikra za kuanza kupya.

  Kwa wenye mazoea ya kufanya tafakari ya maisha watanielewa ninachoongelea.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Umeshawahi kukutana na watu wa aina hiyo? Umeshawahi kutafuta nafasi ya kuwa na watoto wadogo na kuongea nao na kuona kinachojilia nafsini mwako kuongea au kucheza na hawa malaika wasiojua hila wala waa? Huo ndio msukumo wangu wa kuanzisha mada hii.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  May 2, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  "PAX TECUM" Ni neno la lugha ya zamani ya huko Italia (latin) likiwa na maana ya "AMANI KWAKO."
   
Loading...