Kikwete akataa Udikteta kwa hiyo haya ruksa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete akataa Udikteta kwa hiyo haya ruksa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Oct 6, 2009.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naam, tusidanganyane jamani. Suala sio kukataa udikteta. Suala ni uongozi wa nchi umetushinda. Na hili wamelionyesha mapadri. Kisha Masheikh. Mamaneja kama wale wa NHC, NSSF, TANESCO, BOT na kwingineko hawaiogopi serikali na wanafanya wanachokitaka. Na sasa wananchi kwa kuchukua sheria mikononi mwao ni wazi kabisa tamko la karne linatolewa nalo sio lingine ila ni kwamba: NCHI HAINA MWENYEWE!

  Sasa kama bwana mkubwa anasema hataki kutumia udikteta Unguja tunamuuliza maswali haya:
  . Polisi wa muungano wanafanya nini Pemba? Huu sio udikteta?
  . Tume ya Uchagui Zanzibar inafanya nini na uandikishaji wapiga kura? Huu sio wizi na udikteta?
  . Mheshimiwa hivi unapomwambia babu wa miaka 90 akalete wakubwa wawili washuhudie kuwa kweli kazaliwa visiwani una akili au....?
  . Katika sheria mheshimiwa majirani na jamaa huweza kuwa ithibati tosha ya suala linalochunguzwa. Hili haliheshimiki visiwani. Je, huu sio udikteta ?
  . Mheshimiwa redio na televisheni Zanzibar na gazeti la Zanzibar Leo hayaoni gogo lililo kwenye jicho la SMZ lakini linaona kibanzi kwenye jicho la chama mbadala. Je, huu sio udikteta ?
  . Mheshimiwa njama zinafanyika za ndugu kutaka kurithiana urais (au Usultani wa mtu mweusi Zanzibar) je, huu sio udikteta ?
  . Mheshimiwa Waislamu Zanzibar wanatawaliwa na walevi na maamuzi yanafanywa kwenye ulevi, je, huu sio udikteta ?
  . Mheshimiwa viongozi wa Mitaa Pemba wenye njaa kali WANALAZIMISHWA kutii amri za viongozi wasio na haki wala uadilifu -ingawa fika wanajua wanatenda isivyo na dhuluma tupu kwa sababu ya kudangwa na tujihela tudogo tu au vitisho vya kukosa hiki au kile. Je, huu kwako sio udikteta?
  . Mheshimiwa Mahakama Unguja hazina sauti na zimehasiwa. Je, huu sio udikteta?
  . Mheshimiwa Baraza ndio hao hao wanaofanya maamuzi , je mfumo wa check-and-balances uko wapi na sisi wanyonge tuende wapi? Tumlilie nani? Kwako huu sio udikteta?
  . Mheshimiwa chama chako CCM Zanzibar ni cha madikteta watupu, je, utakataaje vipi udikteta wakati wawakilishi wako wote Unguja ni madikteta?
  . Mheshimiwa wabunge wa Muungano Zanzibar hawana kauli wala sauti Unguja. Je, huu sio udikteta?
  . Mheshimiwa Katiba ya Unguja na ile ya Muungano zote ni za kidikteta. Je, utakataaje udikteta?
  . Mheshimiwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ndio CCM na ndio Baraza la Mapinduzi na huu nao sio udikteta.

  Kwa kifupi mheshimiwa tuna tatizo na kauli zako kuhusu hali ha hewa visiwani. Tunaamini kwamba mfupa huu umekushinda. Na katika kutapatapa unataka kujificha nyuma ya pazia la kukataa udikteta ambao tayari upo na haukataliki. Mheshimiwa ipo tofauti kubwa sana ya kuwa na rais na kuwa na kiongozi. Kwetu sisi Wazanzibari tunaamini kwamba rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika yupo lakini hakuna KIONGOZI au wewe unasemaje?  Hakika hapa Tanzania kama kuna viongozi ambao tayari wananunua tiketi ya kwenda motoni moja kwa moja ni wale wa SMZ licha ya sala za unafiki za wajamaa hawa huku wanashindwa kufuata kinavyosema kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu (orijinoo) na sunna za kipenzi chake Mtume wake wa mwisho ambaye itakuwa shudhuda wa yanayofanywa na makafiri ndani ya Uislamu kwa Waislamu wenzao.
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kikwete ni askari goigoi ,yaani hata Pinda alilia pale bungeni baada ya kuona mkuu wa kikosi anashindwa kumkingia kifua na akamuachia msalaba wa maalbino umwangukie pekee.
  Ugoigoi wa Kikwete ulionekana Butiama pale akina Karume na genge lake kutoka Zanzibar walipomkazia sauti na kumtisha ,masikini Kikwete kuona vidume vya zenji vinamkoromea ,akakunja mkia na kuacha ugerman shepherd.
  Kwanini asiwe kama Nyerere na kuwambia tu asietaka kufuata muafaka atoke inje, kama si ugoigoi ni kitu gani ?
   
Loading...