Kikwete aibiwa ng'ombe wake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete aibiwa ng'ombe wake!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Domo Kaya, Jun 20, 2009.

 1. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waungwana ,
  Naomba niiweke hii kitu hapa,ikiwa itabainika kwamba ni udaku basi naomba mods kwa ridhaa yangu waiweke kwenye udaku.

  Kama wiki hii iliyopita nilisikia kwenye kipindi cha asubuihi Clauds FM wakimuulizia afande Kova,yaani haonekani pale kwenye maeneo yake aliyo jipangia kila asubuhi kuongoza magari pale kwenye taa za Saranda bridge (surrender bridge).

  Baadae wiki hiyo nilipata habari kwamba afande Kova yuko Bagamoyo kwenye shughuli maarum ( msako wa kutafuta ngombe wa Muheshimiwa raisi walio ibiwa)

  Wiki kabla ya hiyo,inasemekana watu wasio julikana waliingia shambani mwa muheshimiwa raisi maeneo ya mashamba ya Sanzale na kuiba Ngo;mbe takribani 30 mali ya muheshimiwa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.kitendo kilicho sababisha afande kova kwenda kuongeza nguvu wa msako wa mifugo hiyo,kitendo kilicho sababisha watu takribani sabini kukamatwa kuhusiana na hilo.

  Nikajiuliza kama ni kweli, je inchi hii kuna jeshi la polisi? kiasi cha kwamba mtu mkubwa kama raisi anaweza kuibiwa mifugo yake kweli hivi mali zangu mimi kabwela zitasalimika kweli?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwani kisheria shamba la raisi linalindwa? Huo si utakuwa upotezaji wa pesa kama mali zote za waziri mkuu mpaka raisi zitakuwa zinalindwa kama wao? Raisi analindwa yeye, immediate family, makazi yake rasmi na popote pale anapo tembelea. kama angekua anaishi huko shambani basi kungekuwa na ulinzi wa nguvu huko.
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ng'ombe 30 kwa JK ni kitu gani?. Mihela yote aliyokuwa nayo bado anahangaika kutafuta ng'ombe 30 walichukuliwa na masikini?. Alitoa ahadi maisha bora kwa kila mtu, tumesubiri hayaji ila yeye tu ananehemeka, sasa na sisi masikini tujisaidie kupata maisha bora.
  Na kama walioiba ni wagogo basi mjue ng'ombe washachinjwa zamani na nyama imeuzwa mabucha ya Bagamoyo na Dar. Patamu hapo.
   
 4. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ngombe wa CDA?:cool:
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu sifurahii kwamba JK kaibiwa ngombe, ila nafurahia kwamba walau kilio cha wafugaji bagamoyo kitasikika! kwa maana siku hizi ili jambo litendeke lazima limguse mkulu/kigogo ndo linapewa umuhimu!

  Wafugaji bagamoyo wameibiwa ngombe wengi tu, na si bagamoyo ni kuanzia bagamoyo bunju, boko, tegeta hadi madala, Wezi hao huwasafirisha ngombe hao kwa mashua kwenda visiwani zanzibar ucku wa manane, na ni sindiketi kubwa inayo husisha hadi viongozi wa vijiji, na maaskari polisi walio pigika! kwahiyo wafugaji wakiibiwa wakaenda ripoti polisi, wanazungushwa weeeee, na kuambiwa toa nauli kila siku.. hadi wafugaji wanasalimu amri.

  Inshalah kwa vile mkulu kaibiwa labda itasaidia kuvunja huo msurulu wa uharifu wa kuwatia umasikini watu wanao jipatia riziki kwa ufugaji.
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I am seeing a pattern in this.

  Ze Utamu imekuwepo kwa muda mrefu, wameishughulikia tu pale rais alipotukanwa.

  Ng'ombe wanaibiwa kwa muda mrefu, polisi wanachukua hatua tu anapoibiwa rais.Kwa hiyo watu wakitaka system ifanye kazi jambo la kwanza ni kum victimize rais.

  Halafu huyo Kova kamanda wa sehemu iliyopo Dar Bagamoyo anaenda kufanya nini? Ina maana Bagamoyo hamna polisi? Hii nchi mbona inaendeshwa shagalabagala?
   
 7. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Domo kaya Avanta lako linatisha mzee. Du! usitufanye tuanze kukufikiria kuwa na wewe ni mmoja wa devil worshipers, maana hizo ndo signs zao. Nakusihi kama unaweza kuibadilisha itakuwa vizuri maana linatisha ndugu yangu.
  Asante.
   
 8. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kumbe Rais wetu naye ni mjasiriamali mzuri tu. Pole kwa kuibiwa, manake ndiyo ujue kuwa haya ndo maisha ya kila siku ya Mtanzania wa kawaida, usiku akiwa amelala anawaza kama kesho itafika salama kutokana na wimbi la wizi ambao wakati mwingine huusishwa na walinzi wa usalama wa raia (Polisi)

  Tukimbilie wapi sijui!
   
 9. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #9
  Jun 22, 2009
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kuibiwa ngombe wa Rais ni faida kwa wafugaji wengine maana sasa ulinzi utaimalishwa vizuri zaidi.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo....
   
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  he is practising what is preaching! mjasiriamali.. ...... duh!
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hivi kadhia hii imethibitishwa au ndo yaleyale mambo yetu kutengeza dhana ..halafu dhana inazua dhana.amabyo nayo inazua dhana....halafu thread inaishia hewani kama kawa.
   
 13. F

  Froida JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  aliwatangazia wezi mwenyewe alipokuwa Dodoma kuongea na wazee wa Dodoma na stimulus package wakati fulani alisema ana zizi kubwa sana Bagamoyo manake kila akipita mikoani zawadi yake huwa ni ng'ombe labda ndio maana waliona bora wampunguzie kidogo manake akienda mikoani atazawadiwa wengine
  au waliibwa kabla ya hotuba
   
Loading...